Swali kwenu ma firstborn kwenye familia

Swali kwenu ma firstborn kwenye familia

mcTobby

JF-Expert Member
Joined
Feb 16, 2018
Posts
7,712
Reaction score
22,149
Ndugu firstborn hapo kwa ur baba and ur mama... Nini kilikufanya ukaamini 💯% wewe ndio ulizaliwa wa kwanza kutoka kwenye viuno vya babayo na tumbo la mama yako?..je , haukuwahi kujiuliza kwamba Kuna bro wako mkubwa au sister yako mkubwa alikutangulia sema mimba yake ilikuwa aborted (unplanned pregnancy na mambo ya ujana) ? au kutokana na miscarriage (medical reasons).. ?
FB_IMG_1792204733684.jpg

Anyway .. Kuna darkside chapters kwenye hizi familia zetu za kiafrika..pages zake zilichanwa ili zisisomeke .
 
Kuna jamaa mmoja huwa anajisifu kuwa yeye kwao ni kifunguamimba, na hakuna wa kumwambia kitu. Laiti angejua njemba ambazo mama yake alizitoa tukiwa naye chuo angefunga bakuli lake.

Dinia ina mambo!
 
Ndugu firstborn hapo kwa ur baba and ur mama... Nini kilikufanya ukaamini 💯% wewe ndio ulizaliwa wa kwanza kutoka kwenye viuno vya babayo na tumbo la mama yako?..je , haukuwahi kujiuliza kwamba Kuna bro wako mkubwa au sister yako mkubwa alikutangulia sema mimba yake ilikuwa aborted (unplanned pregnancy na mambo ya ujana) ? au kutokana na miscarriage (medical reasons).. ?View attachment 3696995
Anyway .. Kuna darkside chapters kwenye hizi familia zetu za kiafrika..pages zake zilichanwa ili zisisomeke .
This is purely provocation! Subiri uone visukari na utetezi uchwara.
 
Kabisa nikae nifikirie huu ujinga kweli? Unanihusu nini sasa wakati nina mambo ya msingi ya kuyawaza🙆‍♂️
 
Kama umeambiwa wewe ni firstborn, huna haja ya kufukunyua, amini wewe ni firstborn. Mambo ya ujana wa wazazi wako hayakuhusu kabisa.
 
Ndugu firstborn hapo kwa ur baba and ur mama... Nini kilikufanya ukaamini 💯% wewe ndio ulizaliwa wa kwanza kutoka kwenye viuno vya babayo na tumbo la mama yako?..je , haukuwahi kujiuliza kwamba Kuna bro wako mkubwa au sister yako mkubwa alikutangulia sema mimba yake ilikuwa aborted (unplanned pregnancy na mambo ya ujana) ? au kutokana na miscarriage (medical reasons).. ?View attachment 3696995
Anyway .. Kuna darkside chapters kwenye hizi familia zetu za kiafrika..pages zake zilichanwa ili zisisomeke .
Mimi ni first born na nilishawahi kufikiria hivyo, na nikaishia kuhitimisha kuwa heshima ya mtu haitokani na yeye kuwa wa kwanza kuzaliwa, inatokana na matendo yake.

Kwa hivyo, mtoto yeyote yule atakayekuwa na mchango mkubwa, atakayesaidia vizuri, atakayejali familia kwa namna yenye afya, anajionesha kuwa kiongozi katika familia.

Na inawezekana kabisa first born akawa na kipaji hiki kutokana na ukubwa wake na saikolojia ya u first born. Mara nyingi inakuwa hivi.

Na inawezekana first born akalewa ukubwa, akawa na u Mwinyi, akawa mjinga tu, wadogo zake wakafanya mambo ya maana zaidi.

Kwa hiyo, kuwa first born si muhimu sana kama kuwa ndugu mwema wa kupigiwa mfano.

Fikra hizi zimenifanya niweze kuwasikiliza sana wadogo zangu bila ya kutumia sana karata ya u first born kujiweka mimi kwanza.

Cha ajabu sasa, jambo hili, la kuthamini watu kwa hoja na mchango si kwa ukubwa wao tu, la kujitoa kwa ajili ya wenzangu hata pale ambapo hawana cha kunirudishia, la kusikiliza sana wengine, ndilo limeniongezea heshima maradufu sio tu kwa wadogo zangu tu, bali hata kwa extended family. Bila hata ya kufanya hivyo kwa kupanga.
 
Wewe ni firstborn.. ulikuwa wa kwanza kuzaliwa..

Hayo ya mimba zilitolewa, Kwani zilizaliwa?
Kama hazikufika kuzaliwa unahesabu vipi?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom