Taarifa kutoka Ofisi ya RC Makonda

Taarifa kutoka Ofisi ya RC Makonda

Ila jamaa kama hajatumbuliwa basi ana kitu kuhusu mwenye nchi
Kiongozi wetu akurupuki kwa kufuata miemko ya watu kwanza anayajua hayo makontena tatizo lake kuriko hata nyie.najua wengi ni waumini wa yule jamaa mchungaji kwa hili la makontena mkaona hapa pa kupoza hasira zenu.raisi aongozwi na

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nikechelewa kucheki taarifa ya habari mtanipa mstakabari wa leo kama kuna nini hukoo wana jf jaman
 
Hii sinema ya Makontena, Makonda na Magufuli wanajua sana kuchezea watanzania.

Pamoja na yote, nampongeza Mpango kwa kusimama kidete katika kuhakikisha sheria ya kodi inafuatwa kwa kila mtanzania.

Tunajua lile Hotel la Jiwe Pale Mwanza lilikuwa lina subiri kontena lishushwe.

Sasa Jiwe na Mwanao najua mnatafuta pakutokeaa!!

Sent using Jamii Forums mobile app
Meanwile lita 10000 za maziwa ya Azam kutoka zenji zimekwama bandarini mwezi mzima kisa kodi
We are on the raiti traki

Sent using Jamii Forums mobile app
 
TAARIFA MUHIMU KUTOKA OFISI YA RC MAKONDA

Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam inashangazwa na taarifa zinazo sambaa mtandaoni juu ya kuwepo kwa Mkutano wa Mkuu wa Mkoa, Mh. Paul Makonda na waandishi wa habari siku ya leo tarehe 31/08/2018 katika Hoteli ya Serena muda wa saa sita mchana.
Taarifa hizo hazina ukweli wowote .

Pia Mh Makonda anasikitishwa kuwepo kwa akaunti mbalimbali za mitandao ya jamii ikiwemo Twitter, Instagram na Face book zinazotumia majina yake na kusambaza mitandaoni taarifa mbalimbali ambazo kwa namna moja au nyingine zinajenga au kumoboa na moja kwa moja kumhusisha yeye. Akaunti pekee ya mawasiliano binafsi ni akaunti ya instagram yenye jina baba_keagan na si hizo nyingine.

Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa anaendelea na majukumu yake ya kila siku kama kawaida, anakaribisha wakazi wote waendelee kuja kupata huduma katika ofisi zake na zile za wilaya zake zote.

Mwisho Mkuu wa Mkoa ana kusisitiza wananchi wote kuendelea kuunga mkono jitihada za serikali ya awamu ya tano chini ya Dr John Pombe Magufuli katika kuwaletea maendeleo watanzania wote katika nyanja zote.

Asanteni.

Imetolewa na Kitengo cha Habari,
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa,
Dar es Salaaam.

Sent using Jamii Forums mobile app
Taarifa nzuri kwa watu wote wapenda maendeleo,Makonda chapa kazi maisha hayakosi changamoto

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom