Taasisi za washauri bingwa wa China na Afrika ni muhimu katika kutoa mapendekezo ya maeneo ya ushirikiano kati ya China na Afrika

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,010
1,036
微信图片_20220728110138.jpg

微信图片_20220728110133.jpg

Kuanzia tarehe 20 -21 Mwezi Julai, Mkutano wa 11 wa jumuiya za washauri bingwa kati ya China na Afrika ulifanyika hapa Beijing. Mkutano huo uliwakutanisha mabalozi, maofisa waandamizi wastaafu, maprofesa wa vyuo na taasisi za utafiti wa mambo ya Afrika za China na nchi za Afrika, pamoja na wanahabari wa pande mbili, ambapo kwa pamoja walijadili fursa na changamoto zilizopo kwenye ushirikiano kati ya China na Afrika.

Ushirikiano kati ya taasisi za ushauri bingwa kati ya China na Afrika ni moja ya maeneo mapya ya ushirikiano yanayoshika kasi, na yaliyoshuhudia mapema kufufuka kwa shughuli za ushirikiano kati ya China na Afrika. Zikiwa ni washauri na watoa mapendekezo muhimu kwenye uhusiano kati ya China na Afrika, taasisi hizi zinajikita kwenye kufanya utafiti na kutoa mapendekezo ya kiufundi na kisera kutokana na hali halisi na mazingira ya pande mbili.

Moja kati ya ajenda zilizojadiliwa kwenye mkutano huo, ni namna ya kuhakikisha Pendekezo la Maendeleo Duniani (GDI) lililotolewa mwaka 2021 na Rais Xi Jinping kwenye mkutano wa baraza kuu la Umoja wa mataifa linakuwa na manufaa kwa nchi za Afrika. Mkurugenzi wa mtafiti wa Idara ya masomo ya uchumi wa Taasisi ya China na Afrika Bw. Yang Baorong, alisisitiza umuhimu wa taasisi za washauri bingwa wa China na Afrika kuhakikisha tafiti zinaendana na mahitaji ya maendeleo ya pande mbili. Alisema kuna imani potofu kuwa maendeleo yatatoka nchi za magharibi au kwa kutumia mawazo ya nchi za magharibi, lakini mazingira ya China na mazingira ya Afrika ni tofauti sana na nchi za magharibi. Kwa hiyo ili kuhakikisha kuwa pendekezo Pendekezo la Maendeleo Duniani (GDI) linakuwa na manufaa na kuendana na ajenda ya 2063 ya Afrika, jumuiya za washauri bingwa zinatakiwa kutafiti na kuangalia njia zinazoweza kuleta manufaa kwa pande hizo mbili.

Moja kati ya mambo ambayo yamekuwa yakiigwa kutoka nchi za magharibi, ni kuwa ujenzi wa viwanda unaleta maendeleo. Lakini katika baadhi ya nchi za Afrika ambako kuna dalili ya maendeleo ya viwanda, viwanda hivyo havijaleta matokeo yanayotakiwa. Mtafiti mshiriki katika taasisi ya elimu jamii ya Akademia ya sayansi jamii ya China CASS Bi. Zhang Qian, alitolea mfano wa Ethiopia na kusema hadi sasa maendeleo ya viwanda katika nchi hiyo hayajachochea maendeleo vijijini, kwa hiyo mtindo huo wa kuhimiza maendeleo ambao ni wa kimagharibi, licha ya kuwa una manufaa yake, si shirikishi vya kutosha na unaleta pengo la maendeleo kati ya maeneo ya nchi.

Mkurugenzi mtendaji wa midahalo ya Kusini-Kusini wa Kenya Bw. Stephen Mwangi, alisema Pendekezo la Maendeleo ya Dunia (GDI) msingi wake ni kuhakikisha maendeleo ya dunia yanakuwa shirikishi, na linaendana na ajenda ya 2063 ya Afrika. Kwa sasa nchi za Afrika zinajitahidi kuhimiza utekelezaji wa eneo la biashara huria (AfCFTA) ambalo kimsingi linataka kuondolewa kwa vizuri vyote vya kibiashara kati ya nchi za Afrika. Bw. Mwangi anaona taasisi za washauri bingwa zinatakiwa kuhakikisha miradi ya ushirikiano inayopendekezwa kati ya pande mbili, ihakikishe kuwa makundi yote kwenye jamii yanashirikishwa kwenye maendeleo ya uchumi.

Kujitokezwa kwa taasisi za washauri bingwa za China na Afrika kwenye kutoa mapendekezo ya kisera kwa ajili ya maendeleo kati ya pande hizi mbili, ni hatua moja ya kujikomboa kiuchumi na kuepuka utegemezi kwa nchi za magharibi. Kwa muda mrefu nchi za Afrika zimekuwa zikipokea sera kutoka nchi za magharibi au mashirika ya kimataifa, ambazo mara nyingi zinaendana na mazingira ya nchi za magharibi. Taasisi hizi za China na Afrika kwa sasa zinafanya tafiti kwenye mazingira ya nchi zao na kuzingatia mahitaji ya maendeleo ya nchi zao.
 
Back
Top Bottom