Swali | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Swali

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by MwanajamiiOne, Feb 22, 2010.

 1. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #1
  Feb 22, 2010
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,476
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  habarini wanandugu

  Kuna wakati nilishawahi kuuliza dalili kuwa mwenzio si mwaminifu kwako ni zipi nikashindwapata jibu. Sasa nauliza specifically maana kuna mdogo wangu kaja analalamika kuwa mumewe haeleweki siku hizi kila akija au yeye akienda (wanaishi mikoa tofauti) usiku lazima mume azime simu zake. Akimwuuliza anadai kuwa zina matatizo ya charge!! Yaani hata akiomba kurushiwa credits mr atawasha, amtumie kisha anazima.

  sasa mie alivyoiweka kwangu naona ni kama mr anaavoid kugonganisha magari hewani au nakosea?

  Je mkeo/mumeo akifanya hivi utafikiriaje?
  2. Kafanye nini kutoa huu wasi wasi wake?
   
 2. bht

  bht JF-Expert Member

  #2
  Feb 22, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 10,341
  Likes Received: 211
  Trophy Points: 160
  dalili zaonesha kunaweza kuwa na tatizo
  lakini kuchimba zaidi kunaweza kumpa matatizo zaidi maana ndo atakutana na naked truth humo kwenye simu
   
 3. Sanda Matuta

  Sanda Matuta JF-Expert Member

  #3
  Feb 22, 2010
  Joined: May 9, 2007
  Messages: 950
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Inaweza ikawa kichekesho kwa wengi hapa,hasa ukichukulia wanaume kwa wanawake tunajuana fika tabia zetu.
  Ila ushauri wangu ni huyo ndugu yako asifikili vibaya ama mabaya,anachotakiwa afanye ni kuongeza UAMINIFU kwa huyo mwenza wake,yaani asitiliye shaka au hata kama anashaka shaka na tabia mpya ya huyo mwenza wake basi ajaribu kuficha hizo hisia zake na achukulie na kumuonyesha huyo muhusika kwamba yeye hajari na ni kawaida weither ana zima ama kuwacha wazi.
  Nakuhakikishia this works,mabadiliko utayaona hata kama itachukua muda basi lakini lazima mabadiliko yatakuwepo.
   
 4. drphone

  drphone JF-Expert Member

  #4
  Feb 22, 2010
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 3,561
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 145
  kwa mm lazima nijue ananidanganya tu akuna lingine na atakuwa mshamba kiasi fulani inamana ana mke alafu kadanganya ana mke ndomana akifika kwa mke lazima azime cm kwani anaweza kupigiwa cm mda wowote
   
 5. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #5
  Feb 22, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,834
  Likes Received: 249
  Trophy Points: 180
  MJ1,

  Achana na mambo ya SIMU za mkononi!

  Kila wanandoa waweke "policy" zao "re mobile phone usage"

  Vinginevyo NDOA nyingi zitadondoka!
   
 6. Balantanda

  Balantanda JF-Expert Member

  #6
  Feb 22, 2010
  Joined: Jul 13, 2008
  Messages: 12,371
  Likes Received: 1,093
  Trophy Points: 280
  Bora akae kimya tu afumbe macho(afunike kombe mwanaharamu apite?) maana(pengine) anayoweza kuja kuyakuta kwenye hiyo simu yanaweza kuja kuleta maafa kwenye ndoa yake na kuihatarisha kabisa kisha akaanza kujuta kwa nini simu 'iliwashwa' badala ya kuzimwa kama ilivyo ada
   
 7. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #7
  Feb 22, 2010
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 54,253
  Likes Received: 31,431
  Trophy Points: 280
  Si umeonae?
  Mi bana mke wangu kugusa simu yangu ni STRICTLY PROHIBITED!
  Hii yote ni kwa ajili ya kudumisha ndoa yetu!~
   
 8. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #8
  Feb 22, 2010
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,476
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Baba Enock leo umeamkia upande gani? Maana nondo unazotoa zimekwenda shule haswa.

  Nakubaliana na wewe but yeye anaumia kwa kuwa anasema mbona akiwa yuko mokoani huko mumewe hazimi simu na ni mara nyingi tu yeye huwa anampigia simu na kukuta iko on pamoja na kuwa huwa hapokei!!

  Mimi nadhani kuna umuhimu wa kuresearch athari za simu za mikononi kwa wanandoa ili hata tukikatazwa tuwe tuna reference lol.

  Ila inatia dukuduku hasa unapoanza kuhisi kuwa mwenzio kabadilika!!
   
 9. carmel

  carmel JF-Expert Member

  #9
  Feb 22, 2010
  Joined: Aug 24, 2009
  Messages: 2,840
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  i love this
   
 10. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #10
  Feb 22, 2010
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,476
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  X-Pin kujua kama simu iko on au la si lazima uikague bana, huyu shem wangu yeye akifika tu home usiku anazima matokeo yake sasa rafiki zake au ndugu wakiwa wanampigia inabidi wamcal kupitia kwa wife si ndo wife akamwuliza kwa nini kazima simu? Since then ni mwendo mdundo
   
 11. bht

  bht JF-Expert Member

  #11
  Feb 22, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 10,341
  Likes Received: 211
  Trophy Points: 160
  kweli kabisa......
  ufukunyuku unaweza ukaleta tatizo kubwa zaidi. akae zake kimya tu!!! she is the wife hao wengine huko watajiju.....
   
 12. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #12
  Feb 22, 2010
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,476
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Hapa si ndipo tunapotakiwa kujua? Ndoa ni ukweli na uaminifu sasa tukikubaliana na hali hii ina maana tunaidhinisha kuwa wenzi wetu ni macheaters and that's how they are so tuchukuliane nao hivyo hivyo?? dunia ya sasa ?

  Mimi nilifikiri kuwa mtu unatakiwa kuwa makini mara tu unapoanza kuhisi dalili zisinzo nzuri kwa mwenzi wako?

  mimi nimemwambia ni dalili ya kucheatiwa so awe makini lakini kwa ushauri wenu naona nimetokota!!
   
 13. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #13
  Feb 22, 2010
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,939
  Likes Received: 387
  Trophy Points: 180
  Jamaa lazima atakuwa na Kimada huko anakoishi. ukishaona mwenzi wako ana zima zima simu uiwepo baaasi jua unamegewa mali zako.
   
 14. drphone

  drphone JF-Expert Member

  #14
  Feb 22, 2010
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 3,561
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 145
  no comment
   
 15. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #15
  Feb 22, 2010
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,969
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  hivi huyo ndio afanye umzime cm mke wako wa ndoa? sio yeye apewe masharti mke anapocal akae kimya?...kazi ipo.
   
 16. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #16
  Feb 22, 2010
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 12,039
  Likes Received: 3,873
  Trophy Points: 280
  inawezekana kweli cmu inatatizo la charge..............kama haamini ashuhudie mwenyewe ikichargiwa na iwashwe mpaka asubuhi ili aone kama tatizo la msingi ndio hiklo au kuna lingine baada ya hapo afatilie mambo mengine..........njia ya mwongo ni fupi sana...
   
 17. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #17
  Feb 22, 2010
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,476
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Basi mimi ninaishi dunia ya kufikirika mwenzenu!! na magonjwa haya yaliyopo? itanichukua muda kweli kuafikiana na hii but it seems ndo art
   
 18. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #18
  Feb 22, 2010
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,969
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0

  mhhhhh......
   
 19. bht

  bht JF-Expert Member

  #19
  Feb 22, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 10,341
  Likes Received: 211
  Trophy Points: 160
  Sasa my dear akishajua si ndio vita inaanza?? labda sijui amuulize kwa style gani...
  ndoa inapaswa kuwa yenye uaminifu lakini ulimwengu tuishimo mambo mengi yamebaki ya kusadikika tu.....
   
 20. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #20
  Feb 22, 2010
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 54,253
  Likes Received: 31,431
  Trophy Points: 280
  MJ1 unamaanisha nini kusema AWE MAKINI? Ampige chini au avumilie au aanze kutumia kondom? Hizo si DALILI za kuchitiwa. Ni kwamba anachitiwa tayari!
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...