Swali la mama

Swali la mama

Nyani Ngabu

Platinum Member
Joined
May 15, 2006
Posts
98,492
Reaction score
145,850
Marhaban bial'asdiqa'.

Natumai nyote mu buheri wa afya Jumapili ya leo.

Hivi jamani, eti kwa mama mzazi wa kijana kumwuliza mpenzi wa kike wa huyo kijana wake kuhusu uwezo wake [kijana] wa kitandani ni swali linalofaa kweli?

Mimi naona ni swali ambalo halifai kabisa na linaloingilia faragha ya kijana.

Kwa nini mama mtu atake kujua uwezo wa kugegeda[na] wa kijana wake?

Yeye hayo yanamhusu nini hasa?

Sasa labda mimi sijui...pengine ni kawaida kwa wamama kudadisi mambo kama hayo kuhusu watoto wao wa kiume, hivyo ningependa kusikia mitazamo ya wengine ikoje.

Manake yawezekana mimi nikawa naona haifai kabisa ilhali ni jambo la kawaida hususan kwa wamama.

Nakaribisha maoni yenu.
 
Mama lazima hajue na kuji proud kuwa yuko na kijana mkamilifu na ndio maana wewe hapo kakuona uchi ukiwa na umri 1--13

VIPI HAUPELEKI MAMBO NINI mbona no confidence.



swissme
 
Mkuu haifai kabisa kwanza si adabu nzuri kuanza kuuliza maswali ya kiundani Na ya faragha kama hayo

Na anayauliza anataka nini? Yanamhusu nini?

Si sahihi Na sjui unaanzaje kuyauliza maswali kama hayo

Kuna viumbe mishipa ya aibu imeachia kabisa
 
Ili baadae binti akilalamika jamaa hamfikishi mama ajue jinsi ya kutatua tatizo
 
Mkuu haifai kabisa kwanza si adabu nzuri kuanza kuuliza maswali ya kiundani Na ya faragha kama hayo

Na anayauliza anataka nini? Yanamhusu nini?

Si sahihi Na sjui unaanzaje kuyauliza maswali kama hayo

Kuna viumbe mishipa ya aibu imeachia kabisa

Mtazamo wako ni kama wangu.

I'm like..why the hell do you wanna know?

Good grief!
 
Huenda ana mbinu za kumuwezesha kijana wake aperform jambo vizuri kama ataambiwa yupo legevu ili asichapiwe au kuleta aibu kwa mke wake.

Hawezi kumuuliza kijana moja kwa moja badala yake atamdadisi kupitia mkewe na endapo kutakua na Upungufu wowote atampa mbinu na hata dawa ili aweze kukupatia na uwezo uongezeke.

Wakina mama wengi hasa wa kule kwetu Vijijini wana mbinu nyingi sana na wanajua haya mambo vema na hujionea fahari mtoto wake akisifiwa kuwa yupo vema kunako......
 
Kaanzaje kumulza uyo bnt(mkwewe) duuh mama hana soni uyo
Ujana wake ndo wale wanawauliza mashoga zao uwezo wa mmewe (Shem) Kitandani ..awe na hekima hayamuhusu
 
Sasa huyo mama atalitatuaje hilo tatizo [kama hata ni tatizo]?
Mama ndo anayejua yaliyompata kijana wake utoton,hivyo anaweza tatua kwa kumueleza au kuwatafutia tiba. Ni kama siri ya mtungi aijuae kata
 
Mtazamo wako ni kama wangu.

I'm like..why the hell do you wanna know?

Good grief!

Mkuu juzi nilivyokutania jamaa walinilima ban, yaani jamaa hata hawaulizi.

Bann 1.jpg
 
Inawezekana kwa wamama ambao ni mashangingi wa mjini ila hawa wa kwetu huku ni mwiko.
 
Mama ndo anayejua yaliyompata kijana wake utoton,hivyo anaweza tatua kwa kumueleza au kuwatafutia tiba. Ni kama siri ya mtungi aijuae kata

Hapana kwa kweli.

Huo ni uingiliaji wa faragha [invasion of privacy].
 
Uzi mzuri ila iyo "eti" ungeitoa maana ni neno linalotumika kushitaki mtu/watu KINAFIKI

Mfano; shetan anatumia kutushitakia kwa Mungu ili tu apewe kibal cha kumjaribu mtu (Ayubu)
 
Back
Top Bottom