Swali la Ugomvi: Injinia Kamwelwe mnataka Rais Magufuli awabebeje ATCL?

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined
Mar 10, 2006
Messages
32,874
Points
2,000

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined Mar 10, 2006
32,874 2,000
Hili ni swali ambalo linahitaji kujibiwa kwa usahihi, kwa haraka na kwa umakini. Ni kitu gani ambacho Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) linahitaji kufanyiwa na Rais Magufuli ili liweze kutengeneza hadhi inayostahili shirika la kitaifa? Huku ndiko ninakokuita kubebeka. Hadi hivi sasa Magufuli amelipa pumzi ya uhai na kuliokoa kama mtu aliyeopolewa majini baada ya kuzama na watu wakajitahi kumpa CPR na hatimaye kuona anakohoa maji na kuanza kupumua tena. Magufuli alifanya hivyo lakini pia akaenda mbali zaidi; akalinyanyua na kulipa zana zote zinazohitajika ili liweze kuanza kujiendesha kama shirika la kisasa.

Bahati mbaya, bado kuna malalamiko na manung’uniko yanayohusiana na huduma (service). Kwa kampuni ya ndege huduma ni jambo kubwa na muhimu zaidi. Huduma ya ndege inapimwa kwa ufanisi (efficiency) na usalama wake (safety). Shirika la ndege ambalo halina ufanisi au usalama watu wataliogopa, kulichukia na kulibeza. Na hatimaye linaweza kufa – na kwa kweli linastahili kufa. Mashirika yote ya ndege ambayo yameweza kufanikiwa baada ya muda mrefu yameweza kufanya hivyo kwa kuhakikisha mambo hayo mawili yako ya kiwango cha juu kabisa.

Sasa hivi hatujapata tatizo kubwa lenye kutishia usalama wa ndege zetu. Suala kubwa la sasa hivi ni la huduma. Hapa ndio hoja ilipo na Bw. Kamwele anahitaji kutoa jibu la usahihi, la haraka na makini: wanataka Magufuli alibebe shiriki hili vipi; kwa mbeleko ya sufu?
 

Ngisibara

JF-Expert Member
Joined
Jan 2, 2009
Messages
2,715
Points
2,000

Ngisibara

JF-Expert Member
Joined Jan 2, 2009
2,715 2,000
Yeye si ndio kila kitu , wanafata maelekezo yake. Hivi ile route ya Mpanda aliyoamuru ianze imeshaanza?

Jack of all trade, master of everything.
Naomba kwa pamoja tumshangae huyu Mkjj wetu na tumuulize kwanza kuwa ni lini Mr Kamwele akawa supervisor wa hii ATCL?
 

tindo

JF-Expert Member
Joined
Sep 28, 2011
Messages
26,539
Points
2,000

tindo

JF-Expert Member
Joined Sep 28, 2011
26,539 2,000
Kwa taarifa yako tatizo ya hilo shirika la ndege ni Magufuli mwenyewe, ukishaona mtu anaua ushindani kwa kutumia madaraka yake, basi ujue huko anakokupendelea hakuweza kuwa na ufanisi zaidi ya Viroja. Iwapo shirika lingekuwa linajiendesha kwa ushindani, lazima lingepaswa kupambana kiushindani hivyo lingetoa huduma bora.
 

tindo

JF-Expert Member
Joined
Sep 28, 2011
Messages
26,539
Points
2,000

tindo

JF-Expert Member
Joined Sep 28, 2011
26,539 2,000
Kuiua fastjet ilikuwa ni kuiua Anytime cancelation airline indirect.Mshindani wa kibiashara anauwawa kwa wewe kuboresha huduma yako ili kumzidi yeye na si kumfunga jiwe kiunoni na kumtumbukiza bahari
Huu mchezo pia umeingizwa kwenye kuibeba ccm ili ionekane inakubalika, matokeo yake ndio tunaona ccm isiyoweza kujenga hoja wala kushindana kisiasa zaidi ya kutegemea kupita bila kupingwa!
 

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined
Mar 10, 2006
Messages
32,874
Points
2,000

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined Mar 10, 2006
32,874 2,000
Badilisheni Ile nembo ya TWIGA Kwenye hizo ndege ili MAMBO yaende sawa vinginevyo mtawatafuta WACHAWI bila kujua maana ya TWIGA....... sikuzote huyo mnyama anawakilisha ugoigoi,uzembe na ulofa
Duh.. unataka waweke kama simba au chui? au ndege kama mwewe?
 

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined
Mar 10, 2006
Messages
32,874
Points
2,000

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined Mar 10, 2006
32,874 2,000
Kuiua fastjet ilikuwa ni kuiua Anytime cancelation airline indirect.Mshindani wa kibiashara anauwawa kwa wewe kuboresha huduma yako ili kumzidi yeye na si kumfunga jiwe kiunoni na kumtumbukiza bahari
Sasa si unajua mtoto wako mwenyewe unampa kaupendeleo; lakini akiingia kwenye maisha hakuna kubebwa tena...
 

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined
Mar 10, 2006
Messages
32,874
Points
2,000

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined Mar 10, 2006
32,874 2,000
Yeye si ndio kila kitu , wanafata maelekezo yake. Hivi ile route ya Mpanda aliyoamuru ianze imeshaanza?

Jack of all trade, master of everything.
Kwa vile ameweka hela nyingi sana humo labda ni muhimu kwa yeye kufuatilia hadi departure?
 

Chakaza

JF-Expert Member
Joined
Mar 10, 2007
Messages
33,748
Points
2,000

Chakaza

JF-Expert Member
Joined Mar 10, 2007
33,748 2,000
Hivi kweli namna hii mnataka shirika liendelee? Mtu anatoka likizo kwake kurudi kazini anaagiza Airbus ya biashara kwenda kumchukua kurudi kazini? Ana ndege yake, zipo ndege kibao za serikali lakini hapo nikuonyesha tuu ufahari nyumbani kwao.
Mwanakijiji usijifanye hujui tatizo la ATCL, na kutaka kutupia lawama wengine.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Bujibuji

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2009
Messages
47,289
Points
2,000

Bujibuji

JF-Expert Member
Joined Feb 4, 2009
47,289 2,000
Badilisheni Ile nembo ya TWIGA Kwenye hizo ndege ili MAMBO yaende sawa vinginevyo mtawatafuta WACHAWI bila kujua maana ya TWIGA....... sikuzote huyo mnyama anawakilisha ugoigoi,uzembe na ulofa
Na wakiondoa gu twiga gwa basha Mataka aliyemdushulua marinda Hadi Defao Hadi akalazwa, wasiweke mwenge, maana tutalala kwa huzuni as per Isaya 50: 11
 

Sijijui

JF-Expert Member
Joined
Jan 14, 2018
Messages
3,771
Points
2,000

Sijijui

JF-Expert Member
Joined Jan 14, 2018
3,771 2,000
Sasa si unajua mtoto wako mwenyewe unampa kaupendeleo; lakini akiingia kwenye maisha hakuna kubebwa tena...
Sasa ndo wameshajinyonga wenyewe na huyu incopentent asiyeweza kushindana anyhow akiondoka then wakakubali mshindani wa hadhi ya fastjet au 540 aingie kwenye soko la Tanzania ndo mazishi ya Atc yatakuwa yamefika rasmi
 

Forum statistics

Threads 1,390,495
Members 528,186
Posts 34,052,520
Top