T.B. Joshua amebeba siri gani kifuani, anatumika

T.B. Joshua amebeba siri gani kifuani, anatumika

Hapana.
Wako nusu walohitaji wako wengine hawakuhitaji.
Yule mwenye mapepo makaburini
Yule mtoto alofufuliwa wakiwa njiani.
Hata Lazaro watu wote walimueleza haiwezekani
Kuna wale vilema 10, ambao alirudi mmoja kushukuru.

Na umati wa watu wengi aliwakimbia mara nyingi sababu walikuja wapone tu na si kubadilika.

Na hakuna mahali biblia inamtamka maisha ya Yesu kubadilika kiuchumi sababu ya kuponya watu.

Wala mitume, kama Petro ambaye kivuli chake tu kiliponya.
Aliwasisitiza wamepewa bure watoe bure.


Sent using Jamii Forums mobile app
Sikatai kabisa ndugu, ila ninachojaribu kusema ni kwamba kila aliyekuwa na uhitaji wa kuponywa na kuamini uponyaji kupitia kwa Yesu na kwa jina lake aliponywa.
Hata kama hakuonesha direct, lakini kuna watu wa karibu waliowasadia na kuvuta attention ya Yesu au mitume kuwa wana uhitaji na hivyo walihudumiwa. Mfano kwa lazaro, alikuwa rafiki wa Yesu na hata dada yake alikuwa na uhusiano mkubwa sana na Yesu kwa hiyo aliweka msisitizo sana kumwita Yesu kwa ajili ya lazaro, hata hivyo Yesu akachelewa ili aoneshe ukuu wake.
Kwa yule wa makaburini alikuwa hajiwezi sababu alitawaliwa na mapepo, hivyo yalipokutana na Yesu yakaanza kulalamika...na ndipo Yesu alimwona mtu huyu na kumhurumia... Alimponya na alionesha nia ya kumfuata Yesu baada ya kufunguliwa.

Msisitizo mkubwa ni kuwa na imani katika ile nguvu ya Mungu itendayo kazi ktk kuponya n.k.
Ila sii sahihi kazi hizi zitolewe kwa fedha!
 
UMENENA MKUU.
Ila mwandishi wa hili bandiko ambaye ni muislam anatakiwa kutubu na baadaye awe mfuasi wa KRISTO maana anaonekana kufuatilia sana Ukristo.

Huyu hana tofauti na Manabii wenzake tunaowaona hapa Tanzania, sema yeye ni mjanja mjanja hagombani na serikali wala dini zingine. Kwani Gwajima wetu Enzi za Tanganyika Packers alikuwa na tofauti gani na T.B.Joshua? Gwajima alifunika vidini vingine vyote, kilianza kumuharibikia alipojiingiza mgogoro na Askofu Pengo,sijui ilikuwa makusudi au ilipangwa baada kuona anachanja mbuga zaidi. Kisha akaja kupata mgogoro na serikali tuliona alivyokuwa akiviziwa kama digidigi. Baada ya hapo likaibuka sakata lake na Makonda.Baada ya hapo aka mute, nasikia hata idadi ya waumini ilipungua kutoka ule umati mkubwa wa Tanganyika packers nasikia sikuhizi hata kanisa halijai.
Huyu T.B Joshua hana lolote, hakuna mlemavu, wala mgonjwa wa ukimwi aliponeshwa naye,ni ghiliba kama za wenzake za kupanga. Kama T.B Joshua ananguvu kama tuaminishwavya, mbona nguvu yake iligonga mwamba kwa NEC ya Tanzania. Aliaminishwa Lowassa ana nguvu kisiasa na ilikuwa hivyo, akapewa taarifa akamtabiria Lowassa kuwa angekuwa rais, lakini hakujua Mungu wake hana ubavu juu ya figisu za NEC yetu, Walichakachua mbele ya macho yake hakuamini, akarudi Lagos Mnyoonge.
Nikirudi kwenye mada still sihamini kwamba eti Nabii T.B.Joshua anasiri yoyote yamaana, kama siri ananyo ni siri za waumini wake tu. Kuwa na access na viongozi wetu wenye uchu wa madaraka haimaanishi eti anasiri za serikali au intelligence ya nchi hilo nakataa. Huyu nabii wa uongo tu ila ujanja ujanja kawazidi wenzake anaonekana yuko juu. Marekani kulikuwa na kina Graham walikufa hakuna hata alama iliyobaki, kuna mtu anaitwa TB.jakes alikuwa anahubiri anatokwa jasho utadhani anakimbia marathon, lakini kaisha. Hizi nyakati zake tu kama wale inspirational pastors kama Joel Oesteen muda utafika watamchoka nitakuja mimi nitawasumbuaaaa name wakinichoka unaweza kuja wewe au mwanao. Dini hizi ni ujanja tu. We tizama mamam rwakatare siku hizi havumi kama zamani, Kwasasa anayewasumbua wenzake bado ni Mwingira wa EFATA. lakini naye tutakuja msahau tu.
Siri TB.Joshua HANA zaidi ya zile za waumini wake.
 
Mimi kwenye hii habari kilichonivutia ni kiasi cha pesa anachodaiwa kuwa nacho. Net worth ya USD 15 milion! Kumbe utajiri na umaarufu ni vitu viwili tofauti kabisa. Kwa umaarufu alio nao, na muda aliofumu kwenye game, kwakweli nilidhani ana hela ndefu zaidi, kumbe hata Davido anamzidi mbali. Mfano R. Mengi ana Net worth ya zaidi ya USD 400 milion na sidhani kama anafahamika na kuheshimiwa na wanaijeria kama sisi tunavyomfahamu TB. Ni huyo mimi
 
Pamoja na hayo yote, T. B Joshua ni kati ya watu wachache sana wanaojiita manabii ambao mafundisho yao mengi yanajikita katika maandiko na asilimia kubwa ya ujumbe wake ni kuhusu imani (faith).
Pia ujumbe wake ni rahisi kumjenga mtu akasimama katika imani kama kweli ana nia ya kukua kiimani.

Mengine hayo ni Mungu ajuaye.
Maskini kondoo!
 
Hahahhahaha, kwamba kondoooo! Nimetoa mtizamo ndugu kwa kujaribu kulinganisha hasa content ya mafundisho ya watumishi kadhaa... Kiukweli huyu jamaa anafundisha mafundisho mengibasing on faith with Biblical reference kwa asilimia kubwa. Kwa hilo nampa big up, sasa kwamba ni mtumishi halali au siyo halali kwa kweli ajuaye ni Mungu, mimi siwezi hukumu hilo.
Maskini kondoo!
 
Unasikia tu lkn huna uhakika! Halafu unasambaza maneno ya uwongo! Lowassa hakutabiliwa chochote! Jana nimeona clip moja ya kipindi cha uswazi huko mikoroshini Temeke eti kuna pikipiki imeachwa na mwizi aliiba Tanga akaja kutekeleza hapo Temeke. sasa wazushi kama wewe wakazusha kwamba ile pikipiki kila anayeigusa hufa. Pikipiki imekaa hapo 2yrs na habari zimesambaa mpaka magazeti yakaandika. Zembwela akatafuta ukweli akaupata na akaishika na kuipanda hiyo pikipiki. kumbe mwenyewe alinunua pikipiki mpya hiyo ilimzingua na sababu hapo kijiweni watu wapo 24hrs jamaa akaipaki tu hapo maana kwenye parking za kulipia hawezi mudu. Tunatenda sana kazungumza mabaya ya watu bila kuwa na uhakika. Kijana imani yako itakuponya mwenye nguvu si TB Joshua ni imani yako kwa Kristu. Watu wanakwenda pale anawafundisha jinsi ya kusali na kuwa na imani na wanawaombea watu wanapona.
Mkuu ungesema "siyo kweli" ilikuwa inatosha tu! sasa hayo mengine ni mahubiri, naomba niitikie AMEEEEEEEEEEEEEEEN!
 
Zipo standards za kupima ukweli wa huduma ya mtu lakini wengi tunawaita hao watumishi matapeli kwa habari za kusimuliwa na si kutafiti na kabla ya kutafiti unapaswa kuwa umejiandaa pia kiroho ili uweze kuchambua bila kuchomeka hisia zako binafsi au dhehebu lako.

Siwezi kushabikia matusi kwa watumishi bila valid facts maana wakihama kwa hao wanaowaita matapeli watarudi kwa mapadre!

Chagua moja ya wachangiaji hapa umuhoji vizuri uone kama ana facts! Kwanza utakuta hata mafundisho ya dhehebu lake hayajui! Sasa mtu kama huyu anawekaje standards zaidi ya kuongozwa na hisia tu!

Nikiamua kumpinga mtumishi yeyote lazima niwe na facts na sio hisia.


Sent using Jamii Forums mobile app
well said .hapo umesema sawa
lakini kuna wengine kama sisi fact tuanazo za kumpinga .huyo bwana
iwe kwa physical au spiritual

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Multimedia ndio moyo na uti wa mgongo wa hao jamaa. Bora Roho mtakatifu asiwepo kuliko mtaalam wa graphics na Studio nzima.
Ndio maana ukikagua waumini, lazima ukute wapo watu flani wanafanya eye surveillance na wako makini sana kudetect kama kuna mtu asiyeeleweka humo, ambaye harespond na kureact sawsawa na miongozo kule juu.

Angalia Ile Video ya Mohamed Ali wa Kenya alivyomfanyia investigation pastor Wangui wa Kenya na michezo yake Kanisani kwa kutumia spy camera, na kufanya secret private interview na timu yake. Usanii wa Kiwango cha juu sana. Au Nabii Buhari alipochomekea graphics za midori myeupe na kuaminisha watu malaika wameingia kanisani.

''Watu wangu wanaangamizwa kwa Kukosa Maarifa..'' Nabii Hosea.
Ndio maana tukisema T.B.Joshua ni tapeli kuna manabii au wafuasi na washabiki wamanabii hao wanakuwa wakali hadi kutukana kutetea ujinga huo. Hawawezi kufanya uponyaji wa aina yoyote hadharani, mambo yao ni graphic evidence ukiwaambia wafanye nje ya comfort zone zao hawataki, huyo T.B.Joshua eti ili upone lazima uende kanisani kwake huko Nigeria, kwanini akija hapa Tanzania huwa haponyi?! Kwasababu as you said yuko nje ya crew yake tutamkamata.
Eti kunawatu wanaamini kabisa ni mtumishi wa Mungu. Kweli wajinga ndio waliwao.
 
ahaha duh sawa kaka vp yule pasta Houston wa hillsong church.
naye unamchukuliaje?!

ki ukweli wapo wa ukweli na uongo .

Sent using Jamii Forums mobile app
Hahaha kaka waongo wote hao, kila mmoja anatafuta jinsi ya kutusua, hizi mega churches ni biashara tu. We angalia umaarufu wao ukiisha kwenye makanisa wanabaki kufanya interviews kuuza vitabu tu.Joe Osteen mjanja yeye haponyi anaongea tu. Lakini angeponya labda angewazidi wenzake wote. We kumbuka Gwajima wa Tanganyika markets alikuwa balaaa, alikuwa hadi anafufua wafu. Alipifukuzwa Tanfanyika Parkers tu na nguvu za kufufua misukule ikaisha.
Hawa wachungaji ni mtandao wa kitapeli sema ukiwagusa waumini wao wanakuja juu.
Serikali inahangaika kutibu cancer mimi ningewakusanya wapige kambi ocean road hosputal mpaka waponye na hiyo ndiyo ingekuwa litimus test kwao, akipona unapewa leseni kuendelea na kanisa, huponyi kalime huko acha kutapeli watu.
 
T.B joshua ni mwalimu wa imani hakuna kinachoponya zaidi ya imani kama hauamini muujiza hautokaa ukutokee kwenye maisha yako.
.
Mfatilie bwana mmoja anaitwa NICHOLAS SUGUYE hajui kabisa kufundisha yeye ni makelele muda wote yale yanayopingwa na T.B joshua.
.
Mtafute mwana theolojia yeyote kama atakuwa na doubt juu ya T.B joshua huyo atakuwa na mapungufu, lakini kwa kina gwajima ni sawa kuwafikiria mara nane nane
Daaah T.B joshua ukisikiliza mahubiri yake hutakaa kuacha kumsikiliza ana ujuzi wa kiroho na anajua jinsi ya kumpa mtu mafundisho ya kiimani..Ana imani kubwa sana T.B joshua
 
Anafanya nini sasa, haya yapi?! Kama anaponya wagonjwa next time akija ikulu, wampeleke OCEAN ROAD CANCER HOSPITAL , iko nyuma ya ikulu pale, awaponye wagonjwa. Akifanya hivyo nami nitamfuata. Lakini hizi story sio mpya. Unaweza kuta wewe naye nabii umekusanya wajinga unapiga vijicenti vyao.
kiongozi haya ni maswala ya imani..mwenye imani ataweza kushuudia ukuu wa Mungu.
 
Muislamu anapojaribu kuandika habari za Mkristo...chuki na fitina huwa nyingi kuliko uhalisia.
Mwandishi anaongelea Israel kwa chuki.
Kwa nini haujaandika kuhusu akina Sheikh Yahaya na wafuga majini wengine walivyojiimarisha katika Ikulu mbalimbali za kiafrika nyakati wako hai...
Waislamu acheni WIVU...
Ahmed rajabu hajamsema kibaya chochote TB Joshua amechambua tena kwa kina wajii wa mtu huyu
Pai Ahmed ni miongoni mwa waandishi habari wazuri na maarufu waliobaki Africa ameshakutana na kuhojiana na viongoz na marais kibao ulimwenguni
Naamini iman tofauti na Ahmed lakini hajaandika kwa ubaya haya
 
Sasa kama hao wote ni waongo.. ukweli ni nini? Na kwanini watu watoka waliko kwenda kwao? Makanisa ya yazamani yameshindwa kuhudumia waumini wao kiroho ndiyo maana wanaondoka.


Sent using Jamii Forums mobile app
Wanadanganywa hata wanaoenda huko shida zao haziishi. Nina shemeji yangu alianzia kwa kakobe yulee akiwa kule Mlalakuwa kabla hajajenga kanisa hapo barabarani. Alitaka tuamini Kakobe ni mtumishi tukamgomea, alivyochoka kuna kikanisa kiliwahi kuwa hapo jirani na Joly Bar cha Assemblies of God sio mbali na kakobe, kikafa akawa anaenda kwa karismatic wale wakatoriki wa Nkwera, huko akatoka, akaenda kwa mama rwakatale,huko akatoka akaenda kwa Gwajima, huko akatoka akaenda Efata kwa Mwingira katoka kaka yangu ananiambia sikuhizi mkewe kaamia kanisa moja huko Temeke wanakesha huko kwenye maombi wanauziwa mafuta na maji ya baraka sijui kutoka Israel. Yani vituko tupu haelewi na hajielewi yeye akihamia sehemu anaponda wa huko alikotoka sijui ataishia wapi. Niliisha mwambia hawa MATAPELI wachumia tumbo hakubali mpaka aachane nao, yeye sijui huwa wanamvuna vipi. Na kazi yake ya ualimu huwa nauonea huruma mshahara wake tu. Hata sijui mkweli yupi ila woote matapeli.
 
hapa kwetu naambiwa maamuzi mengi ya serikali huulizwa yye kwanza akisema yes ndio tunatangaziwa
 
kiongozi haya ni maswala ya imani..mwenye imani ataweza kushuudia ukuu wa Mungu.
Hahaha sio kutoka kwa hawa manabii na kwambia. Hawa wasaka tonge. Huduma za kiroho ni bure hawa wanazitumia kama biashara zao kijitajirisha hapo ndio maana mimi nasema ni MATAPELI.
 
Na Ahmed Rajab

T.B. Joshua ni mtu wa ajabu. Kuna wasemao kwamba mzalia huyu wa Nigeria si binadamu wa kawaida. Wanaamini kwamba yeye ni nabii. Wengine wanasema kuwa ni mtume kamili aliyepewa wahyi na miujiza ili aweze kuwahubiria watu na kuwalingania.

Na kuna wanaokana. Wanasema kwamba T.B. Joshua hana unabii wala utume wowote ila yeye ni afiriti, mwana wa ibilisi, shetani anayewaghilibu watu.

Serikali ya Cameroon iliwahi kuliweka jina lake kwenye orodha ya watu wabaya wasiotakikana nchini humo. Na ikawaonya wananchi wake wenye kufunga safari kwenda kumtembelea Lagos, Nigeria, wawe na hadhari wasighilibike.

Serikali ya Zambia nayo iliwahi kuwaonya raia zake wasimwendee Joshua kwa sababu fedha zikiwaishia hukwama huko Nigeria.

Naawe awavyo, apendwe asipendwe, T.B. Joshua hakosi wenye kumfuata. Ana wafuasi wengi miongoni mwa walio katika tabaka aali la watu wenye uwezo katika jamii katika takriban ukanda mzima wa Afrika ya Magharibi. Watu husafiri kila mwaka kutoka sehemu mbalimbali za Afrika kwenda Lagos kulizuru kanisa lake.

Wasiojiweza huuza hata nyumba au mashamba ili wapate fedha za safari. Wanatoka Liberia, Ghana, Sierra Leone, na hata kutoka nje ya Afrika ya Magharibi.

Nakumbuka safari moja nikiwa uwanja wa ndege wa Murtala Muhammed, jijini Lagos, nilikumbana na kikundi cha watu zaidi ya hamsini waliowasili kutoka Nairobi. Wote walikuwa wamevaa fulana za T.B. Joshua. Walikuwa wanaelekea mtaa wa Egbe, huko Lagos, kwenye kanisa la The Synagogue, Church of All Nations (Sinagogi, Kanisa la Mataifa Yote), kwa ufupi SCOAN. Hapo ndipo penye makao makuu ya madhehebu hayo ya kikristo aliyoyaanzisha T.B. Joshua. Hili ni kanisa kubwa Afrika kwa idadi ya wafuasi wake na linazidi kukua.

Septemba 12, 2014 jengo la ghorofa sita la kanisa hilo huko Lagos liliporomoka. Watu wasiopungua 116 walikufa katika ajali hiyo, 85 kati yao walitoka Afrika Kusini. Jamaa wa marehemu hadi leo wanataka kujua nini hasa kilitokea na nani wa kuwajibika. Mwaka 2015 Joshua alifunguliwa kesi ya jinai, yeye pamoja na wahandisi wawili na wadhamini wa kanisa. Bado kesi haijamalizika kwa sababu Joshua amekuwa akikwepa kwenda mahakamani.

Ni wazi kwamba mchungaji huyo na mwinjilisti wa televisheni anaifahamu Afrika na anawafahamu vilivyo Waafrika wenzake, hasa wasomi miongoni mwao. Anafahamu namna akili zao zinavyofanya kazi na jinsi anavyoweza kuzichezea.

Rais wa zamani wa Ghana, marehemu Profesa John Attah-Mills baada ya kushinda uchaguzi alimshukuru kwanza Mungu na halafu akamshukuru T.B. Joshua kwa kumsaidia kushinda uchaguzi huo. Attah-Mills aliwahi kusema hadharani kwamba Joshua alitabiri kweli ya kuwa baada ya kushiriki katika chaguzi tatu ndipo ataposhinda uchaguzi wa urais wa Ghana.

Attah-Mills alikuwa na mazoea ya kumtembelea Joshua kwenye kanisa lake. Alikuwa akenda mara kwa mara kufanya maombi kabla hajawa rais na baada ya kuwa rais. Marais wengine wa zamani wa Kiafrika waliowahi kumzuru Joshua walikuwa Andre Kolingba (Jamhuri ya Afrika ya Kati), Frederick Chiluba (Zambia), Profesa Pascal Lissouba (Congo-Brazzaville), Joyce Banda (Malawi) na Omar Bongo (Gabon).

Miongoni mwa Waafrika mashuhuri waliovutwa na simaku yake ni Prince Johnson na Rais George Weah (wote wawili kutoka Liberia). Kutoka Tanzania ni Edward Lowassa na Rais John Magufuli. Kutoka Zimbabwe Morgan Tsvangirai, kutoka Malawi Sam Mpasu na Walter Nyamilandu, Rais wa Jumuiya ya Soka ya Malawi (FAM).

Kutoka Afrika Kusini Julius Malima, Winnie Mandela, Goodwill Zwelithini (mfalme wa Wazulu), pamoja na waimbaji Yvonne Chaka Chaka na Sechaba.

Hata Gavana-Mkuu wa Bahamas, Sir Orville Turnquest alimpokea Joshua alipomtembelea 2001.

Jambo linalonihangaisha ni ushawishi mkubwa alionao mchungaji huyo kwa baadhi ya viongozi wa Kiafrika. Unaweza ukautafsiri ushawishi huo kwa walau njia mbili. Ama amewateka na kuwatia mikononi viongozi hao au hao viongozi wamemkinai vya kutosha kiasi cha kuwa tayari kumuamini na siri zao ambazo pia huenda zikawa siri za serikali.

Mgeni kuwa na nguvu za aina hizo katika nchi za watu wengine si jambo la maskhara la kuchukuliwa kijuujuu, hasa kwa mtu ambaye dhamira na ajenda zake za kisiasa si bayana. Si jambo la kufumbiwa macho. Hatujui huwa anafanya nini au hutaka kujua nini anapowatembelea viongozi katika Ikulu zao.

Huenda akawa anatumiwa, ama kwa kujua au bila ya kujua. Kwa mfano, tunajua kwamba ana uhusiano mzuri na serikali ya Israel, nchi ambayo amekuwa akiizuru mara kwa mara na ambako amekuwa akionana na wakubwa wake.

Tuijuavyo Israel na weledi wake wa kuelea katika mikondo ya chini kwa chini katika siasa za kimataifa, nadhani ni halali tukiuliza kwa kiasi gani Israel imeweza kumtumia T.B. Joshua kuwafanya baadhi ya viongozi wa Kiafrika wabadili misimamo ya nchi zao kuhusu Israel?

Israel, taifa la majungu lisilopoteza fursa yoyote itayoweza kuinufaisha kimataifa, itakuwa imepoteza moja ya sifa zake kuu lau haikumtumia Joshua kwa maslahi yake. Israel haitokuwa Israel ikiwa haikujaribu kufanya hivyo.

Wenye kuifuatilia mitandao ya wahalifu wa kimataifa wana wasiwasi kwamba huenda kanisa lake la SCOAN likatumiwa, hata bila ya mwenyewe kujua, kuzisafisha fedha chafu zilizopatikana kwa njia za haramu.

La hatari zaidi ni kwamba yeye mwenyewe T.B. Joshua huenda akawa hatari kwa usalama wa taifa kwa kujulishwa mambo na wenye kuendesha nchi au na walio karibu nao, mambo ambayo hastahiki kuyajua.

Yote hayo tunayasema kwa hadhari tu kwani huenda akawa anawachezea akili tu viongozi wa Kiafrika bila ya kuwa na madhara kwa mustakbali wa nchi zao. Hatujui. Lakini hayo ni baadhi ya maswali nyeti yanayostahiki kuulizwa kuhusu ushawishi wake kwa viongozi wa baadhi ya serikali za Kiafrika.

Tatizo lililopo ni kwamba mtu atapokuwa anajaribu kuyauliza maswali hayo atakuwa anayaingilia mambo ya kiroho na ya imani za watu. Hili ni tatizo kubwa. Kuna hatari kwamba katika kuulizauliza kwako ukadhaniwa kwamba unapinga ukristo au unampinga Yesu Kristo. Kosa kama hilo la kuziingilia imani za watu liliwahi kufanywa na Kwame Nkrumah, rais wa kwanza wa Ghana.

Waumini wa T.B. Joshua wanaiona imani yao juu yake kuwa ni sahihi. Kwa hivyo, hawaoni ubaya wowote kwa viongozi wa serikali zao pia kumfuata. Hawa ni watu ambao wanapomuona T.B. Joshua anafanya maombi kwenye vipindi vyake vya televisheni vya Emmanuel TV huugusa uso wa televisheni ili wapate “baraka” zake. Huna cha kuwaambia watu kama hao.

Ikiwa viongozi wa Kiafrika wana itikadi kama hizo basi nchi zao zimekwisha.

Kwa kiwango gani viongozi hao huwa wanamshirikisha wanapokata maamuzi yao. Na yeye huwashauri nini na kwa mantiki gani?

Ni nani hasa huyu T.B. Joshua? Alikwendakwendaje akaibuka kuwa na wafuasi alionao hata katika Ikulu za baadhi ya nchi za Kiafrika? Na ushawishi wake hauko Afrika tu, umevuka bahari ya Atlantiki na umesukumwa na pepo hadi Amerika ya Kusini, ingawa ushawishi huo haukufika bado katika Ikulu za huko.

Hata hivyo, lukuki na lufufu ya watu walihudhuria ibada zake alizozifanya miaka ya hivi karibuni Colombia, Mexico, Peru na Paraguay. Aliziita ibada hizo “vita vya msalaba” au “vita vitakatifu”

Ziara aliyoifanya Paraguay 2017 ilizusha mjadala mkubwa nchini humo, pale bunge la huko lilipoidhinisha atunukiwe nishani ya “Orden Nacional del Merito”. Hiyo ni nishani ya hadhi ya juu kabisa nchini humo na hutunukiwa raia wa Paraguay tu.

Kuna waliokuwa wakihoji kwamba “el profeta” (mtume) Joshua alistahiki nishani hiyo kwa “kuwaponesha” watu waliokuwa na magonjwa makubwa kama saratani au UKIMWI. Inasemekana pia kwamba aliwapunga wenye kudai kwamba walikuwa na mashetani kichwani.

Joshua amechuma fedha chungu nzima kutokana na ziara zake hizo, pamoja na michango na ada anazolipwa na wafuasi wake. Alionyesha ukarimu wake Julai 2014 alipokuwa ziarani mjini Cali, Colombia, ambako watu wasiopungua laki moja walihudhuria mkusanyiko wake aliouita “Muujiza wa Vita vya Msalaba”.

Baada ya kumaliza ibada aliwapa polisi wa huko Cali dola za Marekani laki moja ($100,000) kuwasaidia wanafamilia wa polisi waliouliwa au waliojeruhiwa wakiwa kazini. Fedha hizo ni kama ndururu tu ukizingalisha na utajiri wake binafsi unaokisiwa kuwa si chini ya dola za Marekani milioni 15.

Kwa mtu asiyependa kusafiri Joshua amesafiri sana kwani amewahi pia kuzuru Tanzania, Korea, Singapore, Indonesia na Australia.

Joshua anadai kwamba mazazi yake yalitabiriwa miaka mia moja kabla. Kuzidi kuonesha kwamba yeye si binadamu wa kawaida anadai pia kwamba alikuwa tumboni mwa mama yake kwa muda wa miezi 15 kabla ya mama yake kujifungua Juni 1963.

Jina lake kamili ni Temitope Balogun Joshua, ingawa alipokuwa anasoma skuli akijulikana kwa jina la Balogun Francis.

Masomo yake rasmi ya skuli hayakupindukia ya sekondari ambayo hakuyamaliza. Mwenyewe anasema alivutiwa na masomo ya Biblia tangu akiwa mdogo. Baada ya kumaliza masomo yake ya msingi alifanya kazi mbalimbali za vibarua ikiwa pamoja na kubeba mavi ya kuku katika shamba la kuku.

Anasema mambo yalimfungukia alipoamriwa mbinguni aanzishe kanisa lake. Lakini je, ushawishi wake kwa viongozi wa Kiafrika unamalizika kwa kuwazingua na kuwapunga pepo tu? Au kunaya ziada?


Baruapepe: aamahmedrajab@icloud.com; Twitter: @ahmedrajab



View attachment 984327View attachment 984328

Sent using Jamii Forums mobile app
wote wasanii
tapatalk_1542891877120.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Lakini haombi sadaka,pia hata yeye hakubali kama ana nguvu zote hizo za miujiza bali anaamini kupitia roho mtakatifu huyafanya yote kwa jina la Yesu!!yeye mwenyewe anaamini imani ya mtu ndio ngao na masomo yake yamebase katika mlengo huo!!
 
Ndugu yangu hata kama una uwezo wa kuponya, huwezi ponya kila mtu! Yesu ndiye tunayemwamini na ana uwezo wa kuponya, kufufua na kila kitu, lakini hakuponya wote.... Kanuni iko wazi...... Njooni wote wenye mizigo....which means ni lazima mtu mwenyewe kwa imani achukue hatua ya kumfuata na hapo huweza kupokea muujiza wake tena akiwa na imani. Sasa tukisema kwamba wote waombewe wapone ni mtizamo mzuri lakini sio wa Kibiblia.

So pamoja na kwamba wokovu umekuwepo tangu kifo cha Yesu msalabani, bado ni lazima mtu binafsi achukue hatua ya kumfuata Yesu kikamilifu na sio muujiza tu halafu unarudia yale ya zamani.

Hata huko Ocean Road Hospital, ni wote wanamtaka Yesu kweli?
Hahaha kwenye ugonjwa wangeponya hata wapagani wangemfuata yesu.
Hawa manabii wansjotajirisha wao kupitia dini, na hapo ndio nawaona matapeli. Mbona Yesu hakutoza watu pesa kwenye makusanyiko yake, wao wanatoza hadi kupitiliza. Kuna gharama za kawaida hizo sawa zichangiwe na waumini kama ujenzi wa kanisa, umeme, maji na gharama zinapojitokeza. Lakini sio mchungaji ajenge ghorofa na amiliki private jeti kupitia sadaka huo ni utapeli.
 
Back
Top Bottom