Taarifa kutoka Ofisi ya RC Makonda

Taarifa kutoka Ofisi ya RC Makonda

Ketoka

JF-Expert Member
Joined
Sep 23, 2015
Posts
1,121
Reaction score
1,981
TAARIFA MUHIMU KUTOKA OFISI YA RC MAKONDA

Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam inashangazwa na taarifa zinazo sambaa mtandaoni juu ya kuwepo kwa Mkutano wa Mkuu wa Mkoa, Mh. Paul Makonda na waandishi wa habari siku ya leo tarehe 31/08/2018 katika Hoteli ya Serena muda wa saa sita mchana.
Taarifa hizo hazina ukweli wowote .

Pia Mh Makonda anasikitishwa kuwepo kwa akaunti mbalimbali za mitandao ya jamii ikiwemo Twitter, Instagram na Face book zinazotumia majina yake na kusambaza mitandaoni taarifa mbalimbali ambazo kwa namna moja au nyingine zinajenga au kumoboa na moja kwa moja kumhusisha yeye. Akaunti pekee ya mawasiliano binafsi ni akaunti ya instagram yenye jina baba_keagan na si hizo nyingine.

Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa anaendelea na majukumu yake ya kila siku kama kawaida, anakaribisha wakazi wote waendelee kuja kupata huduma katika ofisi zake na zile za wilaya zake zote.

Mwisho Mkuu wa Mkoa ana kusisitiza wananchi wote kuendelea kuunga mkono jitihada za serikali ya awamu ya tano chini ya Dr John Pombe Magufuli katika kuwaletea maendeleo watanzania wote katika nyanja zote.

Asanteni.

Imetolewa na Kitengo cha Habari,
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa,
Dar es Salaaam.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii sinema ya Makontena, Makonda na Magufuli wanajua sana kuchezea watanzania.

Pamoja na yote, nampongeza Mpango kwa kusimama kidete katika kuhakikisha sheria ya kodi inafuatwa kwa kila mtanzania.

Tunajua lile Hotel la Jiwe Pale Mwanza lilikuwa lina subiri kontena lishushwe.

Sasa Jiwe na Mwanao najua mnatafuta pakutokeaa!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
TAARIFA MUHIMU KUTOKA OFISI YA RC MAKONDA

Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam inashangazwa na taarifa zinazo sambaa mtandaoni juu ya kuwepo kwa Mkutano wa Mkuu wa Mkoa, Mh. Paul Makonda na waandishi wa habari siku ya leo tarehe 31/08/2018 katika Hoteli ya Serena muda wa saa sita mchana.
Taarifa hizo hazina ukweli wowote .

Pia Mh Makonda anasikitishwa kuwepo kwa akaunti mbalimbali za mitandao ya jamii ikiwemo Twitter, Instagram na Face book zinazotumia majina yake na kusambaza mitandaoni taarifa mbalimbali ambazo kwa namna moja au nyingine zinajenga au kumoboa na moja kwa moja kumhusisha yeye. Akaunti pekee ya mawasiliano binafsi ni akaunti ya instagram yenye jina baba_keagan na si hizo nyingine.

Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa anaendelea na majukumu yake ya kila siku kama kawaida, anakaribisha wakazi wote waendelee kuja kupata huduma katika ofisi zake na zile za wilaya zake zote.

Mwisho Mkuu wa Mkoa ana kusisitiza wananchi wote kuendelea kuunga mkono jitihada za serikali ya awamu ya tano chini ya Dr John Pombe Magufuli katika kuwaletea maendeleo watanzania wote katika nyanja zote.

Asanteni.

Imetolewa na Kitengo cha Habari,
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa,
Dar es Salaaam.

Sent using Jamii Forums mobile app
Duu elimu ama kweli ni mzigo! instagram baba keagun nadhani hiyo ni mambo binafsi haikupaswa kutolewa katika taarifa hii ya ofisi ya mkoa.Taarifa Hii ilipaswa kuwa na mawasiliano ya kiofisi tuu.Nadhani huyu bado hajaelewa ndiyo amana hata makontena akaandika jina lake binafsi.
 
Hahahaaaa! Wakati afisa habari wake anaandaa statement hii mkolo alikuwa amejifungia chumbani anaongea na simu kama vile anagombana na mtu/watu! Alisikika akisema "ndo imeshakua hivyo sasa mimi nifanyeje? Hamnitishi bana amueni la kufanya! Hata mimi ni mwanaume msinitishe" hii ni kwa mujibu wa ka NZI kalichoko hapo ofisini kalikokuwa kakisubiri huduma!
 
“Akaunti pekee ya mawasiliano binafsi ni ya Instagram kwa jina la Baba Keagan.”

Akaunti binafsi ya baba Keagan haitakiwi kuongelewa kwenye official statement ya ofisi ya Regional Commisioner.

Yani pale mkoani Ilala hakuna msomi wa kumwambia Makonda mambo yako ya baba Keagan hayatuhusu, acha kuchanganya mambo yako binafsi na yale ya umma.
 
Hahahaaaa! Wakati afisa habari wake anaandaa statement hii mkolo alikuwa amejifungia chumbani anaongea na simu kama vile anagombana na mtu/watu! Alisikika akisema "ndo imeshakua hivyo sasa mimi nifanyeje? Hamnitishi bana amueni la kufanya! Hata mimi ni mwanaume msinitishe" hii ni kwa mujibu wa ka NZI kalichoko hapo ofisini kalikokuwa kakisubiri huduma!

Tehe tehe tehe, kumbeba punguani asiyesoma ni kazi kwelikweli. Pole mzee baba!!!
 
“Akaunti pekee ya mawasiliano binafsi ni ya Instagram kwa jina la Baba Keagan.”

Akaunti binafsi ya baba Keagan haitakiwi kuongelewa kwenye statement ya ofisi.

Yani pale mkoani Ilala hakuna msomi wa kumwambia Makonda mambo yako ya baba Keagan hayatuhusu, acha kuchanganya mambo yako binafsi na yale ya umma.

Shida shule. Ni fa fa fa!!!!
 
Back
Top Bottom