swali

crunkstaa

JF-Expert Member
Aug 4, 2012
331
159
kuna jamaa anaitwa johnson,anamiliki saa saa ya mkononi,siku moja Hamisi akamwomba ile saa ili aende nayo harusini,kesho yake akawa anarudisha ila kabla ajamkabidhi Johnson,akakutana na Shabani ambaye ni rafiki wa Hamisi,nae akamwomba saa ili atoke out.Hamisi akampa ili baadae amrudishie.Baadae Shabani akawa anamrudisha saaHamis, akakutana na rafiki yake Juma ambae nae akamwomba ile saa ili aende nayo club.Wakati Juma anatoka Club alivamiwa na majambazi na wakampora ile saa.

Juma akamwambia Shabani nae akamweleza Hamis.Wote wakakubaliana waende kwa Johnson wamuulize ile saa alinunua shilingi ngapi ili wachange kisha wamlipe.Jibu walilopewa ni 30,000/-i.Hivyo kila mmoja alitoa shiling 10,000/-.wakamkabidhi Hamis.
Hamis alipofika dukani alikuta saa inauzwa 25,000/-,akainunua.kisha akawarudishia Juma,Shabani na yee mwenyewe 1,000/-.Akampa mdogo wake 2,000/- kama asante ya kumsindikiza kisha akanunua saa 25,000/- na kuirudisha kwa mwenyewe.

Swali sasa.

kama kila mmoja alirudishiwa 1,000/-,inamaana watakuwa walichangia 9,000/- kila mmojo.kwa watu watatu inakuwa 27,000/-.ukijumlisha na ile 2,000/- aliyopewa mdogo wa Hamis kama asante ya kumsindikiza inakuwa 29,000/-.sasa 1,000/- imepotelea wapi kama mwanzoni walitoa 30,000/-,ila baada ya kununua saa mahesabu yana kuja 29,000/-?.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom