Taarifa kwa umma kwa wasafiri wanaokwenda Hong Kong

TODAYS

JF-Expert Member
Apr 30, 2014
13,773
21,272
Kumekuwa na matukio ya Watanzania wanaosafiri kwenda Hong Kong kuzuiliwa kuingia au kuhojiwa kwa muda mrefu na maafisa wa Idara ya Uhamiaji ya Hong Kong katika uwanja wa ndege wa Hong Kong.

Hali hiyo imejitokeza zaidi katika kipindi cha hivi karibuni tangu Hong Kong ifungue mipaka yake kuruhusu wageni kuingia baada ya miaka mitatu ya zuio la kuingia Hong Kong kwa ajili ya udhibiti wa maambukizi ya UVIKO19.

IMG_20230702_185815.jpg

Hatua hizo za Mamlaka za Hong Kong zimetokana na matukio ya siku za nyuma ambapo watu wachache waliokuwa na passport ya Tanzania kufanya vitendo vya uvunjivu wa sheria.

Tarehe 30 Machi 2023 Ubalozi wa Tanzania nchini humo umewasiliana na Mamlaka za Hong Kong kueleza kutoridishishwa na hatua inayochukuliwa na Maofisa wa Uhamiaji wa Hong Kong kwa kila anayekuwa na passport ya Tanzania kuhojiwa kwa muda mrefu na wengine kurejeshwa walikotoka.

Mamlaka za Hong Kong zilijibu ofisi ya ubalozi wa Tanzania kwa kueleza kwamba Maafisa wao wataendelea kutekeleza wajibu wao kwa weledi na kwa mujibu wa sheria za Hong Kong.

Na Wametoa rai kwa wasafiri wanaokwenda Hong Kong kuwa na nyaraka zote zinazohitajika, hususan sababu ya wewe kuingia Hong Kong.

Ubalozi wa Tanzania unatoa rai kwa Watanzania wenye safari ya kwenda Hong Kong wahakikishe kuwa na nyaraka zote muhimu kama zifuatazo:

1) Barua ya Mwaliko kutoka kwa Mwenyeji wa abiria anayekwenda Hong Kong- ambaye anaweza kuwa mtu binafsi au kampuni;

2) Tiketi ya ndege yenye kuonesha tarehe ya kuondoka Hong Kong;

3) Booking ya Hoteli inayoonesha jina la msafiri, tarehe ya kuingia na kutoka;

Na muhimu zaidi, kuepuka kuvunja sheria za Hong Hong kwa kubeba vitu/bidhaa ambazo ni kinyume na sheria.

Vitendo hivyo vitazidi kuchagua taswira ya nchi na kuwaathiri watanzania wengine wengi wanaofuata sheria ambao wangependa kwenda Hong Kong.

Aidha, Ubalozi unashauri watanzania ambao wanakwenda China (Mainland) watumie usafiri wa kwenda moja kwa moja katika miji ya China badala ya kupitia Hong Kong ili kuepuka usumbufu.
 
Endapo mtanzania yeyote atahitaji msaada au ufafanuzi zaidi awasiliane na ofisi ya Ubalozi kwa barua pepe/email hii hapa: beijing@nje.go.tz
au kwa njia ya simu kwa Afisa Ubalozi: +86 136 9336 0750.

Usiingie Whatsapp ukatuma ujumbe, number hiyo haitumii whatsapp- piga moja kwa moja afisa atapokea.
 
Kumekuwa na matukio ya Watanzania wanaosafiri kwenda Hong Kong kuzuiliwa kuingia au kuhojiwa kwa muda mrefu na maafisa wa Idara ya Uhamiaji ya Hong Kong katika uwanja wa ndege wa Hong Kong.

Hali hiyo imejitokeza zaidi katika kipindi cha hivi karibuni tangu Hong Kong ifungue mipaka yake kuruhusu wageni kuingia baada ya miaka mitatu ya zuio la kuingia Hong Kong kwa ajili ya udhibiti wa maambukizi ya UVIKO19.

Hatua hizo za Mamlaka za Hong Kong zimetokana na matukio ya siku za nyuma ambapo watu wachache waliokuwa na passport ya Tanzania kufanya vitendo vya uvunjivu wa sheria.

Mnamo Machi 30, 2023 Ubalozi wa Tanzania nchini China umewasiliana na Mamlaka za Hong Kong kueleza kutokuridhishwa na hatua inayochukuliwa na Maafisa wa Uhamiaji wa Hong Kong kwa kila mwenye passport ya Tanzania kuhojiwa kwa muda mrefu na wengine wachache kurejeshwa Mamlaka za Hong Kong zilitoa majibu kwa Ubalozi mnamo Mei 03, 2023 kueleza kwamba Maafisa wao watatekeleza wajibu wao kwa weledi na kwa mujibu wa sheria.

Hata hivyo, Mamlaka za Hong Kong zimetoa rai kwa wasafiri wanaokwenda Hong Kong kuwa na nyaraka zote zinazohitajika - hususan sababu ya kuingia Hong Kong.

Ubalozi wa Tanzania nchini China unatoa rai kwa Watanzania wenye safari ya kwenda Hong Kong kuhakikisha wanakuwa na nyaraka zifuatazo:

1) Barua ya Mwaliko kutoka kwa Mwenyeji wa abiria anayekwenda Hong Kong - ambaye anaweza kuwa mtu binafsi au kampuni.

2) Tiketi ya ndege yenye kuonesha tarehe ya kuondoka Hong Kong.

3) Booking ya Hoteli inayoonesha jina la msafiri, tarehe ya kuingia na kutoka.

Na muhimu zaidi, kuepuka kuvunja sheria za Hong Hong kwa kubeba vitu/bidhaa ambazo ni kinyume na sheria.

Vitendo hivyo vitazidi kuchagua taswira ya nchi na kuwaathiri Watanzania wengine wengi wanaofuata sheria ambao wangependa kwenda Hong Kong.

Aidha, Ubalozi unashauri Watanzania ambao wanakwenda China (Mainland) watumie usafiri wa kwenda moja kwa moja katika miji ya China badala ya kupitia Hong Kong ili kuepuka usumbufu.

Endapo Mtanzania yeyote atahitaji msaada au ufafanuzi zaidi awasiliane na Ubalozi kwa;

Baruapepe: beijing@nje.go.tz

Simu (Afisa Ubalozi); +86 136 9336 0750

(Namba hiyo haitumii WhatsApp - piga moja kwa moja).

20230703_080502.jpg
 
Vipi inawezekana nao wakija huko kwetu wawekewe vikwazo? au sisi hatuna mamlaka hiyo.
 
Aidha, Ubalozi unashauri watanzania ambao wanakwenda China (Mainland) watumie usafiri wa kwenda moja kwa moja katika miji ya China badala ya kupitia Hong Kong ili kuepuka usumbufu.
Kumbe Hong Kong ni kama Zbr huku kwetu
 
Naona ubalozi wa Tz unaongea kwa kufichaficha mambo, shida kubwa ya Watanzania walio wengi zaidi ni kutaka mafanikio ya haraka haraka kwa njia za mkato, hivyo wanajikuta wanalazimika Kufanya Mambo ya uhalifu ya Kusafirisha na Kufanya Biashara ya Madawa ya Kulevya. Hapa Tz, wanalindwa na utawala uliopo, wakumbuke huko nje hakuna CCM ya kuweza kuwalinda. Balozi zote za Tz huko nje zitoe ilani kwa mamlaka za nchi husika kuwashughulikia ipasavyo Watanzania wote wanaojihusisha na biashara haramu ya madawa ya kulevya ili kusafisha jina la nchi huko ugenini.

Jina la Tanzania limechafuka kimataifa kwa sababu ya watu wachache washenzi, ni vyema hao watu wakanyongwa hukohuko ili kuwatia adabu watu wengine waliobaki wenye nia ya kufanya hiyo biashara ya madawa ya kulevya.

Watanzania wamezidi ktk kufanya uhalifu wa kujihusisha na madawa ya kulevya, Passport ya Tanzania imekuwa haifai tena huko duniani kwa sababu ya hao watu wa madawa ya kulevya.

Ndio maana Mimi binafsi nilipokuwa nje ya Tz, sikutaka kabisa kujihusiha kwa namna yoyote ile na Watanzania, sikutaka ku-socialise na Mtz yoyote yule, nilikaa nao mbali sana. Kila sehemu walikopita Watanzania wameacha legacy mbaya ya kujihusisha na uhalifu mbalimbali ikiwamo na hii biashara ya madawa ya kulevya, Watanzania wote sasa hivi tumekuwa hatuaminiki kutokana na ushenzi huu wa watu wachache wanafanya biashara ya madawa ya kulevya. Wanyongwe huko huko China endapo kama Watakamatwa huko, wasiwarudiahe Tanzania.

Najua China ya Visiwani, yaani Hong Kong hakuna sheria ya kunyonga watu wanaojihusiha na madawa ya kulevya, Mimi nazishauri Mamlaka za China Visiwani (Hong Kong), wanapowakamata Watanzania wenye madawa ya kulevya waende wakawafungulie mashtaka katika China Bara (Mainland China), yaani Beijing, miji mingine ya China Bara na kwingineko kwenye sheria ya kunyonga wahalifu wa madawa ya kulevya ili kuwapukutisha na kuwapunguza idadi yao kwa haraka ili vitendo hivyo vikome na hatimaye kulisafisha tena jina la Tanzania kimataifa.

Watanzania wachache wanaojihusiha na uhalifu wa madawa ya kulevya huko nje wanawakoseha fursa Watanzania wengine wenye nia safi ya kutaka kwenda kutafuta fursa za maisha na kufanya shughuli halali huko nje.
 
Wala haijaanza karibuni, ipo mda tu, ukiwa na passport ya Tanzania hata kama mweupe Kama karatasi lazima wakusearch zaidi. Sometime wanakuvua hadi nguo. Nchi ambayo ilikua ikisifika duniani kwa Amani na ucheshi sasa hivi inajulikana kama Nchi ya wasafirisha madawa.
Watanzania tuna shida sana kwa kupenda short cuts , hasa madawa ya kulevya , ukiwa na passport ya kitanzania unaweza kidhalilika kirahisi sana .
 
Watanzania tuna shida sana kwa kupenda short cuts , hasa madawa ya kulevya , ukiwa na passport ya kitanzania unaweza kidhalilika kirahisi sana .
Umeshasema Mainland China na Hong Kong wanasheria tofauti kuhusu madawa ya kulevya, halafu unapendekeza washitakiwa wa Hong Kong wapelekwe Mainland. Kwenye Sheria hakuna kitu kama hicho.
 
Umeshasema Mainland China na Hong Kong wanasheria tofauti kuhusu madawa ya kulevya, halafu unapendekeza washitakiwa wa Hong Kong wapelekwe Mainland. Kwenye Sheria hakuna kitu kama hicho.
Kuhusu sheria na makosa yanayohusu usalama wa nchi na watu wake, ikiwamo na makosa ya madawa ya kulevya, mtuhumiwa anaweza akahamishwa kutoka China Visiwani kwenda China Bara ili akashitakiwe huko Bara.

Hukuona zile vurugu zilizotokea huko Hong Kong kupinga Mabadiliko ya Sheria za Usalama zilzofanywa huko miaka michache iliyopita?
 
Kama iko hivyo basi poa.
 
Back
Top Bottom