Swali la Shyrose kwa Sophia Simba lazua kasheshe katika Mkutano Mkuu UWT

Haya ni matokeo ya makundi ndani ya chama cha magamba ,swali lililoulizwa ni la msingi lakini kwasababu ya kambi ,rushwa ya fedha,ngono nk ndio tunashuhudia haya.kwani ss kafanya nn cha maana kwa umoja huo wa wanawake wa ccm?
 
Ushindi wa Simba ni ushindi wa Lowassa. Hongera Hon. Lowassa, rais mtarajiwa wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 2015.
 
Majibu ya sophia Simba yalikuwa mepesi na ya kukera, hawezi kumwambia muuliza Swali kuwa eti ni mchanga kisiasa na hata huo ubunge wa Afrika Mashariki wamempatia tu.

Je yeye Sophia alipoingia kwenye siasa alikuwa mkomavu? hajui criticism helps to makes one perfect? anataka kuifanya UWT ni himaya yake?

Ni dharau, hata kama Shyrose ana mapungufu fulani lakini ilibidi Sophia ajibu kwa busara. Kwa mtazamo wangu majibu yake yanabeba taswira ya chama chake.
 
Swali tuliloletewa ni.

"Wewe ukiwa mwenyekiti wa UWT kwa kipindi cha miaka minne iliyopita hatujawahi kukuona ukisimama jukwaani kutetea Chama."

Swali kama hili ....
Mkubwa, hakuna swali hapo!

Shyrose amemwambia Sofia "Wewe ukiwa mwenyekiti wa UWT kwa kipindi cha miaka minne iliyopita hatujawahi kukuona ukisimama jukwaani kutetea Chama."

Hicho ndicho tulichonacho jukwaani hapa.

 
.... Wote wanagombea fito wakati wanataka kujenga nyumba moja ......... najua watasameheana, na kauli yao ya kuvunja makundi itafuatia
 
kumwuliza swali gumu Sofia Simba kama ifuatavyo:
"Wewe ukiwa mwenyekiti wa UWT kwa kipindi cha miaka minne iliyopita hatujawahi kukuona ukisimama jukwaani kutetea Chama."
Not that I care for any of these ...., Lakini Hilo ni Swali au Statement

If you ask me naona wote they are just waste of space
 
mimi nazan swali lilivyo ulizwa lilikuwa sahihi ila ukiraza wa huyo mnyama pori(simba) ndio unafanya swali liwe gumu,hata angeulizwa tofauti majibu bado yangekuwa na utata sababu hana uwezo wa kujibu hoja za msing zaid ya kucorrupt na wapiga kura wake ambao ndo anasema wako chini aliko kuimalisha
 

"Wewe ukiwa mwenyekiti wa UWT kwa kipindi cha miaka minne iliyopita hatujawahi kukuona ukisimama jukwaani kutetea Chama."


Jibu la Sofia Simba kwa swali la Shyrose lilikuwa jepesi kama ifuatavyo:
"Inaonekana aliyeuliza swali hajakomaa katika siasa za nchi, ndio maana ameambulia kuzomewa na wajumbe wa mkutano huu. Habwatuki bungeni au majukwaani kwa vile yeye ni serikali, na hata mbunge wa CCM hapaswi kukikosoa chama chake. Mimi si mithili ya upinzania kukaa na kukiosoa chama napaswa kukitetea. Anayesema Sofia Simba hajafanya kitu anajidanganya kwani wapiga kura wako kwenye matawi, kata, wilaya na mikoa, hao ndio wapiga kura wa chama na mimi kama mwenyekiti wa UWT nilijiimarisha katika ngazi za chini."

Shyrose anaweza asiwe mkamilifu lakini ameuliza swali la msingi sana na ni ajabu sana kama wanawake wa CCM wameridhika na majibu ya Sophia Simba! Infact I would go as far as saying ni fedheha kwa wanawake wa Tanzania kama wanaongozwa na fikra za namna hiyo.

TAMWA wamesaidia/wanasaidia wanawake kuliko Wizara ya wanawake inayoongozwa na Sophia Simba. Na chini ya Sophia Simba wanawake wa CCM wamekuwa na sifa mbaya sana mbele ya jamii. Sijui Prof Tibaijuka anafanya huko?
 
Shy bado hajajua kwamba ccm ina wenyewe ambao kwao uwajibikaji si kigezo cha kutofaa kuongoza?
 
Hivi ubaya wa shy-rose uko wapi hapo? Huyu simba ndo hajakomaa pamoja na uzee wake wote.Ukiulizwa swali la mantiki kama hili unajibu kwa facts na sio taarabu.
 
Kama kuna mtu amebebwa na mbeleko kuubwa na hajui kujishikilia ni SS,baada ya JK kubebwa na KK na wakati huo akiwa SS kama kimada wake aliezaa nae,kuanzia hapo JK analipa fadhila sana na hawezi kumuacha hata iweje!maana ni mzee wa fadhila na visasi!(+,-) zote anazo,mzee wa upepo...

...and that is the bottom line, asante mkuu kwa kuliona hilo.
 
Anajua kwa muda aliokaa na mambo aliyofanya hayalingani ndio maana wapambe wake wakamtetea fasata, wala sishangai kwani hata Boss wake si alikuwa anakwepa midahalo kipindi cha kampeni? hawataki maswali magumu, hawana muda wa kufikiri, wamezoea bla blaa, kila kitu kwao ni upepo wanaamini utapita tu......hii ndio CCM ya leo, pole Shyrose maswali magumu nenda kaulize kwenye Bunge la Afrika Mashariki sio CCM hawakawii kukuambia sio raia.
 
Bahari imechafuka tena sana, Chimbo kinayumba sana, nahodha namtafuta simuoni. Ndugu zangu nchi inayumba kila kona, kibaya zaidi ni pale unapoona viongozi wetu hawachaguliwi kwa kuwa sababu ya uwezo wao bali mbinu zingine (200,000).

Hii ni hatari kwa sababu hakuna anayesema hasa miongoni mwao, ndio maana hasira zinapanda wanapoulizwa maswali ya msingi ambayo kwao ni upuuzi
 
Back
Top Bottom