Taarifa Kuhusu Mama Maria Nyerere si za Kweli

Taarifa Kuhusu Mama Maria Nyerere si za Kweli

Kuna taarifa nimepata hapa kuwa mama Maria Nyerere amefariki. Mwenye taarifa zaidi atupashe
jamani Si vizuri kuzushia wazazi wa Watu kifo. Taarifa hizo Si sahihi. Unayetangaza iweke nafasi yako kuwa ni Rosemary nyerere au madaraka Nyerere u naskia Watu wanasambaza Habari za Mzazi wako Kafa utajisikiaje! Usimtendee mwenzio vitu ambavyo usingependa kufanyika kwako.
 
Taarifa nilizopata ni kuwa, TISS walibuni ujinga huu ili kuwapoteza wananchi waache kujadili issue ya Dr. Slaa kutaka kuuawa na TISS kwa kushirikiana na CCM.

Shame on you TISS

Dr Slaa amewaharibu uwezo wenu wa kufikiri.
 
Wenye habari watuze kama ni kweli mama aliyetupigania uhuru hatunaye tena Mungu amuweke mahala pema peponi Mungu ibariki tanzania.
================

TAARIFA RASMI: Ujumbe unaosambazwa kwenye mitandao ya kijamii (JF ikiwemo) kuwa Mama Maria Nyerere kafariki SI SAHIHI. Ukiupata ujumbe upuuze.

JamiiForums.

Mmechelewa sana kukanusha siku nyingine muwe mnawahi kutoa taarifa mbaya kama hii. Mkirudia tena vibarua vinaota nyasi.
 
HAYO NI MAMBO YA MZEE WA MTAMA, NA LEO DADA SHEILA Mbaga kamaliza kazi humu.. Nona Mods wamefuta hizo nyuzi.. kama ni ukweli utabaki ukweli tu, ...
 
Hili ni lazima tulikemee kwa umoja wetu bila kujali itikadi zetu ama dini zetu,

Leo kumezushwa habari yakuwa Mama Maria Nyerere amefariki dunia, habari hii imezushwa na idara maalum nchini chini ya maelekezo ya ccm baada ya kikao cha jana usiku cha viongozi wa ccm na serikali kufuatia kubumburuka kwa mkakati wa kumuua Dr Slaa juzi usiku.

Hali ya ccm ni mbaya sana baada ya kubainika mpango huo, na njia pekee ilikuwa ni kuwaondoa watu kwenye habari hiyo kwakuzusha kuwa Mama Maria Nyerere amefariki.

Hii ni dhihaka kubwa kwa familia ya mama Maria Nyerere na heshima ya Mwalimu Nyerere kwaujumla, ifahamike kuwa leo mda huu kikao cha wafanyabiashara wakubwa na marafiki wa ccm wapo Butiama wakiendelea na kikao cha kumuunga mkono Makongoro Nyerere agombea urais katika kilekile kinachotajwa kuwa ccm hurithishana utawala (utawala wa kifalme), Tujiulize, dhihaka hii inania njema kwa Familia ya Mwalimu Nyerere na Ligancy yake?

Tupinge kwa nguvu zote, Mama Maria Nyerere ni alama ya utaifa na taifa letu. Ccm waendelee kusingiziana wenyewe kwa wenyewe hukohuko Lumumba.
mkuu mods hawajakufanyia fair jana uzi wako wa hicho kikao uliweka wataufuta
 
naona hii mada imesababisha watu wamekula ban toka kwa mod.pole sana familia ya mama nyerere.lakini pia poleni kwa mlio pigwa ban.bila shaka sheria na kanuni za JF zilizingatiwa.:biggrin: CC charminglady and others
ban.jpg
 
HAbari kutoka kwa mtu wa karibu wa familia, ni kwamba Mama Maria Nyerere amefariki dunia.
 
Siku ya mapumziko kitaifa hiyoooooo inakuja wajameni!!
 
Back
Top Bottom