Taarifa fupi ya utekelezaji wa mapendekezo ya kikosi kazi kilichoshughulikia masuala ya demokrasia ya vyama vingi nchini

Venus Star

JF-Expert Member
Dec 6, 2018
19,695
59,850
Nimeambatanisha Ripoti ya mapendekezo ya Kamati. Lakini nitayaorodhesha mapendekeo hayo hapa:-

  1. Kuhusu Mikutano ya hadhara na Mikutano ya ndani ya Vyama vya Siasa
  2. Kuhusu demokrasia ndani ya vyama vya siasa
  3. Kuhusu ruzuku kwa vyama vya siasa inayotolewa na Serikali.
  4. Kuhusu uhuru wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi.
  5. Kuhusu uteuzi wa wajumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi.
  6. Kuhusu matokeo ya uchaguzi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuhojiwa Mahakamani.
  7. Kuhusu watendaji wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi
  8. Kuhusu Bajeti ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi.
  9. Kuhusu Sheria zinazosimamia masuala ya uchaguzi.
  10. Kuhusu matumizi ya TEHAMA katika uchaguzi.
  11. Kuhusu ushiriki wa Wanawake katika Siasa, Demokrasia na Uongozi.
  12. Kuhusu ushiriki wa Watu Wenye Ulemavu katika Siasa, Demokrasia na Uongozi.
  13. Kuhusu ushiriki wa vijana katika Siasa, Demokrasia na Uongozi.
  14. Kuhusu elimu ya uraia.
  15. Kuhusu suala la kuzuia na kupambana na Rushwa katika Siasa na Uchaguzi.
  16. Kuhusu mfumo wa maridhiano ili kudumisha haki, amani, utulivu na umoja wa kitaifa.
  17. Kuhusu uhusiano wa mawasiliano kwa umma, vyombo vya habari na siasa.
  18. Kuhusu Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mambo hayo 18 ndiyo yaliyotolewa mapendekezo
 
Attachments

  • 12.09.2023 Taarifa ya Utekelezaji wa Mapendekezo ya Kikosi Kazi kuhusu Masuala ya Demokrasia y...pdf
    76.3 KB · Views: 3
Nitajaribu kuweka hapa mapendekezo yalitotolewa kuhusu katiba mpya:
 
Nimeambatanisha Ripoti ya mapendekezo ya Kamati. Lakini nitayaorodhesha mapendekeo hayo hapa:-

  1. Kuhusu Mikutano ya hadhara na Mikutano ya ndani ya Vyama vya Siasa
  2. Kuhusu demokrasia ndani ya vyama vya siasa
  3. Kuhusu ruzuku kwa vyama vya siasa inayotolewa na Serikali.
  4. Kuhusu uhuru wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi.
  5. Kuhusu uteuzi wa wajumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi.
  6. Kuhusu matokeo ya uchaguzi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuhojiwa Mahakamani.
  7. Kuhusu watendaji wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi
  8. Kuhusu Bajeti ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi.
  9. Kuhusu Sheria zinazosimamia masuala ya uchaguzi.
  10. Kuhusu matumizi ya TEHAMA katika uchaguzi.
  11. Kuhusu ushiriki wa Wanawake katika Siasa, Demokrasia na Uongozi.
  12. Kuhusu ushiriki wa Watu Wenye Ulemavu katika Siasa, Demokrasia na Uongozi.
  13. Kuhusu ushiriki wa vijana katika Siasa, Demokrasia na Uongozi.
  14. Kuhusu elimu ya uraia.
  15. Kuhusu suala la kuzuia na kupambana na Rushwa katika Siasa na Uchaguzi.
  16. Kuhusu mfumo wa maridhiano ili kudumisha haki, amani, utulivu na umoja wa kitaifa.
  17. Kuhusu uhusiano wa mawasiliano kwa umma, vyombo vya habari na siasa.
  18. Kuhusu Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mambo hayo 18 ndiyo yaliyotolewa mapendekezo
Mbona hamna kuhusu upatikanaji wa majaji na uhuru wa mahakama!
 
Hizi mambo za kusoma ndio Watanzania Huwa hawawezi. Watu wanasubiri Mtu mmoja aandike sentesi Moja tu kisha waanze kutiririka.
 
Kuhusu wajumbe wa tume ya taifa ya uchaguzi.

Kwa maoni yangu bado hiyo tume haitakuwa huru kwasabb viongozi wa tume wanaingia kwa nyadhifa zao amabzo wanazipata kwa kiteuliwa na rais (mwenyekiti wa ccm) ambaye ana maslahi na uchaguzi.

Huu ni uzwazwa. Yaani ndiyo wamekaa wakipoteza muda na fedha zetu halafu wanatuletea upuuzi kama huu???
 
Basi toa mapendekezo yako. Ungependa viongozi wa hiyo tume watoke wapi? Hili huwa ni suala gumu sana.

Huko Zanzibar walikubaliana vyama vya siasa kugawana hizo nafasi za viongozi wa tume ya uchaguzi. Kilichotokea tulikiona na tutaendelea kukiona; yaani vurugu tupu hadi ilifikia kurushiana makonde ndani ya tume na Mwenyekiti wa tume kufuta uchaguzi. Huko Kenya ndiyo balaa zaidi hadi kusababisha vifo vya maelfu ya watu kila baada ya uchaguzi mkuu.

The best practice kwa maoni yangu ni kwamba tufuate mfano wa India ambayo mfumo wa tume ya uchaguzi umewekwa kwenye mfumo wa judicially (mahakama) ya nchi hadi ngazi za chini. Resident or District Magistrates ndiyo wasimamizi wa uchaguzi badala ya wakurugenzi wa halmashauri na kadhalika. Wewe Sexless unapendekeza nini?
 
Ili kufanikiwa ktk hili rais aondolewe madaraka ya kuteua kiongozi yeyote ktk mihimili mmingine (mahakama na bunge). Spika apatikane kwa kumba bila hata ikibidi asiwe mbunge. Tutaondoa tatizo la sheria na mikataba ya hovyo kupitishwa, hivyo sheria bora za uchaguzi zitaundwa.

Na majaji wapatikane kwa njia za ndani ya mifumo ya kitaaluma huko huko kwenye mhimili wao.

Halafu vyama vishirikiane kumpata mwenyekiti wa tume na wajumbe wake.

Hata pakitokea ukiukwaji wa taratinu basi tuwe na Imani kwamba mahakama zitatenda haki na hazitapokea amri kutoka juu.
 
Back
Top Bottom