Taa ya kijani (green light)

Taa ya kijani (green light)

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
376,454
Reaction score
872,085
Kwenye sheria za barabarani kuna taa za aina tatu kijani,nyekundu ,na njano:-

Kijani ni kuruhusiwa kupita au kuendelea na safari

Njano ni tahadhari ya kujiandaa kupita au kusimama

Nyekundu ni hatari usipite

Kwenye mahusiano taa hizo pia zinahusika sana

Kijani umepewa ruhusa hata kama si ya maneno dalili zitaonyesha tu umeshapendwa au umeshakubaliwa.

Njano ina mawili ni tahadhari ya kuachwa kama usipojirekebisha na mambo fulanifulani saa nyingine mfuko unahusika.

Red ni mbaya ukiwashiwa taa hii ujue ndo kwaheri umeshakula kibuti.

kumbuka taa ya kijani ni tamu sana ila red imebeba maumivu !tumo safarini na kila siku kila saa hizi taa zinatuwakia kama kama zinavyowaka zile za barabarani
 
aiseeee naomba taa nyekundu isiniwakie kwenye safari yangu ya mapenzii milele vinginevyo niiwashe mimi
 
Ni kwel hatupend taa nyekundu...
Ila hujui changamoto taa za njano zinaongeza ladha ya penzi na pia inakupa changamoto how to solve problems??
Kijani always.........
 
aiseeee naomba taa nyekundu isiniwakie kwenye safari yangu ya mapenzii milele vinginevyo niiwashe mimi

Kama ilivyo barabarani hata katika mapenzi taa nyekundu imegharimu maisha ya wengi ,wale walionusurika wamebaki na makovu na ulemavu wa hisia milele
 
aiseeee naomba taa nyekundu isiniwakie kwenye safari yangu ya mapenzii milele vinginevyo niiwashe mimi

mkuki kwa nguruwe eeeeeeeeeeeeh...
uwashe wewe kisa?? mwenzio hana mikono au
 
Kwenye sheria za barabarani kuna taa za aina tatu kijani nyekundu na njano
Kijani ni kuruhusiwa kupita au kuendelea na safari
Njano ni tahadhari ya kujiandaa kupita au kusimama
Nyekundu ni hatari usipite
Kwenye mahusiano taa hizo pia zinahusika sana
Kijani umepewa ruhusa hata kama si ya maneno dalili zitaonyesha tu umeshapendwa au umeshakubaliwa
Njano ina mawili ni tahadhari ya kuachwa kama usipojirekebisha na mambo fulanifulani saa nyingine mfuko unahusika
Red ni mbaya ukiwashiwa taa hii ujue ndo kwaheri umeshakula kibuti
kumbuka taa ya kijani ni tamu sana ila red imebeba maumivu !tumo safarini na kila siku kila saa hizi taa zinatuwakia kama kama zinavyowaka zile za barabarani

mie si najitiaga porn star..hua daima ni KIJANI TUU kama bendera ya mkombozi wangu..:eyebrows::eyebrows:
 
Kwasheria za barabarani wewe ukiwashiwa red kuna mwenzako kawashiwa green (anaendesha) na mwengine kwake inawaka yellow. Je mshana jr na huko ulikozungumzia wewe ni same?
 
Last edited by a moderator:
Kwa sie tunaojua vichochoro huwa hatusimami kwenye foleni (kesa eti redi) unless umeamua!
 
Kwasheria za barabarani wewe ukiwashiwa red kuna mwenzako kawashiwa green (anaendesha) na mwengine kwake inawaka yellow. Je mshana jr na huko ulikozungumzia wewe ni same?
Tunaishi katika dunia inayozunguka nothing last forever kuna usiku kuna mchana kuna kupata kuna kukosa nk nk !!!ukiona umependwa ujue kuna mjinga kaachwa ukiona umeachwa ujue kuna mjanja kapendwa ndio maisha yetu mpaka tunakufa .Kumbuka mapenzi kama maisha ya binadamu wanyama miti mimea na vingine vingi huzaliwa kukua na kufa
 
Last edited by a moderator:
Kwa sie tunaojua vichochoro huwa hatusimami kwenye foleni (kesa eti redi) unless umeamua!

Kuna vibaka huko...! Halafu kumbuka Short cut is the longest way you were not going! !!!!
 
Mmmh.. mapenzi bhana kama vile hayana fomula.
 
Back
Top Bottom