Swali la weekend kwa wanafamilia...

Swali la weekend kwa wanafamilia...

Kwanini sasa na wanadai wawezeshwe ili waweze

Na kweli wawezeshwe maana kujisimamia wenyewe hawawezi. ntakupa mfano
kipindi nipo nyumbani kabla sijajitegemea kuna baba mmoja jirani alikuwa ana club ya mbege. mimi na mzee wangu tulikuwa tunaenda kunywa na kurudi nyumbani. hiyo club ilikuwa kubwa sana kwa kijiji chetu. alipofariki yule baba, mama akashika hatamu. wale wahudumu walikuwa wananyanyaswa sana wakaondoka. leo alete huyu kesh afuuze. mwisho wa siku biashara ikaenda mrama, mimi na mzee wangu tukahama kabisa kwa sababu mama hana kauli nzuri. huo ni mfano mdogo

tatizo lao wako makini na hela zao. pochi ya mwanamke inaiingizaga hela kutoa ni mwiko. uwekezaji una riski sana lazima apate apprentice wa kiume kumuongoza namna ya kuwekeza. shida ya wanaume lazima waombe kipochi manyoya kwanza
 
Kipato cha familia ni kwa maana zitatumika kwa familia
kama mmoja kila akipata ni matumizi yake binafsi basi haiwezi kuwa kipato cha familia
Sikumaanisha kila aliyetafuta afanye matumizi binafsi, hapo utakuwa una maanisha hata watoto pia lazima wakatafute za kwao ili wafanye matumizi binafsi.
Kipato cha familia, kinatoka kwa wanafamilia, mgawanyo wa matumizi hauna jibu moja(unategemea na utaratibu za familia)
Usilazimishe Mapato na Matumizi lionekane ni jambo moja, hususani kwa hii case. Otherwise unataka mjadala.
 
Kimsingi pato la familia linatakiwa litoke kwa mwanaume 100%.

Kama huwezi kuhudumia familia kwa mahitaji yote bora usioe.

Pesa ya mwanamke si ya kutegemea, kwanza huenda anahongwa na wanaume wengine hivyo kukufanya wewe mtegemezi wa pesa za wanaume wenzako kupitia kipochi cha mkeo.

Hawa wanawake wewe waone tu ila usifikiri ni ndugu zako.
 
Inategemea na familia na familia. Upendo, uwazi na mgawanyo wa majukumu. Kwa familia yangu hapo kipato cha familia ni laki saba
 
Kipato cha familia ni laki 2

Laki 5 haihusu familia hahaha

kuna mtu mmoja alinambia mwanamke ukimpa lak 5 kwa ajili ya matumizi nyumban sababu unasafiri ikatokea safari ikafa ni kwamba ile lak5 ilishaisha so utoe pesa nyingine ya matumizi

Na hata ukimkopesha mwanamke ujue huruhusii kudai
 
Mkuu kila kitu nimakubaliano katika familia.
kama mke anafanya kazi kwa nini asichangie pato la familia ?
Watu wengi tumezoea mke hachangii pato kwenye familia ila mambo yamebadilika sana sio kama zamani.
 
Katika general sense hapo familia ina laki2, ila ingekuwa ni familia yangu basi tuna laki7.

Maana kipatikanacho ni chetu,we become one.

Heaven Sent ukome kuhack id yangu.
 
kuna vicoba ,kuna michango ya kitchen party,sendoff,familia yake huko,saluni ,mikorogo mambo kibao hata hyo laki tano haitoshi itabidi na hyo laki ya baba imchangie kidogo mkuu
Mkishakuwa wanandoa basi maamuzi ya familia yanafanyika pamoja, kwahiyo kama kuna vikoba sijui michango ya sherehe mnashirikishana na kufanya kwa nafasi iliyopo.

Kuanza kutenga hiki cha huyu hiki cha yule ndipo migogoro huanzia hapo.
 
Kimsingi pato la familia linatakiwa litoke kwa mwanaume 100%.

Kama huwezi kuhudumia familia kwa mahitaji yote bora usioe.

Pesa ya mwanamke si ya kutegemea, kwanza huenda anahongwa na wanaume wengine hivyo kukufanya wewe mtegemezi wa pesa za wanaume wenzako kupitia kipochi cha mkeo.

Hawa wanawake wewe waone tu ila usifikiri ni ndugu zako.
Kama kuhongwa hata wanaume wanahongwa vilevile,mwanaume sio ndugu yako pia.
Haya mambo mbona tunazidi kuyafanya yawe magumu hivi!!!
 
Kama kuhongwa hata wanaume wanahongwa vilevile,mwanaume sio ndugu yako pia.
Haya mambo mbona tunazidi kuyafanya uawe magumu hivi!!!
Hiyo ni special & abnormal case.

Kwenye familia mwanaume ni family protector & provider na mwanamke ni nest defender......sasa kama kuna mwanaume anahongwa na mwanamke hiyo ni kinyume na nature.
 
Mkishakuwa wanandoa basi maamuzi ya familia yanafanyika pamoja, kwahiyo kama kuna vikoba sijui michango ya sherehe mnashirikishana na kufanya kwa nafasi iliyopo.

Kuanza kutenga hiki cha huyu hiki cha yule ndipo migogoro huanzia hapo.
mmmh ile degree unakaribia kugraduate nini
 
Hiyo ni special & abnormal case.

Kwenye familia mwanaume ni family protector & provider na mwanamke ni nest defender......sasa kama kuna mwanaume anahongwa na mwanamke hiyo ni kinyume na nature.
Kufikiria kuwa kama mwanamke anachangia ktk kipato cha familia basi amehongwa ni tatizo, mnapooana it means you become one, we are both working sasa kwanini tusichangie wote ktk maendeleo ya familia? After all ni familia yetu.
 
Back
Top Bottom