T.B. Joshua amebeba siri gani kifuani, anatumika

T.B. Joshua amebeba siri gani kifuani, anatumika

Ni kweli kila mtu anahaki ya kumtafuta Mungu au kwenda popote anapooona panafaa ili kukaka kiu yake...hilo sipingani nalo kabisa....
Je unahisi ni kweli watu wanaenda huko kote kwa lengo la kutaka kumjua Mungu au wanatafuta miujiza??Mimi ninaamini ni miujiza ndo inayowavuta watu....ubashiri..kama kuagua tu..
Sasa swali linakuja je ni kweli hiyo miujiza ipo,sio kwamba watu wanalizwa pesa zao?
Je haya sio kama yale ya kikombe cha babu wa Loliondo....???
Cha kwanza ni kipi Kumtafuta Mungu na kumjua au NI Kutafuta miujiza ns ubashiri??
Kumbuka hata shetani anawezafanya hivyo pia

Sent using Jamii Forums mobile app
Muujiza wa kwanza unapswa uanzie kwa mtu binafsi kwa kukubali na kuukulia wokovu, sasa mengine Mungu anakutendea kulingana na namna gani umejikita kwake na kiasi cha imani yako kwake.
Nakubaliana nawe kuwa wengi wanataka miujiza na majibu rahisi rahisi bila hata kujibidisha katika kukuza imani zao. Sasa shetani huweza pia kutumia baadhi ya fake pastors kuwarubuni watu wa aina hiyo wapenda majibu ya fastafasta.
 
Mungu anaowatu wa kujivunia. Pangekuwa hawapo dunia ingekuwa imeshakula kibiriti.
Watu hao hawafanyi advertizements za miujiza, au wao wenyewe bali Wanamuadvertize Mungu na Maandiko YALETAYO MUUJIZA BORA NA MKUU WA MTU KUBADILIKA MAISHA. HUU NDIO BIBILIA INASEMA UNALETA FURAHA NA SHEREHE MBINGUNI. HII MIDOGOMIDOGO INAYOPIGIWA CHAPUO KWENYE TV NAYO HUFANYWA NA WATU WA KAWAIDA KABISA HUWEZI AMINI, ILA SIO KAZI YAO KUJITANGAZA, AU KUITANGAZA MAANA NI UNBIBLICAL.
Kuna mtu nilimuona akihojiwa Mungu kafanya makubwa kupitia yeye ambayo angeyafanyia advertizement na kuanzisha kanisa angekokota maelfu, ila yeye ni Bible centered na sio miracle centered.

Mtumishi yoyote, kanisa lolote ambalo MIUJIZA ndio inakuwa Kipaumbele kikuu, Huku neno la Mungu linatajwa kwa juujuu na kujirudiarudia na umakini unarudishwa kwenye miujiza huwa siwaamini kabisa. Maana hakuna hiyo scenario kwenye Bibilia.
Ila Mungu anao watu. Hata wanaokosea wakipata neema ya Kutubu Mungu anaweza kuwatumia kama anavyotaka, maana hata unapoombea wagonjwa, Huwa tunaomba mapenzi ya Mungu sio Ya nabii/mtume au mchungaji yatimie.

Ndio Maana hata paulo licha ya Yote na yeye alikuwa mgonjwa kwa mapenzi ya Mungi. Sio yeye tu na watumishi wenzake wengi tu walikuwa wanaumwa pia, soma salamu za nyaraka zake mwishoni. Mpango wa Mungu ni Uponyaji wa Roho sio mwili, mwili ni kama bonus tu na tusifanye virse versa. Ndio maana Mbinguni bibilia inasema Viziwi watasikia, bubu watanena maana yake kutakuwa na wagonjwa watakaoingia mbinguni kwa sababu ni wazima kiroho.
Joel oostein licha ya kutangaza miujiza sana, mke wake alipougua kansa alimkimbiza hospitali fasta hadi akapona, Ila wengine wa aina hii wanawaaminisha watu Mungu lazima afanye wanachotaka wao sio Mapenzi Yake.

Ni mekuelwa ila jua mafanikio ya mwili yasipokuwepo ujue rohoni pia huna kitu, maana biblia inasema lazima mafanikio ya rohoni yawe sawa na mafanikio ya mwilini, refer mtume Paulo. Ni kweli mwili upo kwa sababu ya Roho, lakini vyote vikistawi sana ndiyo ustawi wa uumbaji wa MUNGU, vyote ni muhimu Kimoja ni nyumba na kingine ni Roho ya Mungu. Hata paulo alipoumwa alijua ni kwani ni mwiba umemchoma na ameumwa na ndiyo maana akasema Neema yako yanitosha. ulirudihukohuko kwa MUNGU kuomba msamaha ili apate neema ya MUNGU.

Pitia watumishii wa MUNGU wa kale, Musa, Daudi, ayubu,selemani nk. hakuna aliyekuwa maskni na weak kimwili ispokuwa kwa maajribu na utukufu wa Mungu wa muda fulani.
Swala la Miujiza ni udhaifau wa watmishi tuu, lkn hakuna mtumishai wa MUNGU wa kweli utamtenga na miujiza ya MUNGU kwasababu Miujiza ni chakula cha watoto wa MUNGU, ni miujiza ni tool ya kuongeza imani kwa watu wake. Yesu alifundisha na miujiza alifanya, kunasehemu alianza na muujiza kwanza sehemu zingine neno kwanza. Musa amewatoa wamisri kwa siries ya miujiza havivyo hutuwezi kuwkepa.

Concern Yako ni genuine, pamoja na miujiza watu wafundishwe neno la MUNGU, na nikweli kila mahali watumishi watumia agenda ya miujiza kuwavuta watu, lkn je wakifika huko makanisani kwao wanapata neno ili waelewe? wajitegeme kwa maana ya kukua kiimani? kwa sababu kunalevel mtu akifika kimahusiano na Mungu miujiza sio muhimu sana ispokuwa nikama chakula tuu kushibisha mahusiano na MUNGU. iwepo isiswepo bado mahusiano na MUngu lazima yaendelee.
 
Unaijua story ya oesten kukatalia watu waliokumbwa na flood ethenic

Huko ....

Do you know how people reacted at twitter ....

Bro kwa ushauri , kwanza amini Mungu yupo but use your common sense pale unapokutana na wanaojiita his servant

Sent using Jamii Forums mobile app
ahaa hebu nipe hiyo story kk.
maana now chanzo changu cha habari nimekifanya kuwa jf huko duniani nimeshatoka mazima.
hebu elezea mkasa vizuri

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndugu yangu hata kama una uwezo wa kuponya, huwezi ponya kila mtu! Yesu ndiye tunayemwamini na ana uwezo wa kuponya, kufufua na kila kitu, lakini hakuponya wote.... Kanuni iko wazi...... Njooni wote wenye mizigo....which means ni lazima mtu mwenyewe kwa imani achukue hatua ya kumfuata na hapo huweza kupokea muujiza wake tena akiwa na imani. Sasa tukisema kwamba wote waombewe wapone ni mtizamo mzuri lakini sio wa Kibiblia.

So pamoja na kwamba wokovu umekuwepo tangu kifo cha Yesu msalabani, bado ni lazima mtu binafsi achukue hatua ya kumfuata Yesu kikamilifu na sio muujiza tu halafu unarudia yale ya zamani.

Hata huko Ocean Road Hospital, ni wote wanamtaka Yesu kweli?
Yesu aliponya hata alowakuta barabarani. Akiwahurumia tu walipona.
Mitume waliponya watu walokuwa wamekutana nao tu bila ya wao kufuatwa.
Wengi hata hawakushukuru.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Acha kuhofia wewe.
watumishi wa kweli wa Mungu wanajulikana kwa matendo na mienendo yao.uzuri wake Bible iliwagusia tangu zamani

kwanza tumepewa mamlaka ya kuzijaribu kila roho Cox siyo zote hutoka kwa Mungu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Zipo standards za kupima ukweli wa huduma ya mtu lakini wengi tunawaita hao watumishi matapeli kwa habari za kusimuliwa na si kutafiti na kabla ya kutafiti unapaswa kuwa umejiandaa pia kiroho ili uweze kuchambua bila kuchomeka hisia zako binafsi au dhehebu lako.

Siwezi kushabikia matusi kwa watumishi bila valid facts maana wakihama kwa hao wanaowaita matapeli watarudi kwa mapadre!

Chagua moja ya wachangiaji hapa umuhoji vizuri uone kama ana facts! Kwanza utakuta hata mafundisho ya dhehebu lake hayajui! Sasa mtu kama huyu anawekaje standards zaidi ya kuongozwa na hisia tu!

Nikiamua kumpinga mtumishi yeyote lazima niwe na facts na sio hisia.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Na Ahmed RajabChuki hizo

T.B. Joshua ni mtu wa ajabu. Kuna wasemao kwamba mzalia huyu wa Nigeria si binadamu wa kawaida. Wanaamini kwamba yeye ni nabii. Wengine wanasema kuwa ni mtume kamili aliyepewa wahyi na miujiza ili aweze kuwahubiria watu na kuwalingania.

Na kuna wanaokana. Wanasema kwamba T.B. Joshua hana unabii wala utume wowote ila yeye ni afiriti, mwana wa ibilisi, shetani anayewaghilibu watu.

Serikali ya Cameroon iliwahi kuliweka jina lake kwenye orodha ya watu wabaya wasiotakikana nchini humo. Na ikawaonya wananchi wake wenye kufunga safari kwenda kumtembelea Lagos, Nigeria, wawe na hadhari wasighilibike.

Serikali ya Zambia nayo iliwahi kuwaonya raia zake wasimwendee Joshua kwa sababu fedha zikiwaishia hukwama huko Nigeria.

Naawe awavyo, apendwe asipendwe, T.B. Joshua hakosi wenye kumfuata. Ana wafuasi wengi miongoni mwa walio katika tabaka aali la watu wenye uwezo katika jamii katika takriban ukanda mzima wa Afrika ya Magharibi. Watu husafiri kila mwaka kutoka sehemu mbalimbali za Afrika kwenda Lagos kulizuru kanisa lake.

Wasiojiweza huuza hata nyumba au mashamba ili wapate fedha za safari. Wanatoka Liberia, Ghana, Sierra Leone, na hata kutoka nje ya Afrika ya Magharibi.

Nakumbuka safari moja nikiwa uwanja wa ndege wa Murtala Muhammed, jijini Lagos, nilikumbana na kikundi cha watu zaidi ya hamsini waliowasili kutoka Nairobi. Wote walikuwa wamevaa fulana za T.B. Joshua. Walikuwa wanaelekea mtaa wa Egbe, huko Lagos, kwenye kanisa la The Synagogue, Church of All Nations (Sinagogi, Kanisa la Mataifa Yote), kwa ufupi SCOAN. Hapo ndipo penye makao makuu ya madhehebu hayo ya kikristo aliyoyaanzisha T.B. Joshua. Hili ni kanisa kubwa Afrika kwa idadi ya wafuasi wake na linazidi kukua.

Septemba 12, 2014 jengo la ghorofa sita la kanisa hilo huko Lagos liliporomoka. Watu wasiopungua 116 walikufa katika ajali hiyo, 85 kati yao walitoka Afrika Kusini. Jamaa wa marehemu hadi leo wanataka kujua nini hasa kilitokea na nani wa kuwajibika. Mwaka 2015 Joshua alifunguliwa kesi ya jinai, yeye pamoja na wahandisi wawili na wadhamini wa kanisa. Bado kesi haijamalizika kwa sababu Joshua amekuwa akikwepa kwenda mahakamani.

Ni wazi kwamba mchungaji huyo na mwinjilisti wa televisheni anaifahamu Afrika na anawafahamu vilivyo Waafrika wenzake, hasa wasomi miongoni mwao. Anafahamu namna akili zao zinavyofanya kazi na jinsi anavyoweza kuzichezea.

Rais wa zamani wa Ghana, marehemu Profesa John Attah-Mills baada ya kushinda uchaguzi alimshukuru kwanza Mungu na halafu akamshukuru T.B. Joshua kwa kumsaidia kushinda uchaguzi huo. Attah-Mills aliwahi kusema hadharani kwamba Joshua alitabiri kweli ya kuwa baada ya kushiriki katika chaguzi tatu ndipo ataposhinda uchaguzi wa urais wa Ghana.

Attah-Mills alikuwa na mazoea ya kumtembelea Joshua kwenye kanisa lake. Alikuwa akenda mara kwa mara kufanya maombi kabla hajawa rais na baada ya kuwa rais. Marais wengine wa zamani wa Kiafrika waliowahi kumzuru Joshua walikuwa Andre Kolingba (Jamhuri ya Afrika ya Kati), Frederick Chiluba (Zambia), Profesa Pascal Lissouba (Congo-Brazzaville), Joyce Banda (Malawi) na Omar Bongo (Gabon).

Miongoni mwa Waafrika mashuhuri waliovutwa na simaku yake ni Prince Johnson na Rais George Weah (wote wawili kutoka Liberia). Kutoka Tanzania ni Edward Lowassa na Rais John Magufuli. Kutoka Zimbabwe Morgan Tsvangirai, kutoka Malawi Sam Mpasu na Walter Nyamilandu, Rais wa Jumuiya ya Soka ya Malawi (FAM).

Kutoka Afrika Kusini Julius Malima, Winnie Mandela, Goodwill Zwelithini (mfalme wa Wazulu), pamoja na waimbaji Yvonne Chaka Chaka na Sechaba.

Hata Gavana-Mkuu wa Bahamas, Sir Orville Turnquest alimpokea Joshua alipomtembelea 2001.

Jambo linalonihangaisha ni ushawishi mkubwa alionao mchungaji huyo kwa baadhi ya viongozi wa Kiafrika. Unaweza ukautafsiri ushawishi huo kwa walau njia mbili. Ama amewateka na kuwatia mikononi viongozi hao au hao viongozi wamemkinai vya kutosha kiasi cha kuwa tayari kumuamini na siri zao ambazo pia huenda zikawa siri za serikali.

Mgeni kuwa na nguvu za aina hizo katika nchi za watu wengine si jambo la maskhara la kuchukuliwa kijuujuu, hasa kwa mtu ambaye dhamira na ajenda zake za kisiasa si bayana. Si jambo la kufumbiwa macho. Hatujui huwa anafanya nini au hutaka kujua nini anapowatembelea viongozi katika Ikulu zao.

Huenda akawa anatumiwa, ama kwa kujua au bila ya kujua. Kwa mfano, tunajua kwamba ana uhusiano mzuri na serikali ya Israel, nchi ambayo amekuwa akiizuru mara kwa mara na ambako amekuwa akionana na wakubwa wake.

Tuijuavyo Israel na weledi wake wa kuelea katika mikondo ya chini kwa chini katika siasa za kimataifa, nadhani ni halali tukiuliza kwa kiasi gani Israel imeweza kumtumia T.B. Joshua kuwafanya baadhi ya viongozi wa Kiafrika wabadili misimamo ya nchi zao kuhusu Israel?

Israel, taifa la majungu lisilopoteza fursa yoyote itayoweza kuinufaisha kimataifa, itakuwa imepoteza moja ya sifa zake kuu lau haikumtumia Joshua kwa maslahi yake. Israel haitokuwa Israel ikiwa haikujaribu kufanya hivyo.

Wenye kuifuatilia mitandao ya wahalifu wa kimataifa wana wasiwasi kwamba huenda kanisa lake la SCOAN likatumiwa, hata bila ya mwenyewe kujua, kuzisafisha fedha chafu zilizopatikana kwa njia za haramu.

La hatari zaidi ni kwamba yeye mwenyewe T.B. Joshua huenda akawa hatari kwa usalama wa taifa kwa kujulishwa mambo na wenye kuendesha nchi au na walio karibu nao, mambo ambayo hastahiki kuyajua.

Yote hayo tunayasema kwa hadhari tu kwani huenda akawa anawachezea akili tu viongozi wa Kiafrika bila ya kuwa na madhara kwa mustakbali wa nchi zao. Hatujui. Lakini hayo ni baadhi ya maswali nyeti yanayostahiki kuulizwa kuhusu ushawishi wake kwa viongozi wa baadhi ya serikali za Kiafrika.

Tatizo lililopo ni kwamba mtu atapokuwa anajaribu kuyauliza maswali hayo atakuwa anayaingilia mambo ya kiroho na ya imani za watu. Hili ni tatizo kubwa. Kuna hatari kwamba katika kuulizauliza kwako ukadhaniwa kwamba unapinga ukristo au unampinga Yesu Kristo. Kosa kama hilo la kuziingilia imani za watu liliwahi kufanywa na Kwame Nkrumah, rais wa kwanza wa Ghana.

Waumini wa T.B. Joshua wanaiona imani yao juu yake kuwa ni sahihi. Kwa hivyo, hawaoni ubaya wowote kwa viongozi wa serikali zao pia kumfuata. Hawa ni watu ambao wanapomuona T.B. Joshua anafanya maombi kwenye vipindi vyake vya televisheni vya Emmanuel TV huugusa uso wa televisheni ili wapate “baraka” zake. Huna cha kuwaambia watu kama hao.

Ikiwa viongozi wa Kiafrika wana itikadi kama hizo basi nchi zao zimekwisha.

Kwa kiwango gani viongozi hao huwa wanamshirikisha wanapokata maamuzi yao. Na yeye huwashauri nini na kwa mantiki gani?

Ni nani hasa huyu T.B. Joshua? Alikwendakwendaje akaibuka kuwa na wafuasi alionao hata katika Ikulu za baadhi ya nchi za Kiafrika? Na ushawishi wake hauko Afrika tu, umevuka bahari ya Atlantiki na umesukumwa na pepo hadi Amerika ya Kusini, ingawa ushawishi huo haukufika bado katika Ikulu za huko.

Hata hivyo, lukuki na lufufu ya watu walihudhuria ibada zake alizozifanya miaka ya hivi karibuni Colombia, Mexico, Peru na Paraguay. Aliziita ibada hizo “vita vya msalaba” au “vita vitakatifu”

Ziara aliyoifanya Paraguay 2017 ilizusha mjadala mkubwa nchini humo, pale bunge la huko lilipoidhinisha atunukiwe nishani ya “Orden Nacional del Merito”. Hiyo ni nishani ya hadhi ya juu kabisa nchini humo na hutunukiwa raia wa Paraguay tu.

Kuna waliokuwa wakihoji kwamba “el profeta” (mtume) Joshua alistahiki nishani hiyo kwa “kuwaponesha” watu waliokuwa na magonjwa makubwa kama saratani au UKIMWI. Inasemekana pia kwamba aliwapunga wenye kudai kwamba walikuwa na mashetani kichwani.

Joshua amechuma fedha chungu nzima kutokana na ziara zake hizo, pamoja na michango na ada anazolipwa na wafuasi wake. Alionyesha ukarimu wake Julai 2014 alipokuwa ziarani mjini Cali, Colombia, ambako watu wasiopungua laki moja walihudhuria mkusanyiko wake aliouita “Muujiza wa Vita vya Msalaba”.

Baada ya kumaliza ibada aliwapa polisi wa huko Cali dola za Marekani laki moja ($100,000) kuwasaidia wanafamilia wa polisi waliouliwa au waliojeruhiwa wakiwa kazini. Fedha hizo ni kama ndururu tu ukizingalisha na utajiri wake binafsi unaokisiwa kuwa si chini ya dola za Marekani milioni 15.

Kwa mtu asiyependa kusafiri Joshua amesafiri sana kwani amewahi pia kuzuru Tanzania, Korea, Singapore, Indonesia na Australia.

Joshua anadai kwamba mazazi yake yalitabiriwa miaka mia moja kabla. Kuzidi kuonesha kwamba yeye si binadamu wa kawaida anadai pia kwamba alikuwa tumboni mwa mama yake kwa muda wa miezi 15 kabla ya mama yake kujifungua Juni 1963.

Jina lake kamili ni Temitope Balogun Joshua, ingawa alipokuwa anasoma skuli akijulikana kwa jina la Balogun Francis.

Masomo yake rasmi ya skuli hayakupindukia ya sekondari ambayo hakuyamaliza. Mwenyewe anasema alivutiwa na masomo ya Biblia tangu akiwa mdogo. Baada ya kumaliza masomo yake ya msingi alifanya kazi mbalimbali za vibarua ikiwa pamoja na kubeba mavi ya kuku katika shamba la kuku.

Anasema mambo yalimfungukia alipoamriwa mbinguni aanzishe kanisa lake. Lakini je, ushawishi wake kwa viongozi wa Kiafrika unamalizika kwa kuwazingua na kuwapunga pepo tu? Au kunaya ziada?


Baruapepe: aamahmedrajab@icloud.com; Twitter: @ahmedrajab



View attachment 984327View attachment 984328

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni mekuelwa ila jua mafanikio ya mwili yasipokuwepo ujue rohoni pia huna kitu, maana biblia inasema lazima mafanikio ya rohoni yawe sawa na mafanikio ya mwilini, refer mtume Paulo. Ni kweli mwili upo kwa sababu ya Roho, lakini vyote vikistawi sana ndiyo ustawi wa uumbaji wa MUNGU, vyote ni muhimu Kimoja ni nyumba na kingine ni Roho ya Mungu. Hata paulo alipoumwa alijua ni kwani ni mwiba umemchoma na ameumwa na ndiyo maana akasema Neema yako yanitosha. ulirudihukohuko kwa MUNGU kuomba msamaha ili apate neema ya MUNGU.

Pitia watumishii wa MUNGU wa kale, Musa, Daudi, ayubu,selemani nk. hakuna aliyekuwa maskni na weak kimwili ispokuwa kwa maajribu na utukufu wa Mungu wa muda fulani.
Swala la Miujiza ni udhaifau wa watmishi tuu, lkn hakuna mtumishai wa MUNGU wa kweli utamtenga na miujiza ya MUNGU kwasababu Miujiza ni chakula cha watoto wa MUNGU, ni miujiza ni tool ya kuongeza imani kwa watu wake. Yesu alifundisha na miujiza alifanya, kunasehemu alianza na muujiza kwanza sehemu zingine neno kwanza. Musa amewatoa wamisri kwa siries ya miujiza havivyo hutuwezi kuwkepa.

Concern Yako ni genuine, pamoja na miujiza watu wafundishwe neno la MUNGU, na nikweli kila mahali watumishi watumia agenda ya miujiza kuwavuta watu, lkn je wakifika huko makanisani kwao wanapata neno ili waelewe? wajitegeme kwa maana ya kukua kiimani? kwa sababu kunalevel mtu akifika kimahusiano na Mungu miujiza sio muhimu sana ispokuwa nikama chakula tuu kushibisha mahusiano na MUNGU. iwepo isiswepo bado mahusiano na MUngu lazima yaendelee.
Asante maana kuna mambo tunakubaliana na kuna baadhi tunapishana kidogo.
*Pamoja na Yesu kufanya miujiza ya kila namna, lkn mafanukio yalikuwa hafifu sana. Ila Alipopita Samaria ambapo hakufanya miujiza Lkn alifanukiwa kuwin mji mzima na vijiji vya Jirani.
Neno Kwa wenye kiu linadhamani na uwezo mkubwa kuliko Miujiza.

TATIZO LA MAKANISA YA MIUJIZA
Kutanguliza miujiza, Neno kuwekwa kama Kakitu tu kakusindikizia. Yesu alisema mtaijua kweli (NENO) nayo itawaweka huru. Ila Tunahubiriwa miujiza ndio inaweza huru watu (Uongo, vinginevyo Farao, Bar Yesu, na Watu wa Listra wangekuwa watunwaliohuru kuliko wote dunia nzima).


YESU ALIACHA AGIZO GANI
'' Enendeni ulimwengini mkaihubiri injili''
na ishara hizi zitaambatana nanyi.
Wa Uzoefu wangu hiyo equation imegeuzwa. Nakutana na wapendwa wengi ukiwahoji mambo mengi ya bibilia hawajui, maana yake wanafundishwa kiduchu sana tena selectively.

Ni kweli Mungu anataka watu wake wawe wazima, Ila anaweza kuruhusu waumwe au ikibidi wawe na vilema vya maisha.
Kuhusu paulo sizungumzii Mwiba, Nazungumzia ugonjwa wa kawaida anawaelezea wagalatia alipokuwa huko aliugua, anawataja wtumishi wengine wengi wakiwa wanaumwa.

Leo Jamii imeaminishwa TB Joshua, Mwakasege, Mwingira, Kakobe au wengine ulaya hawawezi kuugua. Lakinj naamini wao nao wanaugua kama binadamu wengine kama watumishi wa Bibilia, Ila Haimfanyi Mungu kuwa hana uwezo.
Pia Ukumbuke Kuugua kwingi sio mpango wa shetani bali ni matokeo ya kuvunja kanuni za afya alizotuwekea Mungu.
Mfano kama anakula vyakula vya chorestral lazima uugue BP Mungu hawezi kuiondoa chorestral kwa maombi.

Kama Shetani aliweza Kufanya miujiza kama Mungu aliyofanya kupitia Musa kwa Farao, hii inaonyesha miujiza haipaswi kuwa right tool ya kuwaaminishia watu Mungu, inanafasi ndio lakini Neno Linapaswa kuwa Paramount. Anaheri anayeamini bila ishara, Kizazi cha leo kinataka kuona ishara ndio kiamini, Ila Kwa Kauli ya Yesu kwa Yule diwani wa Karpenaum ni Kwamba Kumwamini kwanza mengine baadae.

Kuna shift kubwa ya Vipaumbele mkuu. Kwangu MIMI SIAMINI KATIKA MIUJIZA KAMA CHANZO CHA KUWAAMINISHIA YESU MAANA YESU MWENYEWE ALISJINDWA KJWASHAWISHIA MIUJIZA WAYAHUDI WAKAISHIA KUMUUA LICHA YA KUPONYA WATOTO WAO, KUWAFUFUA ETC.
KWANGU MIMI MIUJIZA NI ATTENTION CATCHER, NA KIFAA CHA KUWAFANYA WATU WAWE NA USIKIVU KWA NENO LA MUNGU AMBALO NDIO LINALETA MUUJIZA WA KUDUMU. ZAIDI YA HAPO NIWE NASUKUMWA NA HURUMA ILI WATOTONWA MUNGU WAPATE UNAFUU KIAFYA KAMA WANAVYOFANIKIWA KATIKA ROHO ZAO SIO SOURCE OF INCOME, UMAARUFU BINAFSI. HIVYO WALIPASWA KUONEKANA MIDA MINGI MAHOSPITALINI, KWENYE NYUMBA ZA MASIKINI NA MATAJIRI, NA KILA MAHALA KWA WATU WA HADHI ZOTE BILA ULAZIMA WA CAMERA, NA SIO KUWASUBIRI WAJE WENYEWE KUWAFUATA HUMO KWENYE MAHEKALU.

MAONI.
 
Ni kweli kila mtu anahaki ya kumtafuta Mungu au kwenda popote anapooona panafaa ili kukaka kiu yake...hilo sipingani nalo kabisa....
Je unahisi ni kweli watu wanaenda huko kote kwa lengo la kutaka kumjua Mungu au wanatafuta miujiza??Mimi ninaamini ni miujiza ndo inayowavuta watu....ubashiri..kama kuagua tu..
Sasa swali linakuja je ni kweli hiyo miujiza ipo,sio kwamba watu wanalizwa pesa zao?
Je haya sio kama yale ya kikombe cha babu wa Loliondo....???
Cha kwanza ni kipi Kumtafuta Mungu na kumjua au NI Kutafuta miujiza ns ubashiri??
Kumbuka hata shetani anawezafanya hivyo pia

Sent using Jamii Forums mobile app
Unaposema watu wanafuata miujiza una maana gani?unaowaona pale SCOAN wengine ni raia wa Nigeria wako pale kwa ajili ya kuabudu kwani ni kanisa waliloamua kuabudu,wengine ni wa kutokea mbali wamekwenda pale kwa aajili ya kuombewa shida walizo nazo,sasa unapozungumzia kuwa wanafuata miujiza,ni kama vile wanakwenda pale for fun...
 
Kweli ila ilikuwa lazima waoneshe kuwa wana uhitaji huo kutoka kwake.
Hapana.
Wako nusu walohitaji wako wengine hawakuhitaji.
Yule mwenye mapepo makaburini
Yule mtoto alofufuliwa wakiwa njiani.
Hata Lazaro watu wote walimueleza haiwezekani
Kuna wale vilema 10, ambao alirudi mmoja kushukuru.

Na umati wa watu wengi aliwakimbia mara nyingi sababu walikuja wapone tu na si kubadilika.

Na hakuna mahali biblia inamtamka maisha ya Yesu kubadilika kiuchumi sababu ya kuponya watu.

Wala mitume, kama Petro ambaye kivuli chake tu kiliponya.
Aliwasisitiza wamepewa bure watoe bure.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwandishi una uwezo mkubwa wa uandishi.
Big up sana.

Kwa upande wangu T.B ni nabii wa uongo.
No further discussion.
 
Kama wewe ni mkristo chunga sana unachokisema kwa watumishi wa Mungu. Mimi ni Mkatoliki lakini nachukua tahadhari kubwa kujadili watumishi wa Mungu wa madhehebu mengine au mapadre.

Kama unataka kumkosoa mtu mfatilie anafundisha nini na kama anavua roho kweli kwenda kwa Kristo au kwake. Ili ujue kinachofundishwa kama ni sahihi au si sahihi jitahidi ujifunze kwa undani mafundisho ya dhehebu lako ili ukikubaliana na facts hizo utaweza kuona hayo madhaifu kwa msaada wa Roho Mtakatifu.

Wengi naona wanakurupuka tu kuita wengine matapeli na ukiuliza kwa msingi upi anakupa stori alizosimuliwa!

Kila huduma tutaona matunda yake na kama imetoka kwa Mungu itadumu kama lilivyodumu Kanisa Katoliki kama alivyotabiri Kristo maana Kristo aliacha imani lakini pia visible church yenye kiongozi wake na mitume wengine ambao waliishi kwa ushirika na kupeana madaraja ya kichungaji hadi leo.

Sent using Jamii Forums mobile app
[emoji120][emoji120][emoji120][emoji120][emoji120]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom