Kwanini baadhi ya watu huitwa mafisi?

Apr 25, 2020
29
56
MFAHAMU FISI KIUNDANI ZAIDI

Kuna aina nyingi za fisi ila post hii itaeleza kwa ujumla

• Fisi huishi kifamilia na kwa taarifa fisi hujenga kabisa sehemu wanazokaa ,huzaa watoto kuanzia wawili mpaka wanne bahati mbaya waliyonayo wanyama hawa hupata tabu sana ya uzazi pindi jike linapozaa, watoto wao wengi hufa wakati huo , hivyo kama jike atazaa wakati dume halipo ana nafasi kubwa ya kuzaa watoto wafu, kwani fisi dume hutoa msaada kwa jike wakati wa kuzaa hasa ulinzi.

• Huishi popote sehemu kame, vichakani na hata sehemu ambazo zina majani yenye ukijani sana, hivyo ni mnyama ambaye popote kwake ni kambi.

• Pamoja na kwamba ni mnyama ambaye jina lake linakuzwa sana kwamba anatabia ya kula mizoga, lakini fisi ni mnyama anayewinda na hula nyama fresh, akikosa mawindo yake hufanya uporaji kwa wanyama kama simba na inapokosekana hata nafasi hiyo, basi akikutana na mfupa, mzoga hutafuna.

• Wakati wanyama wengine wengi wakiwa wanaongozwa na madume, ukifika katika koo za fisi majike ndio viongozi, lakini mbali na uongozi pia fisi jike ana nguvu za mwili kuliko dume

• Fisi ni mnyama anayeweza kukimbia umbali mrefu kwa taratibu, we tangulia na spidi 120 yeye atakuja na 30 na atakukuta tuu njiani ukiwa umeanguka au umeishiwa nguvu au misuli kukaza na hapo ndio atakukamata kwa urahisi.

• Fisi huzaliwa akiwa anaona wakati huohuo.

• Fisi jike huwa na maamuzi yote kuanzia mahabani mpaka mgawanyo wa kazi.Fisi dume tunaweza kusema ni mnyama bwege anatawaliwa na jike lake.

• Fisi hunguruma, hucheka pia hutoa milio mbali mbali inategemea na alipo, na hiyo huwa ni lugha wanayotumia kuwasiliana akifanya hivyo wenzie wakisikia wanajua tuu kuna jambo gani limemsibu mwenzao kabisa.

• Watoto wake wanapofikisha umri wa miaka miwili mama yao huwatimua, wakajitegemee.

• Fisi anapokutana na watoto wa simba huwaua pasina huruma.

• Fisi dume halitakagi kusikia habari za watoto, huwa linaamini ni Mali ya jike, hivyo hanaga nao msaada kabisa

• Fisi jike huwa na mwili mkubwa kuliko dume.

• Adui yao mkubwa ni mbwa mwitu, kwakuwa huwapora nyama ambazo wao wametafuta kwa tabu sana, pengine kwa kuhatarisha maisha yao

• Fisi wanaogopa sana dume la simba, wanaweza kuwasumbua majike wa simba watatu lakini likija dume huwa linahakikisha mmoja kati yao anachechemea, hivyo wanapomuona simba dume hupiga kelele za kupeana habari kuna hatari.

• Fisi ni mnyama mnyonge sana na ni mnyama ambaye karibia wanyama wote wawindaji ni wababe kwake, kinachowasaidia ni hali ile ya kutembea makundi makundi yaani kifamilia, ndio huwafanya na wao waonekane kidogo wanajiweza.

• Fisi jike huweza kupiga dume mpaka likahama nyumba, na hutumia sana ujanja huu endapo jike linataka kuishi na mchepuko wake ndani. Fisi huamini pia katika umoja

• Fisi jike linapofika bwawani au kisimani alafu fisi dume linaoga, Basi dume hutoka majini na kulipisha Jike lioge kwanza.

• Mtoto wa fisi huishi maisha raha mstarehe kwa minofu mingi ya kutafutiwa.

Usisahau kulike page
🙄

#Abnockfacts

175918062_287561392958240_3241556145056519036_n.jpg
 
Kuna Nyimbo ya Vijana ( 'sijui nani kaimba) naipenda sana sehemu ya Mistari

'Kama umemchoka tuachie sisi ndo Mafisi ' tutamla had mifupa
 
Back
Top Bottom