Tabia gani usiyoipenda sebuleni?

Tabia gani usiyoipenda sebuleni?

Acha uchoyo kama vipi siungepakulia jikoni hukohuko kila mtu sahani yake. .kwa nini unataka mtu achaguwe kidogo akuachie wewe kikubwa. Ama uliwazaje kuwa anataka nini

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuingia kwangu hovyo hovyo unakuta mtu anakuja sebuleni ghafla tu ashafungua gril ya mlango hee nachefukwa sana nilimtimua mmoja sipendi mazoea ya kipuuzi hivyo jee kama nipo na mpenzi wangu jee

Sent from my GT-S7301 using JamiiForums mobile app
Kwanini usiwe unafunga, mi nikirudi home cha kwanza nalock geti! Sitaki mazoea kabisa ya kijinga..siku watanikuta nabanjuka mubashara na dada yao

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna hii apa...mipira mingi hasa UEFA huchezwa mida mibovu unakuta dogo kaja na wageni kama watano saa nne za usiku alafu wanakomaa hadi muda wa penalty hapo inakuwa saa saba kasoro alafu wanapiga makelele kama wapo Taifa
 
Unamkaribisha mgeni ndan kwako akishaingia anaanza kufanya ukaguz wa macho kwa vitu vilivyomo mule ndani basi kama unavitu kuzidi yeye utaona anaanza kubetua midomo
Mithili ya beberu aliyetoka kunusa mkojo wa mbuz jike hasa kwa sisi ke
Hii Tabia siipendi
Nikaribishe kwako nije kubetua mdomo kama beberu. Utaenjoy sana
 
Habari zenu wa Jf
Kuna tabia ambazo wageni wamekua wakifanya masebuleni mwetu na sisi kiukweli hatuzipendi ila tunashindwa kuwaambia coz ni mgeni unaogopa kumuuzi.
Baadhi ya tabia zinazonikera mimi ni kama ifuatavyo
1. Mgeni kupandisha miguu juu ya kochi, inakera, kama unajisikia kukunja miguu yako si bora ukae chini basi uikunje vizuri. Kuliko kupandisha milonjo yako kochini.

2. Wakati wa chakula labda umekaanga kuku umeweka kwenye bakuli self service unamkaribisha mgeni badala achukue vipisi asepe yeye anaanza kuchakura chakura yani atafukua mpaka kipande cha chini sijui ndio anatafuta kikubwa zaidi inaboa. We ukikaribisjwa fika chukua sepa.

Je wewe ni tabia gani hupendi kutoka kwa mgeni wako? Funguka hapa

Sent using Jamii Forums mobile app
Tabia mbaya una mchunguza mgeni anavyokula? umaskini mbaya sana!
 
Hapo kwenye kipande cha kuku wewe ni mchoyo. Mgeni inabidi ndo ale kipande kikubwa wewe hata usipokula sawa utakula mchuzi inayosha
 
Back
Top Bottom