Taarifa ya CHADEMA kuhusu kesi ya Leticia Nyerere | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Taarifa ya CHADEMA kuhusu kesi ya Leticia Nyerere

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by EMT, May 24, 2012.

 1. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #1
  May 24, 2012
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimepokea nakala ya hukumu ya kesi mbili zilizofunguliwa Marekani dhidi ya mbunge wa Viti Maalum Leticia Nyerere (CHADEMA) zenye kuonyesha mahakama imetupilia mbali kesi hizo. (Rejea Kiambatanisho).

  Kwa mujibu wa mbunge wa Viti Maalum Leticia Nyerere waliofungua kesi hiyo waliingia mitini baada ya kubainika kwa tuhuma kwamba kesi hiyo ilikuwa ni ya kutengenezwa kwa malengo ya kumchafua hali ambayo ingeweza kuwatia hatiani wahusika kwa kuwasilisha madai ya uongo.

  Pamoja na kutupiliwa mbali kwa kesi hizo mamlaka husika za Marekani zinaendelea na uchunguzi wa kumsaka aliyetoa madai kwamba Mbunge Leticia Nyerere amekamatwa na kutaka wananchi wamchangie fedha kwenye akaunti iliyotajwa katika ujumbe uliosambazwa kwa njia ya mtandao.

  Hukumu hii inadhihirisha tahadhari niliyoitoa kwa wanahabari tarehe 17 Mei 2012 ya kuwataka kusubiri maelezo rasmi kutoka kwa Leticia Nyerere na yatokanayo mahakamani kutokana na tuhuma zilizosambazwa kwenye mitandao kuwa na mwelekeo wa siasa chafu kukwaza jitahada zake na viongozi wa CHADEMA kutokana na kazi walizozifanya za kuwezesha watanzania waishio Marekani kuunga mkono mabadiliko.

  Chama kinaendelea kufuatilia kwa karibu suala hili na taarifa zaidi zitatolewa kwa umma katika hatua za baadaye kadiri iwezekanavyo.

  Kurugenzi ya Habari na Uenezi inatumia fursa hii kuwakumbusha watanzania wanaoishi nchini Marekani kuhudhuria kwa wingi katika Mkutano wa CHADEMA utakaofanyika Maryland tarehe 27 Mei 2012 na kuwasiliana na Leticia Nyerere kupitia leticianyerere@rocketmail.com kwa maelezo zaidi.

  Imetolewa
  Tarehe 13 Mei 2012 na:
  John Mnyika (Mb) Mkurugenzi wa Habari na Uenezi


  [​IMG]
   
 2. chitalula

  chitalula JF-Expert Member

  #2
  May 24, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,307
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  watajibeba wanaoangaika na dhoruba la chadema
   
 3. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #3
  May 24, 2012
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Safi sana. The truth will always out.
   
 4. n

  ngwini JF-Expert Member

  #4
  May 24, 2012
  Joined: Apr 5, 2011
  Messages: 469
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mbona hamja2jibu kwann anachukua posho lakini anaishi nje?
   
 5. J

  J4MAYOKA Senior Member

  #5
  May 24, 2012
  Joined: Jul 16, 2011
  Messages: 147
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kwa nini mbunge wa CHADEMA Tanzania afunguliwe kesi USA?

  AU ni mbunge wa nchi 2 tofauti?
   
 6. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #6
  May 24, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,659
  Likes Received: 82,442
  Trophy Points: 280
  ...Yaani imefikia kuchafuana kiasi hiki!? Watu wana roho mbaya sana...Duh!
   
 7. J

  J4MAYOKA Senior Member

  #7
  May 24, 2012
  Joined: Jul 16, 2011
  Messages: 147
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kwanini anatumia e-mail ya rocketmail badala ya chadema?

  Naomba background ya hii kesi tafadhali na picha zake pia
   
 8. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #8
  May 24, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Pamoja na kesi lakini suala la msingi ni kwamba watu walikuwa wakisema huyu mama anaishi marekani na wengine wakasema ana uraia wa marekani lakini anakuwaje mbunge? Hilo ndilo suala kubwa ambalo lilitakiwa kutolewa maelezo na CDM na wala siyo hukumu ya kesi.Suala la kesi zake (amabazo watu walisema ni 7) lilikuja along the way kuonyesha kwamba mtu anayeishi mabagala majimatitu ama kinondoni hawezi kuwa na kesi zote hizo Marekani. Hivyo CDM ingetenda haki kwa kikanusha kwamba Mama Nyerere haishi na hana uraia wa marekani. Baada ya hapo labda ndio ingesema alikuwa na kesi kadhaa na mbili zimefutwa. Hii ingesaidia pia kujua kama kweli alikuwa na idadi iliyotajwa ya kesi. Lakini kusema kesi zimefutwa sijaona tija hapa.
   
 9. nyabhingi

  nyabhingi JF-Expert Member

  #9
  May 24, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 10,898
  Likes Received: 5,360
  Trophy Points: 280
  hata kama hana kesi marekani kwa nini ni mbunge tz halafu anaishi usa?
   
 10. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #10
  May 24, 2012
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Hivi nani amekwambia kuwa Leticia anaishi USA?
   
 11. 1800

  1800 JF-Expert Member

  #11
  May 24, 2012
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 2,217
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Dah mkuu nashndwa hata nikujibu namna gani,maana inaonekana haujuhi hata thamani ya uwepo wako duniani,ushauri wangu,rudi darasani hata kidogo tu
   
 12. WA-UKENYENGE

  WA-UKENYENGE JF-Expert Member

  #12
  May 24, 2012
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 2,904
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Ni suala la mikakati ya kuchukua nchi wakuu. Hii ni vita, huwezi ukapigana na adui ukiwa sehemu moja watakumaliza fasta na kufanya sherehe.
   
 13. k

  kagame Senior Member

  #13
  May 24, 2012
  Joined: Dec 6, 2008
  Messages: 159
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Unadhani kabla ya kuingia kwenye siasa alikuwa anatumia email ipi?
  Kumbuka huyu nu mbunge pia na kila mbunge sharti awe na email address ya kibunge, host name parliament, je mbona hilo hujaliuliza?
  Kutumia host name rocketmail ni uchaguzi wake, ni kama vile mtu anamiliki namba za simu nne tofauti lakini inambidi ataje moja tu so ni uchaguzi wake kuamua atumie namba ipi kama reference.
   
 14. Pasco_jr_ngumi

  Pasco_jr_ngumi JF-Expert Member

  #14
  May 24, 2012
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 1,811
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Asijitambulishe kwa jina la Nyerere, hana hadhi please!!!!!
   
 15. k

  kijiichake JF-Expert Member

  #15
  May 24, 2012
  Joined: Oct 13, 2010
  Messages: 285
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Chadema hamueni kuvua gamba msilirudie na mvae gwanda milele. Naona gamba linawenyemelea polepole mmeanza kulivaa. Mbona taarifaa hii ya kurugenzi ya chadema ina shadidiana sana na taarifa za kurugenzi ya ikulu?
   
 16. Watu8

  Watu8 JF-Expert Member

  #16
  May 24, 2012
  Joined: Feb 19, 2010
  Messages: 47,335
  Likes Received: 2,659
  Trophy Points: 280
  watu wengine ni wavivu wa kufikiria...kilichotolewa hapa ni taarifa, we umeona mahali popote kuna maswali yanayojibiwa? alaaaah
   
 17. Watu8

  Watu8 JF-Expert Member

  #17
  May 24, 2012
  Joined: Feb 19, 2010
  Messages: 47,335
  Likes Received: 2,659
  Trophy Points: 280
  watu kama nyie inabidi tuwasaidie hivi:
  kwa mfano unaishi hapo nchini Kenya na kuna mtu akakutusi ukiwa huko Kenya na binafsi ukafedheheka na kushawishika kumfikisha mtu huyo mbele ya sheria, je utapeleka mashitaka yako kwenye mamlaka ya nchi ipi?
   
 18. CPA

  CPA JF-Expert Member

  #18
  May 24, 2012
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 737
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 45
  Tuache ushabiki wa chama, tujadili hoja! L.nyerere inasemekana
  1. Anakabiliwa na kesi saba, hakuna mtu anayejua ni kesi zinahusu nin?
  2.ana uraia wa nchi mbili.
  3.ana ishi marekan.
  Hayo yote ni tuhuma, hakuna mwenye ushaidi/uwakika kama ni kweli au la. Cha msingi ili kuondoa sitofahamu, ni bora yeye/cdm watoe majibu au maelezo.
   
 19. l

  lyena_ Member

  #19
  May 24, 2012
  Joined: Mar 11, 2012
  Messages: 23
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Unaonaje wewe uchukue jina lake ili roho yako iridhike. Jamani mbona unashangaza kumbe hata majina yanaonewa wivu.Mwambie madaraka, Makongoro, John,Magige au Andrew akuoe wewe ili uitwe Mama Nyerere.Pengine tatizo lako ni wivu ,pole sana kumbe unatamani nawe uwe mkwe wa baba wa Taifa.Bahati mbaya watoto wa mwalimu wote wameshaoa bado Andrew. Ukitaka naweza kukufanyia mpango Andrew akuoe ili na weweuwe na hilo jina.WiVUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUU!
   
 20. Rejao

  Rejao JF-Expert Member

  #20
  May 24, 2012
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 9,239
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Hawa CDM siku zote ndio huwa wanapinga watoto wa viongozi kushika madaraka. Sasa nashangaa ndani ya CDM majina ya Nyerere yametawala.
   
Loading...