Taarifa za njaa: Waandishi wa vituo vya televisheni muonyesheni Rais hali halisi ilivyo

Yuko kwenye mhimili uliojikita Zaidi kuliko mihimili mingine, kituo cha luninga kitakacho tangaza njaa kitafungiwa na kunywng'anywa leseni.

Madam ivi zika vile vimelea vipi kuna harufu au ulikuwa uzushi wa yule mtu kama tulivoaminishwa
 
Kwa kawaida majanga yanapotokea wapo wanaofurahia na wengine kuhuzunika. Wapinzani katika hili la njaa ya ukame mnalitumia kisiasa zaidi kwa malengo yenu binafsi

Lizaboni;
Hao wapinzani wana kitu gani na wewe?? Huko uliko hakuna njaa?? Kwani wapinzani wanasema uongo?? Angalieni jamani, msijemletea laana mh rais wetu.
Kitu kinachosemwa hapa ni kuhusu hali ya chakula nchini. Asiseme tu hakuna njaa, aseme serekali pendwa imehifadhi tani kadhaa kwenye ghala la taifa. Iseme, itatoa kiasi gani kwa ajili ya kukidhi soko chakula kisipungue. Iseme kuwa ina data za nani kaweka wapi mahindi na nafaka zingine ili serekali izinunue na kuzihifadhi. Tusijifariji kwa maneno. Sukari mlitoa bei elekezi, mkashika na za kwenye magodawni, sukari mbona imepaa?? Sidhani kuwa kwa mtindo huu sembe itashuka 1700/= ilipofikia. Wapinzani hawakuweka bei hii
 
Watakaokufa njaa ni haohao wa Chato na Kanda ya Ziwa. Hapo ndo atapata akili..
 
Hizi taarifa za njaa hata kama ni kweli wewe zinakunufaisha nini. Kama una hio taarifa basi chukua hatua binafsi na sio kuichukulia kisiasa kama unavyofanya. Magufuli yupo mpaka 2025 ije mvua lile jua. Tatuta eneo kalime! Hao wafugaji wakiuza Ng'ombe watano tu wanauwezo wa kuchimba kisima na kuweka solar wanapata maji mwaka mzima kunywesha mifugo
Hivi wewe kichwani umejaza ubongo au usaa?! Ukubwa ni jalala, njaa, ukame, tetemeko, maradhi ya mlipuko, kama kuvamiwa yote ni msalaba wa kiongozi mkuu! Lazima aambiwe na kupewa taarifa kwa njia yoyote ile ili achukue hatua, ndio maana tulimchagua! Mficha maradhi kilio humfichua! Maisha ya wananchi, Watanzania masikini anaojinasibu kuwatetea kila siku yako kitanzini rais lazima aambiwe, ndio wajibu wake wa msingi, kulinda na kuwatetea watanzania katika hali kama hiyo. Wacha ukasuku, wacha umbumbumbu!
 
Tanzania ina njaa tangu enzi za mababu, tajeni ni mwaka gani ulikuwa na neema zaidi, kama Arusha mifugo inakufa kwa ukame kila mwaka sasa sijui mwaka huu nini kipya????
Kwani wamesema huu ndio mwaka pekee wa ukame?

Fungeni na TMA kwanini iwepo wakati inajulikana msimu fulani ni wa mvua nk
 
Sawa uzuri alisema kila mtu abebe mzigo wake mimi nadhani kila mtu afe kiume ,hata ukikosa msosi wewe komaa kiume
 
Msipotoshe watu hata sisi vijijini mifugo wanakufa ni kweli lakini si mwaka huu tu hili jambo hujitokeza kila mwaka haswa ikifika kipindi cha mifugo kubadilisha majani yaani kutoka majani makavu ya kiangazi kwenda majani mabichi ya masika
Sasa isiwe habari kwamba eti ni kwasababu ya njaa huo ni unafiki msimdanganye rais
Taarifa mnazozitoa kwenye vyombo vya habari vina lengo la kupotosha ihalisia wa mambo ili matajili wanaowatuma wajinufaishe kibiashara kupitia misamaha ya kodi wezi wakubwa nyie
Kamati za maafa zipo mpaka ngazi ya kijiji wao wanawajibika kutoa taarifa kwa ngazi ya wilaya ili uchunguzi ufanyike kujua mahiyaji
Hatuwezi kutumia wandishi wa habari makanjanja kupotosha umma kwa maslahi ya wafanya biashashara
 
Muda ndio kiboko yenu
 
16 Reactions
Reply
Back
Top Bottom