Taarifa ya kukosekana kwa umeme kwenye baadhi ya mikoa Nchini

Sildenafil Citrate

JF-Expert Member
Jan 29, 2021
573
2,553
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linawataarifu wateja wake kukosekana kwa huduma ya umeme kulikosababishwa na upungufu wa kina cha maji kwenye vyanzo vyetu vya Kihansi na Pangani pamoja na hitilafu iliyotokea kwenye vituo vya Kinyerezi I na Songas leo, Jumanne, Septemba 13, 2022.

Hitilafu hii imesababisha baadhi ya maeneo ya mikoa ya Pwani, Dar Es Salaam, Morogoro, Singida, Tanga, Kilimanjaro, Arusha, Njombe, Ruvuma, Songwe, Iringa, Shinyanga, Tabora, Dodoma, Geita, Mara, Manyara, na Simiyu kukosa huduma ya umeme.

Jitihada za kiufundi zinaendelea kufanyika ili kuhakikisha hitilafu iliyojitokeza inatatuliwa haraka iwezekanavyo. Aidha, tutatoa taarifa mara huduma ya umeme itakaporejea.

Shirika linaomba radhi kwa usumbufu wowote unaojitokeza.

IMETOLEWA NA KURUGENZI YA MAWASILIANO NA UHUSIANO KWA UMMA, TANESCO MAKAO MAKUU.

SIMU
: +255 748 550 000

68145687-8D4E-4330-A4E7-8A46D32B8A3F.jpeg
 
View attachment 2355492
Wakupe na Units za bure
 
Ushaona watu ambao hatujivunii kabisa nchi yetu??? Ndo sisi sasa Watanzania sometimes mtu una-wish ni heri ungezaliwa nchi za Somalia uamue moja kuwa unashika mtutu au ufe kikondoo.... written from bottom of my heart nachukia ufanyaji kazi wa viongozi wetu.
 
Sababu ya hii migao yao kutoaminika, huwa panatokea kauli kinzani toka kwa wataalam wanaoendesha na kusimamia hayo mabwawa, hawa Tanesco siku hizi wamegeuka kama wanasiasa tu, hasa wakati huu ambao nchi iko mikononi mwa watoto wa mjini, ndio hawaaminiki kabisa.
 
Back
Top Bottom