Ni kweli bado tunawahitaji wabunge?

Matongee

JF-Expert Member
Jun 17, 2023
253
629
Leo usiku nilikuwa najisomea namna ya kufanya biashara ya photography studio. Nilijisomea maelekezo mengi mtandaoni. Mabeberu wametoa maelezo ya kutosha jinsi gani unaweza ukafanya hiyo biashara na ukafanikiwa. Katika vitu vya kuzingatia walivyotaja ni kuhusu vibali vyote vya kisheria kutoka serikalini yaani leseni, TIN, fire certificate na vyote vinavyohusika. Na kingine walichotaja ni kuikatia biashara yako bima (insurance). Haya mambo mawili hasa hilo la bima yalinifanya nitafakari sana kuhusu mfumo mzima uliopo nchini kwenye biashara. Yaani ni kizunguzungu kwa kijana anayeanza.

Baada ya kutafakari nikakumbuka kwamba nchi yetu inaendeshwa kwa kufuata sheria zilizotungwa na bunge. Kiukweli mimi naona bunge limepitisha sheria nyingi ambazo hazina urafiki wowote na kijana anayetaka kufanya biashara kihalali. Hii inamuumiza kijana hadi serikali yenyewe. Vijana karibu wote wakati wa kuanza biashara hawana uhiari wa kwenda kuchukua vibali bali wanalazimika hali inayofanya wasiwe wazalendo hata kwenye kulipa kodi. Huko kwenye bima ndo kabisa bado sana. Linahitajika somo zito.

Nadhani ifike wakati wabunge wasidhani bodaboda italeta mabadiliko yoyote ya kiuchumi kwa vijana. Vijana wanahitajika kujiingiza kwenye biashara za kiubunifu zitakazoleta matokeo makubwa. Bodaboda haina ubunifu wowote. Vijana watajiingizaje kwenye mambo makubwa wakati sheria mmetunga za kuwabana? Huko kwenye kilimo nako badala ya kuja na sera nzuri huku mkirekebisha sheria mmekuja na mipango ya muda mfupi isiyo sustainable. Hii kuwachagua uvccm na kuingia gharama za kuwalimia mashamba ni mpango wa hovyo. Ninasubiri tu ripoti ya CAG kujua ni kiasi gani kimepotea kwenye BBN. Hizo pesa mnazotumia kwenye miradi isiyoweza kudumu hata kwa miaka 20 si bora muwanunulie wakulima mbolea?

Mikopo mnayotoa utakuta Tsh 1m ni kwa kikundi cha vijana 10 wa CCM ambao nao huishia kuzitafuna tu. Hivi ni nani aliyetudanganya kuwa umachinga na uchuuzi ndo utatutoa hapa tulipo? Sasa hivi wabunge wengi wameshaanza kuandaa ligi za MBUNGE CUP ili kujiandaa na uchaguzi 2025. Nia yenu ni kuwarubuni tu vijana ila hakuna nia ya dhati kusaidia vipaji vyao. Toka nizaliwe sijawahi kusikia kombe la mbunge limeleta impact yoyote.

Mimi kwa upande wangu naona sihitaji mtu yeyote anayejiita mwakilishi wangu. Kwa teknolojia iliyopo serikali iwe tu inatoa miswada ya kisheria hadharani tuwe tunaijadili na kuipigia kura. Huu mfumo wa kuwakilishwa na mtu anayejua tu kusoma na kuandika tuachane nao. IKUMBUKWE hata hizo sheria zinatungwa wizarani na bunge inachofanya ni kupitisha tu.
 
Ukisoma kwa bidii kwa matarajio ya maisha bora sasa unamaliza Chuo mbele Giza hali ndio huwa namna hii.

By the way bunge halina kazi yeyote, nakumbuka awamu ya tatu Frederick Sumaye akiwa waziri mkuu alilivunja baraza la madiwani la Jiji la Dar na madiwani wote kuondolewa madarakani, badala yake akaunda tume Jiji chini ya Charles keenja ambayo ulifanya vizuri sana ikiwwmo Kujenga secondary ya Benjamin Mkapa.

Kwa kifupi kwa sasa bunge la Tanzania ni Kijiwe cha machawa wa serikali tu kuanzia supika mpaka wabunge wenzake.
 
Naungana na wewe kwa bunge hili kuendelea kuwepo ni matumizi mabaya ya rasilimali fedha.Miswada mingi inaandaliwa na serikali na inaletwa bungeni na kupitishwa ikiwa haina mapendekezo mapya.Kibaya zaidi hata mswada uwe mzuri VP ukipelekwa kwa Rais na kusainiwa kuwa sheria bado shida itakuwa kwenye kanuni ambazo zitatumiwa na waziri husika
 
Ukisoma kwa bidii kwa matarajio ya maisha bora sasa unamaliza Chuo mbele Giza hali ndio huwa namna hii.

By the way bunge halina kazi yeyote, nakumbuka awamu ya tatu Frederick Sumaye akiwa waziri mkuu alilivunja baraza la madiwani la Jiji la Dar na madiwani wote kuondolewa madarakani, badala yake akaunda tume Jiji chini ya Charles keenja ambayo ulifanya vizuri sana ikiwwmo Kujenga secondary ya Benjamin Mkapa.

Kwa kifupi kwa sasa bunge la Tanzania ni Kijiwe cha machawa wa serikali tu kuanzia supika mpaka wabunge wenzake.
Hata wa upinzani pia hakuna kitu.
 
Back
Top Bottom