Taarifa ya CHADEMA kuhusu kesi ya Leticia Nyerere

Taarifa ya CHADEMA kuhusu kesi ya Leticia Nyerere

William kutokana na mipango yako na uzima wako katika siasa kuna malumbano ambayo hutakiwi kuyaingilia, yanakushushia hesima, sikutegema kuona comment ya kitoto kama hio toka kwako, una nafasi ya kukukua na kuemndelea kisiasa ndani au nje ya CCM sasa hizi comment za kitoto na namna hii inakujae tena hapa? Si lazima kila kitu ambacho unaona labda kinagusa kwa namna yoyote ile ukaamua ku-comment tu, please jirekebishe, ni ushauri wa bure tu
- Vincent Nyerere & Leticia Nyerere, au unasema je?

William.
 
Hawa CDM siku zote ndio huwa wanapinga watoto wa viongozi kushika madaraka. Sasa nashangaa ndani ya CDM majina ya Nyerere yametawala.

nani amekwambia leticia ni mtoto wa mwalimu? Basi livingston kilaza ni mtoto wa john lusinde
 
Naomba kuuliza swali ni kwanini baadhi ya mashabiki wa CDM hawapendi ikosolewe?

Wasisahau jina la chama limebeba neno mojawapo muhimu sana DEMOKRASIA
 
1.Hivi Emmanuel Nchimbi anaishi Songea?Hilo huoni kama ni tatizo?
2.Hvi John Komba anaishi Mbinga?
3.Hivi Jenista Mhagama anaishi Peramiho?
4.Abdalah Mtutura anaishi Tunduru?
Jadili hawa pia.Huko Masaki wanakoishi wanawawakilisha kina nani?Masaki hawana Mbunge hadi wao waishi uhamishoni?Huku kwingine ni kwa sababu hakuna Supermarket.

Naona kijana unafananisha matango na mastafeli mifano yako haiendani hata kidogo na swala linalojadiliwa hapa!

Mara ya mwisho nilipoangalia Mbinga, Peraminho, Tunduru na Masaki zote zilikuwa sehemu za Tanzania!
 
Vipi Mbunge wa Tanzania awe na kesi za jinai USA? iwe zimetupwa au hazijatupwa. Kuna mengi yanayohitaji ufafanuzi au anawakilisha jimbo la Maryland kwenye bunge la Tanzania?

Kwani Mbatia anawakilisha jimbo gani kwenye bunge la Tanzania? Fikiria tena!
 
Watoto wenye majina ya vigogo kuwa viongozi si tatizo, tatizo ni mchakato wa wao kuingia kwenye hizo nafasi. Ukoo wa nyerere haubebwi na wala hauhongi kama sioi. Funguka weweeee!!!
 
- Tena wanapinga hayo kufanyika ndani ya CCM tu, ila wakija kwao ni sawa kumbe unajua hili? Sawa sawa kwa mara ya kwanza kuona member anayejua ukweli!

William.

Uongozi ndani ya CDM uko based on merits. Hizi shutuma mbona haziakisi hali halisi ya CDM? Mtu hataachwa kwa sababu ya mtu ni mtoto wa Kigogo. Ndugu William karibu sana CDM lakini lazima upitie chujio na si vinginevyo.
 
Mkuu umesoma taarifa nzima including tarehe iliyotolewa na tarehe ya siku ambayo kesi iliamuliwa?
Nakushangaa EMT kama na wewe bado unang'ang'ania commonly misspelt ya wazi, badala ya trh 23 ikaandikwa trh 13, waachie hizo ligi akina Rejao waendelee nazo wewe leta hoja ya msingi wa hukumu zilizotoka.
 
Last edited by a moderator:
Kwa akili yangu, bado nashawishika kuamini mahakamani marekani huwezi fungua kesi bila documents ya utaburisho ni nani anayefungua kesi. Kama hiyo akili yangu ni sahihi, basi kuingia mitini unakuwa mtuhani mgumu zaidi.

Ama wewe unaona je?
Unaweza kufungua kesi na documents za ukweli na ukapotea au za uongo ndio maana wanatafutwa, usifikiri Marekani huwa hawatafutwi Marekani si mbinguni wala hawaishi malaika, na kwa taarifa yako Marekani ndiyo nchi inayoongoza kwa uharifu pamoja na sheria zao kuwa tight.
 
Ashante kwa taarifa hiyo J. Mnyika (CDM). Angalau tumejua nini kilimsibu mbunge wetu. Lakini tungeomba vilevile taarifa ya kile mbunge wetu anafanya huko Marekani. Lengo sio kufuatilia maisha binafsi ya Leticia bali kufahamu MBUNGE wetu ambaye tunamtegemea kushirikiana nasi hapa nchini anafanya nini Marekani. Natanguliza shukrani zangu za dhati kabisa.
 
Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimepokea nakala ya hukumu ya kesi mbili zilizofunguliwa Marekani dhidi ya mbunge wa Viti Maalum Leticia Nyerere (CHADEMA) zenye kuonyesha mahakama imetupilia mbali kesi hizo. (Rejea Kiambatanisho).

Kwa mujibu wa mbunge wa Viti Maalum Leticia Nyerere waliofungua kesi hiyo waliingia mitini baada ya kubainika kwa tuhuma kwamba kesi hiyo ilikuwa ni ya kutengenezwa kwa malengo ya kumchafua hali ambayo ingeweza kuwatia hatiani wahusika kwa kuwasilisha madai ya uongo.

Pamoja na kutupiliwa mbali kwa kesi hizo mamlaka husika za Marekani zinaendelea na uchunguzi wa kumsaka aliyetoa madai kwamba Mbunge Leticia Nyerere amekamatwa na kutaka wananchi wamchangie fedha kwenye akaunti iliyotajwa katika ujumbe uliosambazwa kwa njia ya mtandao.

Hukumu hii inadhihirisha tahadhari niliyoitoa kwa wanahabari tarehe 17 Mei 2012 ya kuwataka kusubiri maelezo rasmi kutoka kwa Leticia Nyerere na yatokanayo mahakamani kutokana na tuhuma zilizosambazwa kwenye mitandao kuwa na mwelekeo wa siasa chafu kukwaza jitahada zake na viongozi wa CHADEMA kutokana na kazi walizozifanya za kuwezesha watanzania waishio Marekani kuunga mkono mabadiliko.

Chama kinaendelea kufuatilia kwa karibu suala hili na taarifa zaidi zitatolewa kwa umma katika hatua za baadaye kadiri iwezekanavyo.

Kurugenzi ya Habari na Uenezi inatumia fursa hii kuwakumbusha watanzania wanaoishi nchini Marekani kuhudhuria kwa wingi katika Mkutano wa CHADEMA utakaofanyika Maryland tarehe 27 Mei 2012 na kuwasiliana na Leticia Nyerere kupitia leticianyerere@rocketmail.com kwa maelezo zaidi.

Imetolewa
Tarehe 13 Mei 2012 na:
John Mnyika (Mb) Mkurugenzi wa Habari na Uenezi

700345398.JPG

Haya haya ndiyo yaliyowafanya watu kuichukia CCM sasa CDM nao wanayafanya hayo hayo. Kwanini suala binafsi la huyu mama liwe ni suala la chama? It is obvious kuwa huyu mama ana character issues, sasa kwa nini CDM wanaamua nao kujipaka matope yake. Kulindana-lindana mpaka lini? Kwa nini kila mtu asiwajibike kwa yanayomsibu?

Sio kweli kusema kuwa kesi imetupiliwa mbali, 'nolle prosequi' ina maana ya kuwa mwanasheria wa serikali ameamua kutokuendelea na mashitaka na ndio maana plea yake sio ya not guilty. Walioleta mashitaka ni polisi na sio wahuni fulani kama ilivyoandikwa. Mahakama za Maryland makabrasha yao yako wazi kwa mtu yeyote kusoma, kwa nini kudanganya.

Mtu unapokuwa na kesi zaidi ya 7 mahakamani, then kwa vyovyote utakuwa na walakini fulani. Kilichowazi hapa ni kuwa Record za Leticia mbele ya sheria sio nzuri, ingawa ana bahati ya kuonewa huruma na polisi au wanasheria wa serikali wanaomshitaki. Ukiongezea na hili la yeye kupoteza nyumba yake (foreclosure) kwa kushindwa kulipa deni la benki, inaonyesha wazi kuwa kuna mambo yanayohitaji maelezo toka kwake na mambo yake yalishaanza kumshinda US kabla ya kuamua kukimbilia TZ.

Hata hivyo suala la makazi sio vema kumshushumilia yeye tu, inabidi liwe ni suala la kikatiba maana wabunge walio wengi hawaishi kwenye majimbo yao kabisaa. Ingetakiwa kila Mbunge athibitishe kuwepo jimboni kwake kwa angalau 50% ya muda asiokuwepo Bungeni.
 
Kwa wale wanaoisema CDM kuhusu ubunge wa viti maalumu. At least CDM kuna vigezo vinavyoeleweka vya kwapata wabunge wa viti maalumu wa CDM. Alituwekea hapa Dr. Mkumbo Majority tukaridhika, ni vigezo vizuri vya kuwapata hao wabunge.

Sasa ninaomba CCM nao watuwekee vigezo vyao wanavyotumia kuwapata wabunge wa viti maalumu?

Pili mimi sioni shida watoto wa vigogo kupata nafasi za kisiasa kama nafasi zenyewe ni za KUCHAGULIWA (January Makamba). Si ni sisi ndio tumewapigia kura.

Tatizo langu ni hao watoto wa viongozi kupewa nafasi za KUTEULIWA kama ubunge wa viti maalumu, U-katibu mwenezi wa Chama, U-DC, U-RC ubalozi etc. Hapa ndipo tatizo kubwa lipo.
 
Unaweza kufungua kesi na documents za ukweli na ukapotea au za uongo ndio maana wanatafutwa, usifikiri Marekani huwa hawatafutwi Marekani si mbinguni wala hawaishi malaika, na kwa taarifa yako Marekani ndiyo nchi inayoongoza kwa uharifu pamoja na sheria zao kuwa tight.

Ha ha ha
Documents za uongo? kwi kwi kwi kwi Mkuu, uharifu unafanyike nje bila ya documents , mfano jamaa amekuvizia kakupa ya uso, lakini docs tusidanganyane.
 
Haya haya ndiyo yaliyowafanya watu kuichukia CCM sasa CDM nao wanayafanya hayo hayo. Kwanini suala binafsi la huyu mama liwe ni suala la chama? It is obvious kuwa huyu mama ana character issues, sasa kwa nini CDM wanaamua nao kujipaka matope yake. Kulindana-lindana mpaka lini? Kwa nini kila mtu asiwajibike kwa yanayomsibu?

Sio kweli kusema kuwa kesi imetupiliwa mbali, 'nolle prosequi' ina maana ya kuwa mwanasheria wa serikali ameamua kutokuendelea na mashitaka na ndio maana plea yake sio ya not guilty.
Walioleta mashitaka ni polisi na sio wahuni fulani kama ilivyoandikwa. Mahakama za Maryland makabrasha yao yako wazi kwa mtu yeyote kusoma, kwa nini kudanganya.

Mtu unapokuwa na kesi zaidi ya 7 mahakamani, then kwa vyovyote utakuwa na walakini fulani. Kilichowazi hapa ni kuwa Record za Leticia mbele ya sheria sio nzuri, ingawa ana bahati ya kuonewa huruma na polisi au wanasheria wa serikali wanaomshitaki. Ukiongezea na hili la yeye kupoteza nyumba yake (foreclosure) kwa kushindwa kulipa deni la benki, inaonyesha wazi kuwa kuna mambo yanayohitaji maelezo toka kwake na mambo yake yalishaanza kumshinda US kabla ya kuamua kukimbilia TZ.

Hata hivyo suala la makazi sio vema kumshushumilia yeye tu, inabidi liwe ni suala la kikatiba maana wabunge walio wengi hawaishi kwenye majimbo yao kabisaa. Ingetakiwa kila Mbunge athibitishe kuwepo jimboni kwake kwa angalau 50% ya muda asiokuwepo Bungeni.

Hapo kwenye nyekundu, duuu kumbe polisi wanamtafuta polisi aliyepotea? kwi kwi kwi kwi
 
Hawa CDM siku zote ndio huwa wanapinga watoto wa viongozi kushika madaraka. Sasa nashangaa ndani ya CDM majina ya Nyerere yametawala.
Ulitaka familia ya Nyerere wasishiriki kwenye siasa au inakuuma kwa sababu wako Chadema.Leticia na Vicent ni wabunge wenye umakini mkubwa bahati mbaya ccm imewakosa na imebaki kuwamezea mate.
 
- Tena wanapinga hayo kufanyika ndani ya CCM tu, ila wakija kwao ni sawa kumbe unajua hili? Sawa sawa kwa mara ya kwanza kuona member anayejua ukweli!

William.
Mkuu kuwa mtoto wa kiongozi siyo hoja inabidi utumie na zako. Hawa wakina Nyerere ni wabunge machachari na wana hoja zenye mvuto.Kwa hiyo hata watoto wa wakubwa huingia kwenye mchujo kama ilivyokuwa kwako.
 
Naomba kuuliza swali ni kwanini baadhi ya mashabiki wa CDM hawapendi ikosolewe?

Wasisahau jina la chama limebeba neno mojawapo muhimu sana DEMOKRASIA
Umekosoa nini na wakapinga nini, be specific please usi-generalize mambo.
 
Back
Top Bottom