Swali gumu kidogo: Kwanini Urusi iliyosambaratika na dhaifu kuliko USSR inawasumbua sana NATO?

MALCOM LUMUMBA

JF-Expert Member
Jul 26, 2012
20,897
63,783
Umoja wa Kisovieti (USSR au CCCP) taifa lililozaliwa mwaka 1922-1991, lilikuwa ni moja ya taifa lenye nguvu sana duniani lakini lenye mwisho mbaya sana ambao ni aibu kwa watu wake mpaka leo.

Kiuchumi walikuwa wana nguvu sana, kiteknolojia walikuwa mbele, nguvu kubwa ya viwanda, kijeshi walikuwa mbele na mifumo yao ya kitamaduni iliyotokana na ukomunisti ilishawishi dunia kuanzia barani Marekani, Asia hadi Afrika na kubwa ziadi walikuwa na idadi kubwa sana ya watu ambapo takwimu zinasema kwamba walikuwa ni milioni 293.

Lakini baada ya kusambaratika nchi hii ilipoteza kila kitu ambacho ilikuwa nacho kuanzia Idadi ya watu, jeshi, viwanda na teknolojia maana kila nchi iliondoka na watu wake, majeshi yake na sehemu kama Ukraine ikapata viwanda vya bure kabisa, Poland na Georgia nao hawakuwa nyuma kabisa. Ikawa nchi dhaifu na masikini kweli.

Sasa najiuliza kwanini taifa hili dhaifu ambalo lililoshindwa vita baridi linaendelea kumsumbua Marekani (The Only Super Power) pamoja na washirika wake kijeshi ambao ni zaidi ya 25?

CC: chige , FisadiKuu
 
Sasa najiuliza kwanini taifa hili dhaifu ambalo lililoshindwa vita baridi linaendelea kumsumbua Marekani (The Only Super Power) pamoja na washirika wake kijeshi ambao ni zaidi ya 25 ???
Ni vyema ungedadavua, hili taifa linamsumbua Marekani kivipi na katika nyanja ipi? Uchumi? Technology? Nguvu ya ushawishi? Ama una maanisha nini. Hapo sijapaepewa mkuu. Weka mambo sawa.
 
Ni vyema ungedadavua, hili taifa linamsumbua Marekani kivipi na katika nyanja ipi? Uchumi? Technology? Nguvu ya ushawishi? Ama una maanisha nini. Hapo sijapaepewa mkuu. Weka mambo sawa.

KISIASA
1. Amesababisha sintofahamu kubwa ndani ya siasa za Marekani hasa kwa Donald Trump.
2. Anavuruga mipango ya Marekani kwa kutumia VETO kule Umoja wa Mataifa.
3. Amefanikiwa kuugawanya Umoja wa Ulaya (Schroeder wa Ujerumani anafanya kazi Rosneft)
4. Anaisaidia Korea Kaskazini kukwepa vikwazo vya Umoja wa Mataifa.
5. Alimsaidia Raisi wa Uturuki asipinduliwe na kuuwawa ambapo inasemekana CIA walihusika sana.
6. Amemtunza Edward Snowden ambaye kavujisha siri nyeti za Marekani.

KIJESHI
1. Kavamia Ukraine kijeshi na kumega Crimea kwa nguvu mno ya wanajeshi 70,000.
2. Kavuruga mpango wa Marekani na Israel wa kuvamia Syria na kumtoa Assad.
3. Anauza silaha nzito kwa mataifa hasimu wa Marekani kama Iran.
4. Anasidia Korea Kaskazini kukwepa vikwazo vya Umoja wa Mataifa.
5. Amevuruga majimbo ya Lugansk na Donestky hadi leo majeshi ya Ukraine hayana amani.
7. Yeye ndiyo mwenye jeshi la pili kwa ubora hapa duniani mbali na shida zote kiuchumi.

KITEKNOLOJIA
1. Marekani mpaka leo anategemea injini kutoka Urusi kwa ajili ya kurusha roketi zake.
2. Ametengeneza makombora mazito ambayo yanasafiri mara 10 zaidi ya sauti.
3. Walimwekea vikwazo vya injini za ndege kutoka Ukraine lakini katengeneza zake kwa haraka sana.
4. Ana wasomi wa sayansi ambao ni World Class kama 1,000,000 hivi.
5. Teknolojia ya kimtandao (Cyber Technology) yuko mbele sana na amethibitishia dunia mara nyingi.

KIUCHUMI
1. Amefanikiwa kutumia makampuni yake ya nishati kuwaumiza Ulaya hasa NORD Stream 2.
2. Amefanikiwa kutumia ushawishi wa nishati kuyavuta karibu mataifa kama Uchina, India na Uturuki.
3. Uturuki ameagiza silaha kutoka Urusi kitu ambacho kitampa faida za kiuchumi Mrusi.
4. Saudi Arabia ametengeneza viwanda vya Kalashnikov Ak-47 nchini kwake na Urusi karuhusu.
5. Amesaidia kutengeneza vyombo kama BRICS, The Shanghai Cooperation na Eurasia Economic Union

NB: Haya ni machache tu, sasa nchi iliyosambaratika inalisumbuaje taifa kubwa duniani ??
 
Sasa najiuliza kwanini taifa hili dhaifu ambalo lililoshindwa vita baridi linaendelea kumsumbua Marekani (The Only Super Power) pamoja na washirika wake kijeshi ambao ni zaidi ya 25 ???
Wanasema umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu, lakini hili haliko applicable muda wote. Kuna muda unaweza kuwa peke yako na ukafanya mambo yako kwa ufanisi mkubwa.
 
Wanasema umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu, lakini hili haliko applicable muda wote. Kuna muda unaweza kuwa peke yako na ukafanya mambo yako kwa ufanisi mkubwa.
NATO kwa pamoja wana idadi ya watu milioni 603.73.
URUSI peka yake ana idadi ya watu milioni 144.3.
NB: NATO ina watu mara sita zaidi ya Urusi lakini kwanini iwasumbue ??
 
USSR kweli ilimeguka na kudondoka, lakini tusisahau kuwa USSR ilibebwa na mambo yote yaliratibiwa huko Russia, hivyo hata baada ya kuvunjika Russia ilibaki na mambo yote,si kwamba ilisambaratika kabisa kama tunavyoona ila bali bado vyombo vyake viliwndelea kufanya kazi, warusi ni watu ambao sisi tunaona kama wazungu lakini wao wako tofauti kabisa na wazungu. Wakati Ulaya na marekani walikuwa wanaamini russia imekufa lakini rusia yenyewe ilikuwa inahangaika kuhakikisha inanyanyuka, ndo hapo alipokuja kutokea mtu kama Putin, Putin kainyanyua russia muda mfupi sana, si kwasababu ana miujiza ila ni kwasababu walikuwa na kila kitu kasoro kiongozi tu wa kusimamia kukua kwa uchumi wa russia.

Kwanini NATO wanaihofia Russia?
Kwanza warusi ni watu wenye akili nyingi sana, hakuna kitu wanaweza panga wasishindwe kufanya, hivyo kwenye nyanja ya rasilimali watu ipo vizuri ina wasomi wa kutosha na wabunifu kwenye sekta zote kuanzia za ulinzi afya, na technolojia nyingine, kwahiyo NATO inawaogopa kwasababu wana uwezo wa kufanya chochote kwa akili na elimu zao walizonazo.

Wana technolojia, hapo nimekueleza kuwa wana akili na ni wasomi, sasa hivi vyote inawafanya wawe ni wavumbuzi wakubwa wa twchnolojia duniani,moja kati ya maeneno ambayo wamewekeza sana ni kwenye technolojia ya vita, huko hawa watu wana dhana za technolojia ya hali ya juu, wanaweza kupigana na yoyote aliyepopote pasipo hata wao kwenda, wanadhana za kinyuklia zenye uwezo mkubwa sana, wanamfumo mzuri wa mawasiliano pia ndio mabingwa wanaoendesha kituo cha anga cha kimataifa kwa sehemu kubwa, ikumbukwe kuwa maarifa ya anga za mbali urusi inashindana kwa karibu na marekani kuliko taifa lolote.

Urusi ina hadhina kubwa ya mariasili karibia zote duniani,nadhani ndiyo inaongoza kuwa na hiyo hadhina,kwa utajili walionao NATO wanajua kabisa wakimuacha atumie huo utajili kujiendeleza basi wameumia, nimekuambia awali hawa watu wana akili na ni wabunifu, hivyo wanachokosa wao ni uchumi tu wa kusaidia kufanya mambo yao, ana gesi ambayo ulaya nzima wanamtegemea yeye tu, ni miongoni mwa wazalishaji wakubwa wa mafuta na mengine mengi. Kwa hizi rasilimali tu anatoa hofu tosha kwa NATO

Wana jwshi imara, jesho lao ni kubwa sana, ni la pili duniani baada ya lile la marekani,jeshi hili kama nilivyoeleza hapo juu lina dhana za kila aina na lina technolojia kubwa,warusi wanajua kuwa wako hatarini kwahiyo wanawekeza sana kwenye jeshi lao, japo bajeti yao ni ndogo kushinda ya marekani lakini wanafanya ma,bo makubwa sana, uimara wa jeshi hili ni tishio kubwa sana kwa NATO

Uongozi mathubuti, hawa watu kumpata Putin walikula bingo sana, huyu Putin ni mpelelezi mstaafu aliyepikwa na akaiva enzi za KGB, huyu kafanya sana kazi Ujerumani hivyo anawajua wamagharibi nje ndani, ni kiongozi wenye misimamo isiyoyumba,ni kiongozi ambaye anatamani urusi iwe kama zamani, hivyo anaimarisha sana nguvu za urusi ili iwe na ushawishi kimataifa kwa kila jambo, uwepo wa huyu mtu ni tishio tosha kwa NATO.

Historia inawalinda, warusi historia pia inawalinda maana walishawahi kuwa wakubwa wa dunia, vita vya pili ni wao ndo waliompigs mjerumani, wana historia ndefu ya ubabe toka enzi hivyo historia hiyo inawalinda na kuwabeba kitambo na kufanya mataifa mengine waiogope.

Yako mengi ila naomba niishie hapo kwa leo
 
Urusi ina hadhina kubwa ya mariasili karibia zote duniani,nadhani ndiyo inaongoza kuwa na hiyo hadhina,kwa utajili walionao NATO wanajua kabisa wakimuacha atumie huo utajili kujiendeleza basi wameumia, nimekuambia awali hawa watu wana akili na ni wabunifu, hivyo wanachokosa wao ni uchumi tu wa kusaidia kufanya mambo yao, ana gesi ambayo ulaya nzima wanamtegemea yeye tu, ni miongoni mwa wazalishaji wakubwa wa mafuta na mengine mengi....kwa hizi rasilimali tu anatoa hofu tosha kwa NATO

Wana jwshi imara, jesho lao ni kubwa sana, ni la pili duniani baada ya lile la marekani,jeshi hili kama nilivyoeleza hapo juu lina dhana za kila aina na lina technolojia kubwa,warusi wanajua kuwa wako hatarini kwahiyo wanawekeza sana kwenye jeshi lao, japo bajeti yao ni ndogo kushinda ya marekani lakini wanafanya ma,bo makubwa sana, uimara wa jeshi hili ni tishio kubwa sana kwa NATO

Yako mengi ila naomba niishie hapo kwa leo

Ahsante sana mkuu,
Sasa kama Urusi alikuwa na nguvu nyingi zaidi ya hizi za leo kwanini alishindwa Vita Baridi ??
Katika mantiki hii unataka kuniambia kwamba Urusi ya zamani ilikuwa na nguvu kuliko Marekani ??
 
Vita baridi ilikuwa ni vita kubwa sana, ilikuwa ni vita ya kueneza itikadi na kutafutwa kuungwa mkono ulimwenguni baina ya magharibi na mashariki, sasa basi pata picha dunia yote hii baba wa ujamaa na mwenezaji mkuu na mfadhili mkuu wa nchi zote za kijamaa alikuwa ni Urusi,wakati mfadhili na muenezaji mkuu wa ubepari zilikuwa nchi za magharibi pamoja na marekani, hapo utaona ni mzigo mkubwa ambao alikuwa nao urusi na ulihitaji zaidi fedha nyingi na uchumi mkubwa.

Kutokana na kuangalia zaidi mataifa ya nje aliyokuwa anayafadhili akasahau kuimarisha ndani mwake, yaani hakuweka sana mkazo kuyaimarisha maeneo yake mwenyewe, mwishowe watu wakachoka maana waliona muungano wao hauna faidi,iliyonufaika ni moscow na mataifa ya nje, kutokana na hili kwahiyo akawa na maadui wa nje na akazalisha wasaliti wa ndani waliochoshwa na mzigo wa kuzifadhili nchi nyingine. Hapo ndipo kasi ya anguko lake ilipoongezeka.

Ni kweli kabisa, urusi iliwahi kuwa na nguvu nyingi kushinda marekani marekani ilianza kuonekana kwenye uso wa dunia kuwa ina nguvu baada ya vita vya pili vya dunia lakini kabla ya hapo hakuna aliyeiwaza na kuiogopa marekani, mataifa yenye nguvu yalitokea ulaya kama ufaransa,uingereza na ujerumani, ukiyatoa hayo kukawa kuna urusi na japani, ndio maana unaona urusi ina eneo kubwa kuliko nchi zote mpaka leo hii, hiyo inadhihirisha ni jinsi gani aliweza kutanua himaya yake na kuilinda....maana kutanua himaya ni suala la kumpiga mwenzio na kumnyang'anya ardhi na kuhakikisha kila kiapnde cha ardhi hakikuponyoki.

Kwa faida ya wote ni kwamba nchi za magharibi zinaamini mpaka kesho wakifanikiwa tu kumshusha urusi na kumtawala wamefanikiaa kuitawala dunia, hivyo mipango yao ya muda mrefu ni kuiangusha urusi ili wasiwe na kizingiti chochote duniani,maana watakuwa wamepata rasilimali kubwa sana
 
70% ya populayion ya NATO ni US

Sent using Jamii Forums mobile app
Vyovyote vile, lakini kikawaida watu milioni 600 kutoka nchi tofauti zenye teknolojia na utajiri mwingi ni hatari kuliko watu milioni 144 kutoka taifa moja. Raisi wa zamani wa Singapore Lee Kuan Yew alishawahi kusema maneno haya " wakati Uchina inategemea kutumia vipaji wa vya watu wake Bilioni 1, Marekani inategemea kutumia vipaji vya watu Bilioni 7 kutoka duniani kote" hii imetokana na mifumo ambayo Marekani kajitengenezea kuruhusu watu toka sehemu mbalimbali za dunia kuijenga. Sasa hapa nchi vipaji vya watu Milioni 600 utalinganishaje na watu Milioni 144 ???
 
Kwa faida ya wote ni kwamba nchi za magharibi zinaamini mpaka kesho wakifanikiwa tu kumshusha urusi na kumtawala wamefanikiaa kuitawala dunia, hivyo mipango yao ya muda mrefu ni kuiangusha urusi ili wasiwe na kizingiti chochote duniani,maana watakuwa wamepata rasilimali kubwa sana

Hichi ulichokizungumzia hapa kinaitwa The Heartland Theory au Nadharia ya moyo wa dunia.
Iliandikwa mara ya kwanza kabisa na mwanasayansi wa siasa kutoka Uingereza aitwaye Sir Halford McKinder ambaye mwaka 1904 alisema kwamba kama taifa litafanikiwa kutawala eneo la Ulaya Mashariki na Asia (Eurasia) basi litatawala Ulaya yote na Asia. Aliyaandika haya kwenye chapisho lake liitwalo The Geographical Pivot of History na akasema kutokana na utajiri wa rasilimali wa eneo hilo taifa lolote litakalotawala Ufalme wa Urusi basi linaweza tawala dunia.

Ikumbukwe Urusi ndiyo nchi inayoongoza kwa wingi wa rasilimali zenye thamani ya dola za kimarekani trilioni 75. Marekani na ujanja wake wote ana rasilimali zenye thamani ya dola za kimarekani trilioni 45, hivyo Urusi kama ikisambaratika nchi nyingi za Ulaya zinaweza kunufaika sana na utajiri wake.

Wanahistoria wanaamini kwamba moja ya sababu kubwa za Adolf Hitler kuvamia Urusi mwaka 1941 kabla ya nchi nyingine zote ni kwasababu Wanazi waliamini kwenye The Heartland Theory kwamba kama watampiga Urusi mapema basi watatumia rasilimali zake zote kuipiga dunia yote na ndiyo maana mataifa ya Ulaya na Marekani ikabidi watume msaada wa kipesa kwa Urusi. Hata baada ya vita ya dunia kuisha, Vita Baridi ilichangiwa sana na hii nadharia ambayo Waingereza na Wamarekani iliwakaa sana kichwani.

Vita baridi ilikuwa ni vita kubwa sana, ilikuwa ni vita ya kueneza itikadi na kutafutwa kuungwa mkono ulimwenguni baina ya magharibi na mashariki, sasa basi pata picha dunia yote hii baba wa ujamaa na mwenezaji mkuu na mfadhili mkuu wa nchi zote za kijamaa alikuwa ni Urusi,wakati mfadhili na muenezaji mkuu wa ubepari zilikuwa nchi za magharibi pamoja na marekani, hapo utaona ni mzigo mkubwa ambao alikuwa nao urusi na ulihitaji zaidi fedha nyingi na uchumi mkubwa.

Tatizo la Urusi la anguko la Urusi ya Kisovieti lilikuwa siyo kusaidia mataifa mengine lakini mfumo wake mbovu na kukataa kubadilika kwa viongozi wa Kisovieti hasahasa wale kama Leonid Brezhnev. Tukisema kwamba tatizo ni kusaidia mataifa mengine tutakuwa tunasahau kitu cha muhimu sana kwamba hata Marekani naye alisaidia sana mataifa mengi sana duniani tena kwa nguvu nyingi sana kuliko hata Urusi.

Wakati Urusi alikuwa ana washirika wa Kijeshi wa Ulaya tu kupitia The Warsaw Pact, Marekani alikuwa na washirika wa kijeshi dunia nzima Kuanzia NATO, ANZUS, SEATO hadi CENTO. Mpaka leo Marekani ana mikataba ya ulinzi kama 60 hivi.

Misaada ya kiuchumi wote walitoa huku Marekani akianza na The Marshal Plan huku wasovieti wakija na The COMECON. Wote walisomesha watu huko Harvard, Yale, Moscow State University na University of St.Petersburg lakini Urusi aliachwa mbali sana. Kwanini ?? Mfumo mbovu wa kiuchumi au kuruhusu serikali kutawala uchumi kwa kila kitu (Command or Centralization of Economy). Uchumi wa Urusi haukuruhusu ushindani wa ndani ya nchi, wakati Marekani makampuni binafsi yalikuwa yanazalisha bidhaa na kupunguzia serikali mzigo. Uchina chini ya Deng Xiapoing waligundua hili mapema ndiyo wakaruhusu mfumo wa masoko utawale nchi. Hivyo hapa sikubaliani na wewe kidogo mkuu wangu kwasababu kama kusaidia wote walisaidia mataifa ya nje kwa sana tu.

Ni kweli kabisa, urusi iliwahi kuwa na nguvu nyingi kushinda marekani marekani ilianza kuonekana kwenye uso wa dunia kuwa ina nguvu baada ya vita vya pili vya dunia lakini kabla ya hapo hakuna aliyeiwaza na kuiogopa marekani, mataifa yenye nguvu yalitokea ulaya kama ufaransa,uingereza na ujerumani, ukiyatoa hayo kukawa kuna urusi na japani, ndio maana unaona urusi ina eneo kubwa kuliko nchi zote mpaka leo hii, hiyo inadhihirisha ni jinsi gani aliweza kutanua himaya yake na kuilinda....maana kutanua himaya ni suala la kumpiga mwenzio na kumnyang'anya ardhi na kuhakikisha kila kiapnde cha ardhi hakikuponyoki.

Hapa nakubaliana na wewe kwamba Urusi alikuwa na nguvu sana hadi kutanua lile eneo lake lote. Alifanya hivyo kwenye Vita Baridi ya kwanza aliyopigana na Muingereza tokea mwaka 1813 hadi 1907 ambayo iliitwa kama The Great Game au The Tournament of Shadows. Lakini naomba nikukosea kidogo hapo uliposema Marekani alikuwa hana nguvu: Nifahamuvyo mimi mpaka kufika mwaka 1916 Ujerumani alikuwa ameshashinda vita ya kwanza ya dunia na Muingereza alikuwa anajiandaa kusalimu amri, lakini aliyebadilisha mwelekeo ule wote ni Marekani chini ya Prof. Woodrow Wilson.

Mbali na hapo ikumbukwe kwamba Ujerumani alipanga kumvamia Marekani mwaka 1897 na Mfalme Kaiser Wilhelm alimtuma Ebenhard Von Mantey kupanga uvamizi kwa kutuma wanajeshi 100,000 lakini mpango huu ulikufa baada ya Marekani kuonesha nguvu zake kwa kumtwanga vibaya Mhispania kwenye vita ya mwaka 1898 (The Spanish American War)na kumnyang'anya CUBA na makoloni yake muhimu. Hapa utasemaje Marekani alikuwa hana nguvu ???

Unahisi Uingereza angeshinda Vita ya kwanza ya dunia dhidi ya Ujerumani bila Marekani kuingilia kati ?
Pia tusisahau kwamba Urusi ilisalimu amri mapema sana kutoka kwa Ujerumani wakati wa vita ya kwanza ya dunia hadi wakina Lenini wakasaini Mkataba wa hovyo kabisa wa Brest-Litovsk ambao ulikubali kumruhusu Ujerumani achukue sehemu za Urusi kama Poland, Estonia, Finland, Latvia, Ukraine na Lithuania. Bila Marekani kuingia kwenye vita uandhani haya maeneo yangerudi kirahisi ?

CC: Wick , muyovozi , MASAMILA , neo1
 
USSR kweli ilimeguka na kudondoka, lakini tusisahau kuwa USSR ilibebwa na mambo yote yaliratibiwa huko Russia, hivyo hata baada ya kuvunjika Russia ilibaki na mambo yote,si kwamba ilisambaratika kabisa kama tunavyoona ila bali bado vyombo vyake viliwndelea kufanya kazi,warusi ni watu ambao sisi tunaona kama wazungu lakini wao wako tofauti kabisa na wazungu.wakati ulaya na marekani walikuwa wanaamini russia imekufa lakini rusia yenyewe ilikuwa inahangaika kuhakikisha inanyanyuka, ndo hapo alipokuja kutokea mtu kama Putin, putin kainyanyua russia muda mfupi sana,si kwasababu ana miujiza ila ni kwasababu walikuwa na kila kitu kasoro kiongozi tu wa kusimamia kukua kwa uchumi wa russia.

Kwanini NATO wanaihofia Russia?
Kwanza warusi ni watu wenye akili nyingi sana, hakuna kitu wanaweza panga wasishindwe kufanya, hivyo kwenye nyanja ya rasilimali watu ipo vizuri ina wasomi wa kutosha na wabunifu kwenye sekta zote kuanzia za ulinzi afya, na technolojia nyingine, kwahiyo NATO inawaogopa kwasababu wana uwezo wa kufanya chochote kwa akili na elimu zao walizonazo.
Wana technolojia, hapo nimekueleza kuwa wana akili na ni wasomi, sasa hivi vyote inawafanya wawe ni wavumbuzi wakubwa wa twchnolojia duniani,moja kati ya maeneno ambayo wamewekeza sana ni kwenye technolojia ya vita,huko hawa watu wana dhana za technolojia ya hali ya juu, wanaweza kupigana na yoyote aliyepopote pasipo hata wao kwenda, wanadhana za kinyuklia zenye uwezo mkubwa sana,wanamfumo mzuri wa mawasiliano pia ndio mabingwa wanaoendesha kituo cha anga cha kimataifa kwa sehemu kubwa, ikumbukwe kuwa maarifa ya anga za mbali urusi inashindana kwa karibu na marekani kuliko taifa lolote.

Urusi ina hadhina kubwa ya mariasili karibia zote duniani,nadhani ndiyo inaongoza kuwa na hiyo hadhina,kwa utajili walionao NATO wanajua kabisa wakimuacha atumie huo utajili kujiendeleza basi wameumia, nimekuambia awali hawa watu wana akili na ni wabunifu, hivyo wanachokosa wao ni uchumi tu wa kusaidia kufanya mambo yao, ana gesi ambayo ulaya nzima wanamtegemea yeye tu, ni miongoni mwa wazalishaji wakubwa wa mafuta na mengine mengi....kwa hizi rasilimali tu anatoa hofu tosha kwa NATO

Wana jwshi imara, jesho lao ni kubwa sana, ni la pili duniani baada ya lile la marekani,jeshi hili kama nilivyoeleza hapo juu lina dhana za kila aina na lina technolojia kubwa,warusi wanajua kuwa wako hatarini kwahiyo wanawekeza sana kwenye jeshi lao, japo bajeti yao ni ndogo kushinda ya marekani lakini wanafanya ma,bo makubwa sana, uimara wa jeshi hili ni tishio kubwa sana kwa NATO

Uongozi mathubuti, hawa watu kumpata Putin walikula bingo sana, huyu Putin ni mpelelezi mstaafu aliyepikwa na akaiva enzi za KGB, huyu kafanya sana kazi ujerumani hivyo anawajua wamagharibi nje ndani, ni kiongozi wenye misimamo isiyoyumba,ni kiongozi ambaye anatamani urusi iwe kama zamani, hivyo anaimarisha sana nguvu za urusi ili iwe na ushawishi kimataifa kwa kila jambo, uwepo wa huyu mtu ni tishio tosha kwa NATO.

Historia inawalinda, warusi historia pia inawalinda maana walishawahi kuwa wakubwa wa dunia,vita vya pili ni wao ndo waliompigs mjerumani, wana historia ndefu ya ubabe toka enzi hivyo historia hiyo inawalinda na kuwabeba kitambo na kufanya mataifa mengine waiogope.

Yako mengi ila naomba niishie hapo kwa leo
Mwelekeo wa uzi umenifanya niwaze nini kingetokea Hans Kitine kama yule mstaafu mwenye hadhi kama ya Putin angekuwa ndo rais wa JMT
 
Umoja wa Kisovieti (USSR au CCCP) taifa lililozaliwa mwaka 1914-1991,
Lilikuwa ni moja ya taifa lenye nguvu sana duniani lakini lenye mwisho mbaya sana ambao ni aibu kwa watu wake mpaka leo. Kiuchumi walikuwa wana nguvu sana, kiteknolojia walikuwa mbele, nguvu kubwa ya viwanda, kijeshi walikuwa mbele na mifumo yao ya kitamaduni iliyotokana na ukomunisti ilishawishi dunia kuanzia barani Marekani, Asia hadi Afrika na kubwa ziadi walikuwa na idadi kubwa sana ya watu ambapo takwimu zinasema kwamba walikuwa ni milioni 293.

Lakini baada ya kusambaratika nchi hii ilipoteza kila kitu ambacho ilikuwa nacho kuanzia Idadi ya watu, jeshi, viwanda na teknolojia maana kila nchi iliondoka na watu wake, majeshi yake na sehemu kama Ukraine ikapata viwanda vya bure kabisa, Poland na Georgia nao hawakuwa nyuma kabisa. Ikawa nchi dhaifu na masikini kweli....

Sasa najiuliza kwanini taifa hili dhaifu ambalo lililoshindwa vita baridi linaendelea kumsumbua Marekani (The Only Super Power) pamoja na washirika wake kijeshi ambao ni zaidi ya 25?

Lakini baada ya kusambaratika nchi hii ilipoteza kila kitu ambacho ilikuwa nacho kuanzia Idadi ya watu, jeshi, viwanda na teknolojia maana kila nchi iliondoka na watu wake, majeshi yake na sehemu kama Ukraine ikapata viwanda vya bure kabisa, Poland na Georgia nao hawakuwa nyuma kabisa. Ikawa nchi dhaifu na masikini kweli.

Baada ya kusambaratika kwa Soviet Union siyo kweli kwamba kila kitu kilipotea...Mambo mengi yaliridhiwa na Russia federation ambayo ndiyo iliyokuwa kubwa kuliko karibu nchi au jamhuri zote 16 zilizounda USSR...silaha za nyuklia zilimilikiwa na Russia n ikweli kiuchumi karibu asilimia 40 ilipotea, watu karibu asilimia 30 hivi na kadhalika lakini bado Russia ndiyo iliyokuwa mhimili wa USSR ilibaki..vijamhuri kama Georgia vilikuwa na watu karibu milioni 4 tu, Lithunia, Estonia na Lativia karibu milioni mbili tu. Lakini Russia ilikuwa na watu karibu milioni 140.

Russia ndiyo nchi yote kubwa duniani, ina raslimali nyingi na hasa gas na mafuta na pia teknolojia. Russia sasa imepata kiongozi thabiti PUTIN ambaye alikuwa ni jasusi (KGB) na hivyo kuwa well informed na masuala mengi ya dunia na namna USSR ilivyosambaratika. PUTIN amewaweka marafiki zake wa iliyokuwa KGB kwenye madaraka ya nchi na wanajua mengi. PUTIN alichofanya ni kujenga ndani ya RUSSIA suala la nationalism au uzalendo amevivunja vi- NGO vya nchi za magharibi ambavyo huanzishwa kwa kisingizio cha demokrasia kumbe ni wakala wa ubepari na maslahi ya nchi hizo.
 
KISIASA
1. Amesababisha sintofahamu kubwa ndani ya siasa za Marekani hasa kwa Donald Trump.
2. Anavuruga mipango ya Marekani kwa kutumia VETO kule Umoja wa Mataifa.
3. Amefanikiwa kuugawanya Umoja wa Ulaya (Schoeder wa Ujerumani anafanya kazi Rosneft)
4. Anaisaidia Korea Kaskazini kukwepa vikwazo vya Umoja wa Mataifa.
5. Alimsaidia Raisi wa Uturuki asipinduliwe na kuuwawa ambapo inasemekana CIA walihusika sana.
6. Amemtunza Edward Snowden ambaye kavujisha siri nyeti za Marekani.

KIJESHI
1. Kavamia Ukraine kijeshi na kumega Crimea kwa nguvu mno ya wanajeshi 70,000.
2. Kavuruga mpango wa Marekani na Israel wa kuvamia Syria na kumtoa Assad.
3. Anauza silaha nzito kwa mataifa hasimu wa Marekani kama Iran.
4. Anasidia Korea Kaskazini kukwepa vikwazo vya Umoja wa Mataifa.
5. Amevuruga majimbo ya Lugansk na Donestky hadi leo majeshi ya Ukraine hayana amani.
7. Yeye ndiyo mwenye jeshi la pili kwa ubora hapa duniani mbali na shida zote kiuchumi.

KITEKNOLOJIA
1. Marekani mpaka leo anategemea injini kutoka Urusi kwa ajili ya kurusha roketi zake.
2. Ametengeneza makombora mazito ambayo yanasafiri mara 10 zaidi ya sauti.
3. Walimwekea vikwazo vya injini za ndege kutoka Ukraine lakini katengeneza zake kwa haraka sana.
4. Ana wasomi wa sayansi ambao ni World Class kama 1,000,000 hivi.
5. Teknolojia ya kimtandao (Cyber Technology) yuko mbele sana na amethibitishia dunia mara nyingi.

KIUCHUMI
1. Amefanikiwa kutumia makampuni yake ya nishati kuwaumiza Ulaya hasa NORD Stream 2.
2. Amefanikiwa kutumia ushawishi wa nishati kuyavuta karibu mataifa kama Uchina, India na Uturuki.
3. Uturuki ameagiza silaha kutoka Urusi kitu ambacho kitampa faida za kiuchumi Mrusi.
4. Saudi Arabia ametengeneza viwanda vya Kalashnikov Ak-47 nchini kwake na Urusi karuhusu.
5. Amesaidia kutengeneza vyombo kama BRICS, The Shanghai Cooperation na Eurasia Economic Union

NB: Haya ni machache tu, sasa nchi iliyosambaratika inalisumbuaje taifa kubwa duniani ??
Tatizo la ya tilt ya power sasa hivi ni European Union, umoja wa ulaya unazidi kupata nguvu kuliko Marekani. Wanazidi kupata nguvu ya kiuchumi na hili ni tatizo kwa Marekani. Ndio maana kukawa na Brexit ili kudhoofisha umoja wa ulaya kwasababu Uingereza ni mdau muhimu sana wa Ulaya lakini ni sworn ally wa Marekani. Hata juzi Merkel na Trump walipokutana, 45 alikua anamwambia Germany ifanye biashara na USA kama mara tano hivi kwenye press conference lakini Merkel mara zote tano alisema Marekani ifanye biashara na umoja wa ulaya (sio na German).

Nchi zote za Ulaya zilikua dhaifu kiuchumi baada ya vita ya pili ya dunia, pale ndipo Uingereza alituma ujumbe kwa serikali ya Marekani kuwaambia kwamba Uingereza haina nguvu ya kulinda ugiriki tena kuingia kwenye ushawishi wa kisoshalisti wa USSR (Soviet imperialism). Na Marekani akaanza kuzikopesha nchi za Ulaya na kusaidia kupunguza Soviet imperialism. Sasa European Union ikipata nguvu na kuamua kumkaribisha mrusi mezani kufanya biashara na kua nae pamoja, ndio utakua mwisho wa Marekani kua nchi yenye nguvu duniani.

Mrusi anamjambisha USA kwasababu ya European Union kupata nguvu, ila head to head Marekani anaujua sana uchumi kuliko Russia na ndo udhaifu wa Russia ulipo.
 
Back
Top Bottom