Swali

Swali

Mpenzi Mbu nimekuwa nikikutarajia tangu asubuhi mpenzi haya imekuwaje leo?

Tafadhali naomba upitie post za Darck City kwanza then utaona concern yangu darling
(Kaizer habari?)

My Mj'1,

haikuwa nia yangu ku-disappoint kwa kutoa comment kinyume na matarajio yako, ila ukweli ndio huo.

Mkishaanza kuchungana sana kwenye maisha ya ndoa itafikia mtu kunusa hata chupi ya mwenzio,...

Ok, ngoja nipitie posts za DC kwanza...dah, nimelala sana leo hizi kazi za kukesha mnhhh!
 
Ndoa inabeba jukumu kuu ia kuifanya miili miwili yenye jinsia tofauti kuwa mwili mmoja na moja ya nguzo kuu za ndoa ni uaminifu kwani wakati wa kuingia kwenye ndoa unachukua chaguo lako ambalo umeapa kufa nalo.Hayo yaliwezekana miaka mingi iliyopita si leo kwenye zama hizi za utandawizi na uhuru zaidi.zamani mwenye ndoa alikuwa anafungamana nayo na ilikuwa ngumu kumega au kumegwa nje ya ndoa maana hakuna wa kumega kumegwa.Ama wote wana ndoa na wengine wanakuwa wanasubiri wachumba.ilikuwa ni fedheha kumega au kumegwa nje ya ndoa. Dhana hiyo ilifaa kipindi hicho tu. Zama hizi ni maiigizo matupu. Ni upuzi mtupu kuamini kuwa kuna ndoa.ndoa bila uaminifu ni jinamizi hakuna aliyetayari kuukana mwili wake ili uwde mwili mmoja. Kila mtu anataka uhuru pasi kubanwa na kitu kíitwacho ndoa. Hakuma uvumilivu. Kwa sababu ndoa nyingi kama si zote nimekubwa na jinamizi hilo la uaminifu na uadilifu kuwa zero kuna haja ya jamii hii ya kisasa iangalie AINA MPYA YA MAHUSIANO badala ya jinamizi la NDOA linalowakwaza wengi wetu.BINADAMU WA LEO HATAKI KUMILIKIWA ndoa itatoka wapi kama sio maigizo matupu.NAWASILISHA
 
...
Je mkeo/mumeo akifanya hivi utafikiriaje?
2. Kafanye nini kutoa huu wasi wasi wake?

Best (and my personal advice), never ever do it. But if you can't stand the temptation then take that option (red). We always see what we expected to see. If no signs, then you partner is as happy as an angel. Some of us might be in that corridor.
But believe me, it is very safe, really safe for your feelings and your health as well!

...tayari nimemsoma DC, ...na hili alilosema hapo juu namuunga mkono 99.9%... am in the same boat... pale Curiosity inaponizidi uwezo hata mimi hupekua bana... na ukweli it's such a relief ukikuta hakuna kitu japo kiroho mhhnnn!

Kwa ambao tushawahi kuwa cheated na wenza wetu nadhani wananielewa nasema nini juu ya hili. Trust ikishaondoka ndio ishaondoka hiyo... Utashawishika tu kupekua.
 
may be hapendi usumbufu wa kupigiwa pigiwa simu akiwa na la azizi wake.Siunajua tena simu zikianza kuita na hasa kama jamaa anajijua kwamba simu yake iko bize sana.
 
MwanajamiiOne!

Mdogo wako atulie na kujali mambo mengine muhimu..japo swala la kuisha charger kama ni kila usiku nahisi ni la uongo!..Au wanapokuwa mbali simu ya mista inakuwa imezimwa usiku?!!

Anaweza kung'ang'ania kwa nini simu haiwashwi usiku, ikawashwa na sms+calls zikaanza kuingia usiku sana...lazima atakereka na kutaka kujua nani anamtafuta mumewe muda huo..Sasa hizo ni presha tu!!..

Maisha mafupi, presha ikizidi ndo kabisaa!..
 
Suala la fidelity to me is more individual and depends on how you realize yourself. If your perception, your inner belief sees cheating ok, even if you someone will intercept every conversation, every sms, still you will cheat! Fidelity is abstinence and it is leaving according to moral standard! Infidelity crooked, it is pervert, it is selfish and it’s only who abhor this immorality can overcome this temptation

Usimchunge! Wala usitake kudadavua kilichoko nyuma ya pazia maana huwezi kubadili mtazamo wa mtu kwa njia ya ku-monitor isipokuwa kama huna amani ongea nae humbly mwambie kinachokutia wasiwasi kwa upole na unyenyekevu. Kama ni mtu tu mwenye roho ya nyama kama zetu hizi lazima tu atafunguka.
 
Huyu bwana ni mustaarabu na ana mapenzi na mwenza wake.Anazima simu apate muda wa kutosha wa kuongea na mkewe,badala ya kusumbuliwa na miliio ya simu kila mara.Kupata muda mwafaka wa penzi.Sioni kwanini dada yetu anataka miito ya simu badala ya kuvijali na mmewe (Zima simu;zima TV na redio kula raha na mwenzi wako).
 
Baba Enock leo umeamkia upande gani? Maana nondo unazotoa zimekwenda shule haswa.

Nakubaliana na wewe but yeye anaumia kwa kuwa anasema mbona akiwa yuko mokoani huko mumewe hazimi simu na ni mara nyingi tu yeye huwa anampigia simu na kukuta iko on pamoja na kuwa huwa hapokei!!

Mimi nadhani kuna umuhimu wa kuresearch athari za simu za mikononi kwa wanandoa ili hata tukikatazwa tuwe tuna reference lol.

Ila inatia dukuduku hasa unapoanza kuhisi kuwa mwenzio kabadilika!!
hapo kuna walakini kabisa................!?
 
hapa tutaongea simu,imeisha charge ...sijui ikazimwa,sijui ikapelekwa uvunguni mwa kitanda swala zima katika ndoa /mahusiano ni uaminifu
sidhani kama kuna upande ambao utapenda kuibiwa .
Uaminifu ni jambo kubwa na la msingi.
Ukiwa mwaminifu - utakuwa free na simu yako
Ukiwa mwaminifu- hutamfikiria mwenzio mabaya
Ukiwa mwaminifu- utaishi kwa amani siku zote
 
hapa tutaongea simu,imeisha charge ...sijui ikazimwa,sijui ikapelekwa uvunguni mwa kitanda swala zima katika ndoa /mahusiano ni uaminifu
sidhani kama kuna upande ambao utapenda kuibiwa .
Uaminifu ni jambo kubwa na la msingi.
Ukiwa mwaminifu - utakuwa free na simu yako
Ukiwa mwaminifu- hutamfikiria mwenzio mabaya
Ukiwa mwaminifu- utaishi kwa amani siku zote

......Hapo kweli umeongea shost, mtu ukiwa mwaminifu wala huna haja ya kuwa na hofu simu yako, upo free kabisa hata mpenzi wako akishika.
Huyo mwanaume anayejifanya kuzima zima simu ana lake jambo.

Kama simu yake kimeo tatizo battery basi huyo mdada amnunulie battery au simu nyingine maana hapo atamkomesha.........akiona tena anazima zima basi huyo ana mwanamke mwingine nje kama sio wanawake.
 
hapa tutaongea simu,imeisha charge ...sijui ikazimwa,sijui ikapelekwa uvunguni mwa kitanda swala zima katika ndoa /mahusiano ni uaminifu
sidhani kama kuna upande ambao utapenda kuibiwa .
Uaminifu ni jambo kubwa na la msingi.
Ukiwa mwaminifu - utakuwa free na simu yako
Ukiwa mwaminifu- hutamfikiria mwenzio mabaya
Ukiwa mwaminifu- utaishi kwa amani siku zote
Aksante mama!
 
Mtazamo wangu mimi kuhusu simu ya mkononi unabaki pale pale;

Simu ni kama cheti cha kuzaliwa, hakichangiwi;
Simu ni kama kadi ya kupigia kura, haichangiwi;
Simu ni kama kitambulisho cha uraia, hakichangiwi;
Simu ni kama alama za dole gumba, hazifanani na za mtu yeyote hata awe pacha wako!!

Nitaendelea..........!!!!
 
Inaweza ikawa kichekesho kwa wengi hapa,hasa ukichukulia wanaume kwa wanawake tunajuana fika tabia zetu.
Ila ushauri wangu ni huyo ndugu yako asifikili vibaya ama mabaya,anachotakiwa afanye ni kuongeza UAMINIFU kwa huyo mwenza wake,yaani asitiliye shaka au hata kama anashaka shaka na tabia mpya ya huyo mwenza wake basi ajaribu kuficha hizo hisia zake na achukulie na kumuonyesha huyo muhusika kwamba yeye hajari na ni kawaida weither ana zima ama kuwacha wazi.
Nakuhakikishia this works,mabadiliko utayaona hata kama itachukua muda basi lakini lazima mabadiliko yatakuwepo.

Ndugu yangu zama za kuaminiana kibubu zimepita. Ukiwa na mashaka na mwezi wako tafuta ukweli. Ukihakikisha kuwa si mwaminifu mwambie ukweli akikiri na kuomba msamaha na kuahidi kuacha msamehe na endelea kufuatilia nyendo zake na ukigundua hajaacha hata hiyo samahani yake haina maana achana naye. Vinginevyo atakutia kwenye matatizo bure enzi hizi zenye maradhi yasiyotibika.
 
Mtazamo wangu mimi kuhusu simu ya mkononi unabaki pale pale;

Simu ni kama cheti cha kuzaliwa, hakichangiwi;
Simu ni kama kadi ya kupigia kura, haichangiwi;
Simu ni kama kitambulisho cha uraia, hakichangiwi;
Simu ni kama alama za dole gumba, hazifanani na za mtu yeyote hata awe pacha wako!!

Nitaendelea..........!!!!

Mwili wa mtu ni personal property, tena zawadi kutoka kwa Mungu, unachangiwa! Vipi hapo? Kipi ni muhimu kati ya hayo?
 
Mwili wa mtu ni personal property, tena zawadi kutoka kwa Mungu, unachangiwa! Vipi hapo? Kipi ni muhimu kati ya hayo?

DC....ulikuwa wapi wewe lakini
anyway better late than never!!!
 
Back
Top Bottom