Taarifa ya CHADEMA kuhusu kesi ya Leticia Nyerere

Naomba ututajie ili nao tuwajadili hapa

1.Hivi Emmanuel Nchimbi anaishi Songea?Hilo huoni kama ni tatizo?
2.Hvi John Komba anaishi Mbinga?
3.Hivi Jenista Mhagama anaishi Peramiho?
4.Abdalah Mtutura anaishi Tunduru?
Jadili hawa pia.Huko Masaki wanakoishi wanawawakilisha kina nani?Masaki hawana Mbunge hadi wao waishi uhamishoni?Huku kwingine ni kwa sababu hakuna Supermarket.
 
"The above case was heard today 05/22/2012 by Judge R. Russel Sadler..."

Taarifa ya CHADEMA imetolewa tarehe 13 Mei 2012.

Kwi kwiii hii nayo kali? Mnyika toa maelezo please.

Vinginevyo tutaamini CDM mlikuwa tayari na hukumu ya Judge Russel hata kabla ya kusomwa, kama vile CCM walivyo na hukumu ya Mnyika hata kabla ya kusomwa leo!
 
- Unajua kama chama kuwa na msimamo wa kutotaka watoto wa viongozi kuwa viongozi, unless wameingia chama chako ni very dangerous, niamini ninajua ninachokisema ila inasikitisha sana!

William.

Nafikiri hakuna chama cha siasa kinachobagua wanachama wake kwa misingi ya katiba na kanuni za uendeshaji chama; Bali kuna viongozi wa vyama wanaopindisha taratibu za chama kwa madhumuni ya kuwapa uongozi watoto wao au watoto wa jamaa zao. Mambo haya tumeyashuhudia CCM; watoto wa wakubwa wamekuwa wakipewa nafasi kwa upendeleo. Mifano ni mingi...January makamba kwa pendelewa unaibu waziri kwa sababu baba yake alikuwa katibu mkuu. Hussein Mwinyi kapewa uwaziri wa wizara ya afya wakati ni mzanzibari na afya si miongoni mwa mambo ya muungano
 
Hawa CDM siku zote ndio huwa wanapinga watoto wa viongozi kushika madaraka. Sasa nashangaa ndani ya CDM majina ya Nyerere yametawala.

Kwa iyo unataka kusema leticia ni mtoto wa nyerere?? Think the big picture green guard.
 
- Unajua kama chama kuwa na msimamo wa kutotaka watoto wa viongozi kuwa viongozi, unless wameingia chama chako ni very dangerous, niamini ninajua ninachokisema ila inasikitisha sana!

Nafikiri sasa ni muhimu kwa CHADEMA kuondoa hii sintofahamu KUHUSU makazi ya Leticia....suala ambalo ndilo limezua mjadala mkubwa.......

Back to the @W.J. Malecela nafikiri hajafikiri sawasawa.....Hebu mwangalie mtu kama Vicent Nyerere suluba za kisiasa alizopitia kwenye jimbo la Musoma mjini (siasa za huko si lelemama...nimezaliwa huko nazifahamu)..kwa hiyo kwa yeye kuwa hapo alipo ni haki isiyo hojiwa.....

Lakini ninyi wengine vitimbi mnavyofanya kwa kusaidiwa na nasaba zenu ili kuupata ukubwa ndizo zinazofanya watu wawatilie mashaka.....Na hata kama ukishindwa (kama ulivyoshindwa) ni kwa sababu umezidiwa maarifa na baadhi "waharibifu" wenzenu..........Na kama ungeshinda watu wasingeshindwa kuhisi harufu mbaya. Na haya watu wasiokuwa CDM wanayasema na akina siye tusio na chama tunasikia.

Nikuulize na jiulize..mbona alivyoshinda Makongoro watu hawakusema ni mtoto wa mkubwa? si ni CCM!!
 
  • Thanks
Reactions: EMT
Inakuwaje taarifa ya CDM kutolewa kabla ya hukumu ya mahakama? inaonekana hukumu ilitolewa tarehe 22 Mei 2012 na taarifa imetolewa tarehe 13 Mei 2012.

Heri wewe umeliona hilo.
Wabongo we don't read the details
Ndo maana tunaingizwa mkenge kwenye mikataba.
 
Nafikiri sasa ni muhimu kwa CHADEMA kuondoa hii sintofahamu KUHUSU makazi ya Leticia....suala ambalo ndilo limezua mjadala mkubwa.......

Nilitetegemea kwenye taarifa yao ambayo hata hivyo ni backdated wangezungumzia hizo tuhuma. Lakini wameamua kukaa kimya kwa sababu wanazozijua wao wenyewe. Labda ndo maana Mzee Mwanakijiji anasema:

Ukiona wenye hekima wamekaa kimya na wewe tafuta kiti kaa pembeni sikiliza. Mahali pa wenye hekima usiharakishe kuzungumza.
 
Mgetusaidia kuweka majina ya hao waliofungua kesi za kumbambikizia halafu wakaingia mitini. Asha kumu si matusi isije kuta wapo akina William@NY City!

A word of wisdom, CCM huo uhuni wenu fanyeni Bongo sio nchi za wenzetu mtaumbuka!

Hivi kweli siku hizi marekani unaweza fungua case kwa jina bubu na ukaingia mitini vile vile.Mhhh Hii taarifa ya Mnyika inauwalakini sana.
Siku hizi marekani ni TZ nini?
 
Hivi kweli siku hizi marekani unaweza fungua case kwa jina bubu na ukaingia mitini vile vile.Mhhh Hii taarifa ya Mnyika inauwalakini sana.
Siku hizi marekani ni TZ nini?
Kwa akili yako unadhani Marekani hakuna matapeli na kama una wasiwasi na taarifa ya Mnyika tupe yako yenye isiyo na walakini.
 
Hawa CDM siku zote ndio huwa wanapinga watoto wa viongozi kushika madaraka. Sasa nashangaa ndani ya CDM majina ya Nyerere yametawala.

Watoto wa viongozi si wote hawafai kuwa viongozi.......ila wengi wao hamna kitu
 
Chadema wanasema kesi ilikuwa ya kutengenezwa naomba kuuliza maswali machache hapa

1. Kama wanajua ya kutengenezwa nani aliitengeneza si watuambie?
2. Je makosa kama Tresspassing ni jinai au sio jinai huko marekani? kama jibu ni NDIO sasa hapo swala la kutengenezwa kesi linakujaje?
Umeambiwa polisi Marekani wanaendelea na uchunguzi wa aliyetoa madai ya uongo unataka nini zaidi. Mlikuwa mnafikiri wenzetu ni kama nyie kuwa wakishatupilia kesi inaishia hapo, kama mlihusika mtajulikana tu.
 
Nafikiri sasa ni muhimu kwa CHADEMA kuondoa hii sintofahamu KUHUSU makazi ya Leticia....suala ambalo ndilo limezua mjadala mkubwa.......

Back to the @W.J. Malecela nafikiri hajafikiri sawasawa.....Hebu mwangalie mtu kama Vicent Nyerere suluba za kisiasa alizopitia kwenye jimbo la Musoma mjini (siasa za huko si lelemama...nimezaliwa huko nazifahamu)..kwa hiyo kwa yeye kuwa hapo alipo ni haki isiyo hojiwa.....

Lakini ninyi wengine vitimbi mnavyofanya kwa kusaidiwa na nasaba zenu ili kuupata ukubwa ndizo zinazofanya watu wawatilie mashaka.....Na hata kama ukishindwa (kama ulivyoshindwa) ni kwa sababu umezidiwa maarifa na baadhi "waharibifu" wenzenu..........Na kama ungeshinda watu wasingeshindwa kuhisi harufu mbaya. Na haya watu wasiokuwa CDM wanayasema na akina siye tusio na chama tunasikia.

Nikuulize na jiulize..mbona alivyoshinda Makongoro watu hawakusema ni mtoto wa mkubwa? si ni CCM!!

Wapo viongozi wakati wa enzi zao za kutawala misonge walinuka vibaya kwa jamii ya kitanzania na hata sasa hivi wengine ambao bado wako kwenye system wameishanuka na hata family zao zinanuka kwenye jamii ya kitanzania, hivyo mnuko huo unagusa family zao , lakini baadhi ya viongozi hawakuwa na makuu au harufu mbaya ya kuchukiza kwa jamii ya kitanzania, pamoja na kuwa na mapungufu. Mheshimiwa Makongoro hakuwa affected na mnuko wa mzee wake, ndo maana hujasikia maneno yoyote. Pole kwa kutaka kutetea minuko yenye harufu mbaya.
 
Kwa akili yako unadhani Marekani hakuna matapeli na kama una wasiwasi na taarifa ya Mnyika tupe yako yenye isiyo na walakini.

Mkuu umesoma taarifa nzima including tarehe iliyotolewa na tarehe ya siku ambayo kesi iliamuliwa?
 
Mungu akiwa upande wetu, ni nani anayeweza kuwe kinyume nasi?
 
Kwa akili yako unadhani Marekani hakuna matapeli na kama una wasiwasi na taarifa ya Mnyika tupe yako yenye isiyo na walakini.

Kwa akili yangu, bado nashawishika kuamini mahakamani marekani huwezi fungua kesi bila documents ya utaburisho ni nani anayefungua kesi. Kama hiyo akili yangu ni sahihi, basi kuingia mitini unakuwa mtuhani mgumu zaidi.

Ama wewe unaona je?
 
hata kama hana kesi marekani kwa nini ni mbunge tz halafu anaishi usa?

Labda hapa ungenisaidia, hivi Sheria/Kanuni za Bunge zinamtaka Mbunge aishi wapi? Na kama Mbunge atakuwa anaishi nje ya Jimbo lake lakini hapa hapa nchini Sheria/Kanuni inatamkaje kuhusu jambo hilo? Au kanuni imeweka mipaka ya Mbunge anapotakiwa aishi? Kama hakuna Sheria/Kanuni inayomzuia mtu kuishi anapotaka, basi nyamaza kimya, acha majungu!
 
Back
Top Bottom