Sakasaka Mao
JF-Expert Member
- Sep 29, 2016
- 14,948
- 21,023
Thread ya kibabe sana hii.Samaleko...
Nilikutana na binti fulani wenyewe wanasema English figure!, kitoto cheupe rangi ya mtume, kilichonipendeza zaidi ni muonekano wa sura yake!, anamacho fulani hivi akikuangalia unaweza ukahisi anakutaka ama ameshakukubalia!.. basi hicho ndicho kimenifanya niwe taabani majinuni nisiekuwa na hamu!.
Shida ilianzia hapa, siku ya kwanza nilikutana nae eneo lake la kazi nikamsemesha!, ajabu akawa amenikazia macho sana nikamwambia shida yangu akanihudumia japo alikosea order ila siku mind!.
siku nyengine ikawa hivyohivyo kila nikikutananae basi hata kama hatutasemeshana lkn lazima macho yangu na yake yakutane na kwa namna alivyokuwa ananiangalia nikaanza kushituka kuna nini kinaendelea..?!
Shababi bin malavidavi nikajua mtoto ameshanielewa!, nikaona huyu nikiimbisha tu hachomoi tena nikaona sitaki habari zakuomba namba naenda kumface ana kwa ana!.
kama wasemavyo waswahili "usiku wa deni haukawii kukucha!". siku ikawadia nikamuita mtoto nikaanza kuimbisha mubashara, mtoto akawa anaendelea kuniangalia lilelile jicho lake lakunivuruga basi hapo mimi ndo najua kadata na kaelewa mistari, basi jasusi la mahaba nikawa nashuka tu madude!, japo muda mwengine alikuwa akionyesha kama kutokunielewa hivi lkn nikawa natambaa na biti kama Ngwair kwenye wimbo wake wa "She got a gwan".
Nilimwaga sera zangu pale, huku nikijiachia na swaga zangu zakinyamwezi lakini hatima yake alinikataa, yani hakuomba hata anifikirie ni aliichapa palepale!. ule unyamwezi niliokuwa nimeuvaa ukavulika!, yale maneno yakijasusi mahaba yakatokomea pasipo fahamika!.. kwanini..? kwasababu mimi nilienda nikiwa natambua huyu hapindui maana dalili alikuwa ameshanionyesha.
niliondoka lile eneo nikiwa kama mtu alienyimwa kitambulisho cha NIDA!.
Ikapita wiki nikaja kurudi anapofanya kazi sasa hapo ndipo nilipokuja kuelewa kuwa ile angalia yake ilikuwa na maana gani!, kumbe yule mtoto anatatizo la usikivu yani kusikia anasikia lakini usikivu wake si mkubwa!, hivyo mara nyingi anakuwa anaangalia mtu mdomoni anavyoongea ili aweze kuelewa unaongea nini kwa maneno ambayo hatayasikia!..
Mimi baada yakugundua hilo kusema kweli nimejikuta najilaumu sana kwa kushindwa kumuelewa toka awali, hivyo nikaamua kutanguliza hamu zangu kumbe dada wa watu wala hana shida na huba langu!, hapa nipo taabani majinuni sasahivi nahesabika kama jitu la hovyo mbele zake!.
Kuna jambo sitaki uendelee nalo kichwani kukukandamizia saikolojia yako bhana!
Hapo uliplay party vizuri, namaanisha uliwajibika kiume.
Mkadirio wako kwa mwanamke kumpima kama 'kajaa' ama 'kakuelewa', nami hutumia kipimo hicho hicho cha macho, sina kipimo kingine.
Wale wa matabasamu makubwa ama cheko za kujichekesha kila tuangalianapo, hao huwaweka kwenye kundi la mitego ya rushwa za ngono!
Naungana na wewe kwamba, kwa condition hiyo, hata mimi ningedhalilika, maana ningepita mle mle ulimopita wewe, lakini nisingejilaumu!
Wakongwe tunaita 'felia' za kawaida katika harakati za pimbi, wala si za kujali wala kusononekea.