Taarifa za njaa: Waandishi wa vituo vya televisheni muonyesheni Rais hali halisi ilivyo | Page 4 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Taarifa za njaa: Waandishi wa vituo vya televisheni muonyesheni Rais hali halisi ilivyo

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Salary Slip, Jan 11, 2017.

 1. S

  Salary Slip JF-Expert Member

  #1
  Jan 11, 2017
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 25,045
  Likes Received: 37,845
  Trophy Points: 280
  Sitaseme mengi.

  Baada ya Raisi kudai hakuna njaa,nawashauri tembeleeni maeneo mbalimbali na mchukue picha za hali ya mazao mashambani,mifugo wanaodaiwa kufa na mtembelee kwenye masoko.

  Katika kupita kwenu, muhoji wakulima, wafugaji,wafanyabiashara wa mazao na wanaodaiwa kuathirika na njaa.

  Vikwazo vinaweza kuwa ma-DC na ma-RC ila msisahau kuwa kila kazi ina changamoto zake.

  Tulipofika tunahitaji documentary/documentaries.
  ======

  Hoja hii imetumika ktk JamiiLeo
   
 2. Mwana Kwetu

  Mwana Kwetu JF-Expert Member

  #61
  Jan 11, 2017
  Joined: Jul 12, 2011
  Messages: 617
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 60
  Msaidieni huyu PhD holder naona kila kitu kwake ni siasa. Hii ni serious kwani anakataa ukweli wa wazi. Kama hamna njaa Kwa nini debe la mahindi linauzwa 20'000 na gunia la mahindi 100000 hadi 120000. Atuambie hii inasababishwa na nini. Je ngombe walioonyeshwa kwenye TV wamekufa Kwa kitu Gani?
   
 3. Mwana Kwetu

  Mwana Kwetu JF-Expert Member

  #62
  Jan 11, 2017
  Joined: Jul 12, 2011
  Messages: 617
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 60
  Ngombe hawafi kila mwaka acha Ku support ujinga na tumia akili bora unyamaze. Mimi ni mkulima pia Kwa miaka 15 Sasa. Msimu wa kilimo 2016 nililima 12 acres za yellow beans lakini mvua haikutosha na sikupata hata gunia 2 za maharage. Haijawahi tokea hivyo miaka almost 10. Na wote tuliolima mi ndio nilivuna kwani wengine waliambukia majani ya ngombe. Am talking about Arusha. Funga mdomo kama hujui
   
 4. b

  bne JF-Expert Member

  #63
  Jan 11, 2017
  Joined: Oct 11, 2016
  Messages: 1,507
  Likes Received: 1,496
  Trophy Points: 280
  Ndg inaonekana umezoea kura kwa jirani ndio maana huoni shida kutokupika si jirani yupo?
   
 5. b

  bne JF-Expert Member

  #64
  Jan 11, 2017
  Joined: Oct 11, 2016
  Messages: 1,507
  Likes Received: 1,496
  Trophy Points: 280
  Kwa
  Kwa hiyo hata wale wananchi waliomsimamisha mkuu wa mkoa na kulia njaa walitumwa na matajili?
   
 6. M-mbabe

  M-mbabe JF-Expert Member

  #65
  Jan 11, 2017
  Joined: Oct 29, 2009
  Messages: 4,994
  Likes Received: 3,744
  Trophy Points: 280
  usiseme hivo ndugu.

  ile ndoto ya mheshimiwa Lema usiipuze!
   
 7. mzamifu

  mzamifu JF-Expert Member

  #66
  Jan 11, 2017
  Joined: Mar 10, 2010
  Messages: 3,497
  Likes Received: 854
  Trophy Points: 280
  Mkuu ng'mbe wakishakosa chakula hukonda na hawana bei. kwanza anayenunua anawalishia wapi? pia kulima ni kujipanga si sawa na kurusha jiwe!
   
 8. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #67
  Jan 11, 2017
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 31,819
  Likes Received: 36,936
  Trophy Points: 280
  Waandishi wa habari wategemee kuweka jela kwa amri za wakuu wa wilaya na wakuu wa mikoa ambao habari za maeneo yao yenye njaa yakitangazwa.
   
 9. Ngushi

  Ngushi JF-Expert Member

  #68
  Jan 11, 2017
  Joined: Jul 8, 2016
  Messages: 5,873
  Likes Received: 10,568
  Trophy Points: 280
  wapi huko sisi wafugaji tuhamie huko ambako mpaka sasa mvua zinanyesha na nyasi zipo?
   
 10. U

  UWOGA=UMASKINI JF-Expert Member

  #69
  Jan 11, 2017
  Joined: Dec 30, 2013
  Messages: 1,831
  Likes Received: 383
  Trophy Points: 180
  Napata Shida kufikiri
   
 11. m

  mtoto wa maskini JF-Expert Member

  #70
  Jan 12, 2017
  Joined: Jun 28, 2013
  Messages: 1,154
  Likes Received: 549
  Trophy Points: 280
  mpaka 2025 ? duh hii hatari
   
 12. W

  Wamweru Senior Member

  #71
  Jan 12, 2017
  Joined: Jul 29, 2015
  Messages: 115
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 45
  Hivi njaa ya mwaka huu imesababishwa na nini? je ni kweli kwa sababu ya mvua hakuna au kwa ajiri ya wabunge wetu waliruhusu mazao kuuzwa nje? ninavyojua mm ni kuwa hata kama mvua ingenyesha kama kawaida leo hii mazao yangekuwa bado shambani sasa watu wanaposema kutokunyesha mvua ya kutosha kumeleta njaa sielewi sana, ila ukiniambia kuwa kutakuwa na njaa msimu huu nitakuelewa maana hakutakuwa na mavuno ya kutosha
   
 13. Kalamu Yangu

  Kalamu Yangu JF-Expert Member

  #72
  Jan 12, 2017
  Joined: Dec 21, 2016
  Messages: 1,035
  Likes Received: 883
  Trophy Points: 280
  Vyovyote itavyokuwa, si jambo la kushabikia....
  Nikikumbuka mahindi ya 'Yanga' najikuta naumia sana njaa ni zaidi ya utumwa na mateso....  Dunia Uwanja wa Fujo
   
 14. T

  Tabby JF-Expert Member

  #73
  Jan 12, 2017
  Joined: Jan 8, 2008
  Messages: 9,902
  Likes Received: 5,543
  Trophy Points: 280
  Hakuna sababu ya kufanya hivyo.
  Mheshimiwa raisi ameshajibu yote.
  Vituo vinavyotangaza njaa, vimenunuliwa na wafanyabiashara, njaa hakuna.
  Wafugaji wanaolia mifugo inakufa kwa ajili ya ukame, wauze mifugo wapate fedha za kununulia mahitaji ya familia pamoja na chakula.
  Wakulima wanaolia mavuno hakuna, walipashwa kujua mapema kwamba mwaka huu mvua hakuna hivyo wangelima mazao yanayostahimili ukame.
  SERIKALI HAITATOA CHAKULA CHA MSAADA KWA MTU YEYOTE.

  Ninaomba watanzania tutembee pamoja na raisi katika maono yake. Mabishano hayatatusaidia kuokoa watu wetu wanaokufa na njaa, na wala tusitegemee kuna hali yoyote inaweza kumshawishi Mheshimiwa raisi kubadili msimamo wa serikali kwa kuwa ninaamini, anachokitamka, kinakuwa kimefanyiwa uchunguzi na uchambuzi wa kina na ndiyo maana kinatangazwa kama msimamo wa serikali.

  Pengine jambo ambalo ningelishauri lifanyike, Serikali sasa isaidie kutoa taarifa namna hawa Watanzanai waliozembea hadi wakapata njaa, watapata wapi chakula cha kununua. Serikali hapa ianze kuapkua chakula kutoka katika maghala yake na kuwafikishia karibu wananchi kwa utaratibu mzuri, ambapo WATANUNUA CHAKULA HICHO NA WASIDAI KUPEWA BURE KWA KUWA SERIKALI IMESEMA HAITOI CHAKULA CHA MSAADA.

  Mheshimiwa raisi awawajibishe wakuu wa Wilaya katika wilaya ambazo zina njaa kwa kuwa walpashwa kujua na kuhimiza watu kulima mazao sahihi kulingana na hali ya hewa. Vinginevyo vyeo vya wakuu wa wilaya vifutwe kwa kuwa havina faida kwa taifa.
   
 15. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #74
  Jan 12, 2017
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,928
  Likes Received: 83,495
  Trophy Points: 280
  Mkuu umeshawahi kusikia la kuvunda halina utani?
  Tuna tatizo nchini tena si dogo.

   
 16. T

  Tabby JF-Expert Member

  #75
  Jan 12, 2017
  Joined: Jan 8, 2008
  Messages: 9,902
  Likes Received: 5,543
  Trophy Points: 280
  Tanzanai ina misimu mbali mbali ya mavuno . Kuna sehemu wanaanza kvuna mapemba kabla ya Krismasi wakati sehemu zingine ndiyo wanapanda.

  Uuzaji wa mazao ya chakula nje ya nchi unachangiwa na serikali kushindwa kuandaa masoko bora ya ndani yenye tija kwa mkulima. Aidha bei za mazao ya mkulima kutokuwiana na gharama za uzalishaji pamoja na mfumo wa ununuzi usioendana na muda wa mahitaji ya fedha kwa huyo mkulima. Bado Watanzania wanahitaji sera na uelekezi sahihi katika masuala yote.

  Nitatoa mfano, mkulima anahitaji fehda za ada ya mtoto, au ana mgonjwa anahitaji matibabu, ama anahitaji kuezeka nyumba kabla ya msimu mwingine wa mvua kwa mathalani. Soko lililopo ndani linalipa fedha ndogo kwa kuwa ni wakati wa mavuno mazao yako mengi, lakini pia halipwi taslimu anakopwa kwa muda usiojulikana, na wakati wa malipo ukifika, kuakuwa na mabadiliko ya bei kwa kile kinaitwa eti kampuni imekuta bei ya bidhaa hiyo katika soko la dunia inakouza imeshuka. Muda wa malipo haujulikani anaweza kulipwa musimu mwingine kabisa wa mavuno.

  Mkulima huyu, atawezaje kulipa ada za mwanae aende shule kwa muda muafaka? Huyo mgonjwa atamfanyaje ili afya yake iendelee kusubiri malipo ya mazao yaliyokopwa ili akatibiwe? Wakati akisubiri fehda hizo ili aenzeke nyumba, familia yake inakuw ainaishi kwa naman gani? Kabla hatujawalaumu wakulima kuuza nje mazao, ni vyema tukajiweka mahala pao kwanza.

  Lakini all in all, hawa watu wentu wanahitji kula na kuishi. Wapelekewe chakula na bei idhibitiwe ili waweze kununua chakula hata kama hakitatolewa bure kama serikali ilivyotamka. Mengien yatafuata lakini tuokoe uahi wao kwanza.
   
 17. S

  Salary Slip JF-Expert Member

  #76
  Jan 12, 2017
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 25,045
  Likes Received: 37,845
  Trophy Points: 280
  Mkuu mimi nasema katika hili muda ndio utaongea kama tulivyoona kwenye sukari na mambo mengine.
   
 18. b

  bagamoyo JF-Expert Member

  #77
  Jan 12, 2017
  Joined: Jan 14, 2010
  Messages: 4,542
  Likes Received: 2,119
  Trophy Points: 280
  Southern Africa Food Crisis
  Published on 23 Nov 2016
  Southern Africa has experienced its worse drought in years as a result of El Nino. The drought has destroyed crops and harvests leaving 28 million people in need of emergency food assistance. Malawi is one of the hardest hit countries. Maize production is down 12.4% and prices have gone up 40% in some areas. The hunger crisis could grow worse in coming months as the hard-hit countries of Malawi, Mozambique, Madagascar and Zimbabwe are entering the lean months--6.5 million people(39% of the population) will not have enough food stocks to live on in Malawi alone. CARE CEO Michelle Nunn traveled with journalist Mike Cerre to report on how the drought is impacting the people of Malawi. Learn more by visiting http://www.care.org

  Source: CARE
   
 19. b

  bagamoyo JF-Expert Member

  #78
  Jan 12, 2017
  Joined: Jan 14, 2010
  Messages: 4,542
  Likes Received: 2,119
  Trophy Points: 280
  January 11, 2017
  Nairobi, Kenya

  Several regions to experience drought: Authority

  Several regions in Kenya will experience drought, according to the National Drought Management Authority.

  This has been attributed to depressed rainfall during the short rains season that occurs around December in most parts of the country as a result of which several regions that experienced drought last year could not recover.

  A report by the authority titled “National Drought Early Warning Bulletin”, which contains data collected up to December 26, indicated that food shortage would continue to worsen in the coming months.

  Source: DailyNation November 2016
  This also follows reports from the weatherman that there is no prospect of rains in the country. particularly in arid and semi-arid areas until at least March or April.

  The situation is especially dire in Garissa, Isiolo, Kilifi, Lamu, Mandera, Marsabit, Samburu, Tana River, Turkana and West Pokot counties, with the agency asking authorities to be on alert for worsening conditions.

  On Wednesday, Devolution and Planning Cabinet Secretary Mwangi Kiunjuri told the Nation that the government was working day and night to address the situation.

  He said ministries of Devolution, Health, Environment, Treasury, Agriculture, Education and Interior would meet and a collective statement would be issued on Thursday.

  “We have set up a committee to address this issue and all those relevant ministries affected have agreed to work together. We also plan to invite governors from 23 counties which are affected to come dialogue with us on Monday on how to solve the issue,” said Mr Kiunjuri.
  Source: Several regions to experience drought: Authority

  Source: NTV Kenya January 4, 2017
  N.B
  Kenya, Malawi, Mozambique, Madagascar n.k wanakabiliwa na upungufu wa mvua na hivyo tishio la njaa. Tanzania imezungukwa kijiografia na nchi hizo je ni kweli hakuna tishio la njaa?
   
 20. jaji mfawidhi

  jaji mfawidhi JF-Expert Member

  #79
  Jan 12, 2017
  Joined: Feb 20, 2016
  Messages: 3,439
  Likes Received: 2,561
  Trophy Points: 280
  Waandishi wa Aljeera na BBC ndio wanaweza kuja kufanya kipindi na kuonyesha jinsi njaa ilivyo,Natamani pia DW wafanye hivyo!
   
 21. Mwasita Moja

  Mwasita Moja JF-Expert Member

  #80
  Jan 12, 2017
  Joined: Dec 31, 2015
  Messages: 2,908
  Likes Received: 2,548
  Trophy Points: 280
  Tuliosema lowasa ni fisadi ni sisi Mbowe, Lisu, Lema, Mnyika, Msigwa na ushahidi tunao.

  Kama Lowasa anabisha atangulie mahakamani
   
Loading...