Swali Kwa Wataalam wa ndege (birds)

kissa anyigulile

JF-Expert Member
Apr 21, 2017
1,550
1,733
Naomba kujuzwa ni kitu gani hasa kinachomuongoza ndege kuchagua mwenzi wake anayemfaa? Maana huwa napendezwa sana ninapowaona ndege dume na jike wakishirikiana kwa utaratibu na wororo mzuri sana!
 
Naomba kujuzwa ni kitu gani hasa kinachomuongoza ndege kuchagua mwenzi wake anayemfaa? Maana huwa napendezwa sana ninapowaona ndege dume na jike wakishirikiana kwa utaratibu na wororo mzuri sana!

Ndege sehemu kubwa hutumia mbwembwe tu kama kuimba, kunyanyua nyanyua manyoya, kucheza cheza n.k

Na kawaida ndege dume ndiye anayejishembendua kwa ndege jike ili apewe mzigo...
 
Ndege sehemu kubwa hutumia mbwembwe tu kama kuimba, kunyanyua nyanyua manyoya, kucheza cheza n.k

Na kawaida ndege dume ndiye anayejishembendua kwa ndege jike ili apewe mzigo...
Siyo hapo tu. Wanajenga
kiota pamoja, wanakula pamoja, wanapumzika pamoja, wanatoana uchafu pamoja, wanaatamia mayai pamoja, nk
 
NIKO NA BUNDI HAPA NAMALIZIA KUMHOJI MASWALI JUU YA UPENDO NA MAPENZI

Subirini mrejesho
 
Acha uongo. Sijawahi kuona bundi ana mwenzi. Ndege hao mara zote huwa kivyaovyao tu. Hata paka hathubutu kuwasogelea, sembuse wewe?
 
Ndege wengi maisha yao yako kidogo tofauti na unavyoona au kufikiria!

Kila ndege ana mtindo wake wa kunasa soulmate wake!na huwa hawabahatishi kwa sababu aina nyingi za ndege huwa hawachepuki hata mwenza wake akiaga dunia(mate for life).

Kama WEAVER BIRD wao madume ndio hutengeneza kiota kikubwa na kizuri chenye kuvutia!!jike akifika mtini anachagua kiota kipi kizuri anaingia anapigwa mzigo.hiyo inaitwa SOGEA TUISHI.demu ndio hatoki tena hapo geto yeye ni kutotoa tuu.

KORI BUSTARD ni tofauti kidogo yeye hatengenezi kiota sababu ndie ndege mkubwa kuliko wote anaeruka angani.
Yeye anatongoza kiubabe akishapiga mzigo anasepa spidi laki hutamuona tena!!watoto na mayai utalea kisingomaza....

Kunguru ndio babalao akishakuwa na demu wake basi ni huyo huyo hakuna kuchepuka afe jike afe dume hakuna kutoa kwa yoyote hadi nae afe!!real widow...!
 
Back
Top Bottom