Hii njianhuwa salama sana endapo mtu anapata mtu sahihi.
Inatakiwa mwanamke ajiweke katika mazingira ambayo hata mwanaume mwenyewe aone aibu kuomba penzi kabla ya Ndoa.
Lakini kwa mwanamke ambae amejiweka mazingira ambayo mwanaume anashawishika kuomba penzi kabla ya ndoa kwa nini mwanaume asiombe kuzini na huyo mtu?
Kwa sababu kama anavaa kwa kutamanisha na kujiweka mazingira hayo basi kuombwa penzi ndio reaction ya action ya mazingira anayojiweka.
Kila kitendo lazima kiwe na athari zake.
Kitendo cha mwanamke kujiweka mazingira ya kuvutia kingono na kuwatamanisha wanaume wengine basi athari zake ni kuwa mwaanaume hatokubali kumuacha hivi hivi wakati kila siku akimtamanisha kwa mavazi adimu kama hayo.
Na mwanaume hawezi kuamini kwamba ni kweli unajitunza mwanamke wakati mazingira yakko yanaonesha kwamba haupo kwa kujitunza.
WANAWAKE WANAFANYA KOSA KUBWA kuwaamini wapenzi wao(wachumba).
Wanawake sikilizeni : mwanaume pekee unaepaswa kumuamini ni mumeo tu" kwa sababu huna uhakika kwamba huyo utakayempa penzi kama atakuoa au atakuacha.kwa hyo kama anashida kweli akusubiri.
Lakini pia wanaume nao tuna matatizo sana.hivi unamuoaje na kumuamini mwanamke ambae alikubali kukupa penzi kabla ya ndoa?
Kama aliweza kukupa penzi wewe ambae sie mumewe na hujamuoa je atashindwa kuwapa wengine penzi ambao pia sio waume zake na hawajamuoa?... Una nini cha ziada mpaka ujiamini kwamba anakupa penzi peke yako?.
Hahahahhaahha
MOTHER confessor