Taarifa ya CHADEMA kuhusu kesi ya Leticia Nyerere

Acha kuweweseka wewe! Akili zako ni ndogo sana mambo kama haya huwezi kuyapambanua%
- Tena wanapinga hayo kufanyika ndani ya CCM tu, ila wakija kwao ni sawa kumbe unajua hili? Sawa sawa kwa mara ya kwanza kuona member anayejua ukweli!William.
 
Acha kuweweseka wewe! Akili zako ni ndogo sana mambo kama haya huwezi kuyapambanua%
- Tena wanapinga hayo kufanyika ndani ya CCM tu, ila wakija kwao ni sawa kumbe unajua hili? Sawa sawa kwa mara ya kwanza kuona member anayejua ukweli!William.
 
nilifikiri siasa za maji machafu wanafanya watz wa hapa nyumbani kwa sababu ya njaa zetu kumbe kuna wendawazimu na wajinga wanaishi nje nao ni majuha wa siasa chafu. I wish wapatikane mapema then watimuliwe huko warudishwe bongo hawana faida ya kuishi nje kwa ujinga wao
 
Source Nipashe

Mahakama yatupa kesi ya Leticia Nyerere

Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimepokea nakala ya hukumu ya kesi mbili zilizofunguliwa Marekani dhidi ya Mbunge wa Viti Maalum, Leticia Nyerere, zenye kuonyesha mahakama imetupilia mbali kesi hizo. Taarifa iliyotolewa jana na Kurugenzi ya Habari na Uenezi ya Chadema ilieleza kuwa kwa mujibu wa Leticia, waliofungua kesi hiyo waliingia mitini baada ya kubainika kwamba kesi hiyo ilikuwa ni ya kutengenezwa kwa malengo ya kumchafua hali ambayo ingeweza kuwatia hatiani wahusika kwa kuwasilisha madai ya uongo. Taarifa hiyo ilieleza kuwa pamoja na kutupiliwa mbali kwa kesi hizo, mamlaka husika za Marekani zinaendelea na uchunguzi wa kumsaka aliyetoa madai kwamba Leticia amekamatwa na kutaka wananchi wamchangie fedha kwenye akaunti iliyotajwa katika ujumbe uliosambazwa kwa njia ya mtandao. “Hukumu hii inadhihirisha tahadhari niliyoitoa kwa wanahabari Mei17, 2012 ya kuwataka kusubiri maelezo rasmi kutoka kwa Leticia Nyerere na yatokanayo mahakamani kutokana na tuhuma zilizosambazwa kwenye mitandao kuwa na mwelekeo wa siasa chafu kukwaza jitahada zake na viongozi wa Chadema kutokana na kazi walizozifanya za kuwezesha watanzania waishio Marekani kuunga mkono mabadiliko,” ilieleza sehemu ya taarifa hiyo iliyosainiwa na Mkurugenzi wa Habari na Uenezi, John Mnyika. “Chama kinaendelea kufuatilia kwa karibu suala hili na taarifa zaidi zitatolewa kwa umma katika hatua za baadaye kadiri iwezekanavyo.” Kwa mujibu wa nakala ya hukumu ya kesi hiyo iliyotolewa Mei 22 na jaji R. Russelle Sadler Mahakama ya Wilaya huko Maryland. Wakati huo huo, Chadema kiwakumbusha Watanzania wanaoishi Marekani kuhudhuria kwa wingi katika Mkutano wa chama hicho utakaofanyika Maryland Mei 27, mwaka huu na kuwasiliana na Leticia kupitia leticianyerere@rocketmail.com kwa maelezo zaidi.

CCM mje muweke uzi wenu tena juu ya kesi hii
 
Pamoja na kesi lakini suala la msingi ni kwamba watu walikuwa wakisema huyu mama anaishi marekani na wengine wakasema ana uraia wa marekani lakini anakuwaje mbunge? Hilo ndilo suala kubwa ambalo lilitakiwa kutolewa maelezo na CDM na wala siyo hukumu ya kesi.Suala la kesi zake (amabazo watu walisema ni 7) lilikuja along the way kuonyesha kwamba mtu anayeishi mabagala majimatitu ama kinondoni hawezi kuwa na kesi zote hizo Marekani. Hivyo CDM ingetenda haki kwa kikanusha kwamba Mama Nyerere haishi na hana uraia wa marekani. Baada ya hapo labda ndio ingesema alikuwa na kesi kadhaa na mbili zimefutwa. Hii ingesaidia pia kujua kama kweli alikuwa na idadi iliyotajwa ya kesi. Lakini kusema kesi zimefutwa sijaona tija hapa.

Kimbunga@ nakubaliana nawe. Katika mambo kama haya ambayo yanagusa kodi za wananchi, ushabiki wa kisiasa au kiitikadi tuweke kando na kuwa wakweli. Katu ukweli hauwezi kupindishwa na ukipindishwa ipo siku tutaumbuka, hii ndiyo hali halisi.

Kimbunga alivyosema kama mtu haishi huko Marekani iweje awe na mlolongo wa kesi zote hizo saba kwenye kumbukumbu za mahakama huko Marekani? Kiwango cha kesi hizo ndicho kinachotushtua kwani walioibua hayo ni kutokana na dosari zilizojitokeza ambazo Letisia katika utetezi wake hazikani au kukubali ila anajitetea na kulalamika tu kwamba anaonewa.

Kwanza anaonyesha kila dalili ni mvunjaji wa sheria kwa kuwa na kesi zote hizo nchi za nje ya nchi. Pili hoja ya kuwepo Marekani muda mrefu hata kutohudhuria vikao vya bunge ambavyo anawajibika kwa wanachi hajafanya. Na bado anavyojitetea angali huko huko, sasa wananchi tuelewe nini?

Ifahamike kwamba wengi wanaoitetea Chadema si wanachama, ila ni wapenda mabadiliko. Chadema kisijenge mfumo kama wa CCM kuteteana, hayo ndiyo tunayoyakataa CCM sasa yanaanza kila dalili ya kujirudia ndani ya Chadema. Palipo na makosa lazima kukosoana ili kujenga dhamira ya kujisahihisha lasivyo ni kuendekeza yaleyale ya kulindana. Ni kama kauli ya Mweremita mmoja aliyesema: I left men in the monastery to find men in the world.
 
Ha ha ha
Documents za uongo? kwi kwi kwi kwi Mkuu, uharifu unafanyike nje bila ya documents , mfano jamaa amekuvizia kakupa ya uso, lakini docs tusidanganyane.

Utetezi wao dhaifu mno, documental za mahakama anaziteteaje? Taratibu za mahakama za marekani wanaoshtaki mahakamani ni polisi, na hata kama mtu binafsi una kitu cha kulalamika, lazima polisi wafanye uchunguzi na kujiridhisha kwamba ni kesi ya kupelekwa mahakamani, si kama bongo tunavyosanii kila kukicha.
 
Back
Top Bottom