Mimi nafikiri mara nyingi mawazo na hisia zetu kwenye mahusiano, yanatawaliwa zaidi na experience ya mtu binafsi (kwamba amekutwa na mkasa fulani) au hata experience ya jamii inayomzunguka. Mfano rahisi ni mtu aliyelelewa kwenye familia ambayo wazazi walitengana toka yeye mhusika akiwa mdogo, anaweza akawa na mawazo ya kutokuoa au kuolewa kwa hofu ya historia kujirudia.
Mimi naunga mkono hoja ya mchangiaji aliyesema bado suala la mdada kupindukia pembeni ni hulka ya mtu mwenyewe. Ninaweza kuthubutu kusema akina mama/dada wana uvumilivu wa hali ya juu (kila kaka najua mtakuwa wagumu kuamini hili) kushinda akina baba. Mara ngapi zimetokea scenario za baba kukutwa (manake wanadai wao hawafumaniwi bali wanakutwa) na outcome ikawa ni baba kusamehewa, lakini that is NOT THE CASE IF THE SCENARIO IS REVERSED! Sasa, mnachosahau akina baba ni kuwa we are all humans and we have the same feelings, kama unafikiri shubiri ni chungu we feel the same taste, kwetu haijawekwa sukari!
I am very sure kuwa huyo mpindukaji hajawa full committed kwa mwenzie, honestly, when mdada akijicommit she means it.
Kwa hiyo wala usijenge hofu ya mwenzio kukosa uaminifu wakati wewe mwenyewe hujajijengea taswira ya huo uaminifu wenyewe. Tujaribu kujenga mahusiano ambayo yanatawaliwa zaidi na mawasiliano. Mimi huwa najitia ujasiri wa hali ya juu wa kutokugusa simu ya mwenzangu, lakini my cellphone is always popote kiasi kwamba kama atakuwa na kutaka kuipekua basi anaweza akafanya hivyo, and I don't feel different coz I have nothing to hide. Sasa ona yake anavyohangaika nayo, yaani haimtoki usoni...unabaki kuchekea tumboni...
DINA,
You are partly right..but. ..waaminifu walikuwa mama zetu..hata kama dingi amekwenda kutafuta mali akakaa huko miaka mitano..alikuwa anakuta mama yupo anatunza mji na watoto. It was just splendid.
Mfano: Zamani ndoa zilikuwa zinadumu sana kwa sababu baba ndo alikuwa breadwinner. Kwa hiyo hata kama akihamishwa kituo cha kazi atafuatana na mama na watoto. Siku hizi mwanamke kapata emancipation (hiki kwangu ni kitu kizuri-lakini kinakuja na gharama zake vile vile). Leo ukitaka kuwa na mpenzi (ambaye unataka aje agraduate awe mke siku za usoni) lazima muulizane vipi career zenu inakuwaje? mfano dada ni IT expert yupo (Benk ya mafisadi BOT). Wewe ni fani nyingine..ukihamishiwa Rukwa au Ngara....you have to face it..nani amfuate mwingine (ofcourse mnaweza kudiscuss-but "consensus" is not automatic as many of us tend to think). Otherwise abaki Dar mtakuwa mnatembeleana.
Na hapo mgogoro ndo unaanza..mwanaume kapata kazi huko na wewe uko huku. And to me hili halikwepeki..mdada wa watu kasoma mpaka University..leo umwambie awe mama wa nyumbani? Its unfair by all means! The same applies kwa mwanaume...
Make no mistake wanaume wengi wa kiafrika hatujawa tayari-atleast not for now, kukaa nyumbani eti mwanamke afanye kazi....kwamba ataihudumia familia na mwanaume alee watoto! Bado tuko mbali sana kwa hilo..hata kama mwanamke angepata kazi gani sijui...(ofcourse kuna wachache wapo..ila ni negligible).
Harafu hii assumption ya "uaminifu" mi naona ni bullshit! binadamu we re inherently selfish. Kikubwa tutafute safeguard za kuweza kulinda hizi ndoa..mfano serikali kuadopt sera mahsusi kuwasaidia wafanyakazi wake (ofcourse here the danger is: the policy may be abused-but thats the price to pay). Ndo maana kuna tofauti kubwa sana ya sisi waafrika na wazungu..sisi kila kitu utasikia..ni "mapenzi ya Mungu"..au "tunamwachia Mungu". You cant hear that in the western world...watu wanakuja na concrete solutions.
Personally nina marafiki wanafanya kazi kwenye hizi international organizations...wengi ndoa zimevunjika! Imagine unakaa Darfur baba yupo Dar, au uko Peshawar huko Pakistan..mama yupo sehemu nyingine....pata picha yake..well "ni kumwachia Mungu" but its tough.
Uaminifu wa siku hizi unakosekana lakini inachangiwa na vitu vingi sana. Ndo maana as we move forward..Ndoa zinakosa ile flavour yake..as it used to be. Na dunia imekuwa survival for fittest. Watu wanaogopa kukaa bila kazi..kukaa bila security.. career comes first mengine yanafuata.
Sijui kipi kifanyike, lakini naona kabisa "real meaning" ya marriage as we used to know it..is losing its stature among the society. Money has become everything! Though we chase it....we never see enough of it. Sad, but true.