kuna dalili kubwa wanaume watakwepa uzi huu....
wapi Dark City wapi Mtambuzi Asprin Nyani Ngabu The Boss Baba V BAK na wengineo? ingependeza tukapata mtazamo wenu...
Duh, hako katabia nilikaanza bila kujua....
Siku moja baada ya kufanyiana mizaha na Mama Nginaa. Mie na mama Ngina huwa tunafanyiana mizaha na mara nyingi niwapo nyumbani ni kutaniana kwa kwenda mbele bila kukwazana lakini. Basi akatulia na kuniuliza kwa nini nikiwa ofisini akinipigia kuna wakati naongea kwa ukali?
Lile swali lilipenywa masikioni mwangu kama msumari wa moto, sikujua kama huwa naongea kwa ukali, lakini baada ya kuvuta kumbukumbu nikakumbuka kwamba ni kweli ninapokuwa nimetingwa huwa naongea kwa ukali..
Wanawake ni viumbe wa kutaka kusikilizwa, na si wanaume wote wanaolijua hilo, na hata kama wapo wanaojua, lakini kuna kujisahau na hiyo inatokana na ile dhana kwamba wanawake wametoka sayari ya Venus na wanaume wametoka sayari ya Mars, ni vitu viwili tofauti, kwa hiyo kinachotakiwa ni kuishi kwenye urazini (awareness) kujua kila kinachoingia na kutoka ndani yako, la sivyo utajikuta unagombana na mwenzi wako kila mara.
Hebu fikiria uko kazini, halafu uko bize au mkoloni wako kakubana mbaya, mara unapokea simu kutoka kwa wife, unaipokea kwa shauku kujua kuna nini tena, lakini anaishia kuuliza iwapo utapenda akipika chakula cha aina fulani au atakwambia kuwa leo mtoto ameanza kutambaa, au anaweza kukuomba upitie supermarket kununua kitu fulani kwa kuwa yeye amesahau... C' mon, yaani hiyo ndo sababu ya kupiga simu kweli? kwa nini asini text... (mwanaume anaweza kujiuliza). Na hapo ndipo lugha zinakuwa gongana
Kuna haja ya kujirekebisha, mimi nimejitahidi sana siku hizi na nikiona simu ya wife na siko kwa mood, namuomba nimpigie baadae kisha naweka alam ili inikumbushe na alam ikiita nampigia nikiwa na niko positive zaidi.
Hilo tatizo lipo.