Taarifa: Wabunge wanaponda maisha viwanja vya bunge usiku huu

Jan 13, 2011
37
10
Ndugu wana wa jf, usiku huu wabunge wa bunge letu wapo katika viwanja vya bunge wanaponda maisha. Sijafahamu sherehe waliyonayo inahusu nini hasa ila kuna kelele za muziki mtindo mmoja.

Haya yanatokea wakati wanafunzi wa udom wakiwa wamefukuzwa chuo na kunyimwa pesa za kwenda field.

Haya yanatokea wakati watanzania tunahuzuni na hasira kali kwa nchi kughubikwa na giza nene linalotokana na mgao wa umeme usijulikana utaisha lini.

Haya yanatokea wakati bunge letu likiwa limepitisha mpango wa maendeleo wa miaka mitano unaoelekeza matumizi ya serekali yasiyo na tija yaondolewa.

Inanikera sana kwa sababu pamoja na sabau nyingine, hapa chuo tunashindwa kusoma kwa sababu ya kelele za muziki kutoka viwanja vya bunge. Aghhhhhh.............
 
Wanasugua visigino na Twanga Pepeta hao, jana spika makinda alitangaza kwamba Twanga Pepeta watakuwa viwanja vya bunge kwa ajili ya kutoa burudani.

Suala la wanafunzi kutokwenda field sio muhimu kiasi hicho, muhimu ni wabunge kuongezewa mishahara na posho ingawa kasungura kenyewe ni kadogo.
 
au ndio ile harusi ya Canada(Barrick) na bunge letu ndio usiku huu inafungwa??
 
chungulia kama wabunge wa opposition wapo ama ni wale wa ccm pekee. tafadhali

Mkuu nina hasira hata sitaki kuwaona hawa watu.. Kuna mwanachuo kakaribishwa akaniomba niende naye, nilichomjibu naamini hatakaa anisahau maishani.

Yani ni kelele tupu watu ndani ya chuo wamejaa hasira kwani usiku huu ndo hakuna kisoma na mitihani ndo hiyo hapo mbele. Aghhhhhh.!!!!!!
 
Nimemwona john komba kapita na mnofu mkubwa wa nyama hahahahahaaaa! teh! teh!
 
Hee! Yule sio Mdee naona kala kikuu. Shibuda anajiandaa kuburudisha kwa mashairi . Bi.kiroboto kavaa wigi la hair style mpya. Duuh..
Eti mziki ni wa mbowe.
Nita wahabarisha zaidi..
 
Nadhani ni siku ya Canada ndiyo wanafanya mambo yao na kuzima hoja ya mauaji ya Tarime .Wacha kesho tutajua mengi .
 
Yuko wapi mbunge wa CHADEMA Regia Mtei atujulishe hiyo sherehe inahusu nini usiku huu huko Dodoma maana kama kuna
watanzania zaidi ya laki moja hawajabahatika kupata mlo wa usiku wa leo halafu wabunge wanaponda raha huko Dodoma,,,
 
Yuko wapi mbunge wa CHADEMA Regia Mtei atujulishe hiyo sherehe inahusu nini usiku huu huko Dodoma maana kama kuna watanzania zaidi ya laki moja hawajabahatika kupata mlo wa usiku wa leo halafu wabunge wanaponda raha huko Dodoma,,,
Ni Regia Mtema, sio Regia Mtei!
 
Swala la sherehe ktk serikali ya Lover boy wa Msoga ni la kawaida kabisa! Pale magogoni ukiona Loverboy amebahatika kukaa zaidi ya siku tatu tu ikulu basi tegemea pilau!

Loverboy ni muumini mkuu wa mambo ya sherehe tena siku hizi hata ukiwa na send of ukimkaribisha kwa kumjaribu tu, anakuja. Sasa hapo unadhani bunge itakuwaje?
 
na tanzania distillers (sina uhakika na spelling) ltd hawa watengenezaji wa konyagi ndo wadhamini bi kiroboto alitanabaisha hilo
 
Nadhani ni siku ya Canada ndiyo wanafanya mambo yao na kuzima hoja ya mauaji ya Tarime .Wacha kesho tutajua mengi .


Hongera kwa kuwafumbua wale wachochezi waliokuwa tayari wamepitisha hukumu kwa kitu wasichokijua. Chuki nyingine bwana!
 
Back
Top Bottom