Education Mentor
JF-Expert Member
- Oct 26, 2016
- 396
- 687
Sawa kabisa mkuu uko sawa,
Lakini unadhani ni sawa kabisa kwa hatma ya nchi ndogo kuamuliwa na mataifa makubwa ???
Nadhani Urusi na Pakistan wanashirikiana tu, lakini hawana umoja wa kujihami kijeshi. Nazungumza hivi kwasababu ya mahusiano makubwa ya Kihistoria baina ya India (Adui mkubwa wa Pakinstan) na Urusi. Nakumbuka vita ya mwaka mwaka 1971 baina ya India na Pakistan USSR alikuwa upande wa India huku Uchina akiwa upande wa Pakistan. Pia miaka 1970's Pakistan aliwasaidia sana Wamarekani na Mujahedeen kuua maelfu ya Warusi nchini Afghanistan. Hawa ni washirika tu lakini hawana umoja: Mwaka 2001 Iran ndiyo ilimsaidia Marekani kuvamia Afghanistan na kuwatoa Taliban lakini mwaka 2003 wakawa maadui.
NB: Huu ni ushirika wa kimaslahi tu na utapita....
Kweli mkuu duniani hakuna urafiki wa kweli baina ya nchi changa na mabepali huwa haitokei ni kimasirahi zaidi