Taarifa kutoka Ofisi ya RC Makonda

Taarifa kutoka Ofisi ya RC Makonda

TAARIFA MUHIMU KUTOKA OFISI YA RC MAKONDA

Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam inashangazwa na taarifa zinazo sambaa mtandaoni juu ya kuwepo kwa Mkutano wa Mkuu wa Mkoa, Mh. Paul Makonda na waandishi wa habari siku ya leo tarehe 31/08/2018 katika Hoteli ya Serena muda wa saa sita mchana.
Taarifa hizo hazina ukweli wowote .

Pia Mh Makonda anasikitishwa kuwepo kwa akaunti mbalimbali za mitandao ya jamii ikiwemo Twitter, Instagram na Face book zinazotumia majina yake na kusambaza mitandaoni taarifa mbalimbali ambazo kwa namna moja au nyingine zinajenga au kumoboa na moja kwa moja kumhusisha yeye. Akaunti pekee ya mawasiliano binafsi ni akaunti ya instagram yenye jina baba_keagan na si hizo nyingine.

Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa anaendelea na majukumu yake ya kila siku kama kawaida, anakaribisha wakazi wote waendelee kuja kupata huduma katika ofisi zake na zile za wilaya zake zote.

Mwisho Mkuu wa Mkoa ana kusisitiza wananchi wote kuendelea kuunga mkono jitihada za serikali ya awamu ya tano chini ya Dr John Pombe Magufuli katika kuwaletea maendeleo watanzania wote katika nyanja zote.

Asanteni.

Imetolewa na Kitengo cha Habari,
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa,
Dar es Salaaam.

Sent using Jamii Forums mobile app
Bado yupo ofisini mpaka sasa? Huyu itakuwa mshipa wa busara, aibu na fahamu ulishakatika!
 
Na hapo vipi?
IMG-20180830-WA0035.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
walimu wa dar mna gundu sana mlipoambiwa mtakuwa mnafiri bure dili likabuma now mnaletewa sofa bado dili limebuma kwani tataizo nini ndugu walimu wetu wapedwa
 
Katika hali isiyo ya kawaida jana katika mitaa ya kinondoni hasa mitaa ya Ufipa(makao makuu ya wauza madawa ya kulevya) kumesikika miziki na watu wakinywa pombe sana huku wakishangilia taarifa ya Makonda kukemewa na rais kuhusu suala la makontena.

Wauza madawa hawa wanaona muda wa Makonda kuondoka Dares salaam umefika hivyo kuwaachia uhuru wa kufanya biashara yao bila kubanwa.

Ikumbukwe tu kuwa biashara ya madawa ya kulevya haiathiri Makonda wala familia yake ,hao hao mnaoshangilia watoto wenu na ndiyo watatumia hayo madawa na kuwa vibaka wa kuja kuwaibia huko na wengine watakuja kuwa mazezeta.



Sent using Jamii Forums mobile app
Naona umelewa matapu tapu ujinga gani huu unaandika??

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hamu ya wa Tanzania kwa sasa ni Kusikia Huyu Bwana ameachia ngazi
 
Badala ya kuendelea kusikia blabla za Makonda nilitegemea kusikia taarifa ya Makonda kalipa kodi ya makontena.
 
Ameanza ku panic. Wale wote aliowavunjia heshma na kuwaita wauza madawa atakutana nao mitaani muda si mrefu. Ikumbukwe atakua hata ule ulinzi wa askari nane mpaka ishirini
Ipambe post na picha ya Makonda ikikagua gwaride
 
Back
Top Bottom