Swali kuhusu Mahakama ya Kadhi tafadhali

Barbarosa

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2015
Posts
22,584
Reaction score
27,838
Nina swali kuhusu Mahakama ya kadhi! Ina maana kwa Muislamu atakuwa anahudumiwa na hii Mahakama tu na hii Mahakama iamuacho ndiyo mwisho?

Yaani kwa mfano mwanamke anapenda kuachana na mumewe na kwa sababu zake binafsi labda tu amemchoka au sijui kamfumania na wanakwenda Mahakama ya kadhi, je vipi kuhusu haki ya mwanamke kwenye mali? Ni nani anaamua hili? Na je kama sheria ya Kiislamu haitambui kuhusu kugawana mali sasa inakuwaje kwa huyu mwanamke? ina maana Mahakama zetu za JMT haziwezi kuingilia hapo?

Na je Mzazi wa Kiislamu akitaka kumuoza mtoto wake kabla ya kutimiza umri ambao sheria ya JMT imeweka yaani miaka 18, sasa nini kitatokea?

Kwa maana kwa kiislamu hakuna kitu kama umri wa kuoa au kuolewa sasa kama Mahakama ya kadhi ikiamua mtoto wa JMT aolewe ndiyo ataolewa kweli na Serikali ya JMT haiwezi kumuokoa huyu Mtoto?
 
Hahaha.. tunakoenda sipo, mana hapo sasa ni mihimili miwili yenye kutoa hukumu mbili tofauti.. Nina mashaka sana juu ya hili.
 
Wala usipotezu Muda wako.

HAKUNA MAHAKAMA YA KADHI KATIKA QURAN.

Hicho kitengo ni cha akina Nonda Ally Kombo na FaizaFoxy. Allah hakuteremsha wala sema MaQafir wa Kiislam watumie Mahakama ya Qadhi
 
Kadhi kazi yake ni kusikiliza kadhia zinazoletwa mbele yake. Nnauhakika umewahi kulisikia au kulisoma neno la Kiswahili "kadhia", jee unajuwa limetoka wapi hilo neno na maana yake?

Kabla hujajibu hilo, pata kidogo darsa:

"Indeed we sent Our Messengers with the clear signs, and We sent down with them the Book and the Balance so that men might uphold justice. And We sent down iron, wherein is great might, and many uses for men, and so that God might know who helps Him, and His Messengers, in the Unseen. Surely God is All-Strong, All-Mighty". (57:25)

"Whoso judges not according to what God has sent down-they are the un-believers". (5:44)

"Whoso judges not according to what God has sent down-they are the evil-doers". (5:45)
"Whosoever judges not according to what God has sent down-they are the ungodly". (5:47)

"O believers, be you securers of justice, witnesses for God, even though it be against yourselves, or your parents and kinsmen ...". (4:135)
 
Hiii nyimbo siimeshachuja hii mbona mnaipa airtime tena wakati haiuziki??
 
Hii mahakama ni kama ndoto za Bunwasi kutokea Tanganyika.Tunajadili kesi isiyoweza kutokea hata katika ndoto..
 
Nina swali kuhusu Mahakama ya kadhi! Ina maana kwa Mwislamu atakuwa anahudumiwa na hii Mahakama tu na hii Mahakama iamuacho ndiyo mwisho?

Yaani kwa mfano Mwanamke anapenda kuachana na Mumewe na kwa sababu zake binafsi labda tu amemchoka au sijui kamfumania na wanakwenda Mahakama ya kadhi, je vipi kuhusu haki ya Mwanamke kwenye mali? Ni nani anaamua hili? Na je kama sheria ya Kiislamu haitambui kuhusu kugawana mali sasa inakuwaje kwa huyu Mwanamke? ina maana Mahakama yetu ya JMT haiwezi kuingilia hapo?

Na je Mzazi wa Kiislamu akitaka kumuoza mtoto wake kabla ya kutimiza Umri ambao sheria ya JMT imeweka yaani miaka 18, sasa nini kitatokea?

Kwa maana kwa kiislamu hakuna kitu kama umri wa kuoa au kuolewa sasa kama Mahakama ya kadhi ikiamua mtoto wa JMT aolewe ndiyo ataolewa kweli na Serikali ya JMT haiwezi kumuokoa huyu Mtoto?

Nadhani ni hiari ya mwanamke kwenda huko au kuacha. Kama mswalihina aende na akubali matokeo!
 
Hiii nyimbo siimeshachuja hii mbona mnaipa airtime tena wakati haiuziki??

Hii kitu ilishabuma kitambo, na tulishaanza kuisahau.

Naona mleta mada kaamua kuwakumbusha waislam machungu.
 
Nina swali kuhusu Mahakama ya kadhi! Ina maana kwa Mwislamu atakuwa anahudumiwa na hii Mahakama tu na hii Mahakama iamuacho ndiyo mwisho?

Yaani kwa mfano Mwanamke anapenda kuachana na Mumewe na kwa sababu zake binafsi labda tu amemchoka au sijui kamfumania na wanakwenda Mahakama ya kadhi, je vipi kuhusu haki ya Mwanamke kwenye mali? Ni nani anaamua hili? Na je kama sheria ya Kiislamu haitambui kuhusu kugawana mali sasa inakuwaje kwa huyu Mwanamke? ina maana Mahakama yetu ya JMT haiwezi kuingilia hapo?

Na je Mzazi wa Kiislamu akitaka kumuoza mtoto wake kabla ya kutimiza Umri ambao sheria ya JMT imeweka yaani miaka 18, sasa nini kitatokea?

Kwa maana kwa kiislamu hakuna kitu kama umri wa kuoa au kuolewa sasa kama Mahakama ya kadhi ikiamua mtoto wa JMT aolewe ndiyo ataolewa kweli na Serikali ya JMT haiwezi kumuokoa huyu Mtoto?
Kwa nchi iliyo potoka kimaadili na kuwa na mwingiliano wa kiimani sidhani kama jambo hili la mahakama ya kadhi litawezekana. Pia wanapotaja Mahakama wajue huo ni mhimili muhimu wa kimaamuzi pia kuna kundi kubwa la watu wanaopaswa kuajiriwa, swali ajira yao itapitia sekretariet ya ajira au tataundwa chombo kingine cha kiutumishi kuwapata hao makadhi wa kata, wilaya, mkoa na wa kitaifa?
 
Umeuliza maswali mengi mfululizo, ngoja tuanze na moja moja.

Kwanza yapaswa uelewe ni mambo yepi ambayo huamuliwa na mahakama ya kadhi.

Mahakama ya kadhi "haitahudumia" kesi za jinai na pia kesi za madai ya kibiashara.

Mahakama ya kadhi itahusika na kesi za haki za msingi kwa Waislam ambazo ni mirathi, ndoa, talaka na wakfu za Waislam tu.

Naam, tulitakalo sisi kuwa Mahakama hii ikiamua basi iwe ndiyo mwisho kuhusu hayo niliyoyataja.
 
Na vipi kuhusu kuchinjana,mwizi kukatana mikononi na mzinifu wa kike kupigwa mawe??? Nasikia hizo sheria zote za kuuwana zipo ndani ya mahakama ya kadhi je ni kweli???
 
Yaani kwa mfano Mwanamke anapenda kuachana na Mumewe na kwa sababu zake binafsi labda tu amemchoka

Kwanza kabisa ni vyema ukafahamu kuwa ndoa katika Uislam ni mkataba baina ya waliooana, kuwa wataishi pamoja wakifuata sharia na mila za Kiislam katika maisha yao na kama kuna mambo ya zaidi ya kukubaliana ambayo hayakiuki sharia za Kiislam basi yanaweza yakaainishwa katika huo mkataba, lakini mara nyingi (99.9%) huwa hakuna haja ya kuweka vipengele vingine zaidi kwani Uislam sharia zake zimekamilika.

Na mkataba huo unaweza kuvunjika (talaka) iwapo yeyote kati ya hao waliooana atakiuka sharia na mila za Kiislam na atakapoonywa au kukumbushwa na jozi wake (kuoana ni kuwa jozi "pair") hatozingatia na ataendelea kuyafanya kwa kusudi.

Katika Uislam talaka inaweza kutolewa kwa hizo sababu za kukiuka Uislam na nyinginezo ambazo zitamkosesha mmoja raha ya maisha au matarajio yake, bila kukiuka sharia na mila za Kiislam. Kama vile mke au mume kutokuzaa, mume au mke kuwa mlevi, mume au mke kuwa hamridhishi mwenza wake, mume au mke kuwa mgonjwa wa kudumu, mume au mke kuwa mbali na jozi yake kwa muda mrefu, mume au mke kujihusisha na mambo yanayokatazwa katika Uislam. Hizo ni baadhi tu ya sababu zinazoweza kupelekea kutalikiana.

Amma kumuacha mume tu hivi hivi kama ni kwa kumchoka tu basi kama ni mke itabidi alipe mahari aliyopewa wakati wa kuoana.

Kuachana Kiislam kuna namna zake na si nimekuacha tu basi yamekwisha, haifai hivyo. Kuna suluhu inabidi zipitikane kabla ya kuachana, kuna kusameheana, kuna wazee kuitwa na kupitisha suluhu, kuna eda, kuna kurudiana hata inapofikia mkaachana na baadae ikapita suluhu.

Ikibidi na hakuna budi, na ili kila mmoja awe katika amani, basi talaka haina budi lakini ni sharti iwe kitu cha mwisho kabisa. Kwani kuachana si kwema.

Hata kadhi kwanza huanza kutazama namna ya kusuluhisha ndoa kabla hajaamua kuwa hapa inabidi pawe na talaka.

Natumai hilo swali lako nimelijibu na Mwenyeezi Mungu ndiyo ajuae zaidi na mimi nimejitahidi kadri ya uwezo wangu na kama wachangiaji wengine watakuwa na mengine wanaweza kusherehesha zaidi.

Ntarudi kuendelea kukujibu maswali yako mengine.
 
Nina swali kuhusu Mahakama ya kadhi! Ina maana kwa Mwislamu atakuwa anahudumiwa na hii Mahakama tu na hii Mahakama iamuacho ndiyo mwisho?

Yaani kwa mfano Mwanamke anapenda kuachana na Mumewe na kwa sababu zake binafsi labda tu amemchoka au sijui kamfumania na wanakwenda Mahakama ya kadhi, je vipi kuhusu haki ya Mwanamke kwenye mali? Ni nani anaamua hili? Na je kama sheria ya Kiislamu haitambui kuhusu kugawana mali sasa inakuwaje kwa huyu Mwanamke? ina maana Mahakama yetu ya JMT haiwezi kuingilia hapo?

Na je Mzazi wa Kiislamu akitaka kumuoza mtoto wake kabla ya kutimiza Umri ambao sheria ya JMT imeweka yaani miaka 18, sasa nini kitatokea?

Kwa maana kwa kiislamu hakuna kitu kama umri wa kuoa au kuolewa sasa kama Mahakama ya kadhi ikiamua mtoto wa JMT aolewe ndiyo ataolewa kweli na Serikali ya JMT haiwezi kumuokoa huyu Mtoto?

Hakuna lazima ya mtu kuhukumiwa na mahakama ya kadhi, hiki kitu kinasemwa kila siku. Ni kwa ridhaa tu ya wawili hao, iwapo mmoja wa wanandoa hatokubali kwenda huko then mahakama hiyo haitoweza kusikiliza shauri hilo.
Mahakama ya kadhi haiamui mtu kuolewa, inafungisha ndoa baada ya wahusika kuwa wamekubaliana, kwa mujibu wa sheria zilizopo.
Halafu, hivi sheria ya ndoa ya nchi hii imeweka umri wa mwanamke kuolewa ni miaka 18???
 
je vipi kuhusu haki ya Mwanamke kwenye mali? Ni nani anaamua hili? Na je kama sheria ya Kiislamu haitambui kuhusu kugawana mali sasa inakuwaje kwa huyu Mwanamke? ina maana Mahakama yetu ya JMT haiwezi kuingilia hapo?

Katika Uislam tunahimizwa sana tuandikiane makubaliano yetu. Soma Qur'an 2:282 limehimizwwa hilo.

Mali ya mume ni ya mume, mali ya mke ni ya mke. Na ikiwa mtafanya biashara pamoja basi kanuni za mikataba zifuatwe ipasavyo na hisa zakila mmoja ziwe wazi na kisheria ili kusiwe na shaka ndani yake. Na ikiwa mtajenga pamoja basi kanuni za kuandikisha jengo/majengo kwa majina ya wote na hisa zao zifuatwe ili isije kuwa taabu mtakapoachana amma mmoja kufariki.

Na ikiwa mnachuma pamoja basi nayo pia muandikiane kiuwazi kabisa na mashahdi wawepo na ikiwezekana kwa mwanasheria ili kila mmoja aijuwe kabisa haki yake ni kama mkataba wowote wa ubia ulivyo, sioni sababu ya kutaka kugawana mali isiyo yako na ikiwa hukufata kanuni na sharia itakavyo. Kwani kuna wanawake wana mali nyingi kuliko wanaume na pia kuna wanaume wana mali nyingi kuliko wanawake. Na kila mmoja ana haki na mali zake.

Na ikiwa hamjaandikiana mikataba ya wazi kabisa katika mali zenu basi hakuna wa kumlaumu ila ni nyinyi wenyewe na upumbavu wa aliyeiandika mali yote kwa jina la mwingine.

Na ikiwa wote mnafata Uislam ipasavyo basi sidhani kama atatokea ambae atataka mali ya kudhulumu kwa mwenzake.

Kwanini kusiwe na mikataba wakati mambo yote ni mazuri?

Hili nawaasa sana Waislam wote na hata wasio Waislam, hususan wanawake, msifanye uvivu wa kuandikiana mikataba ya mali mnazochuma pamoja kisheria na kikanuni.

Mimi namshukuru Mwenyeezi Mungu, kila kitu changu kipo kimaandishi na kisheria, mali zangu zinajulikana za Gozi langu zinajulikana, za watoto zinajulikana. Hakuna leo kitokee chochote aje mtu ooooh hii ya mumewe, hiii ya mkewe. Kila kitu wazi tena kwa wakili na mashahidi ni Masheikh na ndugu wa upande wangu na upande wake na endorsed na mawakili na mahakamani.

Tumefanya hivyo kwa nia njema kabisa, kwani tumeiona dunia na tumeona watu wanaodharau mikataba wanavyopata taabu ilhali mikataba imesisitizwa kwenye Qur'an.
 
Nina swali kuhusu Mahakama ya kadhi! Ina maana kwa Mwislamu atakuwa anahudumiwa na hii Mahakama tu na hii Mahakama iamuacho ndiyo mwisho?

Yaani kwa mfano Mwanamke anapenda kuachana na Mumewe na kwa sababu zake binafsi labda tu amemchoka au sijui kamfumania na wanakwenda Mahakama ya kadhi, je vipi kuhusu haki ya Mwanamke kwenye mali? Ni nani anaamua hili? Na je kama sheria ya Kiislamu haitambui kuhusu kugawana mali sasa inakuwaje kwa huyu Mwanamke? ina maana Mahakama yetu ya JMT haiwezi kuingilia hapo?

Na je Mzazi wa Kiislamu akitaka kumuoza mtoto wake kabla ya kutimiza Umri ambao sheria ya JMT imeweka yaani miaka 18, sasa nini kitatokea?

Kwa maana kwa kiislamu hakuna kitu kama umri wa kuoa au kuolewa sasa kama Mahakama ya kadhi ikiamua mtoto wa JMT aolewe ndiyo ataolewa kweli na Serikali ya JMT haiwezi kumuokoa huyu Mtoto?

Kwanza kabisa, nijuavyo sheria ya Tanzania umri wa kuoa kuolewa ya mwaka 1971 ni miaka 14 au 15. Hii sheria ya miaka 18 sijui imeanza lini, naomba unisaidie.

Pili, Uislam unasisitiza kutokuvunja sheria za dola mradi haziingilii Uhuru wa Muislam kuabudu na kumtoa katika Uislam wake.

Hebu kwanza tupate uhakika wa umri wa kuoana Tanzania kabla hatujalumbana zaidi katika hili, au unaonaje?
 
Kwa nchi iliyo potoka kimaadili na kuwa na mwingiliano wa kiimani sidhani kama jambo hili la mahakama ya kadhi litawezekana. Pia wanapotaja Mahakama wajue huo ni mhimili muhimu wa kimaamuzi pia kuna kundi kubwa la watu wanaopaswa kuajiriwa, swali ajira yao itapitia sekretariet ya ajira au tataundwa chombo kingine cha kiutumishi kuwapata hao makadhi wa kata, wilaya, mkoa na wa kitaifa?

Hata saizi kazi za mahakama hazipiti sekretariati ya ajira.
 
Kwanza kabisa ni vyema ukafahamu kuwa ndoa katika Uislam ni mkataba baina ya waliooana, kuwa wataishi pamoja wakifuata sharia na mila za Kiislam katika maisha yao na kama kuna mambo ya zaidi ya kukubaliana ambayo hayakiuki sharia za Kiislam basi yanaweza yakaainishwa katika huo mkataba, lakini mara nyingi (99.9%) huwa hakuna haja ya kuweka vipengele vingine zaidi kwani Uislam sharia zake zimekamilika.

Na mkataba huo unaweza kuvunjika (talaka) iwapo yeyote kati ya hao waliooana atakiuka sharia na mila za Kiislam na atakapoonywa au kukumbushwa na jozi wake (kuoana ni kuwa jozi "pair") hatozingatia na ataendelea kuyafanya kwa kusudi.

Katika Uislam talaka inaweza kutolewa kwa hizo sababu za kukiuka Uislam na nyinginezo ambazo zitamkosesha mmoja raha ya maisha au matarajio yake, bila kukiuka sharia na mila za Kiislam. Kama vile mke au mume kutokuzaa, mume au mke kuwa mlevi, mume au mke kuwa hamridhishi mwenza wake, mume au mke kuwa mgonjwa wa kudumu, mume au mke kuwa mbali na jozi yake kwa muda mrefu, mume au mke kujihusisha na mambo yanayokatazwa katika Uislam. Hizo ni baadhi tu ya sababu zinazoweza kupelekea kutalikiana.

Amma kumuacha mume tu hivi hivi kama ni kwa kumchoka tu basi kama ni mke itabidi alipe mahari aliyopewa wakati wa kuoana.

Kuachana Kiislam kuna namna zake na si nimekuacha tu basi yamekwisha, haifai hivyo. Kuna suluhu inabidi zipitikane kabla ya kuachana, kuna kusameheana, kuna wazee kuitwa na kupitisha suluhu, kuna eda, kuna kurudiana hata inapofikia mkaachana na baadae ikapita suluhu.

Ikibidi na hakuna budi, na ili kila mmoja awe katika amani, basi talaka haina budi lakini ni sharti iwe kitu cha mwisho kabisa. Kwani kuachana si kwema.

Hata kadhi kwanza huanza kutazama namna ya kusuluhisha ndoa kabla hajaamua kuwa hapa inabidi pawe na talaka.

Natumai hilo swali lako nimelijibu na Mwenyeezi Mungu ndiyo ajuae zaidi na mimi nimejitahidi kadri ya uwezo wangu na kama wachangiaji wengine watakuwa na mengine wanaweza kusherehesha zaidi.

Ntarudi kuendelea kukujibu maswali yako mengine.

Dah! umejaribu kufafanua kiasi mwili umenisisimka, but vipi kuhusu mgawanyo wa mali ambazo walizichuma kama wanandoa je? mwanamke akipewa talaka atapata mgao wa mali?
 
Nimelijibu hilo katika post namba 15.

Pole kwa kusisimkwa na mwili.
 
Kadhi kazi yake ni kusikiliza kadhia zinazoletwa mbele yake. Nnauhakika umewahi kulisikia au kulisoma neno la Kiswahili "kadhia", jee unajuwa limetoka wapi hilo neno na maana yake?

Kabla hujajibu hilo, pata kidogo darsa:

"Indeed we sent Our Messengers with the clear signs, and We sent down with them the Book and the Balance so that men might uphold justice. And We sent down iron, wherein is great might, and many uses for men, and so that God might know who helps Him, and His Messengers, in the Unseen. Surely God is All-Strong, All-Mighty". (57:25)

"Whoso judges not according to what God has sent down-they are the un-believers". (5:44)

"Whoso judges not according to what God has sent down-they are the evil-doers". (5:45)
"Whosoever judges not according to what God has sent down-they are the ungodly". (5:47)

"O believers, be you securers of justice, witnesses for God, even though it be against yourselves, or your parents and kinsmen ...". (4:135)
Bado unaweweseka tu. Nipe aya ambayo Alla anateremsha Qadhi. Sina muda na blahing zako.
 
Back
Top Bottom