Mamlaka ya hali ya hewa Tanzania (TMA) yatahadharisha ujio wa ukame, njaa

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,899
MAMLAKA ya hali ya hewa hapa nchini (TMA), imewaonya wananchi juu ya ukame na baa la njaa, ambavyo huenda vikalikumba taifa kutokana na kukosekana kwa mvua katika maeneo mengi ya nchi kati ya mwezi Oktoba na Desemba mwaka huu, anaandika Charles William.

Akizungumza na wanahabari leo, Dk. Agness Kijazi, Mkurugenzi Mkuu wa TMA amesema, kutokana na kukosekana kwa mvua kati ya Desemba na Oktoba mwaka huu katika maeneo mengi ya nchi, migogoro baina ya wakulima na wafugaji pia itaongezeka.

“Mvua zinatarajiwa kuchelewa kuanza na zikianza zitakuwa chini ya wastani, wakulima wanashauriwa kuandaa mashamba na pembejeo mapema na wazingatie ushauri wa maafisa kilimo kwa kuwa waangalifu katika kuhifadhi akiba ya chakula waliyonayo,” amesema.

Dk. Kijazi pia ametahadharisha kuwa, huenda kukosekana kwa mvua hizo kukasababisha upungufu wa maji katika mabwawa yanayozalisha umeme na hivyo kuathiri uzalishaji na upatikanaji wa nishati hiyo muhimu.

“Matukio ya migogoro baina ya wakulima na wafugaji yanatarajia kujitokeza pia kutokana na uhaba wa maji na malisho kwaajili ya mifugo na hata wanyama pori hivyo mamlaka zinazozunguka jamii husika zijiandae kuchukua hatua stahiki,” Dk. Kijazi amesisitiza.

Utabiri huo wa TMA, umeonyesha kuwa mikoa ya Singida, Dodoma, Morogoro, Kigoma, Rukwa, Katavi na Tabora ndiyo inayotarajiwa kukumbwa na uhaba wa mvua zaidi na hivyo wananchi wa mikoa hiyo wametakiwa kuchukua tahadhari.

Hata hivyo, katika mikoa ya pembezoni mwa Ziwa Victoria, ikiwemo Mwanza, Kagera, Shinyanga, Musoma, Simiyu na Geita pamoja na mikoa ya Kusini mwa nchi, Lindi na Mtwara, mvua zinatarajiwa kuwepo kwa kiwango cha kuridhisha.

Mbali ya ukame na migogoro ya wakulima na wafugaji, TMA imetahadharisha kuwa, athari nyingine ya kukosekana kwa mvua hizo itakuwa ni mlipuko wa magonjwa kutokana na uhaba wa maji salama sambamba na matumizi mabaya ya mifumo ya majitaka katika miji.

Itakumbukwa kuwa, mwezi mmoja uliopita, Rais John Magufuli akiwa katika ziara ya kikazi katika mikoa ya Kanda ya Ziwa, alitangaza kuwa serikali haitatoa chakula cha msaada kwa wananchi watakaokumbwa na tatizo la njaa kwa mwaka huu.

Chanzo: Mwanahalisi


========




TAARIFA KWA UMMA JUU YA UPUNGUFU WA MVUA NA UKAME UNAOWEZA KUIATHIRI NCHI YETU

Kaimu Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Hali ya Hewa, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Usalama wa Chakula, Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Wanahabari, Mabibi na Mabwana, Awali ya yote karibuni sana katika ukumbi huu Ofisi ya Waziri Mkuu. Nia ya kuwaiteni nyote hapa, ni kuwapatia utabiri wa hali ya hewa kwa kipindi cha miezi mitatu ambayo ni mwezi huu wa Oktoba, Novemba na Disemba, athari zitakazojitokeza na hatua za kuchukua kupunguza madhara ya athari hizo.

Ndugu wanahabari,

Katika mkutano wa leo, nimeambatana na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa (Dr. Paschal Waniha, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Usalama wa Chakula – Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi MaryStela Mtalo, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa atazungumza utabiri wa msimu, Mkurugenzi wa Idara ya Uratibu wa Maafa nitatoa Tahadhari na hatua za kuchukua na Mkurugenzi wa Idara ya Usalama wa Chakula ataeleza hatua stahiki za kuchukua ili kujilinda zaidi na usalama chakula.

Ndugu wanahabari, nichukue fursa hii kumkaribisha Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Hali ya Hewa atupatie utabiri wa msimu na hali ilivyo sasa.

Mamlaka ya Hali ya Hewa

Muelekeo kwa Msimu wa Mvua kwa kipindi cha Octoba - Disemba kama ilivyotolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa tarehe 05 Septemba, 2016 ni kama ifuatavyo:-
  • Kwa miezi ya Octoba hadi Disemba, 2016 mvua chache zinatarajiwa katika maeneo mengi ya Nchi, wakati maeneno ya pembezoni mwa Ziwa Victoria pamoja na yale ya Kusini mwa nchi mvua zinatarajiwa kuwa za kuridhisha
  • Katika maeneo mengi nchini Mvua zinatarajiwa kuchelewa kuanza. Aidha, Mvua hizi zinatarajiwa kuanza katika Ukanda wa Ziwa victoria na pia katika maeneo machache ya Pwani ya kaskazini katika mwezi Oktoba, 2016.
Hali ilivyo sasa,
  • Tathmini ya Mifumo ya Hali ya hewa inaonesha uwepo wa La-Nina hafifu katika eneo la bahari ya Pacific.
  • Kwa maeneo yanayopata mvua mara mbili kwa mwaka, msimu wa mvua umeanza katika maeneo machache ya ukanda wa ziwa Victoria japo mvua hizo bado ziko chini ya wastani kwa sasa na mtawanyiko wake sio wa kuridhisha. Hali hiyo pia inatarajiwa kujitokeza katika maeneo mengi ya nchi hususan katika miezi ya Oktoba na Novemba.

Athari zinazoweza kujitokeza

Kutokana na Utabiri huu, tahadhari zifuatazo zinaweza kujitokeza:-

  • Vipindi virefu vikavu ndani ya msimu wa mvua vinatarajiwa kusababisha unyevunyevu mdogo katika udongo na hivyo kupelekea kuathiri ustawi wa mazao ya kilimo katika maeneo mengi ya nchi
  • Kutokana na mtiririko mdogo wa maji vina vya mito na mabwawa vinatarajiwa kupungua kutoka katika hali yake iliyopo katika msimu wa vuli, 2016 kutokana na mvua chache zinazotarajiwa katika maeneo mengi
  • Milipuko ya Magonjwa inaweza kujitokeza kutokana na Uhaba wa maji salama na matumizi mabaya ya mifumo ya maji taka katika miji
  • Uhaba wa malisho kwa mifugo na wanyama unatarajiwa katika maeneo mengi ya nchi kutokana na kupungua kwa maji katika ma bwawa na visima.

URATIBU WA MAAFA

Kutokana na utabiri huo Ofisi ya Waziri Mkuu – Idara ya Uratibu wa Maafa inatoa tahadhari kwa Wizara , Taasisi za Kiserikali, Mamlaka za Mikoa na wadau wengine wa usimamizi wa maafa kuchukua hatua muhimu ili kukukabiliana na athari hizo.
    1. Kulima mazao ya muda mfupi na yanayostahimili ukame,
      Kuhifadhi chakula vizuri
    2. Kuzuia matumizi ya nafaka kutengenezea pombe
    3. Aidha wananchi wahimizwe kuweka akiba ya chakula cha kutosha hasa kwa maeneo yatakayopata mvua chini ya wastani
    4. Kuchimba au kukamilisha na kukarabati mabwawa na malambo kwa ajili ya kuvuna maji ya mvua
    5. Hospitali na Zahanati zijiandae kukabiliana na magonjwa ya mlipuko endapo yatatokea
    6. Wafugaji wanashauriwa kuhifadhi chakula kwa ajili ya malisho ya mifugo, kuvuna mifugo ikiwa katika hali nzuri kiafya ili kupunguza idadi/kundi kubwa la mifugo kipindi cha uhaba wa malisho, na kuipatia mifugo chanjo.
    7. Maofisa Ugani kutoa ushauri kwa wakati kuhusu mazao ya kupanda
    8. Udhibiti wa usafirishaji holela wa mazao ya chakula nje ya nchi
IDARA YA USALAMA WA CHAKULA

Kutokana na utabiri huu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa na Maelekezo ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Idara ya Usalama wa Chakula inatoa utafanya yafuatayo:-
    1. Kitengo cha usalama wa Chakula Sehemu ya Uratibu wa Mazao na Tahadhari ya Njaa kitafanya kazi ya uratibu, ufuatiliaji, ukusanyaji na utoaji wa tarifa ya chakula nchini kwa wakati
    2. Wakala wa Taifa Hifadhi ya Chakula wanaelekezwa kununua na kuhifadhi akiba ya chakula cha kutosha kukabiliana na upungufu kutoka kwenye maeneo yenye ziada mapema
    3. Bodi ya Nafaka na Mazao mchanganyiko wanaelekezwa kununua mazao ya wakulima kwa wingi ili kuongeza wigo wa biashara na soko la mazao ya wakulima sambamba na kuyaongezea thamani

    4. Mikoa na Halmashauri zake zisimamie na kuimarisha mifumo ya kuhifadhi chakula baada ya mavuno ili kupunguza upotevu wa chakula na kuhakikisha upatikanaji wa chakula wakati wote
    5. Taasisi husika zihamasishe uwekezaji katika viwanda vya usindikaji wa mazao ili kuyaongezea thamani

    6. Mikoa na Halmashauri zake zihamasishe na kufuatilia kwa karibu akiba ya chakula kwa wafanyabiashara ili kuwezesha kupata takwimu sahihi za kiasi cha chakula kilichopo nchini
    7. Tathmini ya kina ya hali ya chakula na lishe itafanyika mapema ili kubaini kaya zitakazoathirikia na kupendekeza hatua stahili za kuchukua
HITIMISHO

Ofisi ya Waziri Mkuu inawashauri watumiaji wote wa taarifa za hali ya hewa ikiwa ni pamoja na wakulima, Wafugaji, Mamlaka za Wanyamapori, Mamlaka za Maji na Afya wafuate ushauri wa wataalamu wa sekta husika.
 
Naona mungu anatuongezea adhabu nyingine hii ameona haitutoshi mimi uwa sijaribiwi
 
TMA acheni uchochezi. Sisi tunataka tuwapunguze vijana huku mjini waende kulima, sasa nyie mkisema mwaka huu kuna ukame si mtarudisha nyuma juhudi hizi?
 
Kwenye tafsiri ya kiroho ina maana gani?
Je ni ile peku peku ya Nabii mwenye mbawa?
Je ni lile bao la mkono?
Je ni dhikaha ya kutaka kuombewa?
Ukiandika sana unaweza kujikuta shimo la tewa hapa ndani au kule nje!
 
Katika hali isiyo kuwa ya kawaida leo mkurugenzi wa mamlaka ya hali ya hewa, ametangaza kutokea bala la njaa. Hi ni kwasababu ya kutonyesha kwa mvua za kutosha,

Sasa rais alisema....Serkali yake haitatoa msaada wa chakula.

Mungu atuma salamu ikulu, na kumueleza kuwa, "Hili ni taifa langu na si la kwako magufuli. Usiwatishia kufa wale watakao kosa chakula, kwani kuna sababu nyingi ikiwemo ya kutonyesha mvua za kutosha"
 
Katika hali isiyo kuwa ya kawaida leo mkurugenzi wa mamlaka ya hali ya hewa, ametangaza kutokea bala la NJAA. Hi ni kwasababu ya kutonyesha kwa mvua za kutosha,

SASA RAIS ALISEMA....SERKALI YAKE HAITATOA MSAADA WA CHAKULA.

MUNGU ATUMA SALAMU IKULU, NA KUMUELEZA KUWA, "HILI NI TAIFA LANGU NA SI LA KWAKO MAGUFULI. USIWATISHIA KUFA WALE WATAKAO KOSA CHAKULA, KWANI KUNA SABABU NYINGI IKIWEMO YA KUTONYESHA MVUA ZA KUTOSHA"
Wewe kama kubwa ujinga vileee! Sijui nakufananisha!
 
Wakuu wa wilaya wajiandae kujiuzulu serikali haina chakula cha msaada fanyeni kazi.Kazi kucheza pool tu.Asiyefanya kazi asile.Msema kweli ni mpenzi wa mungu.
 
Back
Top Bottom