Education Mentor
JF-Expert Member
- Oct 26, 2016
- 396
- 687
Russia licha ya kusambaratika lakini bado ana hazina kubwa ya Nyuklia duniani na bado ana Spheres of influence ambazo inajikuta mara kwa mara kimasirahi anazozana na nato....Umoja wa Kisovieti (USSR au CCCP) taifa lililozaliwa mwaka 1914-1991,
Lilikuwa ni moja ya taifa lenye nguvu sana duniani lakini lenye mwisho mbaya sana ambao ni aibu kwa watu wake mpaka leo. Kiuchumi walikuwa wana nguvu sana, kiteknolojia walikuwa mbele, nguvu kubwa ya viwanda, kijeshi walikuwa mbele na mifumo yao ya kitamaduni iliyotokana na ukomunisti ilishawishi dunia kuanzia barani Marekani, Asia hadi Afrika na kubwa ziadi walikuwa na idadi kubwa sana ya watu ambapo takwimu zinasema kwamba walikuwa ni milioni 293.
Lakini baada ya kusambaratika nchi hii ilipoteza kila kitu ambacho ilikuwa nacho kuanzia Idadi ya watu, jeshi, viwanda na teknolojia maana kila nchi iliondoka na watu wake, majeshi yake na sehemu kama Ukraine ikapata viwanda vya bure kabisa, Poland na Georgia nao hawakuwa nyuma kabisa. Ikawa nchi dhaifu na masikini kweli....
Sasa najiuliza kwanini taifa hili dhaifu ambalo lililoshindwa vita baridi linaendelea kumsumbua Marekani (The Only Super Power) pamoja na washirika wake kijeshi ambao ni zaidi ya 25 ???
CC: chige , FisadiKuu
Kuanguka kwa Ussr haikumaanisha ndio kaanza 0.....
chukulia mfano mzuri wa anguko la Britain as super power lakini bado ana sphere of influence kubwa tu......
Bahati mbaya kwa Russia ni bado ana migongano na Nato kimasirahi kuanzia Ukraine, Black Sea na pia Military alliance na China Pakistan nk