Taarifa zinachanganya ubinafsishaji wa mabasi ya mwendokasi; kipi ni kipi?

Sitta huyuhuyu aliyejenga ofisi ya Spika Urambo? Sitta huyuhuyu aliyehujumu mchakato wa katiba Mpya Kwa maslahi binafsi ili aje kugombea Urais?

Sitta huyuhuyu yeye na mke wake wote wapo bungeni wanakamuwa Kodi za Watanzania?
Mkuu umeonesha kiwango kidogo sana kwenye kujadili hoja.
Hoja hapo sio Sita alifanya nini ila Sita alisema nini.
Ukitaka yule asiye na kando lolote ndie awe na haki ya hoja yake kujadiliwa hutampata kamwe!
Hata wewe mwenyewe nafsi yako haitaweza kujijadili sabab wewe pia sio msafi
Asiye na hili ana lile!
 
Hizi taarifa zinachanganya!

Tarehe 23 march niliangalia taarifa ya habari, Taarifa zinasema Serikali ina mpango wa kutafta mwekezaji ambaye ataleta mabasi na kutoa huduma kama mzabuni.

Tarehe 25 march katika taarifa ya habari wanasema mzabuni tayali kashaanza kuigiza mabasi! Swali tenda ilitangazwa lini?

Anyway! Wanaendelea kusema Mabasi hayo yatakuwa ya mzabuni hadi pale yatapofikia uchakavu ndipo yatakuwa mali ya serikali. Swali serikali kama imeshindwa kuyasimamia yakiwa mapya watawezaje kuyasimamia watapokabidhiwa yakiwa mabovu?

Huyu mzabuni ni nani? Kwanini mkataba useme mabasi chakavu itakabidhiwa serikali ili iweje?

Waandishi hebu fuatilieni tuwe tunapata taarifa zilizonyooka!
"Black people are not complete human beings because they don't have a good brain to govern the society as White people. They are still under the process of becoming the complete human beings."
Pieter W. Botha, a former President of South Africa during the Apartheid era.

Nafikiri ifike mahali tunatakiwa kumuelewa Botha kwa hicho alichosema. Japokuwa ni chungu lakini tunatakiwa kumeza hivyo hivyo. Hakuna jinsi.
 
Back
Top Bottom