JIDULA NGASHA
New Member
- Jan 17, 2016
- 1
- 4
MAAJABU KUMI YA SHIRIKA LA TPDC CHINI YA KAULI MBIU-HAPA KAZI TU-PART 1.
1. Ni shirika pekee ambalo ajira zake zimekuwa zikifanywa kwa upendeleo mkubwa bila kujali kwamba kuna vyombo vya dola vinavyoweza kubatilisha wala kukemea upuuzi wao. Ni hivi majuzi tu shirika limetangaza nafasi za kazi za mameneja wa vitengo mbali mbali lakini ajabu na kweli waombaji kutoka nje ya TPDC waliopata nafasi za kazi si zaidi ya watatu kati ya nafasi zaidi ya 15. Hata hao waliopata, wawili kati yao wameshikwa mkono na ‘wakubwa’ wa shirikani. Vigezo vilivyowekwa kwenye tangazo ilikuwa ni kuwahadaa watanzania kwani havikufuatwa wakati wa zoezi zima. Hii ni aibu kwa Shirika na Wizara ya Nishati na Mamlaka zinazosimamia ajira nchini.
2. Ni shirika pekee la Umma linaloweza kuajiri bila kuomba kibali cha ajira kutoka Ofisi ya Rais Utumishi Kama taratibu zinavyotaka. Mfano, nafasi hizo za managers zimetangazwa na kuajiriwa bila kuwa na kibali cha ajira kutoka mamlaka husika. Anayebisha aende kwenye mamlaka za ajira akathibitishe hili. Hii ni kashfa kubwa ya matumizi mabaya ya ofisi.
3. Ni shirika pekee ambalo linapuuza taaluma na baadala yake kujikita kwenye uzoefu tu wakati wa kuajiri watumishi wake. Ni aibu kwa Shirika kubwa kama TPDC kuamua kuajiri mtu kwenye nafasi nyeti tena ya manager wa hesabu na fedha bila kuthamini taaluma kama CPA ambacho kilikuwa kigezo cha lazima kwa mujibu wa tangazo. Kama waombaji wenye sifa walijitokeza, kuna sababu gani ya kuajiri mtu mwenye sifa za mashaka? Aibu aibu aibu!
4. Ni shirika pekee ambalo linaweza kuajiri baadhi ya watumishi wake bila kuwafanyia vetting. Taratibu zinataka watumishi wote ilimradi wanapewa majukumu mapya (tena hawa wanapewa majukumu makubwa zaidi na ni nafasi za uteuzi). Unajiuliza katika nchi hii inayofuata misingi ya haki na utawala bora, kwanini watumishi waajiriwe kwenye nafasi kubwa bila kufanyiwa vetting? Haya ni makusudi yenye nia ya kulipaka shirika matope. Waliofanya hivi wanajua walikuwa na malengo gani….waulizeni labda wanayo majibu! Mkurugenzi Edith Semtengu na meneja wake Rwechungula waeleze walitumia kanuni gani katika kufanya haya.
5. Ni shirika pekee ambalo Mkurugenzi wa Utawala kwa kushirikiana na Kaimu Meneja wa HR ambao ni marafiki wakubwa wanaweza kujiamulia kupanga na kuidhinisha viwango vya mishahara ya Mameneja bila kupata idhini ya Bodi ya Wakurugenzi, Msajili wa Hazina au Mkurugenzi Mtendaji. Hakuna Waraka wowote wa Mshahara unaoonyesha viwango vya mishahara wanavyotakiwa kulipwa Mameneja kwa sababu vyeo hivi havikuwahi kuwepo shirikani. Kama waraka upo basi wauonyeshe. Wawili hawa waulizwe wamepata wapi kibali cha kupanga mishahara ya mameneja? Itakumbukwa kuwa vigogo hawa wa idara ya Utawala wamekuwa wakishirikiana hata kuwahamisha watumishi shirikani hasa wale ambao hawaelewani nao. Ni kweli mamlaka haziyaoni haya?
6. Ni shirika pekee ambalo nafasi za ajira zinaweza kutangazwa na baadaye nafasi mojawapokuondolewa ili kumnufaisha mmojawapo wa waombaji. Wakati wakurugenzi wote waliomba kazi na kufanya usaili, Mkurugenzi mmojawapo wa shirika ameendelea kutesa bila kufanya usaili. Bado tuendelee kuamini kwamba ni shirika lenye fursa sawa kwa wote? Ukihoji unahamishwa.
7. Ni shirika pekee ambalo mshindi kwenye usaili anakosa nafasi na nafasi yake kwenda kwa mteule mwingine hata kama hakushinda usaili kwa kutumia kigezo cha uzoefu. Bora mwombaji ashinde usaili lakini ashindwe kwenye vetting, hapo hakuna shaka. Lakini hapa hadithi ni ni tofauti kabisa. Swali rahisi la kujiuliza hapa ni kwamba, kama uzoefu kilikuwa ni kigezo kwanini mtu aitwe mpaka kwenye usaili wa hatua za mwisho?Je, si ilikuwa busara kumuondoa mtu huyo ili kuwaacha wenye sifa sawa wapambane mpaka mwisho ili mshindi apate haki yake? Hiyo ndiyo TPDC bwana.
8. Ni shirika pekee la Umma ambalo haliogopi mamlaka kwani limeendelea kuajiri mameneja hawa hata bila kuwa na approved scheme of service kwa nafasi za managers. Unawezaje kuajiri bila kuwa na nyenzo hii muhimu? Msajili wa Hazina na Utumishi wa Umma wapo lakini labda hawana taarifa. Wakati haya yakitendeka, Mkurugenzi wa Utawala na Kaimu Meneja wa HR wameendelea kuchapa kazi bila kuona kama wanatenda ‘uhalifu’. Hakika hii ni kali kuliko.
9. Ni shirika pekee ambalo masuala ya ajira kwa kiasi kikubwa yamekuwa yakifanywa na watu wasiokuwa na uzoefu wa Utumishi kwenye mashirika hasa ya mafuta na gesi. Maamuzi yote hayo yamekuwa yakifanywa kwa kiasi kikubwa na Mkurugenzi wa Utawala na Kaimu Meneja HR ambao walishirikiana kuwaondoa aliyekuwa Mkurugenzi wa Utawala na Fedha na Kaimu Meneja HR waliokuwa wanafanya kazi zao kwa weledi mkubwa. Wamebaki na wameachwa wakiendelea kulihujumu shirika kwa muda sasa. Hii ni hatari kwa ustawi wa utumishi wa umma.
10.Ni shirika pekee ambalo, tunaamini TAKUKURU na vyombo vingine vimeshindwa kulifikia labda kutokana na kuwasubiri Mh. Rais au Waziri Mkuu wafike ili kujionea wenyewe. Ni wazi uchunguzi ukifanyika yatabainika mengi zaidi ya haya. Je huu ni uungwana?