Taa za barabarani ni kero/zinadumaza uchumi

Mparee2

JF-Expert Member
Sep 2, 2012
2,586
4,274
Nimekuwa napita kwenye taa za barabarani maarufu ka traffic light Naona zimekuwa ni kero saana kwani zina fanya barabara kuu highway itumike muda mfupi sana.

Na maanisha kwa barabara zimekutana kama cross (jumlisha) barabara hufungwa karibia masaa sita kwa siku ( kila moja)
Hii ni upotevu mkubwa wa muda na rasmali watu, na pukunguza uzalishaji.

HUWA NAJIULIZA:
1. Hivi hawa wataalam wetu wameshindwa kuweka sensor itakayo fanya taa iwashe ule upande wenye magari/mengi kwa muda mrefu zaidi, na kama upande hauna magari haiwashi au kama gari moja likipita inazima na kuwasha pengine.

2. Hivi wataalam wameshindwa kufanya tu timing kwa taa zilizopo karibu karibu kuwa, wakati ya kwanza ina zima ya mbele yake iwake ili watu wasisogee dakika moja na kusimama tena.

3. Kama hatuwezi kupata hizo solution kwa mtazamo wangu wangetoa baadhi ya taa ziende makumbusho, badala yake waweke tu Round about na pengine kubwa kama ile ya Msamvu, Morogoro. pale ni hub kubwa ila hakuna traffic jam hata siku moja.

Tatizo letu tunasubiri kila kitu hadi wazungu waanze, we don't think out of box zaidi utashangaa eti mtu wa University anasema amegundua gari/ndege/etc with 25% efficiency?

Badala ya kubuni vitu/technologia mpya ya kurahishia watu maisha.
 
Wabongi wajuaji kweli! Waliwahi sema pale kijazi interchange inayovuka toka urafiki kwenda ubungo maji magari makubwa hayatopita pale ni padogo
images%20(16).jpg
 
2. Hivi wataalam wameshindwa kufanya tu timing kwa taa zilizopo karibu karibu kuwa, wakati ya kwanza ina zima ya mbele yake iwake ili watu wasisogee dakika moja na kusimama tena
Kwa uzoefu wangu wa barabara chache za Dar, ikiwemo mpya kutoka Mwenge hadi Morocco taa ziko coordinated. Ukiweza kupata taa moja kijani unaweza kupita zote kutoka Mwenge hadi Morocco. Vile vile nishashuhudi zaidi ya mara moja nimepita green kuanzia st.peters mpaka taa za maktaba kuu pale kote unakutana na green.
 
Kama zina work in harmony basi ni sahihi sababu hai make sense uzuie gari zinazokwenda uelekeo mmoja yani!

Unakuta gari inaruhusiwa Tazara pale mfugale inaenda kuzuiwa Taa za temeke pale! Inaruhusiwa Taifa inaenda kuzuiwa taa za kurasini!

Taa zote zinatakiwa ziwake na kwa muda mfupi mfupi! Ili kuzuia kuwaweka watu mda mrefu wanasubiria taa halafu zinawaka kidogo tu na kuzima kama taa za kuelekea sinza makaburin pale sam nujoma road! Zinaweka green mda mfupi sana ila red mda mrefu kichizi hadi zinakera.
 
Akishakaa mtu(askari wa usalama barabarani) hakuna tena ile coordination ya robot.
 
Taa zote zinatakiwa ziwake na kwa muda mfupi mfupi! Ili kuzuia kuwaweka watu mda mrefu wanasubiria taa halafu zinawaka kidogo tu na kuzima kama taa za kuelekea sinza makaburin pale sam nujoma road! Zinaweka green mda mfupi sana ila red mda mrefu kichizi hadi zinakera.
Hata hii pia sio nzuri. Inatakiwa ziwake kulingana na wingi wa magari kwenye barabara husika. Mfano pale aga khan zinawaka kwa muda sawa matokeo yake kunakuwa na foleni uelekeo wa posta/mwenge huku uelekeo wa aga khan hospital hamna kabisa magari. Sehemu kama hii inabidi kwenye njia kuu ziwake muda mrefu.

Taa za makutano ya kinondoni na kenyata ikifika saa mbili au tatu usiku zinaanza kubadilika kwa muda mfupi mfupi zenyewe, ikifika saa nne na kuendelea inawaka ile ya njano pande zote kuwa tumieni utashi wenu muda huu hamna magari mengi. Mida hii ndio unaosha taa zote hadi uendako!
 
Na hao mi ndio naona wanasababisha foleni yani! Wangeacha taa zifanye kazi
Kama kuna foleni peak hours wasipokaa hawa jamaa watu wanafunga njia! Kuna ile taa zimeruhusu ila njia imejaa magari watu wanaenda kurundikana katiktaki ya junction! Madereva wengi bongo vichaa!
 
Kinachokera pale Ubungo kwa sasa ni zile rasta upande wa barabara inayotokea na kuelekea Mbezi...

Zile rasta zimekuwa ni chanzo cha foleni wakati wa busy hours na shida yote ni kwa sababu ya kulazimisha kuweka kituo cha BRT karibu na daraja...

Upande mmoja wa daraja kuna kituo, na upande mwingine tena kuna kituo...
 
Kama kuna foleni peak hours wasipokaa hawa jamaa watu wanafunga njia! Kuna ile taa zimeruhusu ila njia imejaa magari watu wanaenda kurundikana katiktaki ya junction! Madereva wengi bongo vichaa!
Watu wakikaa kwny junction asipokuja trafic hamtoki mnabaki kurushiana matusi tu kila mtu anaona mwenzie ndio kazingua
 
Kama kuna foleni peak hours wasipokaa hawa jamaa watu wanafunga njia! Kuna ile taa zimeruhusu ila njia imejaa magari watu wanaenda kurundikana katiktaki ya junction! Madereva wengi bongo vichaa!
Ahaaa dah bongo nyoso kweli yani kila mtu anajifanya ana haraka 😅😅😅 hata round about ya Mlimani pale kazi ni hio hio!
 
Kwa uzoefu wangu wa barabara chache za Dar, ikiwemo mpya kutoka Mwenge hadi Morocco taa ziko coordinated. Ukiweza kupata taa moja kijani unaweza kupita zote kutoka Mwenge hadi Morocco. Vile vile nishashuhudi zaidi ya mara moja nimepita green kuanzia st.peters mpaka taa za maktaba kuu pale kote unakutana na green.
Kama wamefanya hivyo ni vizuri
Japo kwa miji mingine niyopita kama Arusha bado kabisa (Kuna taa kabla ya sanawari (Nafikiri Philips), halafu Sanawari/Mianziri/ triple A zote hazicommunicate
Ila ukweli Suluhisho ni Sensor
Hivi ni kweli kuwa hatuwezi kutengeneza Sensor???, wakati wachina wanatengeneza sensor hata za kuweka kwenye taa za shs 5000, Mbona rahisi ; tuwape tenda watutengenezee
YAANI UNAWEZA KUPOTEZA 10mins KUSUBIRI TAA IWAKE WAKATI HUKO ILIKORUHUSU HAKUNA GARI HATA MOJA, UTAFIKIRI TUPO KARINE YA 18...TUNAHITAJI KUCHUKUA HATUA!!!
 
Back
Top Bottom