Swali kuhusu Mahakama ya Kadhi tafadhali

Nina swali kuhusu Mahakama ya kadhi! Ina maana kwa Mwislamu atakuwa anahudumiwa na hii Mahakama tu na hii Mahakama iamuacho ndiyo mwisho?

Yaani kwa mfano Mwanamke anapenda kuachana na Mumewe na kwa sababu zake binafsi labda tu amemchoka au sijui kamfumania na wanakwenda Mahakama ya kadhi, je vipi kuhusu haki ya Mwanamke kwenye mali? Ni nani anaamua hili? Na je kama sheria ya Kiislamu haitambui kuhusu kugawana mali sasa inakuwaje kwa huyu Mwanamke? ina maana Mahakama yetu ya JMT haiwezi kuingilia hapo?

Na je Mzazi wa Kiislamu akitaka kumuoza mtoto wake kabla ya kutimiza Umri ambao sheria ya JMT imeweka yaani miaka 18, sasa nini kitatokea?

Kwa maana kwa kiislamu hakuna kitu kama umri wa kuoa au kuolewa sasa kama Mahakama ya kadhi ikiamua mtoto wa JMT aolewe ndiyo ataolewa kweli na Serikali ya JMT haiwezi kumuokoa huyu Mtoto?

Kuoa au kuolewa kwa mtu yeyote haiamui mahakama yoyote,Bali ni makubaliano ya wawili(mwanamke na mwanaume) wenye vigezo vya kuoana na kuyamudu maisha ya ndoa.

Yaani katika uislam HALAZIMISHWI MTU kuoa/kuolewa.

Mfano: Hawa kampenda Adam,Hawa ana kila 7bu ya kuolewa.lakini Adam hajampenda hawa,moyo wake haujisikii kuishi na hawa.hata akabembelezwa amkubali hawa bado Adam akakataa.HAPA HAKUNA NDOA.

Katika uislam
Ndoa ni makubaliano kati ya mwanamke na mwanaume WALIOPENDANA na wakaridhiana kuishi kama wanandoa kwa baraka za wazazi/walezi wao kwa kufuata sheria za mwenyezi mungu.

Hiyo ndio ndoa.
Mahakama haisemi wewe oa wewe olewa,
Kazi ya mahakama ni kusuluhisha migogoro mbalimbali (sio ya ndoa pekee) inayowahusu wahusuka.

Kama zilivyo mahakama zingine,MNAVYOUZIANA,mnauziana kwingine ila mkidhurumiana mnaenda mahakamani kutafuta suluhu.
Lakini mahakama haikusema,wewe uza,wewe nunua,Lakini INASULUHISHA.

Kuhusu mirathi..
Wataohukumiwa na mahakama ya kadhi ni waislamu tu! Nayo ni wale walioridhia kuhukumiwa na mahakama ya kadhi.
Na kwa kua sharia za mahakama ya kadhi haitungwi na mtu IPO TAYARI! inakuwa ni kutafsiriwa tu! Kama tu haujakosewa kutafsiriwa basi mwislam ana takiwa kukubali suluhu itakayotolewa,na kama ataona haridhiki,(WATU WANATOFAUTIA ELIMU NA UELEWA sio katika mahakama ya kadhi tu ila kwenye nyanja zote za kimaisha)
Anaweza omba abadilishiwe jaji.anaweza omba tena abadilishiwe jaji.
Na wote wakitoa jibu moja moja,atapaswa aikubali kama muislam na aliridhia kusuluhishwa na mahakama iyo.

Hawawezi wote kutofautiana kabisa kwa kuwa kitabu na sheria (ni moja) inayotumiwa na wote.

Ila katika uislam
Muislam anatakiwa kuzitii na kuziheshimu mamlaka zilizopo duniani kama tu HAZIMNYIMI UHURU WA KUABUDU!

kwa Hiyo ni matumaini yangu mahakama ya kadhi itazitambua mahakama za serikali,katika mambo yasiyohusiana na Dini,
Na ni imani yangu pia,kutokana na sharia za nchi yetu,hatolazimishwa mtu kwenda kusuluhishwa kwenye mahakama ya kadhi isipokua kwa wale tu WALIORIDHIA KUSULUHISHWA KATIKA MAHAKAMA HIYO.

aminini, waislam wa kweli wake kwa waume,wanapendezwa suluhu zao zipatikane kwa misingi ya dini ili waridhike na waridhiwe na mola wao mtukufu.
 
Nina swali kuhusu Mahakama ya kadhi! Ina maana kwa Mwislamu atakuwa anahudumiwa na hii Mahakama tu na hii Mahakama iamuacho ndiyo mwisho?

Yaani kwa mfano Mwanamke anapenda kuachana na Mumewe na kwa sababu zake binafsi labda tu amemchoka au sijui kamfumania na wanakwenda Mahakama ya kadhi, je vipi kuhusu haki ya Mwanamke kwenye mali? Ni nani anaamua hili? Na je kama sheria ya Kiislamu haitambui kuhusu kugawana mali sasa inakuwaje kwa huyu Mwanamke? ina maana Mahakama yetu ya JMT haiwezi kuingilia hapo?

Na je Mzazi wa Kiislamu akitaka kumuoza mtoto wake kabla ya kutimiza Umri ambao sheria ya JMT imeweka yaani miaka 18, sasa nini kitatokea?

Kwa maana kwa kiislamu hakuna kitu kama umri wa kuoa au kuolewa sasa kama Mahakama ya kadhi ikiamua mtoto wa JMT aolewe ndiyo ataolewa kweli na Serikali ya JMT haiwezi kumuokoa huyu Mtoto?

Swali lako sehemu ya kwanza ni kuwa:
Ndilo jambo la msingi ambalo Waislaam wameiomba serikali na ikaridhia kwa kutayarisha muswada na kuupeleka Bungeni. Waislaam kupitia Ulamaa (Academicians) wanataka maamuzi ya Kadhi yawe yenye 'authority' na undisputed hivyo yatambuliwe na Serikali. Kadhi akitoa hukumu basi taasisi zote za serikali ziutambue kuwa ni halali na watekeleze maamuzi.
Kwa taarifa yako sheria za Kiislaam (Kadhi Laws) zipo katika Mahakama za Tanzania na zinatolewa maamuzi na Mahakimu ambao hawa ujuzi nazo na wakati mwingine wazipindisha kwa kadiri wanavyoona inafaa. Huo mdo msingi wa maombi ya Mahakama ya Kadhi kuendesha na Waislaam wenyewe.
Kimsingi ili mtu aweze kuhukumiwa na Mahakama hii lazima vigezo na masharti vizingatiwe.
Kama ndoa ni ya Kiislaam na imetimiza vigezo vyote, then upande wowote kati ya mume au mke hawana sababu ya kyikwepa au kukataa. Kukataa maana yake ni kuikana Dini taki. Hiyo pia ina maana hukuwa Muislaam bali mnafiki.
Hata ukienda Mahakama ya Serikali inaweza ikaamua kesi yako kurudishwa katika Mahakama ya Kadhi, kwani ndoo yenu ilifungwa kwa taratibu za Kiislaam.
Huwezi kushiriki mashindano ya mpira wa miguu wenye sheria 17 halafu ukakataa baadhi ya sheria. Kama kukataa kupigwa kona, penalt au wachezaji wawe 12 badala ya 11 !
 
Haki ya mwanamke kwenye Mali.

Katika Uislaam ndoa si biashara, bali ni ndoa. Uhusiano wa mwanamme na mwanamke katika kujenga familia. Ni wajibu wa mwanamme kulisha na kutunza familia pamoja na kuilinda.
Mali yeyote, ni mali ya muhusika mwenye mali. Kama mwanamme amejenga nyumba kwa jasho lake, hiyo nyumba ni yake. Na mwanamke kama amerithi nyumba kutoka kwa Babake, hiyo ni yake.
Wakati wowote kama itatokea kuachana, mwanamke atabaki na xhake na mwanaume na chake.
Sharti kuu, mwanaume anatakiwa ahakikishe anamuwezesha mtalaka wake aweze kuanza/kuendesha maisha yake mara anapotoka kwake. Hii ni pamoja na kumpa vitu na kiinua mgongo (cash) kwa ajili hiyo. Ni sawa na mfanyakazi dereva aliye ajiriwa kutoa huduma ya udereva na alikuta kampuni ina gari 2. Wakati anaachishwa kazi, kampuni ina gari 10. Hivyo, hawezi kudai apewe gari moja kwakuwa amekuwa sehemu ya mchango wa mafanikio ya Kampuni.
 
Serikali ya Jamhuri kupitia sheria ya ndoa ya mwaka 1974, mwanamke anaweza kuolewa kuanzia miaka 14.
Aliyetunga shefia na kuipitisha hawezi kuizuia sheria halali anayoitambua isitekelezwe!
Mara nyingi serikali huingilia ndoa ya umri chini ya miaka 18, kwa kisingizio cha elimu.
 
Mna paparikia msivo vijua Sheria hizo zime kamilika haki zamke na mume mnapo achana au kufa zime tajwa wazi
 
Na vipi kuhusu kuchinjana,mwizi kukatana mikononi na mzinifu wa kike kupigwa mawe??? Nasikia hizo sheria zote za kuuwana zipo ndani ya mahakama ya kadhi je ni kweli???

Ingawa umeuliza kwa kebehi, tutakujibu kwa faida yako na wapita njia.
Mtindo wa hukumu za ki mahakama katika Uislaam imegawanyika katika pande mbili.
1. Hukumu za makosa ya kijamii (Umalati)
haya ni kuhusiana na ndoa, mirathi, talaka, malezi ya watoto na mambo ya kijamii.
2. Hukumu za makosa ya Kihalifu - Jinai (Jinailati)
Ni kuhusians na wizi, uzinifu, ifisadi, kuua, ujambazi, ujangili, kufuru, rushwa, uhujumu uchumi, na yanayo fanana na hayo.
Hiki kipengele cha pili ni kigumu kukitekeleza kwakuwa kuna mambo ya kimsingi ya kiuadilifu jamii inatakiwa iyatekeleze kabla kuingia huko.
Jamii inatakiwa itoe zaka (kodi) kwa haki, masikini walishwe na kupewa haki zao. Kusiwepo na uonevu.
Waislaam wa Tanzania wana nia ya kipengele cha 1. (Umalati)
 
Barbarosa una maswali?.....kuna mahali hujaelewa ?
Wako Waislaam watakusaidia, ingawa uzi wako imevamiwa na kiwavi jeshi
 
Last edited by a moderator:
Inahuzunisha kiongozi wa dini kufanya mauwaji haya.
John-Canning-prison150.jpg

Mchungaji John Nelson Canning
images

Mchungaji Canning na mkewe siku alipowafungisha ndoa Bwana Leo Gleese na Bibi Hazel Gleese katikati
canning-at-funeralcp1

Mchungaji Canning siku ya mazishi ya ajuza hao

Mnamo January 3, 1995 mchungaji mmoja aitwae John Nelson Canning alikwenda katika kituo cha Polisi cha mji mdogo wa Sebring ulioko katika jimbo la Florida nchini Marekani na kutoa taarifa juu ya mauaji ya vikongwe wawili mtu na mkewe Bwana Leo na bibi Hazel Gleese.

Mchungaji huyo aliyekuwa na umri wa miaka 59 wakati huo aliwaeleza Polisi kwamba aligundua mauaji hayo baada ya kuwa amewatembelea nyumbani kwao kama ilivyo kawaida yake ya kuwatembelea waumini wake na kukuta miili ya vikongwe hao ikiwa imelala sakafuni kwenye dimbwi la damu.Mchungaji Canning aliendelea kuwaeleza Polisi kwamba bwana na bibi Gleese ni waumini wa siku nyingi katika kanisa la Fountain of life ambalo yeye ni muanzilishi wake.

Mchungaji huyo alibainisha kwamba katika kipindi cha miaka ya karibuni alikuwa ni muangalizi wa vikongwe hao ambao hawakubahatika kupata watoto katika maisha yao ya ndoa ambapo waliamua kumuasili (Adopt) mchungaji huyo na kumfanya mtoto wao na hivyo akawa anawaita Baba na Mama.
Mara baada ya kupata taarifa hizo Polisi walikimbilia kwenye eneo la tukio na kukutana na hali ya kutisha katika eneo la tukio ambayo hawatakuja kuisahau.

Kwani waliukuta mwili wa Bibi Hazel Gleese ambae alikuwa na umri wa miaka 90 wakati huo umelala jikoni ukiwa umetapakaa damu.
Na mwili wa mumewe Leo Gleese nao pia ulikutwa ukiwa umeegemea ukuta wa chumbani. Wote walikuwa wanaonyesha kwamba walikuwa wamepigwa na kunyongwa. Katika eneo ambalo miili ya ajuza wale ililala polisi wa upelelezi walikuta pia baadhi ya nyaraka za kibenki zikiwa zimesambaa pale sakafuni huku baadhi ya nyaraka hizo zikiwa zimelowa damu, pia kulikuwa na dalili zote kwamba kulikuwa na purukushani za kupigana kati ya bibi Gleese na mtuhumiwa au watuhumiwa wa mauaji.

Siku ya mazishi ya maajuza hao umati mkubwa wa watu wa mji wa Sebring walihudhuria mazishi hayo na yaliyoongozwa na mchungaji John Nelson Canning.
Akiongoza mazishi hayo mchungaji Canning, kwa maneno yake mwenyewe alisema “Miongoni mwenu mlikuwa marafiki wa muda mrefu wa baba na mama yangu hawa, lakini ninayo mashaka kwamba hakuna mtu yeyote aliyekuwa karibu na na familia hii zaidi yangu na mke wangu.”

Huku akitokwa na machozi, mchungaji huyo aliendelea kusema “Najivunia familia ya ajuza hawa kuniomba waniasili (Adopt) niwe mtoto wao, na nilijivunia kuwaita baba na mama kama wazazi wangu.” Familia ya Gleese haikubahatika kupata watoto katika maisha yao ya ndoa ndio sababu waliamua kuwaasili Canning na mkewe Judy hapo mnamo mwaka 1994.

Hata hivyo wakati wa mazishi hayo bado Polisi wa upelelezi walianza kumtilia mashaka mchungaji huyo kwa kumhusisha na mauaji ya ajuza wale. Polisi hao wa upelelezi walianza kumtilia mashaka mchungaji Canning tangu siku ile ya kwanza alipokwenda kutoa taarifa ya kutokea kwa mauaji ya ajuza wale ambao aliwachukulia kama wazazi wake.

Akiandikisha maelezo yake Polisi namna alivyogundua mauaji ya Bi Hazel na bwana Leo Gleese, Canning aliwaeleza Polisi akiwa katika hali ya kawaida kabisa. Kwa maneno yake mwenyewe Canning alisema “kwa kweli niligundua mauaji hayo jana asubuhi.” Polisi wa upelelezi walistushwa na habari hizo, kwani kwa mujibu wa maelezo yake ilionyesha kuwa miili ya Hazel na Leo Gleese ilikuwa imelala pale sakafuni kwa masaa 24 tangu kuuwawa pamoja na kuwa mchungaji Canning alifahamu kuhusu kutokea mauaji tangu jana asubuhi.

Alipoulizwa kwamba kwa nini hakutoa taarifa mapema, mchungaji Canning alidai kwamba aliogopa kutoa taarifa kwa sababu hapakuwa na shahidi mwingine zaidi yake, hivyo aliogopa kuwa mtuhumiwa wa kwanza kuhusishwa na mauaji yale. Kwa maneno yake mwenyewe Canning alsema “Niliingia ndani na kustushwa na mauaji yale, nilichanganyikiwa na kufunga mlango kisha nikaondoka kwani niliogopa kutoa taarifa za vifo hivi kwa kuhofia kwamba nitahusishwa navyo mpaka leo ndio nikakata shauri nije nitoe taarifa.”

Mchungaji Cunning aliendelea kuwaambia polisi wa upelelezi kwamba akiwa ameshikwa na kihoro alishinda kutwa nzima akifikiria jinsi atavyotoa taarifa za vifo vile. Alipoulizwa kwamba siku hiyo ya kihoro aliitumia akiwa wapi, Mchungaji Canning aliwashangaza polisi kwa kuwaambia kuwa alishinda ufukweni mwa Bahari akiwa na marafiki zake na kisha usiku wakaungana pamoja kwenye mghahawa mmoja kwa ajili ya kupata mlo wa usiku.

Kwa ujumla maelezo ya Mchungaji Canning yalikuwa yanatia mashaka kwani Polisi wa upelelezi walibaki wakijiuliza kuwa, hivi hiyo ndio tabia ya mtu aliyeshuhudia mauaji ya kikatili ya watu ambao aliwafanya kuwa wazazi wake? Kuanzia hapo Polisi wa upelelezi walianza kumuhoji Mchungaji Canning kwa makini zaidi. Msemaji wa Polisi Phil Ramer akizungumza na waandishi wa habari alisema “Kama inamchukuwa mtu siku nzima kutoa taarifa za vifo vya watu wanaomuhusu waliouwawa kikatili, hiyo haiwezi kuwachukuwa wanasayansi wa kutengeneza Roketi kugundua kwamba muuaji ni nani.”

Kwani kwa jinsi Canning anavyojieleza, ndivyo anavyozidi kudhihirisha kwamba kuna jambo analificha kuhusiana na mauaji hayo, alibainisha askari wa upelelezi anaeongoza timu ya wapelelezi wanaochunguza mauaji hayo Sajent Steven Carr. Kwa muda mfupi wapelelezi wa polisi walikuja kugungua kuwa Mchungaji Canning na familia ya Gleese walikuwa na uhusiano wa karibu sana.Historia inaonyesha kuwa awali Mchungaji Canning alikuwa ni Mchungaji wa kanisa moja lilipo katika mji wa Maine lakini baadae akaja akahamia katika mji wa Sebring na kuanzisha kanisa lake mwenyewe aliloliita Fountain of life hapo mnamo mwaka 1980.

Miongoni mwa waumini wa kanisa hilo kulikuwa na wazee zaidi ya 50 ambao walikuwa ni wafuatiliaji wazuri wa mahubiri ya mchungaji Canning kupitia luninga kabla ya kujiunga na kanisa hilo.
Hapo ndipo kwa mara ya kwanza ilipotokea Leo Gleese mhasibu mstaafu na mkewe Hazel mwana mitindo wa zamani kujuana na mchungaji Canning. Ni katika kipindi hicho ndipo familia ya Gleese ilipomuasili mchungaji Canning na mkewe na kuwaamini kiasi cha kuwafanya kama watoto wao ambapo kutokana na hali zao kuwa dhaifu kwa sababu ya uzee walimpa mamlaka ya kumiliki akaunti zao na kuwa mshauri wa familia hiyo katika maswala ya kifedha, kosa ambalo lilikuja kuwagharmu maisha yao.

Pia polisi wa upelelezi walikuja kugundua kwamba mchungaji Canning hakuwa ameaminiwa na familia ya Gleese tu bali pia waumini wengi katika kanisa lake walimuamini na kumfanya mshauri wao wa maswala ya kifedha. Pia wapelelezi hao wa polisi walikuja kushangaa baada ya kugundua kwamba, kwa takribani miaka 15 kanisa la Fountain of life lilikuwa likiendeshwa katika ghala chakavu alilolinunua mara baada ya kuhamia Sebring, na katika kipindi cha miaka kadhaa mchungaji Canning alikuwa kichangisha fedha kwa waumini wake ili ajenge jengo la kisasa la kanisa lake ambalo mwenyewe alisema litakuwa ni la karne.

Ni katika kipindi hicho ambapo ujenzi wa kanisa hilo ulipoanza ndipo mauaji ya Gleese na mkewe yalipotokea. Polisi wa upelelezi waliona ni vyema wakaanza upelelezi wao kwa kuangalia vyanzo vyake vya mapato pamoja na matumizi. Katika upelelezi wao ndipo walipokuja kugundua kwamba ndani ya wiki moja tangu mchungaji Canning apewe jukumu la kusimamia akaunti za familia ya Gleese ndipo alipolipa deni lake lote la manunuzi ya lile ghala aliloligeuza kuwa kanisa, na baada ya hapo akaanza matumizi makubwa ya fedha kwa kununua nyumba mbili zenye thamani ya dola 83,000, na wakati huo huo alianza upanuzi wa nyumba aliyokuwa akiishi kwa kuifanya kuwa ya kisasa zaidi.

Kwa muda mfupi akaunti za familia ya Gleese ilikuwa imekauka ikiwemo akaunti yao nyingine ya akiba iliyokuwa na kiasi cha dola 16,000, zilikuwa zimetoweka kusikojulikana. Polisi wa upelelezi walipowahoji marafiki wa familia ya Gleese, walidai kwamba wiki moja kabla ya kuuwawa kwao mke wa Gleese bibi Hazel Gleese alianza kumtilia mashaka mchungaji Canning kuhusiana na namna anavyosimamia fedha zao. Bi Hazel aliwaambia majirani zake kwamba anapanga kwenda katika benki jijini New York alipoweka fedha zao ili kuonana na meneja wa benki ili kupata taarifa ya fedha zao kwa mwaka mzima, lakini ikiwa imebaki siku chache kabla ya bi Hazel kwenda benki wakakutwa waameuwawa na hiyo ilitokea baada ya familia hiyo kugundua kwamba mchungaji Canning alikuwa ameghushi sahihi zao na kujiandikia hundi ambapo alikuwa akijilipa yeye mwenyewe.

Polisi wa upelelezi waliamua kuhamishia upelelezi wao katika benki hiyo iliyoko katika jiji la New York ambapo walikwenda na zile taarifa za benki (Bank statements) walizozikuta zimesambaa sakafuni baada ya mauaji yale kutokea. Hata hivyo mpaka kufikia hapo, bado polisi walikuwa hawajapata ushahidi wa kina wa kumfungulia mchungaji Canning mashitaka kuhusiana na mauaji ya ajuza wale.

Msemaji mwingine wa timu hiyo ya upelelezi wa Robert Glick alisema kwamba wanao ushahidi mwingine kutoka kwa raia mwema anaeishi jirani na kanisa la mchungaji Canning ambae alibainisha kwamba siku ile yalipotokea mauaji alimuona mchungaji huyo akienda na kurudi mara kwa mara kwenye shimo la taka lililoko jirani na kanisa hilo ambapo inasemekana kwamba huenda alikuwa anatafuta namna ya kuizika miili ya ajuza wale.Askari wa upelelezi walipoenda kuchunguza nyumbani kwa mchungaji huyo walikuta saa ya mkononi ambayo ilikuwa na matone ya damu, damu hiyo ilipochunguzwa katika maabara ilikuja kugundulika kuwa ilikuwa ni ya Leo Gleese.

Mpaka kufikia hapo Polisi wakawa na uhakika kwamba sasa wamembaini muuaji wa Leo na Hazel Gleese, nae si mwingine bali ni Mchungaji John Nelson Canning. Siku chache baada ya kuongoza mazishi ya ajuza wale mchungaji Canning alikamatwa na kushitakiwa kwa mauaji ya ajuza hao. Katika kesi hiyo mchungaji Canning alikiri kuwa aliwauwa Leo na mkewe Hazel Gleese kwa kuwapiga kwa kitu kizito na kisha kuwanyonga usiku wa Januari 3, 1995, hiyo ilitokea baada ya kuwa amebanwa na ajuza hao kuhusiana na namna alivyotumia fedha zao huku wakimuonyesha taarifa ya benki inayoonyesha kwamba alijiandikia hundi na kujilipa yeye mwenyewe.

Mnamo Februari 1996 mchungaji John Nelson Canning alipatikana na hatia ya kuhusika na mauaji ya Leo na Hazel Gleese ambapo alihukumiwa kifungo cha maisha jela bila ya uwezekano wa kupata msamaha wa kifungo cha nje (Parole). Mara baada ya kusomwa hukumu hiyo msemaji wa Polisi Phil Ramer aliwaambia wandishi wa habari kwamba hili ni tukio ambalo hatakuja kulisahau katika maisha yake.
Kwa maneno yake mwenyewe alisema “ni vyema watu wakawa waaminifu, ni jambo la kushangaza kukuta mchungaji ambae ameaminiwa na waumini wake kisha anakuja kuwauwa baadae kwa sababu ya pesa”
 
Ingawa umeuliza kwa kebehi, tutakujibu kwa faida yako na wapita njia.
Mtindo wa hukumu za ki mahakama katika Uislaam imegawanyika katika pande mbili.
1. Hukumu za makosa ya kijamii (Umalati)
haya ni kuhusiana na ndoa, mirathi, talaka, malezi ya watoto na mambo ya kijamii.
2. Hukumu za makosa ya Kihalifu - Jinai (Jinailati)
Ni kuhusians na wizi, uzinifu, ifisadi, kuua, ujambazi, ujangili, kufuru, rushwa, uhujumu uchumi, na yanayo fanana na hayo.
Hiki kipengele cha pili ni kigumu kukitekeleza kwakuwa kuna mambo ya kimsingi ya kiuadilifu jamii inatakiwa iyatekeleze kabla kuingia huko.
Jamii inatakiwa itoe zaka (kodi) kwa haki, masikini walishwe na kupewa haki zao. Kusiwepo na uonevu.
Waislaam wa Tanzania wana nia ya kipengele cha 1. (Umalati)

Mkuu samahani iko kipengele cha umalati na janailat vyote hivyo vipo ndani ya kadhi?? Na Kama vipo sheria ya kadhi inaruhusu kuchagua kifungu hiki nakukiacha hiki?
 
Hii kitu ilishabuma kitambo, na tulishaanza kuisahau.

Naona mleta mada kaamua kuwakumbusha waislam machungu.

Machungu haya yatatoweka kwa waislam mwezi wa kumi yatahamia kwa ccm .
Hili la mahakama ya kadhi ni bakora ya kuichapia ccm tanganyika.
La kina mzee moyo na himidi na kina shekh farid ni bakora nyingine ya ccm kwa upande wa znz.
Achilia mbali bakora nyingine ya ccm ya katiba pendekezwa na rasimu ya warioba ambayo wakiristo hawaitaki hata kuisikia.
Kwahiyo haya machungu ya waislam ndii kifo cha ccm.
Kama ccm hajajua makosa yao haya basi watakuwa wamesha choka kutawala.
 
Mambo yanayofanyika ni makubwa nyuma ya pazia
John-Canning-prison150.jpg

Mchungaji John Nelson Canning
images

Mchungaji Canning na mkewe siku alipowafungisha ndoa Bwana Leo Gleese na Bibi Hazel Gleese katikati
canning-at-funeralcp1

Mchungaji Canning siku ya mazishi ya ajuza hao

Mnamo January 3, 1995 mchungaji mmoja aitwae John Nelson Canning alikwenda katika kituo cha Polisi cha mji mdogo wa Sebring ulioko katika jimbo la Florida nchini Marekani na kutoa taarifa juu ya mauaji ya vikongwe wawili mtu na mkewe Bwana Leo na bibi Hazel Gleese.

Mchungaji huyo aliyekuwa na umri wa miaka 59 wakati huo aliwaeleza Polisi kwamba aligundua mauaji hayo baada ya kuwa amewatembelea nyumbani kwao kama ilivyo kawaida yake ya kuwatembelea waumini wake na kukuta miili ya vikongwe hao ikiwa imelala sakafuni kwenye dimbwi la damu.Mchungaji Canning aliendelea kuwaeleza Polisi kwamba bwana na bibi Gleese ni waumini wa siku nyingi katika kanisa la Fountain of life ambalo yeye ni muanzilishi wake.

Mchungaji huyo alibainisha kwamba katika kipindi cha miaka ya karibuni alikuwa ni muangalizi wa vikongwe hao ambao hawakubahatika kupata watoto katika maisha yao ya ndoa ambapo waliamua kumuasili (Adopt) mchungaji huyo na kumfanya mtoto wao na hivyo akawa anawaita Baba na Mama.
Mara baada ya kupata taarifa hizo Polisi walikimbilia kwenye eneo la tukio na kukutana na hali ya kutisha katika eneo la tukio ambayo hawatakuja kuisahau.

Kwani waliukuta mwili wa Bibi Hazel Gleese ambae alikuwa na umri wa miaka 90 wakati huo umelala jikoni ukiwa umetapakaa damu.
Na mwili wa mumewe Leo Gleese nao pia ulikutwa ukiwa umeegemea ukuta wa chumbani. Wote walikuwa wanaonyesha kwamba walikuwa wamepigwa na kunyongwa. Katika eneo ambalo miili ya ajuza wale ililala polisi wa upelelezi walikuta pia baadhi ya nyaraka za kibenki zikiwa zimesambaa pale sakafuni huku baadhi ya nyaraka hizo zikiwa zimelowa damu, pia kulikuwa na dalili zote kwamba kulikuwa na purukushani za kupigana kati ya bibi Gleese na mtuhumiwa au watuhumiwa wa mauaji.

Siku ya mazishi ya maajuza hao umati mkubwa wa watu wa mji wa Sebring walihudhuria mazishi hayo na yaliyoongozwa na mchungaji John Nelson Canning.
Akiongoza mazishi hayo mchungaji Canning, kwa maneno yake mwenyewe alisema “Miongoni mwenu mlikuwa marafiki wa muda mrefu wa baba na mama yangu hawa, lakini ninayo mashaka kwamba hakuna mtu yeyote aliyekuwa karibu na na familia hii zaidi yangu na mke wangu.”

Huku akitokwa na machozi, mchungaji huyo aliendelea kusema “Najivunia familia ya ajuza hawa kuniomba waniasili (Adopt) niwe mtoto wao, na nilijivunia kuwaita baba na mama kama wazazi wangu.” Familia ya Gleese haikubahatika kupata watoto katika maisha yao ya ndoa ndio sababu waliamua kuwaasili Canning na mkewe Judy hapo mnamo mwaka 1994.

Hata hivyo wakati wa mazishi hayo bado Polisi wa upelelezi walianza kumtilia mashaka mchungaji huyo kwa kumhusisha na mauaji ya ajuza wale. Polisi hao wa upelelezi walianza kumtilia mashaka mchungaji Canning tangu siku ile ya kwanza alipokwenda kutoa taarifa ya kutokea kwa mauaji ya ajuza wale ambao aliwachukulia kama wazazi wake.

Akiandikisha maelezo yake Polisi namna alivyogundua mauaji ya Bi Hazel na bwana Leo Gleese, Canning aliwaeleza Polisi akiwa katika hali ya kawaida kabisa. Kwa maneno yake mwenyewe Canning alisema “kwa kweli niligundua mauaji hayo jana asubuhi.” Polisi wa upelelezi walistushwa na habari hizo, kwani kwa mujibu wa maelezo yake ilionyesha kuwa miili ya Hazel na Leo Gleese ilikuwa imelala pale sakafuni kwa masaa 24 tangu kuuwawa pamoja na kuwa mchungaji Canning alifahamu kuhusu kutokea mauaji tangu jana asubuhi.

Alipoulizwa kwamba kwa nini hakutoa taarifa mapema, mchungaji Canning alidai kwamba aliogopa kutoa taarifa kwa sababu hapakuwa na shahidi mwingine zaidi yake, hivyo aliogopa kuwa mtuhumiwa wa kwanza kuhusishwa na mauaji yale. Kwa maneno yake mwenyewe Canning alsema “Niliingia ndani na kustushwa na mauaji yale, nilichanganyikiwa na kufunga mlango kisha nikaondoka kwani niliogopa kutoa taarifa za vifo hivi kwa kuhofia kwamba nitahusishwa navyo mpaka leo ndio nikakata shauri nije nitoe taarifa.”

Mchungaji Cunning aliendelea kuwaambia polisi wa upelelezi kwamba akiwa ameshikwa na kihoro alishinda kutwa nzima akifikiria jinsi atavyotoa taarifa za vifo vile. Alipoulizwa kwamba siku hiyo ya kihoro aliitumia akiwa wapi, Mchungaji Canning aliwashangaza polisi kwa kuwaambia kuwa alishinda ufukweni mwa Bahari akiwa na marafiki zake na kisha usiku wakaungana pamoja kwenye mghahawa mmoja kwa ajili ya kupata mlo wa usiku.

Kwa ujumla maelezo ya Mchungaji Canning yalikuwa yanatia mashaka kwani Polisi wa upelelezi walibaki wakijiuliza kuwa, hivi hiyo ndio tabia ya mtu aliyeshuhudia mauaji ya kikatili ya watu ambao aliwafanya kuwa wazazi wake? Kuanzia hapo Polisi wa upelelezi walianza kumuhoji Mchungaji Canning kwa makini zaidi. Msemaji wa Polisi Phil Ramer akizungumza na waandishi wa habari alisema “Kama inamchukuwa mtu siku nzima kutoa taarifa za vifo vya watu wanaomuhusu waliouwawa kikatili, hiyo haiwezi kuwachukuwa wanasayansi wa kutengeneza Roketi kugundua kwamba muuaji ni nani.”

Kwani kwa jinsi Canning anavyojieleza, ndivyo anavyozidi kudhihirisha kwamba kuna jambo analificha kuhusiana na mauaji hayo, alibainisha askari wa upelelezi anaeongoza timu ya wapelelezi wanaochunguza mauaji hayo Sajent Steven Carr. Kwa muda mfupi wapelelezi wa polisi walikuja kugungua kuwa Mchungaji Canning na familia ya Gleese walikuwa na uhusiano wa karibu sana.Historia inaonyesha kuwa awali Mchungaji Canning alikuwa ni Mchungaji wa kanisa moja lilipo katika mji wa Maine lakini baadae akaja akahamia katika mji wa Sebring na kuanzisha kanisa lake mwenyewe aliloliita Fountain of life hapo mnamo mwaka 1980.

Miongoni mwa waumini wa kanisa hilo kulikuwa na wazee zaidi ya 50 ambao walikuwa ni wafuatiliaji wazuri wa mahubiri ya mchungaji Canning kupitia luninga kabla ya kujiunga na kanisa hilo.
Hapo ndipo kwa mara ya kwanza ilipotokea Leo Gleese mhasibu mstaafu na mkewe Hazel mwana mitindo wa zamani kujuana na mchungaji Canning. Ni katika kipindi hicho ndipo familia ya Gleese ilipomuasili mchungaji Canning na mkewe na kuwaamini kiasi cha kuwafanya kama watoto wao ambapo kutokana na hali zao kuwa dhaifu kwa sababu ya uzee walimpa mamlaka ya kumiliki akaunti zao na kuwa mshauri wa familia hiyo katika maswala ya kifedha, kosa ambalo lilikuja kuwagharmu maisha yao.

Pia polisi wa upelelezi walikuja kugundua kwamba mchungaji Canning hakuwa ameaminiwa na familia ya Gleese tu bali pia waumini wengi katika kanisa lake walimuamini na kumfanya mshauri wao wa maswala ya kifedha. Pia wapelelezi hao wa polisi walikuja kushangaa baada ya kugundua kwamba, kwa takribani miaka 15 kanisa la Fountain of life lilikuwa likiendeshwa katika ghala chakavu alilolinunua mara baada ya kuhamia Sebring, na katika kipindi cha miaka kadhaa mchungaji Canning alikuwa kichangisha fedha kwa waumini wake ili ajenge jengo la kisasa la kanisa lake ambalo mwenyewe alisema litakuwa ni la karne.

Ni katika kipindi hicho ambapo ujenzi wa kanisa hilo ulipoanza ndipo mauaji ya Gleese na mkewe yalipotokea. Polisi wa upelelezi waliona ni vyema wakaanza upelelezi wao kwa kuangalia vyanzo vyake vya mapato pamoja na matumizi. Katika upelelezi wao ndipo walipokuja kugundua kwamba ndani ya wiki moja tangu mchungaji Canning apewe jukumu la kusimamia akaunti za familia ya Gleese ndipo alipolipa deni lake lote la manunuzi ya lile ghala aliloligeuza kuwa kanisa, na baada ya hapo akaanza matumizi makubwa ya fedha kwa kununua nyumba mbili zenye thamani ya dola 83,000, na wakati huo huo alianza upanuzi wa nyumba aliyokuwa akiishi kwa kuifanya kuwa ya kisasa zaidi.

Kwa muda mfupi akaunti za familia ya Gleese ilikuwa imekauka ikiwemo akaunti yao nyingine ya akiba iliyokuwa na kiasi cha dola 16,000, zilikuwa zimetoweka kusikojulikana. Polisi wa upelelezi walipowahoji marafiki wa familia ya Gleese, walidai kwamba wiki moja kabla ya kuuwawa kwao mke wa Gleese bibi Hazel Gleese alianza kumtilia mashaka mchungaji Canning kuhusiana na namna anavyosimamia fedha zao. Bi Hazel aliwaambia majirani zake kwamba anapanga kwenda katika benki jijini New York alipoweka fedha zao ili kuonana na meneja wa benki ili kupata taarifa ya fedha zao kwa mwaka mzima, lakini ikiwa imebaki siku chache kabla ya bi Hazel kwenda benki wakakutwa waameuwawa na hiyo ilitokea baada ya familia hiyo kugundua kwamba mchungaji Canning alikuwa ameghushi sahihi zao na kujiandikia hundi ambapo alikuwa akijilipa yeye mwenyewe.

Polisi wa upelelezi waliamua kuhamishia upelelezi wao katika benki hiyo iliyoko katika jiji la New York ambapo walikwenda na zile taarifa za benki (Bank statements) walizozikuta zimesambaa sakafuni baada ya mauaji yale kutokea. Hata hivyo mpaka kufikia hapo, bado polisi walikuwa hawajapata ushahidi wa kina wa kumfungulia mchungaji Canning mashitaka kuhusiana na mauaji ya ajuza wale.

Msemaji mwingine wa timu hiyo ya upelelezi wa Robert Glick alisema kwamba wanao ushahidi mwingine kutoka kwa raia mwema anaeishi jirani na kanisa la mchungaji Canning ambae alibainisha kwamba siku ile yalipotokea mauaji alimuona mchungaji huyo akienda na kurudi mara kwa mara kwenye shimo la taka lililoko jirani na kanisa hilo ambapo inasemekana kwamba huenda alikuwa anatafuta namna ya kuizika miili ya ajuza wale.Askari wa upelelezi walipoenda kuchunguza nyumbani kwa mchungaji huyo walikuta saa ya mkononi ambayo ilikuwa na matone ya damu, damu hiyo ilipochunguzwa katika maabara ilikuja kugundulika kuwa ilikuwa ni ya Leo Gleese.

Mpaka kufikia hapo Polisi wakawa na uhakika kwamba sasa wamembaini muuaji wa Leo na Hazel Gleese, nae si mwingine bali ni Mchungaji John Nelson Canning. Siku chache baada ya kuongoza mazishi ya ajuza wale mchungaji Canning alikamatwa na kushitakiwa kwa mauaji ya ajuza hao. Katika kesi hiyo mchungaji Canning alikiri kuwa aliwauwa Leo na mkewe Hazel Gleese kwa kuwapiga kwa kitu kizito na kisha kuwanyonga usiku wa Januari 3, 1995, hiyo ilitokea baada ya kuwa amebanwa na ajuza hao kuhusiana na namna alivyotumia fedha zao huku wakimuonyesha taarifa ya benki inayoonyesha kwamba alijiandikia hundi na kujilipa yeye mwenyewe.

Mnamo Februari 1996 mchungaji John Nelson Canning alipatikana na hatia ya kuhusika na mauaji ya Leo na Hazel Gleese ambapo alihukumiwa kifungo cha maisha jela bila ya uwezekano wa kupata msamaha wa kifungo cha nje (Parole). Mara baada ya kusomwa hukumu hiyo msemaji wa Polisi Phil Ramer aliwaambia wandishi wa habari kwamba hili ni tukio ambalo hatakuja kulisahau katika maisha yake.
Kwa maneno yake mwenyewe alisema “ni vyema watu wakawa waaminifu, ni jambo la kushangaza kukuta mchungaji ambae ameaminiwa na waumini wake kisha anakuja kuwauwa baadae kwa sababu ya pesa”
 
Mkuu samahani iko kipengele cha umalati na janailat vyote hivyo vipo ndani ya kadhi?? Na Kama vipo sheria ya kadhi inaruhusu kuchagua kifungu hiki nakukiacha hiki?

kutokana na mazingira halisi, umalati (sheria za jamii) ndio zinazoweza kutekelezeka. Jinailati haziwezi kutekelezeka! Huwezi kukata mikono wezi wakati vijana hawana ajira au viongozi wa serikali wakisaidia uuzaji wa madawa ya kulevya. Waumini wana wajibu wa kutoa zaka ambazo ni haki ya Masikini.
Umalati inatekelezeka kwakuwa inatatua masuala kama ndoa mirathi na talaka
David Harvey
 
Last edited by a moderator:

MASWALI AMBAYO WAISLAMU HAWAWEZI KUJIBU
************************************************************

Mohammad alikufa akiwa na miaka 60 ambayo, katika enzi hizo tunasema, alikuwa bado kijana tukizingatia kuwa mtu aliyeishi miaka mingi kwenye Biblia ni Methusellah (aliyeishi miaka 969). Na hadi karne ya sasa, kuna watu wangali wanaishi miaka zaidi ya 100, kama vile, yule ajuza wa Japan (Misao Okawa) aliyefikisha miaka 116 mwaka 2013.
1. Ni nini kilichomuua 'mtume' wa mwisho na wa kweli wa Allah?
2. Kwanini Allah hakumnusuru Mohammad kwenye kifo licha ya kuombewa na Jibril?
3. Kwanini kifo cha Mohammad hakizungumziwi sana? Kwani hakina maana?
4. Ni nini tunafichwa tusijue???

****FUATILIA POST ZANGU ZINAZOFUATA ILI UJUE UKWELI WASIOTAKA UJUE***

TATIZOZO LAKO NI UONGO NA UZUSHI

Mtume amefariki akiwa na umri wa miaka 63.
Na si 60 kama unavovunja amri kuu ya saba mbele ya wakristo wenzako bila hata aibu.

Mtume Muhammad (saw) aliugua maradhi kabla ya kifo chake kama wanavougua watu wengine.

Mtume yeyote ni mtu kama mimi nawewe.na kila mtu ana nafsi,na kila nafsi itaonja mauti.
Alikufa sababu siku yake ilikua imefika.
Mtume ametangulia na sisi tunafuata kila mmoja kwa wakati wake aliopangiwa.
Maana sisi wote ni wa mwenyezi Mungu na kwake tutarejea.

Kifo cha Mtume Muhammad hakizungumzwi sana?
Ni uongo.
Waislam huwaidhika na mauti,mauti yanapomkuta binadamu mwenzio ni lazima kwa muislam kumkumbuka mungu,na yeye kujiandaa na hicho kifo kwa kufanya matendo mema.
Kifo cha mtume Muhammad kina maana sana kama vifo vya mitume wengine,isipokua yesu,maana yesu hakufa,yesu mpaka leo yupo mawunguni na kuna siku atarudi,na ataishi naye ndipo atakufa kweli,ila sio hiki kifo cha laana mlichomzushia mtumishi wa mungu,
Fanyeni hima mtubu,maana yesu akirudi milango ya toba itafungwa.
 
Bado haujajibu swali, zaidi ya kujihami.
 
Dada faiza mi naomba kuuliza km mume alijiweka nyuma ktk utafutaji kila kitu anafanya mke mfano ktk ujenzi wa nyumba je mkiachana mume ana haki ktk nyumba hyo Wakati hakusaidia au awe amechangia asilimia 5/100
 
Bado haujajibu swali, zaidi ya kujihami.

Eleza kivipi nimejihami..
Nimejibu inavyotakiwa.
Sijajibu unavyotaka wewe.

Kwanza we ni muongo,wapi mtume kafa akiwa na miaka 60?

Kwahiyo kwa kua swali lako ulidanganya,unataka namimi nikudanganye kwenye majibu ndio uone nimejibu la,

Nimekuandikia ukweli.ndo maana huoni kama nimejibu.

We baki na uongo wako.
 
Back
Top Bottom