Taarifa ya CCM kwa vyombo vya habari

Taarifa ya CCM kwa vyombo vya habari

Naam hiki ndio chama bana, kina hazina ya viongozi na taratibu zinazoeleweka sio kama hizo saccos

Mbona mnamsahau Mtela Mwampamba, nilitegemea naye mtamgawia pande, atapunguza speed ya kuikandia CDM
 
Wezi tu viwanja vya serikali wamedhurumu watanzania ufisadi mpaka kupigisha kura marehemu bunge LA katiba
 
magamba hayooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooo
 
CCM kweli ni matapeli! mali walizipataje? kitu chochote kilichojengwa na serikali kabla mfumo wa vyama vingi ni mali ya umma! kumbe ndo maana wanaendekeza ufisadi!
 
Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) jana Oktoba 16, 2014 katika siku ya kwanza ya kikao chake cha siku mbili kinachoendelea mjini Dodoma chini ya Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete imejadili na kupitisha Sera ya CCM ya kujitegemea kimapato na kiuchumi.


Sera hiyo inalenga kuwa muongozo wa kuifanya CCM ianze kuzitumia rasilimali zake kuzalisha ili iweze kujitegemea kiuchumi. Kama inavyofahamika CCM ina rasilimali nyingi wakiwemo wanachama wake, viwanja na majengo ambavyo kwa pamoja vkitumika vizuri vitasaidia kukifanya chama kuondokana na utegemezi wa ruzuku na badala yake kujitegemea.


Aidha Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM imefanya uteuzi wa wagombea kwa nafasi za Uenyekiti wa CCM katika wilaya mbili pamoja na wagombea Ujumbe wa NEC katika wilaya tatu zilizokuwa na nafasi wazi.


WALIOTEULIWA KUGOMBEA UENYEKITI WA WILAYA NI;-


Wilaya ya Njombe:-Ndugu Edward Pius Mgaya Ndugu Vallence Mtenzi Kabelege Ndugu Betram Simon Ng’imbudzi


Wilaya ya Misenyi:-Ndugu Sosthenes Rweyemamu Kabandwa Ndugu Said Ibrahim Seruh Ndugu Erica Kiiza Stephen


WALIOTEULIWA KUGOMBEA UJUMBE WA HALMASHAURI KUU YA CCM TAIFA NI:-


Wilaya ya Tandahimba:-Ndugu Lutavi Abdula Suleman Ndugu Malela Mohamed Chibwana Ndugu Nanyundu Ally Salum


Wilaya ya Mkuranga:-Ndugu Ally Mohamed Msikamo Ndugu Maulid Hamis Zowange Ndugu Wakati Nassoro Mtulia Ndugu Zawadi Ally Kilapo


Wilaya ya Njombe:-Ndugu Christian Marcus Fwalo Ndugu George Benedict Mng’ong’o Ndugu Oscar Michael Msigwa Ndugu Justin Nusulupia


Imetolewa na:-


Nape Moses Nnauye, KATIBU WA HALMASHAURI KUU YA TAIFA, ITIKADI NA UENEZI 17/10/2014

hii ndio taarifa
 
acha wafu wazike wafu wao ccm ni wapuuzi sana wamekutana dodoma kwenda kubariki rushwa DR SLAA ndo kiboko wa ccm wakisikie hili jina wanatamani ardhi ipasuke wazame huko chini ccm ni janga la taifa.
View attachment 194199
CHADEMA MWENDO MDUNDO MPAKA IKULU
 
Hawa jamaa wanafanya mambo utafikiri hiki chama kimezaiwa jana! Hata aibu hawana. Miaka yote chama hakijajitegemea? Ni wizi tu!
 
Wapuuzi wameongeA upuuzi wapuuzwe...

Kutokana na Hali mbaya kwenye Mikutano yao nakutokukubalika pia hili lakuongeza Bajeti yakuwapa wananchi chakula kwenye mikutano ya ccm hilehali wananchi wanaendelea kuteseka kwa kukosa mambo mbalimbali pia lilikua ajenda yenu ya jana pic inajieleza namna gani mnarubuni wananchi kwenye mikutano
 

Attachments

  • IMG-20141017-WA0035.jpg
    IMG-20141017-WA0035.jpg
    26.4 KB · Views: 79
CCM wana mali zipi zaidi ya zile walizopora kutoka kwa umma. Ccm imebaki kuwa genge la wahuni,wezi,wauza unga,wala rushwa na wajinga kama alivyosema kinana jangili.SISI CCM NI WAPUUZI NA WALA RUSHWA,hii ni kwa mujibu wa KINANA
 
Naam hiki ndio chama bana, kina hazina ya viongozi na taratibu zinazoeleweka sio kama hizo saccos

Sina upande naoshabikia,hivi huwezi kuisifia Ccm bila kuitaja Chadema au ndo kama viongozi wa dini,hawawez kuhubili bila kumtaja shetani? ,Napita tu ndugu.
 
Wakuu wa ccm wanasemaje hapo kuhusu rasimu mpya pendekezwa na hasa muda wa kuipigia kura ? Leteni fununu hapa Lizaboni
 
Last edited by a moderator:
Ukiwa una uwezo mdogo wa kufikiri,uadhani hii ni mipango.je,hapo kabla walizitumia hizi pesa kwa shughuli gani?
 
Back
Top Bottom