Sikonge...
umenifadhaisha sana na comments zako ndugu..T.I na Soulja Boy unawaweka kundi moja?ama?na wimbo mmoja wa Neyo ndio unakufanya uamue kuwa direction ya mziki inabadilika?uchambuzi wa aina gani huo?miaka ya 70 hakukuwa na artists wengi wala miziki mingi kama ilivyo sasa,hiyo ni moja ya sababu za miziki ya wakati huo kukaa kwenye chati kwa muda mrefu...with all due respect,Michael Jackson hawezi kaa kwenye chati kwa muda mrefu sasa hivi kama alivyofanya kwenye thriller miaka ya 80 hata iweje...nikatalie nikuskie!si ni Michael yuleyule?nini tatizo?ama hajui kuimba na kucheza nae siku hizi?industry imebadilika,na hii ndio ya wakati wetu...tafadhali uje na respect japo kidogo kwa kazi tunazoziheshimu wakati mwingine...God bless you!
Semjato,
Pamoja na heshima yote kwa wasanii wa sasa. Wengi wao tuseme ukweli wanalipua kazi. Mtu anaweka bits mbili tatu basi kamaliza kazi na mengine yanabaki kuwa ni maneno tu (RAP). Sijui una umri gani ila kuna siku utakuja kumbuka maneno yangu kuwa kila baada ya miaka 10 mziki duniani unabadilika. Sasa hivi utakuja kutawala wa speed kali. Nipe miaka miwili tuje tuongee. Ila hii sidhani kama itakaa sana na watapunguza kidogo speed. Ni kama mwisho wa 80 na mwanzoni mwa 90 walipotokea akina Technotronic, Mc Hammer, Bobby Brown, Vanilla Ice etc. Hawa hawakudumu sana. Miaka ya 60 kulikuwa na miziki mizuri sana pamoja na kuwa ilikuwa michache. Ndiyo maana duniani hadi leo unaona akina Ringo Star wanakataa hadi kusign autograph. The Beetles, Chuck Berry, Elvis, Jackson 5, Diana Ross etc. Na hata kwa Tanzania tukawa na akina Sallum Abdallah, Juma Kilaza, Marijan Shabaan etc. Miziki yao hadi leo inapigwa. Miaka ya 70 ilikuwa ovyo hadi Tz wakawa wamehamia Congo na RSA. Ndipo akina Mangwana, Luambo, Tabu Ley, Lipua Lipua, Soul brothers etc wakapa umaarufu sana. Kwa Ulaya ni akina ABBA kutoka Sweden wakawa marufu sana. Mwisho wa 70 ndipo ukaja mfumuko wa bendi. Kool & the Gang, Earth wind and Fire, Bee Gees, Michael Jackson, Comadoes, Bobby Marley, Tosh, Marvin Gaye, tina Turner etc wakaja juu sana na ushindani ukawa mkali si kawaida. Ila ni kweli album zilikuwa chache. Ila Miaka ya 90 hapo usiseme kijana. Computer zikawa nyingi na CD madukani kibao. Ushindani hadi wanauwana (2Pac & BIG). Miziki ilikuwepo ya kila aina. Rap, soul, dancehall, na hadi akina Vaneca Mae na kizeze chake akapata dakika 5 zake. Hapa usiseme kuwa kushika chart wakati huo ilikuwa rahisi. Kumbuka hata wakali kama Dr. Dre, George Clinton na Roger Troutman (wimbo wa 2Pac Califonia Love) walikuwa wanajificha kwenye migongo ya vijana kwani na ukali wao wote, soko lilikuwa lisingewakubali. Wengi wakakimbilia kuwa maproducer. Mfano mzuri ni watu wote walikokuwa Zomba wakideal na Billy Ocean, ndiyo hao hao wako na Britney Spear. Nafikiri hata mwenyewe yuko nyuma ya mafanikio ya wanamuziki kadhaa.
Imeingia miaka ya 2000, mhh kivumbi kikaanza. Mziki unavyokuwa mbaya, ndivyo unavyozidi kupendwa. Ila mapenzi hayo yanakuwa ya muda mfupi. Siwezi sema kuwa miziki yote ilikuwa mibaya. Kuna miziki ambayo hata kama ingelikuwa imetengenezwa miaka ya 90 bado ingelipanda sana kwenye chart. Nyimbo kama za 50 cents akiwa na Dre & Scott Storch, Eve, Akon, T-Pain etc ni miziki mizuri sana na baadhi yake itaendelea kupigwa kwa muda mrefu tu pamoja na wingi wa miziki. Shida imeanza baada ya USA yenyewe kugawanyika kila state na miziki yake. Hii staili ta Atlanta ndiyo inakuwa kama inadominate kwa sasa. Chicago naona yao imekwama kabisa maana hiyo kucheza inabidi uwe na afya kweli (wimbo wa Miss Elliot - Loose Control).
All in all, miaka 10 inaisha na mziki lazima ubadilike. Utakwenda direction gani siwezi kujua ila ninajua moja, utabadilika. Na wewe pia Mungu akubariki, asante.
NB: Umesahau kuwa miaka hiyo, ili uwe mwimbaji, ilibidi uwe na sauti kama Chiriku. Ndiyo maana waimbaji na bendi zilikuwa chache. Leo hii inatosha una-RAP bila kujali sauti lako likoje wee utapata fweza yako, sana sana uwe na mwili wa afya njema. Michael Jackson, James Taylor, Bee Gees, Marvin Gaye, Lionel Ritchie, Phillip Bailey, Phil Collins, Michael Bolton, Celine dion, SVW, Whitney Houston, Luther Vondrous, Elton John, George Michael, Atlantic Star, Sallum Abdallah, Maneti, Patrick Balidya, etc.