Swali gumu kidogo: Kwanini Urusi iliyosambaratika na dhaifu kuliko USSR inawasumbua sana NATO?

KISIASA
1. Amesababisha sintofahamu kubwa ndani ya siasa za Marekani hasa kwa Donald Trump.
2. Anavuruga mipango ya Marekani kwa kutumia VETO kule Umoja wa Mataifa.
3. Amefanikiwa kuugawanya Umoja wa Ulaya (Schroeder wa Ujerumani anafanya kazi Rosneft)
4. Anaisaidia Korea Kaskazini kukwepa vikwazo vya Umoja wa Mataifa.
5. Alimsaidia Raisi wa Uturuki asipinduliwe na kuuwawa ambapo inasemekana CIA walihusika sana.
6. Amemtunza Edward Snowden ambaye kavujisha siri nyeti za Marekani.

KIJESHI
1. Kavamia Ukraine kijeshi na kumega Crimea kwa nguvu mno ya wanajeshi 70,000.
2. Kavuruga mpango wa Marekani na Israel wa kuvamia Syria na kumtoa Assad.
3. Anauza silaha nzito kwa mataifa hasimu wa Marekani kama Iran.
4. Anasidia Korea Kaskazini kukwepa vikwazo vya Umoja wa Mataifa.
5. Amevuruga majimbo ya Lugansk na Donestky hadi leo majeshi ya Ukraine hayana amani.
7. Yeye ndiyo mwenye jeshi la pili kwa ubora hapa duniani mbali na shida zote kiuchumi.

KITEKNOLOJIA
1. Marekani mpaka leo anategemea injini kutoka Urusi kwa ajili ya kurusha roketi zake.
2. Ametengeneza makombora mazito ambayo yanasafiri mara 10 zaidi ya sauti.
3. Walimwekea vikwazo vya injini za ndege kutoka Ukraine lakini katengeneza zake kwa haraka sana.
4. Ana wasomi wa sayansi ambao ni World Class kama 1,000,000 hivi.
5. Teknolojia ya kimtandao (Cyber Technology) yuko mbele sana na amethibitishia dunia mara nyingi.

KIUCHUMI
1. Amefanikiwa kutumia makampuni yake ya nishati kuwaumiza Ulaya hasa NORD Stream 2.
2. Amefanikiwa kutumia ushawishi wa nishati kuyavuta karibu mataifa kama Uchina, India na Uturuki.
3. Uturuki ameagiza silaha kutoka Urusi kitu ambacho kitampa faida za kiuchumi Mrusi.
4. Saudi Arabia ametengeneza viwanda vya Kalashnikov Ak-47 nchini kwake na Urusi karuhusu.
5. Amesaidia kutengeneza vyombo kama BRICS, The Shanghai Cooperation na Eurasia Economic Union

NB: Haya ni machache tu, sasa nchi iliyosambaratika inalisumbuaje taifa kubwa duniani ??
Kwa haya uliyoyasema unahisi jamaa ni dhaifu???
 
Mkuu mbona Georgia na Ukraine sio wanacahama wa NATO ? ninachofahamu ni kwamba nchi zote mbili zinataka kujiunga NATO lakini kwa sasa si wanachama bado.

Ni kweli kabisa usemavyo, ila nilikuwa namjibu Malcom ambaye alikuwa akijaribu kuwaona warusi kama si kitu akisema kuwa hao Warusi wameshindwa kuzuia Ukraini na Geogia kujiunga NATO. Aidha nilichomuelewa ni kuwa NATO wanabwata sana katika kuzitetea nchi hizo mbili, kanakwamba tayari ziko katika hifadhi yao.

Nilikuwa najaribu kutoa picha juu ya influence ya Urusi katika maamuzi ya nchi hizo mbili kujiunga NATO.
 
Nimekupata,ila naomba umsome tena Malcom,kwenye post zake nyingi ni pro-Russia. Jaribu kusoma uzi kuanzia mwanzo ndo utapata picha nzuri. Siku njema mkuu.
 
Kinachoipa nguvu Urusi kwa sasa ni silaha za nyuklia (Silaha za maangamizi) alizo nazo ambazo Marekani na nchi za magharibi zinahofia ndo maana wanasita kuitenga Urusi kwenye jukwaa la kimataifa hakuna jingine zaidi ya hilo.
 
Pot Malcom Lumumba aka Prof Mwandosya aka Ndugai tuko pamoja,ila wambie wasihofu wewe ni mkulima wa miwa tunakufahamu.

Binafsi naamini kuwa na super powers wawili dunia inakua mahali salama kuliko kuwa na mmoja atakaetupelekesha.

Kuna mahali umegusia kuhusu demokrasia ya India ilivyo wazi na matatizo yanayoikabili ya rushwa nk, na siasa za uchina zisizoruhusu hizo mademokrasia ila wanamaadili bora zaidi ndani ya nchi,binafsi namejifunza kwamba with or without demokrasia tunaweza kusonga.
 
Rejea hotuba ya Putin ya mwaka 2007 huko Ujerumani kwenye kongamano la usalama la kimataifa. Alisema hivi( tafsiri isiyo rasmi), " Russia haina ela ya kutengeneza silaha za bei kubwa kama hiyo project f35 ili ile ulinganifu wa nguvu za kijeshi duniani, baada ya kuona kuna nchi moja inatumia vibaya nguvu zake za kijeshi kuharibu ustawi wa dunia. Lakini lazima Russia ilejeshe ulinganifu huo kwa kutumia mtindo wa Asymmetry ( wanamahesabu watasaidia kufafanua hili). Kwa NATO kuleta silaha za kujilinda karibu na mipaka ya Russia kisa eti ni kujilinda dhidi ya Iran na North Korea hiyo haikubaliki, Russia itatengeneza silaha ya bei rahisi ambayo itaweza kukwepa silaha hizo za kujilinda dhidi ya NATO" mwisho wa kunukuu.

March, 2018 Putini kautangazia ulimwengu kuwa ulinganifu wa nguvu za kijeshi duniani unaelekea kurejeshwa. Silaya ya kukwepa' THAAD ' mitambo nadhani iliyosimikwa Poland na kwingineko ya US tyari Russia kashaipata. Na wamsikilize sasa. Asymmetry hiyo.

US walitengeneza stealth plane ya bei kubwa kabisa...lakini ndege hiyo performance yake ni utata...kudhibitisha hilo, US anagoma kumuuzia Turkey ndege hizo kisa tu Turkey kapanga kununua S400 za Russia...na US hawafichi wanasema hiyo mitambo ita'compromise' ndege hizo...Sasa kama Yuesi(US) alitengeneza stealth plane...kweli inakuwaje anakuwa na wasiwasi na S400!? kuna Stealth plane hapo..kweli?!.hata hivyo ni kukumbushe tu ahadi ya Putin, ya ASYMMETRY...! ahadi hiyo ameifanyia kazi pia kwa stealth plane ya US.
----
Leta hoja nyingine, mkuu kuhusu hili. Karibu.
Hapo naona umechemka,unacho kizungumzia hapo niushabiki mbaya,lakini tukizungumza mambo jinsi yalivyo utagundua kwamba Russia ana woga Fulani ndani mwaka,na tunapojadiliana issue Kama hizi zakisiasa Basi tuwe tunaweka ndani maneno yavitabu vitakatifu. Kitabu kitakatifu biblia ukisoma Daniel 2;31-42 kinaonesha nguvu za marekani.nataka nikuoneshe kidogo kwamba urusi iwe nakiasi Gani cha ndege,iwe Na hizo silaha zakujilinda zidi yamarekani,popotepale,iwe baada yamiaka 100 Russia atakapotangaza Vita namarekani ataangamia tena kwakiasi kikubwa,kwakuwa mandiko matakatifu yanasema Nate atakuwa nanguvu kuliko wote nayeyote Yule atakae jiandaa kumpinga Basi atapondwa pondwa Kama udongo.kwaiyo mrusi machina sijui Na hao wakorea nawaarabu ambao kwasasa wanataabika navikwazo vya kuuza mafuta nje hata wakijikusanya mahali pamoja kumpinga marekani (wayahudi) hawatomweza kwakuwa tayarii yametabiriwa.
 
kama ya kweli haya upo nondo aisee
KISIASA
1. Amesababisha sintofahamu kubwa ndani ya siasa za Marekani hasa kwa Donald Trump.
2. Anavuruga mipango ya Marekani kwa kutumia VETO kule Umoja wa Mataifa.
3. Amefanikiwa kuugawanya Umoja wa Ulaya (Schroeder wa Ujerumani anafanya kazi Rosneft)
4. Anaisaidia Korea Kaskazini kukwepa vikwazo vya Umoja wa Mataifa.
5. Alimsaidia Raisi wa Uturuki asipinduliwe na kuuwawa ambapo inasemekana CIA walihusika sana.
6. Amemtunza Edward Snowden ambaye kavujisha siri nyeti za Marekani.

KIJESHI
1. Kavamia Ukraine kijeshi na kumega Crimea kwa nguvu mno ya wanajeshi 70,000.
2. Kavuruga mpango wa Marekani na Israel wa kuvamia Syria na kumtoa Assad.
3. Anauza silaha nzito kwa mataifa hasimu wa Marekani kama Iran.
4. Anasidia Korea Kaskazini kukwepa vikwazo vya Umoja wa Mataifa.
5. Amevuruga majimbo ya Lugansk na Donestky hadi leo majeshi ya Ukraine hayana amani.
7. Yeye ndiyo mwenye jeshi la pili kwa ubora hapa duniani mbali na shida zote kiuchumi.

KITEKNOLOJIA
1. Marekani mpaka leo anategemea injini kutoka Urusi kwa ajili ya kurusha roketi zake.
2. Ametengeneza makombora mazito ambayo yanasafiri mara 10 zaidi ya sauti.
3. Walimwekea vikwazo vya injini za ndege kutoka Ukraine lakini katengeneza zake kwa haraka sana.
4. Ana wasomi wa sayansi ambao ni World Class kama 1,000,000 hivi.
5. Teknolojia ya kimtandao (Cyber Technology) yuko mbele sana na amethibitishia dunia mara nyingi.

KIUCHUMI
1. Amefanikiwa kutumia makampuni yake ya nishati kuwaumiza Ulaya hasa NORD Stream 2.
2. Amefanikiwa kutumia ushawishi wa nishati kuyavuta karibu mataifa kama Uchina, India na Uturuki.
3. Uturuki ameagiza silaha kutoka Urusi kitu ambacho kitampa faida za kiuchumi Mrusi.
4. Saudi Arabia ametengeneza viwanda vya Kalashnikov Ak-47 nchini kwake na Urusi karuhusu.
5. Amesaidia kutengeneza vyombo kama BRICS, The Shanghai Cooperation na Eurasia Economic Union

NB: Haya ni machache tu, sasa nchi iliyosambaratika inalisumbuaje taifa kubwa duniani ??
 
Pot Malcom Lumumba aka Prof Mwandosya aka Ndugai tuko pamoja,ila wambie wasihofu wewe ni mkulima wa miwa tunakufahamu.

Binafsi naamini kuwa na super powers wawili dunia inakua mahali salama kuliko kuwa na mmoja atakaetupelekesha.

Kuna mahali umegusia kuhusu demokrasia ya India ilivyo wazi na matatizo yanayoikabili ya rushwa nk, na siasa za uchina zisizoruhusu hizo mademokrasia ila wanamaadili bora zaidi ndani ya nchi,binafsi namejifunza kwamba with or without demokrasia tunaweza kusonga.
Kwahiyo mimi ni Mwandosya ?
Kufananishwa na moja kati ya watu wenye akili sana hapa nchini kwangu ni sifa njema kweli. Japo bahati mbaya sana maishani mwangu mwote mimi sijawahi kuwa mwanasiasa tena wa CCM.
 
Nimequote wananzengo wanavyokuita humu mkuu Le prof Malcom Lumumba,but since unaitwa majina mazito ya hawa jamaa ingawa wako ccm hii ni dalili nzuri kwako mkuu.
 
If you ask about Russia economy, you will be told it is the same size as Italy. Yet, Russia not only is a nuclear superpower, it manufactures its own rockets, airplanes, ships, submarines, power stations...

USA depends a lot on Russia in their space programs. Yaani, Russia iko mbele ya marekani mambo ya satellite. Hebu soma mambo ya Kinzal missile uelewe vile Urusi iko mbele mambo ya teknologia.
 
Ivi mtu akisema bila Putin tutegemee kuona Urusi dhaifu atakuwa yuko sahihi? Au Urusi ilivyo ni matokeo ya sera za Putin na kwa sasa hajaonekana wa kumrithi ndani ya Urusi ni sawa? Au Putin =Urusi?
Russia was a global power even before Putin was born, before the soviet union placed the first man in space. And yes even before America was a country.....
 
Back
Top Bottom