Stories of Change - 2022 Competition

Charles16

New Member
Jul 20, 2022
1
0
TAALUMA YANGU MASHAKANI.

Elimu Tanzania imekuwa sekta ambayo inatazamwa kama chanzo au nyenzo kuu ya kuzalisha wasomi au watatuzi wengi wa matatizo yanayoikumba jamii katika nyanja zote za maisha lakini imekuwa tofauti hadi sas wasomi kuzalaulika kwa jamii na kuonekana kama wajinga maana wasomi Hao Hao ndo wanataka msaada wa utatuzi wa matatizo ya maisha Yao.

Sekta ya elimu imekuwa ikikumbwa na kashfa kubwa ya ushalilishaji na unyanyasi wa kijinsia, rushwa, na hata ubadhilifu wa fedha kwa (level) ya Taifa(wizara) hadi kwa mwalimu mmoja mmoja.

Rushwa imekuwa tatizo kubwa katika maisha ya elimu ya juu, rushwa ya ngono, rushwa ya fedha: Inaumiza sana unasoma usiku kucha kesho ukafanye mtihani lakini rafiki yako amekesha club na kesho hafanyi mtihani na matokeo yanatoka mwenzako alokesha club(kumbi za starehe) amejaziwa matokeo na amefaulu kuliko wewe hapo amempa pesa kuja ziwa matokeo ya semester nzima lectures au IT wa chuo kwake maisha Safi na GPA ya juu kabisa first class au Second upper class masikini wasio na pesa wala asset wanaendeleaje teseka inaumiza sana.

Lakini mtu huyo anapata ajira shule au college kufundisha kwasababu selikari inasajili kutokana na GPA lakini hawaangalii ufanisi wa kazi ndo mwisho anakuwa mtumishi anaendeleza rushwa na mwanafunzi anapata tatizo la kuhitaji msaada wa kisaikolojia anashindwa msaidia kwasababu yeye mwenyewe anahitaji hyo huduma maana ni mgonjwa.

Ubadhilifu wa fedha za selikari katika nyanja ya elimu hasa elimu ya juu (vyuo vikuu) ni mkubwa selikari inatenga bajeti ya mikopo ya elimu ya juu kwa wanafunzi wote wenye sifa kuwapatia lakini baada ya kuwapatia huo mkopo je wanafuatilia pesa inatendewa haki hao wanaowapa? Uhalisia upo hivi vijana wengi wanaopewa mkopo wapo wanajua wajibu wao lakini kuna wimbi la hawa ambao wanasoma semester moja ya masomo au mwaka mmoja lakini miaka inayofuata huyu mtu hasomi tena anasaini mkopo anaenda kufanya starehe na mkopo unaingia bila selikari kujua kama walompatia mkopo je anaufanyia kazi kama walivyotaraji jibu hakuna ufuatiliaji.

Mitaala ya vyuo vikuu inakidhi mahitaji ya nchi na kasi ya uchumi wa blue wa nchi na dunia kwa ujumla? Jibu hapana Mitaala haikidhi wengi wanasoma nadharia (theoretical) na cyo vitendo (practical) mwanafunzi wa chuo kikuu anasomea degree ya ualimu miaka mitatu (3) anavaaa joho anasherekea either kwa GPA kubwa au ndogo lakini mwalimu huyo huyo amemaliza kozi miaka mi3 hajui hata kuwasha laptop au kutumia kompyuta hata kuandaa document za shule au zake tu hajui na ni mwalimu anaenda kumuandaa mwanafunzi?

Nini kufanyike!
Ili sekta ya elimu iiepuke rushwa ya pesa, mali au penzi katika kumpatia matokeo mwanafunzi mzembe masomoni kwa kutumia fimbo ya pesa au mwili wake kupata matokeo ni vyema ingetumia mfumo kama wa shule za sekondari mtihani wa kozi husika uandaliwe na taasisi husika ya vyuo vikuu Tanzania (Tanzania Commission University. TCU) kutokana na kuwa na watu waadilifu tu na wanaweza kulifanikisha hilo. Na hata usahihishaji wa mitihani ya kozi husika Hao Hao wawajibike kusahihisha na kupanga matokeo ya kozi husika kabisa kama shule za msingi, sekondari imewezekana hata huku inawezekana kupitia hilo idara ya elimu rushwa itakwisha kabisa na pia itazalisha wasomi na sio waigizaji wasomi. Kwasababu bila kutatua tatizo la rushwa huku chini taasisi ya kupambana na kuzuia rushwa haitafaikisha lolote zaidi ya kupoteza wakati ila suluhishi ni hili.

Kutatua tatizo la ubadhilifu wa fedha vyuo vikuu selikari chini ya bodi ya mikopo Higher Education Students Loan Board(HESLB) inapaswa kutengeneza ufuatiliaji thabiti kila mda wa kusaini pesa ya kujikimu ili kujua nani yupo chuoni na yupi hayupo lakini kutuma fomu kusaini tu bila uhakiki wengi wao wanasainiwa na marafiki ma hadi wakuu wa idara wanawasainia ili tu pesa ya ada iingie bila kujua kwamba ni hasara kwa nchi na ndo maana miaka nenda rudi bodi ya mikopo haipati marejesho badala ya hasara tu ufuatiliaji thabiti uwepo vyuoni hilo tatizo litakuwa lishatatuliwa hasa vyuo vya asasi binafsi au mashirika.

Mitaala vyuoni ipitiwe upya na kubadilishwa au kufanyiwa marekebisho kwa level ya chuo kikuu kutokana na kasi ya maendeleo ya teknolojia ya dunia kwasasa kozi yoyote chuo kikuu iwepo kozi ya kompyuta Kama ya lazma na kwa level zote hiyo itamsaidia mwana chuo kumaliza chuo na kuweza kujua kutumia kompyuta na pia kujifunza mambo mengi mtandani na kupelekea kujiajiri.

Kozi ya usuluhishi na saikolojikalia ipewe kipaumbele vyuoni kutokana na matatizo mengi yanaikumba jamii ya Tanzania na watu wake hasa wanafunzi wote Tanzania ifundishwe na iwe heshma kutokana wanafunzi wengi wanaptia matatizo ya kustahili kupewa ushauri lakini wanashidbwa PA kuyapeleka kupewa msaada kutokana na kuwa na wataalamu wachache kwenye swala hilo ila kupitia kuzalisha wasomi wengi wa saikolojikalia na usuluhishi itamsaidia kutatua matatizo mengi kwenye jamii, shuleni na hata vyuoni.

Hitimisho Tanzania nakupenda kwa moyo wote! Watu wako wakijua wajibu wao katika kazi zao zaidi ya kudai haki zao basi jina lako Tanzania litang’aa na kila jirani yako atatamani kuwa kama wewe haswa. Naomba uwaambie watu wako kila mtu ajue wajibu wake na si kudai tu haki hasa ndugu zetu walimu waambie wasidai kupandishwa madaraja wakati wajibu wake wa kundisha hajui, Naomba muulize unataka kupanda daraja siyo? Je tangu uanze kazi ya kundisha umebadidilisha maisha ya wangapi? Je umepata A.,B.,C ngapi? Unetatua matatizo ya kijamii ya mwanafunzi binafsi wangapi? Akikujibu vyema mpandishe daraja. Ila mkumbushe

#HAKI BILA WAJIBU NI KAZI BURE.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom