Swali la Ugomvi: Injinia Kamwelwe mnataka Rais Magufuli awabebeje ATCL?

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,474
39,987


Hili ni swali ambalo linahitaji kujibiwa kwa usahihi, kwa haraka na kwa umakini. Ni kitu gani ambacho Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) linahitaji kufanyiwa na Rais Magufuli ili liweze kutengeneza hadhi inayostahili shirika la kitaifa? Huku ndiko ninakokuita kubebeka. Hadi hivi sasa Magufuli amelipa pumzi ya uhai na kuliokoa kama mtu aliyeopolewa majini baada ya kuzama na watu wakajitahi kumpa CPR na hatimaye kuona anakohoa maji na kuanza kupumua tena. Magufuli alifanya hivyo lakini pia akaenda mbali zaidi; akalinyanyua na kulipa zana zote zinazohitajika ili liweze kuanza kujiendesha kama shirika la kisasa.

Bahati mbaya, bado kuna malalamiko na manung’uniko yanayohusiana na huduma (service). Kwa kampuni ya ndege huduma ni jambo kubwa na muhimu zaidi. Huduma ya ndege inapimwa kwa ufanisi (efficiency) na usalama wake (safety). Shirika la ndege ambalo halina ufanisi au usalama watu wataliogopa, kulichukia na kulibeza. Na hatimaye linaweza kufa – na kwa kweli linastahili kufa. Mashirika yote ya ndege ambayo yameweza kufanikiwa baada ya muda mrefu yameweza kufanya hivyo kwa kuhakikisha mambo hayo mawili yako ya kiwango cha juu kabisa.

Sasa hivi hatujapata tatizo kubwa lenye kutishia usalama wa ndege zetu. Suala kubwa la sasa hivi ni la huduma. Hapa ndio hoja ilipo na Bw. Kamwele anahitaji kutoa jibu la usahihi, la haraka na makini: wanataka Magufuli alibebe shiriki hili vipi; kwa mbeleko ya sufu?
 
Kwa taarifa yako tatizo ya hilo shirika la ndege ni Magufuli mwenyewe, ukishaona mtu anaua ushindani kwa kutumia madaraka yake, basi ujue huko anakokupendelea hakuweza kuwa na ufanisi zaidi ya Viroja. Iwapo shirika lingekuwa linajiendesha kwa ushindani, lazima lingepaswa kupambana kiushindani hivyo lingetoa huduma bora.
 
Kuiua fastjet ilikuwa ni kuiua Anytime cancelation airline indirect.Mshindani wa kibiashara anauwawa kwa wewe kuboresha huduma yako ili kumzidi yeye na si kumfunga jiwe kiunoni na kumtumbukiza bahari

Huu mchezo pia umeingizwa kwenye kuibeba ccm ili ionekane inakubalika, matokeo yake ndio tunaona ccm isiyoweza kujenga hoja wala kushindana kisiasa zaidi ya kutegemea kupita bila kupingwa!
 
Badilisheni Ile nembo ya TWIGA Kwenye hizo ndege ili MAMBO yaende sawa vinginevyo mtawatafuta WACHAWI bila kujua maana ya TWIGA....... sikuzote huyo mnyama anawakilisha ugoigoi,uzembe na ulofa
Na wakiondoa gu twiga gwa basha Mataka aliyemdushulua marinda Hadi Defao Hadi akalazwa, wasiweke mwenge, maana tutalala kwa huzuni as per Isaya 50: 11
 
Na wakiondoa gu twiga gwa basha Mataka aliyemdushulua marinda Hadi Defao Hadi akalazwa, wasiweke mwenge, maana tutalala kwa huzuni as per Isaya 50: 11
Tena wazo zuri labda mwenge maana unaangaza mbali na ni mojawapo ya alama za taifa...
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom