El Roi
JF-Expert Member
- May 29, 2020
- 263
- 502
Moja ya mawaziri wazuri wachapa kazi ktk awamu hii ni Dorothy Gwajima na Ummy Mwalimu.
Uchapakazi wao ni makini na wanaooneka wanapenda kazi. Yaani, wanaishi Ili wafanye kazi, na siyo wanafanya kazi Ili waishi. (They live to work and not work to live).
Kwa maana ya kuongezea thamani uchapakazi wao na hivyo kuongeza ufanisi katika wizara tajwa, yangefanyika mabadiliko, ya kiufundi kwa maana ya kubadilishana wizara.
Dorothy Gwajima ni daktari wa binadamu kitaaluma na juu ya hapo ni mahiri( specialist) kwenye masuala ya utawala wa afya (Masters in Public Healthy). Ukimuona huyu mama kwa maana ya taaluma, amesheheni Kila kitu kinachohitajiwa na wizara hii. Yaani utaalamu (expertise) wenyewe, na component ya utawala wa ki- tiba.
Na kwa haiba yake ya ukali kiasi na ufuatiliaji( Aggressiveness) angesaidia sana, wizara hii kufanya vizuri zaidi, maana anazijua corridor zote zilizoko kwenye "utabibu".
Na kwa kuwa ni mfuatiliaji na mkali kiasi, issue za uzembe, kujificha kwenye taaluma wakati unafanya makosa na vitendo vya rushwa,vingepungua kama siyo kuporomoka kwa kiwango kikubwa.
Kwa ajili ya ufanisi mkubwa huyu mama, ikimpendeza Rais basi apelekwe wizara hii.
Kwa Ummy Mwalimu, wizara ya maendeleo ya jamii, jinsia, wanawake na watoto ilikuwa wizara hasa inayomfaa kwa maana ya anakotoka na utaalamu wake( background).
Huyu ni mwanasheria na mwanaharakati ambaye aligeuka kuwa mwanasiasa.
Kabla ya kuwa mwanasiasa alijihusisha sana na mambo ya utetezi wa jamii katika maeneo mbalimbali.
Kwa kuwa Kuna hitaji kubwa la kuwa na Sheria zinazoendana na wakati na hasa kwa kuifanya jamii kuwa sawa katika makundi mbalimbali ya jamii, component ya Sheria ambayo mama huyu anayo, ingeweza kusaidia sana.
Na kwa kuwa taaluma yake ni Sheria, kusukuma mambo katika wizara hii ingekuwa rahisi maana ana jicho tayari la kujua kinachopaswa kufanyika kwa sababu ya ujuzi wake wa Sheria.
Wakati huu Kuna uhitaji mkubwa wa haki za watu na utetezi wa makundi maalumu. Background yake ya uanaharakati (Activism) ungesaidia sana kusukuma mambo na hivyo kuifanya wizara hii iyafikie malengo yake haraka.
Nimuonavyo huyu mama akiwa kwenye uga anaouelewa vizuri kama hivi wa sheria na utetetezi wa haki za watu ataifanya kazi hiyo kwa raha.
Kuwabadilisha hawa akimama wachapa kazi Ili wakae kwenye wizara ambazo zinaendana na asili yao ya utaalamu ( expertise) ni kama kumchukua Samaki na kumrudisha majini. ( Utafanya aishi kwa raha na kujitanua).
Kama itawapendeza wenye mamlaka walione hili kwa jicho kama langu na hakika wizara hizi zitapaa sana na nchi itajengwa vema kwa maana hiyo.