Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,476
- 39,995
Hili ni swali ambalo linahitaji kujibiwa kwa usahihi, kwa haraka na kwa umakini. Ni kitu gani ambacho Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) linahitaji kufanyiwa na Rais Magufuli ili liweze kutengeneza hadhi inayostahili shirika la kitaifa? Huku ndiko ninakokuita kubebeka. Hadi hivi sasa Magufuli amelipa pumzi ya uhai na kuliokoa kama mtu aliyeopolewa majini baada ya kuzama na watu wakajitahi kumpa CPR na hatimaye kuona anakohoa maji na kuanza kupumua tena. Magufuli alifanya hivyo lakini pia akaenda mbali zaidi; akalinyanyua na kulipa zana zote zinazohitajika ili liweze kuanza kujiendesha kama shirika la kisasa.
Bahati mbaya, bado kuna malalamiko na manung’uniko yanayohusiana na huduma (service). Kwa kampuni ya ndege huduma ni jambo kubwa na muhimu zaidi. Huduma ya ndege inapimwa kwa ufanisi (efficiency) na usalama wake (safety). Shirika la ndege ambalo halina ufanisi au usalama watu wataliogopa, kulichukia na kulibeza. Na hatimaye linaweza kufa – na kwa kweli linastahili kufa. Mashirika yote ya ndege ambayo yameweza kufanikiwa baada ya muda mrefu yameweza kufanya hivyo kwa kuhakikisha mambo hayo mawili yako ya kiwango cha juu kabisa.
Sasa hivi hatujapata tatizo kubwa lenye kutishia usalama wa ndege zetu. Suala kubwa la sasa hivi ni la huduma. Hapa ndio hoja ilipo na Bw. Kamwele anahitaji kutoa jibu la usahihi, la haraka na makini: wanataka Magufuli alibebe shiriki hili vipi; kwa mbeleko ya sufu?